Mange Kimambi Amlilia Diamond Amsamehe Baba Yake

Mange Kimambi amemuandikia ujumbe wa wazi staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz kuhusu kumsaidia baba yake mzazi Mzee Abdul Juma ambaye anatajwa kuwa mgonjwa.

Kwa muda mrefu kumekuwa na Ugomvi wa kifamilia kati ya Diamond na baba yake ambapo amewahi kuweka wazi kuwa hajalelewa na baba yake bali na Mama yake ambaye ndiye anayemjali.

Wiki iliyopita Baba yake na Diamond aliweka wazi kuwa anaumwa na anasumbuliwa na maradhi mbali mbali ikiwemo miguu ambayo ipo katika hali mbaya na kumlilia mwanaye amsaidie japo akapate matibabu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mange amemuomba Diamond aweke tofauti zao pembeni na amsaidie baba yake ambaye yupo katika hali mbaya:

https://www.instagram.com/p/Bt-nyKVBEgD/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=tevtyrdp2c9w

Mange Kimambi Amtolea Povu Zito Hamisa Mobetto

Mange Kimambi ameibuka na kumtolea Povu zito Msanii Hamisa Mobetto ambaye pia ni mdogo Wake wa hiyari Baada ya kuweka picha mtandaoni akiwa na mpenzi Wake Mpya.

Siku ya jana Mobetto aliingia kwenye vita ya mtandaoni na mrembo mwingine anayeitwa Tahiya Baada ya kumtuhumu Mobetto kwa kumchukulia mwanaume wake anayeitwa Alex.

Hamisa na Mpenzi Wake Alex

Ili kudhihirisha kuwa Mobetto hajamuiba mwanaume bali ni Mpenzi Wake na sio wa Tahiya Hamisa aliposti picha Kupitia ukurasa wake wa Instagram akiwa na bwana huyo huku akimrushia vijembe Tahiya.

Baada ya sakata Hilo Mange alimjia Mobetto na kumtaka aache kujianika na wanaume tofauti katika mitandao ya kijamii ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram alimuandikia ujumbe huu:

https://www.instagram.com/p/Bs1kmnTAnLN/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=4sk802wnincs

Mange Kimambi Ampokea Shetta Kwa Mikono Miwili

Mwanamama maarufu kwenye mitandao ya kijamii Mange Kimambi amefunguka na kusema yupo tayari kuolewa na staa wa Bongo fleva Shetta Baada ya kuweka wazi hisia zake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Shettta aliweka wazi kuwa anamkubali sana Mange Kimambi na hata kudai kuwa angependa kama angeweza kuwa Mpenzi Wake na hatimaye kufunga naye ndoa.

Mange amemjibu Shetta na kusema kuwa yupo tayari kufunga naye ndoa na kwa pamoja waweze kulea watoto wao.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mange amemuandikia Shetta Ujumbe huu:

https://www.instagram.com/p/BrQ5ZsigamT/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1xb5kl9rsf6ch

Shetta Atangaza Ndoa na Mange Kimambi

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Shetta ameibuka na kukiri mapenzi yake kwa Mange Kimambi na kudai yuko tayari hata kufunga naye ndoa kwani anampenda sana.

Shetta ameweka wazi mapenzi yake kwa Mange ambaye Hivi karibuni aliwahi kuposti katika ukurasa wake wa Instagram na kusema wazi kuwa anamkubali.

Kwenye mahojiano aliyofanya na mtandao wa Bongo 5, Shetta amefunguka haya kuhusu mahusiano yake na Mange Kimambi:

Mange ni my girlfriend wangu mpya na labda naona kama naweza kuona kwamba naweza kukaa pale maana ananikosha sana kwa picha zake anazoposti.

Halafu pia nina mpango wa kumuoa na kumuweka ndani yule Dada maana ni mzuri hasa maziwa yake yaani mi hoi”.

Shetta anafanya vizuri na ngoma yake ya ‘Hatufanani’ aliyowashirikisha wasanii Kama  Mr. Blue na Juma Jux.

Mange Amtaka Wolper Asirudi Kwa Harmonize Maana Ameachwa na Mzungu

Mange Kimambi ameibuka na kumfungukia Staa wa Bongo movie Jacqueline Wolper kuhusu kurudiana na Ex Wake Msanii wa Bongo fleva Harmonize na kumtaka asijaribu.

Mange ameongea hayo Baada ya kuwepo kwa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Wolper na Harmonize wamerudiana Baada ya kuonekana pamoja wakiwa beneti kwenye tamasha la Wasafi Festival.

Mange amemchana Wolper na kumtaka kutorudi kwa Harmonize kwa sababu hana mapenzi ya kweli kwake kwani amerudi Baada ya kuachwa na Sarah ambaye amemtimua Nyumba waliokuwa wanaishi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mange Kimambi ameandika:

https://www.instagram.com/p/Bq8-aiHAvPK/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=wwhqlwlkrzki

Ali Kiba Ndiye Msanii Pekee Asiyehitaji Kiki Wala Matusi Kujaza Shoo-Mange Kimambi

Mwanaharakati wa mambo ya siasa mtandaoni Mwanamama Mange Kimambi ameibuka na kumpigia  saluti staa wa Bongo fleva Ali Kiba na kudai kuwa hakuna Kama yeye Bongo nzima.

Mange ameongea hayo Baada ya shoo iliyofanyika Wiki iliyopita mjini Kahama kujaza nyomi la ajabu pamoja na kwamba Ali Kiba hakuipigia promo shoo Ile Kama ilivyokuwa kwa Wasafi Festival na Fiesta.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mange Kimambi ameandika maneno haya:

Ujumbe huo umeonekana Kama Dongo kwa mpinzani wa Ali Kiba Diamond Platnumz na tamasha lake la Wasafi Festival ambao walionekana kutoa promo ya nguvu Lakini pia Fiesta ambayo ilikuwa katika majobizano na Wasafi.

Mange Amtaka Ruby Apunguze Kiburi Ili Afanikiwe

Mwanaharakati wa mambo ya siasa mtandaoni Mange Kimambi ameibuka na kumchana live mwanamuziki wa Bongo fleva Ruby na kumtaka aache kiburi.

Lwa muda mrefu kumekuwa na taarifa kwamba Ruby amekuwa hana maelewano mazuri na watu anaofanya nao kazi na kupelekea kuzidi kushuka kimuziki.

Mange amempa makavu Ruby na kumtaka apunguze kiburi kama anataka kufanikiwa kwani watu wengi wanashindwa kufanya naye kazi kutokana na jeuri na kiburi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mange amemuandikia Ruby ujumbe huu:

https://www.instagram.com/p/BqIdS2bA8qX/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=ww4uerb3oa9a

Mange Adai Ali Kiba Atapotea Kimuziki Bila Bifu na Diamond

Mwanaharakati wa mambo ya siasa kwenye mitandao ya kijamii Mange Kimambi amefunguka na kudai Bifu linaloendelea kati ya Diamond Platnumz na Ali Kiba linamfaidisha zaidi Kiba.

Sakata hilo limekuja baada ya msanii Diamond kutaka kumaliza Bifu lake na Ali Kiba Siku ya Jana Baada ya kumualika kushiriki katika tamasha lake la Wasafi Festival.

Mange amepima uzito ishu hiyo na kusema kuwa Ali Kiba Hatakiwi kupatana na Diamond kwani year ndio anafaidishwa na Bifu hilo Babu bila Bifu hilo ana hatihati ya kupotea kimuziki.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mange Kimambi ameandika:

Sio kama nachochea ugomvi ila nimeongea fact tu. Tujikumbushe Ray na Kanumba. Mnalikumba beef lao? Siku Kanumba alipokosekana na lile bifu lilipokosekana Ray si alishuka na umaarufu ukapungua vibaya mno mpaka akapotea. .
So lile beef ndio lilikuwa linaibeba career ya Ray. Kwenye situation kama hizi yule ambae ndio msanii mkubwa zaidi huwa ana gain kiki kwenye beef ila anae gain sana ni yule mwingine. Beef la Ray na Kanuamba aliegain sana ni Ray ndo maana Kanuamba kukosekana akafulia.

Sasa naomba mu-ally hii concept to Diamond and Kiba. Then mtaelewa kwanini nasema hao wakipatana Diamond will win Kiba will loose. Diamond ndio ana benefit kwenye hili beef ila ana benefit kidogo mnoo anae benefit zaidi ni Kiba na ukijumlisha na dharau anazomfanyia ndio anazidi kupanda hata bila kutoa nyimbo ??. Ila wakipatana Diamond will gain everything and Kiba will loose everything. Wakipatana hao ndio utakuwa confirmation ya Diamond as the ONLY main artist wa Tz. Na Diamond is very strategic amelijua hili, keshajua kugombana na Kiba kuna faida ndogo sana kwake na faida kubwa sana kwa Kiba.Amestuka kuwa anamfaidisha Kiba. Na anajua akipatana na Kiba ni faida kubwa mnooo kwake na Kiba atapata faida ndogo. Ndo maana mnamuona Dai anahangaika staili izote ili mradi aelewane na Kiba. Anajua akielewana nae anampoteza mazima. Diamond sio mtu wa kujishusha kwa mtu kiasi hiki. He is very smart. Ana mahesabu yake. Ila na Kiba nae keshausoma mchezo ndo maana anampotezea tu ??. Na Diamond naamini amerealize hiki kitu kwenye seduce Me, maana alivyoleta ushindani ndio nyimbo ya Kiba ilinoga mara 1000 na watu waliisapoti kwa ushabiki na hasira ili wamkomeshe Dai. So So kaona bora amsogeze karibu ili ammalize kabisa abakie yeye ndio Konki Masta pekee wa bongo flava. .

Irene uwoya Amshukuru Mange Kimambi

Mwanadada Irene Uwoya ameonekna kufurahia na kumshukuru sana Mange Kimambi baada ya kutoa siri iliyokuwa imejificha muda mrefu kuhusu uwepo wa mahusiano ya siri kati ya Dogo janja na wema sepetu siku za nyuma.

Katika mvurugano uliotokea hapo karibuni baada ya Wema kuweka picha ya mume wake mpya mtarajiwa, mange kimambi aliamua kuvuruga kila kitu na kuweka mawasiliano yake na dogo janja aimuomba asisieme lolote kuhusu waliowahikuyafanya na wema.

Hata baada ya kuvujisha mazunguzmoa hayo, irene alianaidka chini ya cption hizo kumshukuru mange kimambi kwa kitendo cha kuyasema hayo yote hadharani kwa sababu yeye hasingeweza kuaminiki ingawa siku za nyuma alisema sababu kubwa ya kuachana na Dogo janja ni kuchepuka kwa mume wak nawanawak wengine.

Mange Kimambi Amshauri Hamisa Asirudi Kwa Diamond Adai Ana Gundu

Mwanaharakati wa Mambo ya siasa Mtandaoni Mange Kimambi ameibuka na kumshauri Hamisa Mobetto asithubutu kurudi tena  kwa mzazi mwenzake Diamond Platnumz kwa madai kuwa ana gundu.

Hamisa aliweka wazi kuwa yeye na mzazi mwenzake staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz waliachana Mwanzoni mwa mwezi huu baada ya kuwa pamoja kwa miaka kadhaa.

Lakini baada ya kuachana Hamisa aliingia kwenye mgogoro na Familia nzima ya Diamond ambao waliishia kumtangaza kama mchawi mara baada ya kuwaendea kwa mganga.

Mange Kimambi ameibuka na kumshauri Hamisa asirudiane Tena na Diamond kwa madai kuwa familia nzima ya Diamond ilikuwa inampa gundu tu kwani sasahivi tangu ameachana nao amekuwa akipata madili mengi ya ubalozi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mange ameandika maneno haya:

https://www.instagram.com/p/BoGFxI6larV/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1o9n4uzj4l67d

Wastara Sajuki Atangaza Vita na Mange Kimambi

Muigizaji wa Bongo movie mwanamama Wastara Juma maarufu kama Wastara Sajuki ameingia katika sintofahamu na Mwanaharakati wa siasa mtandaoni Mange Kimambi.

Sakata kati ya Wastara na Mange Kimambi lilianza siku za nyuma mara baada ya kumtuhumu Wastara kwa Kula pesa za Michango ambayo alichangiwa na wananvhi kwa ajili ya kufanyiwa matibabu nchini India.

Siku ya jana Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari, Wastara alimmwagia povu zito Mange na kudai aliumizwa na madai yake ya kwamba alikula pesa za Michango na kusema Yupo Tayari kupambana naye kwani amemchafulia jina.

Asubuhi ya leo Mange aliandika Kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa akipata muda lazima atampa kichambo Wastara na mara moja Wastara akajibu mashambulizi na kusema anamsubiri kwa hamu:

 

Kisa Hamisa, Mange Kimambi Awashambulia Esma Na Mama yake .

Baada ya kuibukakwa tuhuma za uchawi kutoka kwa mwanadada Hamisa Mobeto kuwa amekuwa aikiiloga familia ya Diamond Platinumz, mwanaharakati mashghuli Mange Kimambi aliamua kuingilia kati swala hilo na kuamua kumtetea Hamisa dhidi ya wanafamilia ya Diamond.

Mambo yanazidi kuwa mambo baada ya Mange kuamua kuituka familia ya diamond na ndipo familia hiyo hasa dada wa Diamond alipoamua kujibizana na Mange katika mitandao ya kijamii.siku ya jana ilizid kuchafuka katika ukurasa wa instagram baadaya wawili hao kuingia katika ligi ya kutukanana matusi huku kila mmoja akijitaidi kutetea upande wake.

Kwa upande wa Mange anasema kuwa familia hiyo haukupaswa kumtuka hamisa ukizingatia wamekuwa wakimsema kuwa kila mtoto ana baba yake ilhali hata esma nae ana watoto ambao kila mtu na baba yake.

Hata hivyo Mange anaendelea kutoa siri kuwa kutokana na maswala ya uchawi ndio maana hata aliwahi kumuua mtoto wake wa kwanza ambae watu wengi hawakuwahi kumjua alipokuwa akiumwa na kushindwa kumpelea hospitali kwa madai kuwa amelogwa hivyo kumpeleka kwa waganga.

Esma nae hakukaa kimya na kuseme akuwa mara nyingi mange amekuwa hajielewi na ndio maana amekuwa akiongea maneno yasiyokuwa na uhakika nayo na kikubwa zaidi ni pale Esma nae alipoamua kuanza kuongea kuhusu familia ya Mange huku akiwataja baba na mama yake mzazi na mtoto wa kwwanza wa kike wa mange ambae inasemekana amekuwa akifanya biashara ya ngono akiwa bado na umri mdogo.

Bado ligi inazidi kuendelea huku masabiki wakitaka kujua ni nani anaweza kukaa kimya baada ya kutukana na kwa muda mrefu.

Mange Amtupia Wema Tuhuma Nzito Za Kwenda Kwa Waganga Kama Mobetto

Mange Kimambi ameingia Kwenye bifu zito na msanii wa Bongo movie Wema Sepetu baada ya sakata la uchawi la Hamisa ambalo lilishika kazi baada ya voice note kuvujishwa mtandaoni.

Mange na Wema walianza kurushiana maneno baada ya Mange kumtuhumu Wema kwa kushabikia kesi ya Mobetto ambapo Mange alimwambia Wema asishabikie sana kwani yeye mwenyewe ameshawahi kupata skendo za waganga.

Baada ya maneno hayo kusemwa ndipo vita ya maneno na matusi ilianza kwani Wema alikataa kuwa hajawahi kwenda kwa waganga hata siku moja na kuweka posti hii:

https://www.instagram.com/p/BnUKOienUro/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1swhan939ccq1

Mange alimjia juu Wema juu ya tuhuma za Kwenda Kwa Waganga na kuweka video ya miaka ya nyuma ambayo Mama Wema aliongea na kukiri mtoto wake ana tabia za kwenda kwa waganga:

https://www.instagram.com/p/BnUWEWHlxF5/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=imnibw87yviy

Mange Kimambi amkingia Kifua Hamisa, Amvaa Ray C

Mwanaharakati kupitia mitandao ya kijamii Mange kimambi amefunguka na kumtolea povu zito msanii wa muziki wa bongo fleva Ray c baada ya msanii huyo kuonekana kama anamganda sana kooni mwanadada Hamisa Mobeto hasa baada ya haisa kutoa wimbo wake mpya wa madam hero.

Katika moja ya post zake , Ray c alionekana kutopendezwa na wimbo huo na kusema kuwa ni bora asngeimaba kabisa.

Hata hivyo  Mange kimambi aliguswa na maneno ya Ray c kwenda kwa Hamisa na ndipo alipoamua kumtola povu zito Ray c na kumshauri amuache binti ambae hawaendani hata umri.

Usikose kusikiliza nyimbo ya madam hero kutoka kwa hamisa , endelea kupambana mama najua ukifika umri wa vizee kama wetu utakuwa umefikia mafanikio makubwa sana.sijui watu huwa wanawaza nini kufananisha mafanikio ya mtoto wa miaka 23 na wao wa miaka 40  watanzania bhana sijui mnanini, inabidi mumfananishe na watu wa umri wake sio wa sisi vizee.

Hata hivyo Mange kimambi amempa moyo Hamisa na kumwambia aendelee kupambana na atafika anapopataka.

 

Mange Kimambi Aibuka Kidedea Tuzo za beffta

Waandaaji wa tuzo za beffta wametoa matokea ya tuzo mbalimbali, ambapo katika kipengele cha Most Inspirational African Female  Politics ameshinda mwanadada Mange Kimambi mtanzania anaeishi Marekani.

Katika ukurasa wake wa instagram, Mange kimambi amendika yafuatayo baada ya kutangazwa “‘i’m honoured  to every person who voted for me , thank you .”

Tuzo hiyo iliyolewa kwa mange kimambi iliangazwa katika mitandaoa na kuwataka watu  wananchi kumpigia kura mshiriki wanaeona anafaa kupewa tuzo hiyo.

 

Mange Ashutumiwa Kuiba Akaunti ya Makonda.

Mwanadada mwanahrakati katika mitandao ya kijamii mwenye asili ya Tanzania lakini anayeishi Marekani, Mange Kimambi  ameshutumiwa na watu wa page mbalimbali za udaku baada ya akaunti ya mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam kuibwa na watu wasiojulikana na kuvuta kila kitu katika akaunti hiyo.

Mwanadada huyo ambae hapo awali alishutumiwa kuiba akaunti ya Wema sepetu na baada kurudishwa ameingizwa katika swala hilo tena baada ya kuona kuwa aliyeiba akaunti hiyo kufuta na kuwaun-follow watu wote na kuacha jina la mange kimambi tu kama mtu anayemfuata .

Hata hivyo mwanadada huyoa ambae amekuwa akivumbua siri nyingi sana za huku tanzania na pia kusaidia watu wengi kupitia ukurasa wake hajazungumza chochote kama ambavyo imekuwa ikizoeleka kwamba kinapotea kitu kuhusu yeye uongea katika ukurasa wake.

Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa mwanadada huyo kuambaiwa amefanya vit vya kuumiza  mtu mmoja au mwingine tena hasa kwa upande wa Mkuu wa Mkoa hasa kwa sababu hakuna maelewano mazuri kati ya mwanadada huyo na Mh Mkuu wa Mkoa.