Maua sama ajivunia mafanikio ya Iokote

Mwanadada Maua Sama ameonyesha kupata mafanikio makubwa kutokana na wimbo ulifanya vizuri sana mwaka 2018 uliojulikana kwa jina lka Iokote ambao ulivuma sana ndani na nje ya tanzania.

Maua sama ansema kuwa idadi kubwa ya mashabiki zake waliopenda wimbo huo walimfanya apate hata nguvu ya kupush wimbo huo kutokana na wao kuupokea vizuri.

Hata hivyo mwanadada huyo anazidi kuwapa moyo mashabiki zake kutokana na mafanikio hayo hasa baada ya kununu gari ya rav4 inayosemwa kuwa na thamani ya zaidi ya milion 20 na hata sasa kununua kwanja tayari kwa ujenzi.

Mwanadada huyo ambae amekuwa kimya asietaka kuonyesha nini anafanya, Amfanya vizuri sana kwa mwaka uliopita huku mashabiki wakisubiri ujio mpyta baada ya Iokote.

Mafanikio Ya ‘Iokote’ Yampelekea Maua Sama Kuporomosha Mjengo

Msanii wa muziki wa Bongo fleva ambaye mwaka jana alifanya vyema na wimbo wake wa ‘Iokote’ amefunguka na kusema nguvu ya mashabiki katika kumpa sapoti kumemsaidia kuweza kununua gari na sasa kujenga Nyumba.

Maua Sama ambaye siku si nyingi aliweka wazi gari aina ya Toyota Rav 4 ambalo alikiri kuwa alinunua kutokana na wimbo wake wa Iokote kufanya vyema Lakini sasa amesema ameweza kununua kiwanja kwa ajili ya kujenga Nyumba yake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Mchanganyiko, Maua Sama alisema kuwa kwa sasa ameanza ujenzi wa ‘bangaloo hatari’ maeneo ya Mbweni jijini Dar.

Mashabiki wangu ndiyo wamenipa mafanikio na kunifanya niweze kununua kitu ambacho nakitaka, hata hili gari limetoka kwao hakuna mtu mwingine zaidi ya mashabiki wangu na nipo mbioni kumalizia mjengo wangu kwa nguvu zao”.

 

Kamwe Sitakaa Niusahau Mwaka 2018- Maua Sama

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Maua Sama aliyefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Iokote’ amefunguka na kuweka wazi kuwa kamwe hatakaa asahau mwaka 2018.

Mwaka jana Maua Sama alijikuta katika wakati mgumu mara Baada ya kuwekwa mahabusu kwa muda wa siku 10 bila dhamana Baada ya kudaiwa kuidharau na kuichezea pesa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Maua Sama amesema kuwa anaukaribisha Mwaka Mpya wa 2019 vizuri, lakini hatausahau 2018 kwani alipitia Mengi na kujifunza mengi.

Namshukuru sana Mungu nimemaliza mwaka salama japokuwa nimekutana na changamoto kubwa ambayo sikuitarajia kuipata ile ya kuwekwa ndani kutokana na ngoma hiyo ya Iokote.

Lakini nashukuru soo liliisha salama na nilijifunza ninatakiwa kuheshimu kila kitu, kwa hiyo sitarajii kitokee kitu kama kile tena katika maisha yangu.

Kwa sasa ninajikita zaidi kwenye kazi ya sanaa kwa kuwa najua nimejaliwa kipaji na nitatoa kazi ambazo wapenzi wa Maua wanahitaji ili niweze kukonga nyoyo zao”.

 

Maua Sama Haogopi Nafasi ya Iokote Kutambulisha Wimbo Mpya.

Mwanadada Maua sama anasema kuwa katika maisha yake ya muziki kwa sasa pamoja na kwama wimbo wake wa Iokote ni wimbo ulifanya kazi vizuri sana kwa mwaka huu lakini bado anaona kuwa sio kitu yeye kuogopa kufanya wimbo mwingine akihofia nafasi ya ule uliopita.

Maua anasema kuwa hataki kusumbuliwa na presha ya  Iokote kwa sababu hata wakati anatoa wimbo huo hakuwa amefikiria kama utachukua nafasi kubwa kiasi hicho.

Maua Sama anasema ” Unajua wasanii wengine wamekuwa wakipotea kwa sababu ya kufanansiah nafasi ya wimbo waliotoa na ule uliopita, lakini kwangu ni tofauti kwa sababu tayari nimeshajianda kuja na muziki wangu ambao  ni kawaida kuwakonga nafsi za mashabiki.”

Maua anasema kuwa hakuna wimbo ambao aliona anaweza kukosea kama wimbo wa iokote kwa sababu haikuwa style yake ya muziki lakini ndio umefanya vizuri mpaka anashangaa.

Maua Sama Afuata Nyayo Za Rostam Kwa Hili

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini aliyofanya vyema na ngoma yake ya ‘Iokote’ Maua Sama amefunguka na kuweka wazi anaunga mkono msemo wa wakali wa Hip Hop Roma na Stamina (Rostam).

Roma na Stamina Wameunda msemo wao wa ‘Tunafunga Jumla jumla’ kwa ajili ya kuufungia mwaka 2018 kikazi zaidi kwa njia ya Sanaa ya muziki.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Mchanganyiko, Maua Sama anayetamba na Ngoma ya Iokote alisema kuwa, ametokea kuvutiwa na msemo huo baada ya kuusikia na kwamba anatamani kuja na wimbo wenye jina hilo.

Nimependa kwa kweli, kwa sababu msemo kama huu kutumika mwishoni mwa mwaka huwa mzuri, unaweza kuta mtu umefanya biashara zako sasa unafunga jumla jumla ili ufungue mwaka mwingine.

Nitajaribu kuongea na Rostam ikiwezekana nitatoka na wimbo wa tunafunga jumla jumla baada ya hii ya Iokote”.

Maua Sama licha tu ya kuvutiwa na msemo wa Roma na Stamina ‘Tunafunga jumla jumla’ na kutaka kufanya wimbo Lakini pia wasanii hao wametangaza kufanya baadhi ya shoo pamoja.

Rostam na Maua Sama Wawasanua Mashabiki Zao

Wasanii wa muziki wa Bongo fleva wanaounda kundi la Rostam Roma na Stamina pamoja Maua Sama Wake wateja Mashabiki zao Baada ya kuanzisha msemo wa Tunafunga Jumla jumla.

Katika kurasa zao kwenye mitandao ya kijamii, wawili hao wamekuwa wakiposti picha zao na wakati mwingine wa tukio fulani wa­kiambatanisha na maneno Tunafun­ga Jumla Jumla, jam­bo ambalo mashabiki wengi wamekuwa wak­ishindwa kung’amua maana yake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi, Roma alisema neno hilo alianza kuliona kwa Stamina lakini anashangaa wengine wameanza kuliiga huku wengi wakiomba ufafanuzi.

Ukiniuliza maana yake sielewi ila ni misemo kama ilivyo misemo mingine. Mfano Mangi anaweza kufunga duka akasema nafunga jumla jumla, au mama n’tilie, muuza maji, karanga na wengine wengi kwa hiyo suala la biashara kuna kufunga jumla jumla”.

 

Maua Sama Afananishwa na Darasa

Mwanadada Maua Sama ambae kwa sasa amekuwa habari ya mjini kwa wimbo wake wa Iokote anafananishwa na Darasa baada ya wimbo wke huo ku-trend sana kila mahali na hata nje ya nchi huku watu wakipata wasiwasi kuwa isije kuwa kama alivyopotea darasa baada ya kutoa wimbo wa muziki na kisha kuwaancha mashabiki na kiu ya muziki wake.

Ikumbukwe kuwa Darasa alianza taratibu katika muziki na hata baadae kutoa wimbo ambao ulikuwa kama wimbo wa taifa na kupendwa na mashabii wote lakini baada ya muda mchache wimbo huo kufanya vizuri mashabiki walitegemea kuwa Darasa atatoa nyimbo nyingine nzuri kuliko hiyo lakii cha ajabu alikatisha mapenzi ya mashabiki baada ya kupotea abisa.

Ujumbe kwa Maua Sama ni kwamba mashabiki hawataki kuangushwa kama inavyotokea kwa wasanii wengine wenye mfano kama darasa, wanachotaka ni burudani na uwepo wako katika game.

 

Maua Sama Akana Kutumia Uchawi Kupata Mafanikio

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Iokote’ Maua Sama amefunguka na kuweka wazi kuwa hajawahi kutumia nguvu za giza ili kupata mafanikio katika kazi zake za kimuziki.

Maua ametoa siri ya mafanikio yake na kusema ni Mungu pekee ndiye amempa mafaniko katika kazi zake za kimuziki.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Maua alisema anachoamini siku zote kwenye maisha yake kuwa wakati wa Mungu ndio sahihi siku zote hivyo mpaka wimbo wake huo unatokea kupendwa hivyo ni kwamba amewapa mashabiki wake wanachotaka.

Unajua mtu mwingine anaweza kujua ni uchawi kumbe sio kabisa ni muda sasa wa Mungu ameamua kukurudisha kwa kasi kwa mashabiki wako na hicho ndio kitu muhimu sana”.

Maua amezidi kung’aa na wimbo wake huo ambao umekuwa ukihit sana na mpaka sasa unashukilia chati katika vituo mbali mbali vya redio an televisheni lakini pia kuwa na watazamaji mamilioni katika mtandao wa Youtube.

Maua Sama Afungukia Mafanikio Ya ‘Iokote’

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Maua Saleh maarufu kama Maua Sama amefunguka na kuongelea mafanikio ya wimbo wake wa ‘Iokote’ ambao unaendelea kufanya vyema.

Licha ya Maua kufanya nyimbo kadhaa nzuri huko nyuma lakini wimbo wake wa ‘Iokote’ ndio umekuwa kama umemtambulisha sana Kwenye ulimwengu wa Bongo fleva.

Katika mahojiano yake na Global Publishers , Maua aliyeimba wimbo huo kwa kushirikiana na ndugu wa marehemu Banza Stone, Hanstone alisema kuwa, katika maisha yake hajawahi kutegemea kama ataachia wimbo wa kumchanganya kiasi hicho ambapo tangu autoe umezidi kumpa shoo hadi anachanganyikiwa.

Yaani sijui hata nisemaje, Iokote imenifanyia maajabu makubwa sana hata nashindwa nielezeaje, kama huko nje ya nchi hadi sasa napata shoo hadi nachanganyikiwa nitajigawaje. Ukiingia mitaani, kwenye usafiri ndiyo nakuwa chizi kabisa”.

Licha ya mafanikio aliyopata Maua Sama Kupitia wimbo huo Lakini pia alipitia kipindi kigumu mara baada ya kuwekwa rumande kwa muda wa wiki nzima baada ya kukamatwa

Maua Sama Atembea Kifua Mbele kwa WCB.

Mwanadada Maua Sama ameonyesha juhudi zake mbele ya wasanii wengine baada ya wimbo wake wa iokote kufanya vizuri  katika mitandao na station mbalimbali za burudani.Maua ambae hivi karibuni amekuwa katika wakati mgumu kutokana na kuweka rumande kwa zaidi ya siku tano anaonyesha kufurahishwa na jambo hilo.

Wimbo wa Iokote ndio uliomfanya Maua  kuwekwa rumande kutokana na hisia za mashabiki katika wimbo huo na kushtakiwa kwa kosa la kudharirisha pesa ya Tanzania.

Hata hivyo tangu akiwa bado polisi rekodi ya wimbo huo kufanya vizuri ilikuwa ikionekana na  mpaka sasa wimbo huo unaonekana kuendelea kufanya vizuri  na kuwashinda wasanii wa WCB na nyimbo zao mpya ambazo nyingi zimetoka hivi karibuni.

“Nimepitia Kipindi Kigumu Sana” Maua Sama Afunguka Baada Ya Kuachiwa Huru

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva anayefanya vyema na kibao chake cha ‘Iokote’ Maua Sama amefunguka kwa mara ya kwanza tangu aachiwe huru kwa dhamana na jeshi la polisi.

Maua Sama na Mtangazaji wa Clouds Media Soudy Brown walitiwa mbaroni wiki iliyopita baada ya kuchapisha Kwenye mitandao ya kijamii maudhui ya watu wakicheza na kukanyaga pesa.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Maua Sama amefunguka na kueleza jinsi alivyopitia kipindi kigumu katika siku 10 ambazo alikuwa chini ya ulinzi:

Soudy Brown na Maua Sama Waachiwa Kwa Dhamana

Mtangazaji wa Clouds Fm Soudy Brown na Msanii wa Bongo fleva Maua Sama wameachiwa kwa dhamana na jeshi la polisi baada ya kukaa rumande kwa wiki moja.

Soudy Brown na Maua Sama walishikiliwa na jeshi la polisi baada ya kuhusishwa na video waliyoisambaza Kwenye mitandao ya kijamii iliyoonyesha watu wakichezea na Kukanyagawpes

Soudy Brown, Maua Sama na Meneja wake Fadhili Kondo waliachiwa jana Septemba 25, jioni lakini wote wanatakiwa kesho kuripoti kituo cha kati (Central Police Station) saa 4 asubuhi.

Watatu hao jana walirudishwa mahabusu baada ya kupata dhamana ya kesi ya kwanza ya kuweka maudhui mitandao bila kibali kutoka kwa mamlaka husika, lakini waliendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa kile kilichodaiwa kuwa bado wanakosa lingine la kujibu, huku Mawakili wao wakizungumzia tukio la kukanyaga fedha ya Tanzania.

Wasanii ni Wanafiki Wanasubiri Kutoa Pole Badala Ya Kusaidia”- Steve Nyerere

Msanii wa Bongo movie na komedian maarufu Steve Nyerere amefunguka na kutaka Wasanii Wenzake waache unafiki na kupaaza sauti sasa ili Soudy Brown na Maua Sama waweze kuachwa huru.

Maua Sama na Soudy Brown wamewekwa  ndani tangu siku ya Ijumaa mpaka leo hawajapata dhamana baada ya kuposti video clip iliyowaonyesha kundi la watu wakicheza wimbo wa Iokote wa Maua Sama huku wakirusha pesa na kuzikanyaga.

Steve Nyerere amewatolea povu wasanii Wenzake na kuwataka wajitoe kuwasaidia wasanii wenzao katika kipindi hiki cha shida badala ya kukaa kimya halafu kuja kutoa pole wakija kutoka hapo baadae.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Steve Nyerere amemwaga povu hili:

Sisi wasanii ni waoga na wanafiki, limeanza kuhusishwa sijui kuna ugomvi na RC Makonda hawa wamekosea, sio wakitoka ndio tuanze kutoa pole, Ndio nilipanga kufanya hivi, Hapana muda ndio huu tuombe radhi kwa serikali vijana wetu wapewe dhamana”.

 

 

Vanessa Mdee Amfariji Maua Sama “Usijali Utatoka Tu”.

Staa wa Muziki wa Bongo fleva Vanessa Mdee amefunguki ishu ya Msanii mwenzake Maua Sama kuwekwa Ndani kwa siku tano mfululizo bila ya dhamana.

Maua Sama anewekwa  ndani tangu siku ya Jumapili mpaka leo hajapata dhamana baada ya kuonekana kwenye video clips akiwa anakanyaga  pesa huku akicheza wimbo wake wa ‘Iokote’.

Vanessa ameibuka n kumtaka Maua kuwa mjasiri na kumtaka kuwa mvumilivu kwani siku si nyingi atatoka na akisha toka watacheka na kusahau yote yaliyotokea.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Vanessa Mdee kamuandikia ujumbe huu:

https://www.instagram.com/p/Bn8Tpg3CHhO/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=rtlm6iay8rzk

Wolper Awaombea Msamaha Soudy Brown na Maua Sama Wanaosota Rumande

Msanii wa filamu za Bongo Movie na mjasiriamali Mrembo Jacqueline Wolper ameibuka na kuwaombea msamaha mtangazaji wa Clouds Fm Soudy Brown na msanii wa Bongo fleva Maua Sama.

Maua na Soudy wamewekwa ndani tangu siku ya Jumapili mpaka leo hawajapata dhamana baada ya kuonekana kwenye video clips wakiwa wanakanyaga pesa.

Wolper amejikuta akiguswa na kitendo hicho cha kuwekwa ndani ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram, amesema anaomba viongozi wakubwa wa nchi wawaachie wasanii hao kwani walikuwa kwenye utafutaji na badala yake adhabu waliyoipata kwa siku hizi tatu liwe funzo kwa wengine.

 

Katika utafutaji Kuna mitihani Mingi Sana. Nachoweza kusema Nikuomba Tuu wakubwa muwasamehe vijana wenzetu Naamini katika Hili lililotokea Basi wengine wengi watajifunza kitu kupitia hili Naomba niwaombee masamaha wa Dhati kabisa Ndugu zetu Na wawe huru kuendelea Na majukumu yao inshallah. Maua & Soudy na wengine wore mliopo Ndani Juu ya hili sio sawa kutaja wote lakini hawa niwawakilishi poleni saanaa Jamani Ndani sio kuzuri“.

Mpaka sasa inadaiwa wawili hao bado wapo ndani bila dhamana.

Idris Sultan Amuombea Msamaha Maua Sama

Msanii wa Bongo movie na Comedian maarufu Idris Sultan ameibuka na kumuombea msamaha Msanii wa Bongo fleva Maua Sama baada ya kuwekwa rumande kwa siku tatu.

Siku chache zilizopita Maua Sama na mtangazaji wa Clouds FM, Soudy Brown walitiwa nguvuni na jeshi la polisi baada ya video iliyowaonyesha wakiwa wanakanyaga pesa kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii.

Baada ya kusambaa kwa video hiyo toka jumapili mpaka leo Soudy Brown na Maua bado hawajapata dhamana.

Idris Sultan ameibuka na kumuombea radhi Maua Sama na kuomba aachwe huru na Awe mfano wa kuigwa na jamii:

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Idris Sultan ameandika:

https://www.instagram.com/p/Bn6REJDhCPF/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1j9q2eztrp313