Ndoa ya Mc Pilipili Kufanyikia Uwanja wa Taifa

Ndoa ya moja ya wachekeshaji maarufu nchii Mc pilipili yategemewa kufanyka uwanja wa taifa kama inavyoripotiwa na yeye mwenyewe alipokuwa akiongea na waandishi wa habari.

Akiongea na waandishi, Mc plipili anasema kuwa ndoa hiyo ambayo iko karibu inawagahrimu sana kufikiria sehemu nzuri na kubwa ya kufanyia ukizingatia kuwa wanategemea kuwa na watu wengi hivyo kutafuta ukumbi mkubwa kwa ajili  yake.

Mc pilipili anasema kuwa mpaka sasa wamekuwa wakizunguka kwa ajili ya kutafuta ukumbi wa kufanyia harusi hiyo lakini bado hawajapata lakini kati ya sehemu wanazopendekeza ni uwanja wa taifa.

Anasema “mimi na kamati bado tunaangalia sherehe tuifanyie wapi, nimejaribu kuuliza kati ya uwanja wa taifa, uwanja wa Uhuru  na leaders , lakini pia tunaangalia na mlimani city.

 

MC Pilipili Ajibu tuhuma za kuiba mwanamke kwa kutumia pesa

Mchekeshaji maarufu bongo, Emmanuel Mathias ‘MC Pilipili’ ambaye hivi karibuni amemvisha pete ya uchumba, mchumba wake, amefunguka juu ya tuhuma zinazodaiwa kuwa ametumia pesa kumpata mwanamke huyo kutoka kwa mwanaume wake wa zamani.

Akiwa kwenye Mahojiano alichukua nafasi kujibu tuhuma hizo kwa kusema kuwa “Aisee nampa pole, Tanzania inaonesha wanawake ni wengi kuliko wanaume, kwa hiyo sio rahisi kwa yeye kutembea na mwanaume mwingine, lakini ni rahisi kupata mwanamke, atapata mwanamke mwingine, kwani wanawake ni wengi Tanzania na duniani”

Itakumbukwa hivi karibuni Mc pilipili alimvisha pete mchumba wake huyo na kuangusha kilio mbele za waliokusanyika kushuhudia tukio hilo huku baadhi ya watu kwenye mitandao wakitafsiri tukio hilo kama ni udhaifu kwa mtoto wa kiume kulia.
TOA MAONI YAKO HAPA

Mc pilipili Amewadhalilisha Wanaume Wote :-Mwijaku

msanii wa maigizo maarufu kama mwijaku amefunguka na kumtupia lawama msanii mwenzake upande wa vichekesho mc pilipili kwa kitendo alichokifanya wikiend hii na kumuita kuwa ni zuzu.

Mc pilipili ambae aliweza kumvalisha pete mchumba wake phinomena wikiendi iliyopita na kuzua gumzo sana kutoka katika mitandao ya kijamii kwa sababu alimwaga machozi kipindi akimvalisha pete mwanamke huyo kitu ambacho hakikuwa cha kawaida katika matendo hayo.

Mwijaku anasema kuwa alichokifanya MC pilipili ni kuwa zuzu kwa sababu huwezi kulia mbele za watu kwa sababu ya mwanamke na kwmaba amewadhalilisha wanaume wote wa dar kutokana na kitendo icho.

Mwijaku anasema kuwa kulia sio dhambi lakini dhambi ni pale unapolia mbele ya watu lkwa sababu ya mwanamke.

Sio dhambi kulia, dhambi ni kulia mbele za watu kwa sababu ya mwanamke .

Hata hivyo Mwijaku anasema kuwa amekuwa akimfahamu sana Mc pilipili naamekuwa akimueleza mengi kuhusu yake anayoyapitia katika mahusiano yake.

 

“Nililia Machozi Ya Furaha Baada Ya Kupitia Misukosuko Mapenzini”-Mc Pilipili

Mchekeshaji maarufu Bongo Emmanuel Mathias ‘Mc Pilipili amefunguka na kuweka wazi kuwa furaha ndio iliyompelekea kuangua kilio siku chache zilizopita.

Mwanzoni mwa Wiki hii Mc Pilipili alizua gumzo baada ya kuangua kilio wakati wa kumvisha pete Mpenzi Wake Philomena Thadei huku akiwa amepiga goti.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Mchanganyiko, Mc Pilipili alieleza kuwa alilia kutokana na changamoto alizokuwa amezipitia kwenye masuala ya uhusiano wa kimapenzi na msichana huyo.

Alisema hadi kufikia hatua hiyo ya kumvisha pete na binti huyo kukubali, halikuwa jambo rahisi bali alikumbana na ugumu hivyo alipoyakumbuka hayo, alijikuta machozi yakimtoka.

Nimepata misukosuko mingi sana kwenye uhusiano ndiyo maana hadi machozi yamenitoka kwa furaha kwa kuwa nimefikia hatua nzuri, natarajia kuanza vikao vya maandalizi ya harusi hivi karibuni na vitakuwa vya muda mchache kwa kuwa ninataka kufanya haraka iwezekanavyo”.

Lakini pia Mc Pilipili amesema harusi yao inategemewa kufanyika mwaka huu hapo baadaye na wanategemea kualika wageni kama 2,000.

Mc Pilipili Atoa Onyo Kali Kwa Wanaommendea Mchumba Wake

Mchekeshaji MC Pilipili amefunguka na kuwamwagia Povu zito wanaume wote ambao watakuwa wanamnyemelea Mpenzi Wake Philomena Thadey ‘Mina’.

Siku chache zilizopita Mc Pilipili alitengeneza headlines Baada ya kuangua kilio wakati anamvalisha pete Mpenzi Wake ambapo alisema ilikuwa ni Furaha.

Lakini siku chache Baada ya tukio hilo Mc Pilipili amewatolea Povu wanaume wakware wote ambao wameanza kumtolea macho mpenzi wake Baada ya kuona amemgharamikia ikiwemo kutoa mahari  ya milioni 8.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mc pilipili ameweka video hii ambayo amewatahadharisha ambao walikuwa wanammendea mchumba Wake:

https://www.instagram.com/p/BsV-GpOgF2f/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1xmhvk6r5v53q

Mc Pilipili Amtaka Ben Pol Amuoe Mpenzi Wake Mpya

Mshehereshaji maarufu Emmanuel Mathias maarufu kama Mc Pilipili ameibuka na kumpa ushauri staa wa Bongo fleva Ben Pol wa kumtaka amuoe Mpenzi Wake Mpya.

Wiki chache zilizopita Ben Pol alianika mapenzi yake hadharani na binti wa Kikenya anayeitwa Anerlisa Mugai ambaye anatajwa kuwa mtoto wa kigogo na pia binti anayeogelea kwenye pesa.

 

Mc Pilipili ameibuka na kutia neno kwenye mahusiano ya Ben Pol na Anerlisa ambapo  amesema watu wa kabila lake siku zote huwa wanapenda kweli kweli, hivyo akamtaka Ben Pol kuchukua maamuzi ya kuoa.

Wagogo tukipenda hua tunapotelea kabisa Ben Pol nakuelewa kaka yangu huu mwaka wetu kama tulivyoongea kaka”.

Mc Pilipili amekuwa kwenye headlines kwa siku mbili hizi Baada ya video yake alipokuwa anamvisha pete Mpenzi Wake na kuangua kilio  kusambaa kwenye Mitandao ya kijamii.

Hatugusani Mpaka Ndoa :-Mc pilipili

Wikiedn iliyopita , mchekeshaji mc pilipili amemvisha pete ya uchumba , mchumba wake wa siku nyingi tayari kwa ajili ya ndoa , lakini kutokana na sherai na taratibu za dini, mchekeshaji huyo anasema kuwa hawako tayari kufanya mapenzi maka pale watakapofunga ndoa .

Mc pilipili aliweka wazi kuwa alitoa mahali ya binti huyo kiasi cha shilingi milioni 8,  na wala haoni shida kusubiri mpaka atakapofunga ndoa na binti huyo ambae ni chaguo lake.

ni kweli nimeokoka na ndioa maana kwenye sherehe ya mahaki hakukuwa na vinywaji vikali, hatyuishi pamoja na mpenzi wangu ila anaweza kuja nyumbani kupika, hatutagusana na mpenzi wangu mpaka tutakapofunga ndoa.

Mc ilipili anasema kuwa waliweza kukubaliana na mshenga kiasi cha shilingi milioni 8 lakini waliweza kuongea na kulipa milion 5 , mpaka sasa anadaiwa milioni 3.

Mc Pilipili Amwaga Machozi Baada ya Kumvisha Pete Ya Uchumba Mpenzi Wake

Mshereheshaji Emmanuel Mathias ‘MC Pilipili’ amemvalisha pete ya mpenzi wake (Mke mtarajiwa) Philomena Thadey, nyumbani kwa wazazi wa mwanamke maeneo ya Boko, Tegeta jijini DSM, sherehe hiyo imehudhuriwa na watu mbalimbali wa Serikali na taasisi zisizo za kiserikali.

Kwenye tafrija hiyo iliyotrend kwenye Mitandao ya kijamii Mc Pilipili alionekana kuangua kilio cha Mtoto mdogo Baada ya kumchumbia Mpenzi Wake huyo wa siku nyingi.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amefunguka baada ya MC Pilipili kumvalisha pete mpenzi wake huyo ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika:

https://www.instagram.com/p/BsQunD_FtZg/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=u3aqic6vlfu7

Mc Pilipili Amshauri Ben Pol Kumuoa Anerlia

Msanii wa maigizo ya vichekesho nchini  mc pilipili matoa ushauri wa bure kwa msanii mwenzake ben pol ambae pia ni kabila moja na yeye kwa kusema kuwa kwa jinsi anavyowajua watu wa kabila lao  huwa wanapendwa kweli kweli hivyo afanye hima aweze kuishi na mwanamke alieyenae kwa sasa katika mahusiano.

Mc pilipili anasema hayo baada ya kuona kuwa kuna penzi zito na jpya linaloshamiri kati ya ben pol na mwanadada mmoja kutoka kenya, hivyo amemshauri ben kuamua kufanya uamuzi wa kuoa mapema kabla mambo hayjaharibika kabisa.

Wagogo tukipenda huwa tunapotea kabisa, Ben pol ninakuelewa kabisa kaka yangu , huu mwaka wetu kama tulivyoongea kaka.

Kama alivyotangaza Mc pilipili kuwa mwaka huu ataoa basi ndio anamwambia na Ben pol kuwa wafanye wakamilishe lengo mwaka huu.

Mbasha Azidi Kumchokonoa Mc Pilipili

Msanii wa nyimbo za Injili nchini Emmanuel Mbasha ameibuka na kumtupia madongo Mshehereshaji maarufu Emmanuel Mathias ‘Mc Pilipili’ baada ya kupiga picha akiwa na mpenzi wake.

Siku chache zilizopita Mc Pilipili aliposti picha Mtandaoni akiwa na mpenzi wake anajulikana kama Qute Mena lakini mara moja Mbasha alimtolea povu Mc Pilipili na kudai kwa kufanya hivyo amekiuka taratibu za kidini.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Mbasha alisema lengo la kumuandikia ujumbe mrefu MC Pilipili kwenye ukurasa wake wa Instagram, lilikuwa ni kumjenga pamoja na kumuelimisha kwamba kitendo anachokifanya sio sahihi.

Unajua sio vizuri kumuanika wazi wazi mchumba wala kuwa naye karibu kiasi ambacho hata watu wakiwaona watashangaa, kwa sababu tunafundishwa kwamba, ukishamchumbia mtoto wa kike hutakiwi kufanya naye kitu chochote mpaka pale utakapo muoa na kumfanya mke wako.

Sasa Napata wasiwasi kwa huyu ndugu yangu MC Pilipili na huyo mchumba wake, nimepata taarifa kwamba wapo Zanzibar sasa sijajua kama wamechukua vyumba tofauti au wanaishi kwenye chumba kimoja, kitendo ambacho si kizuri, ila lengo la kumuandikia ule ujumbe kwenye akaunti yangu ni kumuelisha kwa sababu yeye ni kioo cha jamii na watu wanahitaji kujifunza kutoka kwake”.

 

 

MC Pilipili Amuanika Mpenzi Wake na Kutangaza Naye Ndoa

Mchekeshaji na Mshehereshaji maarufu wa sherehe nchini Emmanuel Mathias ‘Mc Pilipili’ amemuanika mpenzi wake mpya na kutangaza rasmi kuwa anataka kufunga naye ndoa.

MC Pilipili alitangaza ndoa yake Kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo aliweka video na picha mbali mbali za baadhi ya watu watakao husika katika maandalizi ya Harusi hiyo.

https://www.instagram.com/p/BmDfez8DDlB/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=qokxdefv96ez

Kufanya Comedy Ukiwaiga Wanawake ni Style ya Zamani:-Mc Pilipili

Mcheshaji maarufu nchini Mc pilipili ameponda style wa wachekeshaji wenzake kuwa wakiiga  sauti za kike na kuwa wakiigiza na kuvaa uhusika wa kike wakati wao ni wanaume,Mc pilipili anasema kuwa style hiyo ni ya kizamnai sana lakini kwa sasa wakifanya hivyo wanakuwa wanaharibu biashara yao ya sanaa ya uchekeshaji.

Mc Pilipili  nasema kuwa katika sanaa hii ya uchekeshahi zamani waliokuwa wakifuatiliawalikuwa ni kama wajinga na ndio maana walikuwa wakipenda kile walichokuwa wakiigiza  lakii sasa hivi audience inataka uhalisia na sio kuigiza igiza tu.

Hiyo ni style ya zamani hiyo tena zamani kabisa,kwa upande wengi sijaikubali kabisa na hao wengi ni wale wacheshi wa mitandaoni,lakini mimi ni professional na hii ni kazi yangu na audience wa sasa hivi sio wajinga kama wale wa zamani, na kama unakuwa mwanaume alafu unaigiza ki kike wakati wewe ni mwanaume kuna kuwa hakuna reality unakuwa unawachanganya tu watu.

Mc Pilipili Afunguka Kuhusu Aliyefungua Shampeni kwa Mdomo.

Mchekeshaji na mshereheshaji maarufu nchini, Mc pilipili amefunguka na kuongelea kwa undani kuhsu video iliyokuwa inesambaa sana katika mitandao ikimuonyesha bibi mmoja akiwa anafungua shampeni kwa mdomo ikiwa katika sherehe hiyo akiwa ni mshereheshaji .

Mc Pilipili anakiri kuwa mtu huyo alikuwa ni ndugu wa bibi harusi lakini anaonekana alikuwa aamekwisha pendeza huku waliomuandaa kwa ajili ya shughuli hiyo wakiwa hawajamuandaa kwa hilo.

sio kwamba kule bagamoyo watu hawajui kufungua shampeni kwa sababu muda wa kufungua ulipofika nilitakiwa kuwaita watu walioandaliwa sasa sijui kama yule alikuwa tayari ameandaliwa sijui, lakini ukiandaliwa ni kwamba unakuwa umeikamia sherehe,yule mama alikuwa tayari ameshapendea na hata alipokuja pale wengine walikuwa tayari wameshafungua na nikagundua kuwa ni yeye pee yake ndio bado hajafunfua shanpeni na tkiwa tunakuwa uwa tunaambiwa fungua soda kwa mdomo kwaio nahisi na yeye aliamua kujichanganya pale akijua ni kazi rahisi.

Mc pilipili anasema kuwa bibi yule alikariri kuwa kinywahi chochote cha kwenye chupa basi kinafunguliwa na mdomo, na kwa upande wake huwa anaongea kama utani kuwa ukiweza fungulia hata mdomo na ndipo alipoona isiwe tabu.

 

Mc Pilipili Augulia Maumivu Baada ya Aliyekuwa Mpenzi wake Kufunga Ndoa

Mchekeshaji Emmanuel Mathias maarufu kama Mc Pilipili amefumguka na kuongele maumivu aliyoyapata bada ya mwanake aliywahi kuwa nae kufunga ndoa na mwanamke miwngine huku yeye akiwekwa kama mc wa shughuli hiyo.

Ingawa bado haijafahamika kama ni kiki au vipi lakini kupuia ukurasa wake wa instagram, Mc Pilipili aliweka picha ikimuonyesha Nicole Franklyn akiwa na Mc Pilipili na kuandika maneno yenye kuonyesha maumivu sana  kwa kitendo alichoamua kukifanya.

Nicole huyu ni wewe ukinivua koti nilipokuwa nimetoka kuchekesha, ukiwaumevaa jezi yangu ya SIMA MABINGWA kweli umeamua kuolewa na huyu MWIJAKU  ambae hanigusi kwa lolote  wigi lako bado liko nyumbani ilo ulilovaa hapo na kanga yako pia  , USIACHE MBACHAO KWA MSAALA UPITAO.

 

 

 

Mc Pilipili Ashinda Tuzo Nchini Nigeria

Mchekeshaji maarufu nchini  ameshinda tuzo ya Scream Award zilizokuwa zikitolewa nchini Nigeria.Mchekeshaji huyo wa siku nyingi amepata tuzo hiyo ambapo alikuwa akishindana na wachekeshaji wengine wengi wanaotokea nchini Nigeria na nchini Ghana huku mtanzania akiwa peke yake.

Mc Pilipili ameshinda tuzo hiyo katika kipengele cha Youth  Comedian Of the year ,akiwa ni mmoja kati ya washiriki 12 kutoka afrika.

Hii ni dalili nzuri kwa tasnia ya sanaa tena hasa upande wa maigizo ya vichekesho ambayo kwa hapo mwanzo yalikuwa hayapewi tija sana kama sanaa nyingine zinavyoangaliwa kwa upana wake.

Hii pia inatoa fursa na kufungua njia kwa wasanii wengine wa vichekesho kuendelea kukaza buti na kujuliakna nje ya nchini ili kuendelea kukuza tasnia hiyo amabyo imekuwa ikidharaulika sana tofauti  sanaa nyingine zote.

Mc Pilipili Atamani Kuoa Baada Ya Kuona Joti Kaoa

Msanii wa maigizo ya uchekeshaji  Mc Pilipili amefunguka na kusema kuwa hata yeye ametamani sana kuoa baada ya kumuona msanii mwenzie wa maigizo ya vichekesho  Joti kuwa ameoa lakini kuna baadhi ya mambo yanayomtilia vikwazo katika ndoa yake .

Msanii Joti ambae amekuwa ni mmoja wa wasanii wa maigizo ya vichekesho alifanikiwa sana katika kazi yake na kwa sasa amekuwa ni moja ya mabaolozi wakubwa wa makampuni mbalimbali nchini ameoa weekend iliyopita ya tarehe 28 Oktoba na harusi kufanyikia Mlimani City jijini Dar Es Salam.

Nilipenda sana kuoa mwaka huu  tena hasa mwezi huu wa kumi  ila imeshindikana kwa sababu mpaka mwezi wa kumi umefika bado sijapata mchumba wa kumuoa, lakini  mpaka mwezi wa kumi mwakani ninaamii kitu kikubwa sana kitatokea” alisema Mc Pilipili.

Hata hivyo Mc Pilipili anawapa tahadhari wadada wa mjini mabao wamekuwa wakiona dharau sana kuwa na uhusiano wa kimapenzi wa wasanii wa maigizo ya vichekesho na kusema kuwa hata wao pia ni watu, kauli hii inajirudia tena kwa baadhi ya wasanii wa vichekesho .

Moja wa wasanii wa vichekesho anaejulikana kama Mkali Wenu alishawahi kutoa lawama hiyo na kusema kuwa wdada wengi wamekuwa hawachukulii umakini pale wanapofatwa na wasanii wa maigizo ya vichekesho kwa ajili ya mahusiano, inakuwa kama wanawatania kumbe wao wanakuwa serious na maneno yao.

Mc Pilipili ambaye anasema mpaka sasa hajapata mchumba alishawahi kuwa katika mahusiana ya kimapenzi na wasichana maarufu Tanzania kama Nandy ambae ni msanii na anafanya vizuri katika game na pia alishawahi kutoka na Nicole Franklin amabye alishawahi kutwaa taji la Miss Shinyanag 2014.