Master J Apasua Kuwa Shaa Ameacha Mziki na Kugeukia Kilimo

Mtayarishaji wa Muziki maarufu na Mkongwe Katika tasnia ya Bongo fleva Master J ameweka wazi kuwa msanii wa Bongo fleva Sarah Kaisi maarufu kama Shaa ameachana na Mziki na kugeukia kilimo.

Master J ambaye amekuwa Kwenye Mahusiano ya kimapenzi na Shaa kwa miaka mingi amesema ukimya wa Shaa Kwenye muziki ni kutokana na maamuziki ya kuweka sanaa pembeni.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Master J amedai Shaa ameamua kuacha muziki na kufanya kilimo kinachomuingizia kipato kikubwa zaidi na sasa yupo mkoani Mbeya.

Shaa ni mfanyabiashara sasa hivi yupo busy na kulima kule Mbeya naona inalipa zaidi nimejaribu kumshawishi arudi Kwenye muziki lakini ananiambia subiri apige kazi apate pesa ndio atarudi tena kwenye  muziki”.

Lakini pia Master J ameweka wazi kuwa yeye na Shaa bado wapo wote Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi.

Harmonize Wa Bongo Star Search Alikuwa Mbovu- Master J

Mtayarishaji wa muziki wa Bongo fleva mkongwe kabisa nchini Master Jay ameweka wazi kuwa Harmonize wa Bongo Star Search hakuwa mkali kama wa hivi sasa.

Sio Siri Harmonize ni moja kati ya wasanii anayefanya vyema sana hivi sasa katika tasnia ya Bongo fleva lakini kabla ya mafanikio haya Hatmonize alishawahi kushiriki katika mashindano ya Bongo Star Search.

Kwenye mashindano hayo Harmonize alitolewa na kukosolewa lakini miaka michache baadae alikuja kusainiwa na Wasafi Records na mpaka leo ni Msanii mkubwa Tanzania.

Siku ya jana Shindano la BSS lilitangazwa kurejea Rasmi na moja kati ya jambo ambalo liliulizwa sana kwa Majaji ni Ishu ya Harmonize ambapo Master Jay ameweka wazi kuwa Wakati Harmonize anashiriki BSS alikuwa Msanii mbovu.

Harmonize aliyekuja Kwenye BSS miaka ile alikuwa mbovu iko wazi kabisa hata mimi nimeweka ile clip Kwenye page yangu yaani Harmonize aliyekuja Kwenye BSS siyo huyu wa leo anayefanya vizuri”.

 

Master J Adai Ma-Prodyuza Hawalipwi Vizuri Kama Zamani

Producer mkongwe wa Muziki wa Bongo fleva Joseph Kimario maarufu kama Master J amefunguka na kuweka wazi kuwa watayarishaji wa muziki wa sasa hawalipwi vizuri kama ilivyokuwa kwao siku za nyuma.

Master J alijizolea umaarufu kutokana na kutengeneza hits songs kibao kwa wasanii wakongwe Kupitia Music Label yake ya MJ Records.

Kwenye mahojiano yake na EFM, Master J amefunguka na kusema kwamba kuna watayarishaji wengi wahalipwi vizuri kuliko wale ambao wanalipwa vizuri kidogo.

Maproducer wengi hawapati kitu, yaani msanii akikuheshimu sana atakupa laki mbili au laki tatu lakini hawa wengine wote ni laki kushuka chini wimbo mzima mpaka beat”.

Lakini pia Master J amewataka Maprodyuza kuhakikisha wanakuwa wabunifu ili kutengeneza Muziki utakaosanifu uhalisia wa Bongo fleva:

Kiukweli Muziki wetu umepoteza uhalisia tunakopy sana kutoka kule Nigeria, Maproducer waongeze ubunifu kidogo ili tuweze kuwa na aina ya Muziki wetu . Kwa maana hili sio zuri maana tuna makabila Zaidi ya 120 tunaweza kuchanganya na kupata uhasilia wetu” .

Master J alitangaza kuachana na kutengeneza muziki na kuamua kuangalia biashara zake nyingine  na kuwakabidhi MJ Records vijana wengine.

Harmorapa Amuomba Radhi Master J Kwa Upuuzi Aliomuongelea

Mwanaumuziki wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kurap Harmorapa ameibuka tena na safari hii amedai kuwa anamuomba msamaha producer maarufu Bongo Master J.

Harmorapa amemuomba radhi producer mkongwe bongo baada ya kudai kuwa hamfahamu wala hajawahi kumsikia hapo kabla. Master J ni moja kati ya waanzilishi wa mziki wa bongo fleva kwa kuhusika katika kuvumbua vipaji vingi kupitia studio yake ya Mj Records.

Harmorapa alifunguka hayo alipokuwa anahojiwa kwenye kipindi cha Enews ya East Africa TV na kusema katika mwaka huu wa 2017 amemkosea sana Master Jay kufuatia kauli yake aliyoitoa kipindi cha nyuma kupitia katika kipindi hicho ambapo alidai kuwa hamjui wala hamtambui mtayarishaji huyo mkongwe wa Bongo fleva.

Kwa kweli niligundua kuwa nilifanya makosa makubwa sana, unajua kipindi kile nasema vile nilikuwa sijamjua vizuri Master Jay hivyo naomba anisamehe”.

Kipindi cha nyuma Harmorapa aliwahi kumkana mtayarishaji huyo wa muziki na kudai kuwa hamjui wala hatambui kipaji chake Harmorapa alitokwa na povu hilo baada ya kusikia Master J akidai kuwa Harmorapa hana kipaji chochote cha kuimba wala kucheza labada ajaribu fani ya uchekeshaji maneno yaliyomchoma Harmorapa kupita kiasi.