Miriam Odemba Kuwa Mstari Wa Mbele Kusheherekea Siku Ya Wanawake Duniani

Mwanamitindo mkongwe ambaye anafanya kazi zake nchini Ufaransa Miriam Odemba amefunguka na kuweza wazi mipango yake ya kurudi Tanzania kwa ajili ya kusheherekea siku ya wanawake duniani.

Miriam Odemba anatarajia kuwa mmoja wa wanawake watakaohudhuria katika Onesho la Tanzanite Women Forum and Lunch linalotarajiwa kufanyika Machi 9, mwaka huu ambayo ni siku ya wanawake duniani litakalofanyika katika Hoteli ya Double Tree jijini Dar.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la ijumaa, Odemba alisema kuwa anafurahia sana kuwa mmoja wa wanawake waliopata mualiko maalum katika shughuli hiyo na kusema kuwa itakuwa ni kitu kizuri mno kwa wanawake kukutana na kujadili mambo mbalimbali pia kuangalia vitu vizuri vinavyofanywa na wanawake wenzao.

Hakuna kitu ninakipenda kama kurudi nyumbani na kukutana na wanawake wenzangu mbalimbali na kujadiliana vitu vizuri hivyo ni vyema watu wangenunua tiketi zao mapema ambazo zinapatikana sehemu mbalimbali kama Zurii House of Beuaty na Malika Designer”.

 

Miriam Odemba- Nimekumbuka Sana Nyumbani

Mlimbwende mkongwe Bongo Miriam Odemba ambaye kwa miaka mingi amekuwa akiishi nchini Ufaransa amefunguka na kukiri kuwa amekumbuka sana nyumbani.

Miriam Odemba ametoa la moyoni kuwa akili yake kwa sasa amekuwa akiwaza nyumbani Tanzania hivyo kukosa raha.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Miriam Odemba alisema kuwa hata mtu akae nchi za watu kwa miaka mingi, lakini bado picha ya nyumbani haifutiki akilini.

Siyo kwamba hakuna maisha mazuri au sipati ninachotaka, lakini siku zote nyumbani kuna ladha yake. Nimekumbuka sana nyumbani na kungekuwa karibu kwa kweli kila wakati wangeniona”.

Pamoja na kuishi mbali na Tanzania, Lakini Miriam Odemba ameanzisha taasisi yake ya kujitegemea inayoitwa ‘Run with Odemba’.

Miriam Odemba Akiri Kutamani Kuzaa na Diamond

Mwanamitindo na mlimbwende Miriam Odemba anefunguka na kuanika mapenzi yake kwa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz na kukiri kuwa anatamani kumzalia Mtoto wa nne.

Ijumaa Wikienda linaripoti kuwa Miriam Odemba alifunguka hayo kwenye mahojiano waliyofanya naye kwa njia ya simu kutokea nchini Ufaransa anapoishi sasa.

Kwenye mahojiano hayo Miriam alijikuta akimfungukia Diamond kwa kusema amekuwa akiangalia mwenendo wake na kumuona ni ‘baba bora’ hivyo si vibaya akimzalia mtoto mmoja.

Odemba alisema anafuatilia watoto wa Diamond, wale wawili aliozaa na mwanamama mjasiriamali wa Kiganda, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ na yule wa mwanamitindo Hamisa Mobeto na kugundua anawalea vizuri, kitu ambacho kinamshawishi na yeye awe tayari ‘kumtunuku’.

Diamond nampendaga pia anavyojua kuangalia watoto wake mpaka kuna wakati natamani mimi ningezaa naye mtoto mmoja pia ni  kijana mdogo, lakini anaweza kujali familia yake na watoto wake japokuwa hayupo vizuri na mama wa watoto hao (Zari na Mobeto), hapo ndipo anaponikosha sana”.

Alipoambiwa afafanue kwa njia gani anaona Diamond anawajali watoto wake, Diamond alifunguka:

Unajua mara nyingi naweza kumuona anatoka Tanzania na kwenda Sauz (Afrika Kusini), kwa ajili ya kuona watoto wake japokuwa hayuko tena kwenye mapenzi na mzazi mwenzake”.

 

Miriam Odemba Amtolea Povu Zito Diamond Platnumz

Mlimbwende mkongwe Tanzania Miriam Odemba amemjia juu staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz baada ya kudai amemfhalilisha mama mtoto wake Hamisa Mobetto.

Miriam Odemba ameibuka na kumpa vipande vyake kuwa, hakustahili kumsema vibaya mzazi mwenzake, Hamisa Mobeto kwa kumrushia tuhuma nzito ambazo zimemfanya

Kwenye mahojiano na Risasi Jumamosi akiwa nchini Ufaransa, Odemba alisema kuwa hakuna kitu kibaya kama kumtolea maneno ya kashfa mzazi mwenzio na hata kama kuna sehemu aliteleza, busara inatakiwa kutumika:

Yaani mimi sijapendezwa kabisa na alivyofanya Diamond, kwa maana anapaswa kuheshimu hata kile kiumbe kilichowaunganisha. Kama kuna matatizo ya kifamilia ni vyema kukaa chini na kumalizana, lakini siyo kuyaweka kwenye kadamnasi kama alivyofanya Diamond. Kuna siku watakutana kama wazazi, hivi atajisikiaje? Amekosea sana”.

 

Odemba Akubali Kuporwa Mume

Mwanadada ambae amekuwa katika mitindo kwa muda mrefu Miriam Odemba anekiri kuachana na mume wake kwa muda sasa baada ya bwana huyo kushindwa kukaa nae kutokana na u-bize wa kazi anazofanya za uana mitindo , hivyo kujikuta akishawishika kujiingiza katika mahusiano na mwanamke mwingine aliyekuwa akimpatia muda mwingi.

Habari za hapo awali za chii chini zilikuwa zikisema kuwa mwanadada huyo kwa sasa amekuwa akiishi peke yake na kulea mtoto mwenyewe huko mume wake akimwachia majukumu hayo.

Habari kutoka kwa watu wa karibu wa Odemba walipotoa taarfa hizo,GPL waliamua kumtafuta miriam mwenyewe na kukiri kuwa kwa sasa nyumbani kwake anakaa pekee yake na mtoto.

Anasema ” okay ngoja niweke wazi kwa sababu naona mmeshapata habari, unajua mimi mara nyingi nimekuwa mtu wa kusafiri safiri kutokana na kazi zangu, kwaio baada ya kusafiri mwenzangu akapata vishawishi na kwa sababu mwenzangu ana jina kubwa sana huku kwaio nikaona bora mimi nikae pembeni tu. ‘Hata msichana mwenyewe pia ninamjua naomba ifahamike kuwa mimi na yeye ni mtu na mzazi mwenzie tu na hatukuwahi  kufunga ndoa.