Monalisa na Mwanaye Washangaza Umati Kwa Hili

Msanii mkongwe wa Bongo movie Yvonne Cherry maarufu kama Monalisa na Mtoto Wake Sonia walishangaza watu Baada ya kuonekana wakiangua kilio mbele ya hadhara.

Monalisa na Mwanaye walishikwa na huzuni na kuanza kulia walipokuwa wakikabidhi misaada kwenye kituo cha kulea watoto yatima cha Yoko kilichopo Mbezi- Mwisho jijini Dar.

Aliyeanza kulia ni mtoto wa staa huyo, Sonia baada ya kupewa kipaza sauti azungumze ambapo alishindwa, akaanza kulia huku mama yake akimkumbatia, wakajikuta wakilia pamoja na baadae Watoto wa kituo kile nao walionekana wakilia.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, rafiki wa karibu wa Sonia ambaye alikuwa ameongozana nao alitoa sababu iliyomfanya mpaka akaanza kulia:

Masikini Sonia, anaonekana ana huru­ma na machozi yanamtoka kwa sababu na yeye anakumbuka amempoteza baba yake pia”.

Monalisa alifunguka na kusema kuwa ameamua kujitoa kusaidia wazo hilo la mtoto wake kwa sababu ameona anafanya jambo jema.

Monalisa: Sina Bifu na Kajala

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Yvonne Cherry maarufu kama Monalisa ameibuka na kuweka wazi kuwa hana Bifu na msanii mwenzake Kajala Masanja bali watu wanataka tu kuwagombanisha.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi, Monalisa alisema watu wamekuwa wakizungumza maneno mengi ambayo yanaweza kusababisha wagombane wakati wao wako vizuri, hawana tofauti yoyote kama watu wanavyosema.

Sina bifu na Kajala ila naona watu ndiyo wanataka kutugombanisha, naomba watu waache maneno jamani ili maisha mengine yaendelee maana kila siku ni hilohilo tu“.

Monalisa amesema Baada ya sakata la matokeo ya kidato cha nne yaliyotoka Wiki chache zilizopita amvbapo Watoto wa wasanii hao walikuwa wanasoma shule moja Lakini Baada ya Mtoto wa Kajala Kufeli na Mtoto wa Monalisa kufaulu kuna maneno ya uchochezi yalizungumzwa kupelekea kuonekana kama wana bifu.

Monalisa Kuja na Tamasha Kwa Ajili Ya Wanawake

Msanii mkongwe wa Bongo movie Yvonne Cherry maarufu kama Monalisa ametangaza Fursa kwa ajili ya wanawake ambao ni wasanii pia kwa ajili ya kuuza kazi zao.

Monalisa amezungumza na waandishi wa habari na kutazangaza good news aliyowaletea wanawake wakitanzania wanao jihusisha na sanaa haswa wale watayarishaji wa filamu wakike ambao watapata nafasi ya kuonesha kazi zao kwenye tamasha la AWAFEST  litakalo fanyika siku tatu hapa hapa bongo.

https://www.instagram.com/p/Btyyl15BkAu/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=3v9i2d28xd6o

Monalisa Amefungukia Video Ya Kajala na Mwanaye

Msanii mkongwe wa Filamu za Bongo movie Yvonne Cherry maarufu kama Monalisa amefunguka na kupima uzito video ya Kajala na Mtoto Wake Paula.

Siku chache zilizopita and Kajala na binti yake wa miaka 16 Paula walitengeneza headlines Baada ya video yao iliyowaonyesha wakikata mauno kusambaa kwenye Mitandao ya kijamii.

Monalisa ambaye ana ukaribu na Kajala Lakini pia Watoto wao wamesoma wote amefungukia Sakata hilo na kusema kuwa haoni tatizo mama kucheza na Mtoto wake.

Kwenye mahojiano aliyofanya mtandao wa Millard Ayo, Monalisa amedai kuwa pamoja na kwamba hajaiona video hiyo Lakini pia hajaona tatizo Kama ni mama tu anacheza na Mtoto Wake.

Monalisa Athibitisha Kuwa Balozi Wa Duka La Nguo

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Ivyonne Cherry maarufu kama Monalisa amefunguka na kukiri kuwa yeye ni balozi wa duka kubwa la nguo na hivyo huwa anauza pia.

Gazeti la Ijumaa linaripoti kuwa limemkuta msanii Monalisa akiwa maeneo ya Magomeni Usalama  jijini Dar es Salaam akiwa ndani ya duka Bannat World akiwahudumia wateja kama kawaida.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Monalisa alisema kuwa yupo dukani hapo kwaajili yeye ni balozi wa duka hilo na mara nyingi mwisho wa mwezi wanafanya punguzo la bei hivyo nakuwepo dukani hapo kwaajili ya kuwahudumia wateja wanaokuja hapo.

Niko hapo nawahudumia wateja kama balozi wa Bannat World na mara mwisho wa mwezi nakuwepo hapa nawahudumia wateja” .

Monalisa Akiri Kumkumbuka Tyson Baada Ya Matokeo Ya Mtoto Wake

Msanii mkongwe wa Bongo movie Ivyonne Cherry maarufu kama Monalisa amefunguka na kukiri Kumkumbuka baba wa mtoto wake Marehemu George Otieno ‘Tyson’ katika kipindi hiki.

Monalisa amekiri kuwa baada ya mwanaye Sonia George Tyson kufaulu kidato cha nne na kupata daraja la kwanza huku somo la Hesabu akiwa amepata A, ame­jikuta akibubujikwa machozi ya fu­raha na kutamani uwepo wa baba wa Sonia, George Tyson aliyetan­gulia mbele ya haki.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wik­ienda, Monalisa alisema kuwa alipopata taarifa hizo alishindwa hata kulala lakini kingine kilichowa­tia huzuni ndani ya furaha hiyo ni baa­da ya kukumbuka kwamba baba yake huyo alikuwa akipenda sana mtoto wake huyo asome sana ili aweze kufika elimu ya juu.

Siwezi kusema furaha ambayo ninayo kwa mtoto wangu huyo lakini Tyson angekuwepo ange­shuhudia ukuu wa Mungu, kwa sababu alipenda sana Sonia asome tena aongoze kitaifa, ndio kitu alichokuwa akikipenda lakini tunashukuru Mungu kwa kuibuka na daraja la kwanza kwani ni wengi waliotamani lakini wameshindwa kupata, yeye amewe­za”.

 

Monalisa Aomba Msamaha kwa Ajili ya Mwanae

Mwanadada monalisa amefunguka mbele ya waandishi wa habari na kuwaomba msamha watanzania wote kwa ajili ya mtoto wake wa kike sonia amabe alihojiwa na vyombo vya habari kutokana na ufaulu wake huku akimuongelea mtoto wa kajala ambae pia alikuwa akisoma ane shule moja lakini inavyosemekana ni kuwa hakufaulu vizuri kama mwenzake.

Mtoto huyo alisema kuwa wamekuwa wakisoma wote na muda mwingi amekuwakuwa akitumia kumfundisha lakini kitu kikubwa kajala alikuwa akiongea kukipenda ni fashion na mitindo hivyo anaminikuwa akili yake ipo katika kufanya hivyo.

Hata hivyo watu katika mitandao walimshambulia sana mtoto wa Kajala na kumuita hana akili bila kujua kuwa kufaulu au kufeli kunatokana na sababu tofauti tofauti.

Hata hivyo, monalisa alichukua nafasi hiyo kuomba jamii msamaha kwa kile alichokisema mtoto wake kwakuwa akimetasfiriwa vibaya na watu hata kufikia hatua ya kuwalinganisha jambo ambalo sio sawa.

Monalisa anasema ‘jamani naomba radhi kama kauli yangu kwa mtoto wa kajala  paula imetasfiriwa vibaya , hakukuwa na nia mbaya na hata wakati anazungumza nilikuwepo na wala sikuona ubaya.”

Mtoto Wa Monalisa Apiga Division 1 Matokeo Ya Form Four

Mtoto wa muigizaji mkongwe wa Bongo movie Ivyonne Cherry ‘Monalisa’ na mtayarishaji wa filamu Marehemu George Otieno, Sonia Otieno amepata division katika matokeo yake ya form four.

Siku ya jana Baada ya matokeo kutoka Monalisa alishea kwenye Mitandao ya kijamii kuwa mwanaye ambaye alimaliza kidato cha nne mwaka jana amepata division 1 na hata kupata A ya hesabu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Monalisa aliweka wazi Furaha ya binti yake kufaulu na kuandika maneno haya:

https://www.instagram.com/p/BtBI2JxF34B/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=179h5h8ajn4ag

Monalisa Kuipeperusha Vizuri Bendera ya Tanzania.

Kazi zake zimekuwa za kimya kimya sana lakini amekuwa akonekana na watu mbalimbali kwa yale anayoyafanya ambayo yanaleta mtazamo chanya kwa jamii inayomzunguka.

mwanadada monalisa kutoka Tanzania kiwanda cha filamu, ameshinda tena tuzo nyingine nchini Uganda baada ya kuibuka kidedea baada ya kupewa tuzo ya Woman of  Africa Icon substance  baada ya kkabidhiwa medali iyo na miss uganda nchini humo.

Monalisa anakuwa moja ya wasichana wachache sana katika kiwanda cha sanaa kupeperusha bendera ya tanzania vizuri hasa kwa mwaka huu baada ya kuonekana na kuiwakilisha vyema nchini katika matkio mbalimbali makubwa ya nje na ndani ya Tanzania na Afrika pia.

Monlisa akikabidhiwa medali izo na miss Uganda.

Monalisa Awatolea Povu Wanaomuita ‘Bibi’

Muigizaji mkongwe wa filamu za Bongo movie Ivyonne Cherry maarufu kama Mobalisa amewatolea Povu zito watu ambao walimuita bibi Baada ya kuonekana kwenye video ya msanii Ben Pol.

Mwezi uliopita Staa wa Bongo fleva Ben Pol aliachia video yake ya wimbo wake wa Ntala Nawe na ndani yake alimuweka Monalisa Kama Video Queen Wake uwamuzi uliozua hisia mbalimbali kutoka kwa mashabiki.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Enews cha EATV, Monalisa amefunguka na kusema hakushangaa comments za mashabiki wa Ben Pol waliomuhoji kwanini hakuchukua Wasichana wadogo wa kuendana naye.

Kila mtu ana mtazamo Wake na kwangu Mimi hicho ni kitu cha kawaida  watu lazima tu wataongea midomo wameumbiwa ili kuongea ila poleni sana na itabidi tu muangalie video kwa sababu Ben Pol ndiye mtu ambaye amenichagua na ameona ninapendeza kwenye video yake”.

Lakini pia Monalisa ameweka wazi kuwa yeye ni shabiki namba moja muziki wa Ben Pol hivyo alipopata nafasi ya kuwa video queen alikuwa tayari hata kufanya bila malipo lakini Ben alimpa kiasi fulani cha pesa ambapo halukitaja hadharani.

 

Monalisa Ashinda Tuzo Nyingine Nchini Uganda

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Ivyonne Cherry maarufu Kama Monalisa amepata tuzo nyingine kutoka nchini Uganda Kupitia Sanaa yake ya maigizo.

Monalisa amejipatia Tuzo ya heshima kama Mwanamke wa Mfano na mwenye Ushawishi kwa Jamii kupitia kazi zake za Uigizaji ambapo Tuzo hiyo kutoka nchini Uganda atakabidhiwa Tarehe 1 Disemba 2018 jijini Kampala.

Baada ya kutangazwa kupata tuzo hiyo jana tarehe 08/11/2018 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) Bi. Joyce Fissoo amempongeza na kumtaka Monalisa kuwa Balozi mzuri wa Tasnia ya Filamu nchini mara baada ya kupata Tuzo ya heshima kutoka nchini Uganda.

Bi. Fissoo ametoa pongezi hizo ofisini kwake ambapo alimkumbusha Monalisa na Wadau wote wa Sekta ya Filamu na uigizaji umuhimu wa kuendelea kutoa taswira chanya katika jamii hatimaye kuwa mfano wa kuigwa kwenye jamii.

Wewe ni mfano wa kuigwa katika jamii kutokana na kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, kuithamini na kuiheshimu kazi yako, niwakumbushe Wadau wote kujifunza yale mambo chanya kutoka kwako”.

Lakini pia Monalisa alifunguka Baada ya kupokea salamu hizo za pongezi kutoka kwa Bifu ya Fulani Tanzania:

Bodi ya Filamu imekuwa ni muhimili mkubwa katika kuiongoza Tasnia ya Filamu nchini hivyo nitahakikisha naendelea kushirikiana nayo bega kwa bega ili tuweze kuipa heshima Tasnia na nchi yetu kwa ujumla kupitia kazi bora tutakazo zizalisha”.

 

Monalisa Adaiwa Kumwaga Machozi Ukumbini

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Ivyonne Cherry maarufu kama Monalisa amedaiwa kuangua kilio ukumbini baada ya kuguswa na mabinti wanatarajia changamoto Kwenye sanaa.

Monalisa alishindwa kujizuia pale alipokuwa anawaongelea jinsi wasichana wadogo wanavyonyanyaswa kingono sehemu wanazokwenda kuomba kusaidiwa ili kuingia katika sanaa.

Monalisa aliangua kilio hicho ndani ya Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta jijini Dar ambapo alikuwa akizindua mpango wa kuwaendeleza mabinti wenye vipaji vya kuigiza uitwao Monalisa ACT.

Mona alifunguka kuwa anajua mabinti wengi wakienda kwa watu kuomba kusaidiwa ili waoneshe vipaji vyao, wengi huishia kudhalilishwa kingono ndipo wasaidiwe, jambo ambalo alililaani vikali.

Ukweli mabinti wengi wana vipaji vya filamu lakini wanaishia kukata tamaa na vipaji vyao kupotea, hii ni kwa sababu wanapokwenda kuomba msaada wameishia kuombwa rushwa ya ngono, jambo ambalo siyo zuri kabisa“.

Alifunguka Mona huku machozi yakimlengalenga na hata aliposhuka na kwenda kuwakumbatia baadhi ya mabinti alijikuta akilia.

Ben Pol Afungukia Mapenzi Yake Kwa Monalisa

Ben Msanii wa muziki wa RnB Bongo, Benard Paulomaarufu kama Ben Pol amefunguka na kuelezea jinsi anavuomkubali mwanamama Mkongwe katika tasnia ya Bongo Movie Ivyonne Cherry ‘Monalisa’.

Ben Pol ameweka wazi kuwa Monalisa ndiye mwanamke namba moja kwake kuliko wasanii wote wa kike wa muziki na filamu Bongo.

Monalisa ameonekana kama video queen katika video ya nyimbo mpya ya Ben Pol inayofanya vizuri hivi sasa ‘Ntala Nawe’.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Ben Pol amefunguka na kuweka wazi kuwa anamkubali sana Monalisa kutokana na kazi zake Lakini pia amekuwa akimuhamisha kufanya Muziki bila kiki.

Ananihamasisha kwa kweli kwa namna anavyojitunza, nimefarijika sana kugundua kwamba Monalisa pia anapenda muziki wangu same way mimi ninavyopenda kazi zake za filamu, nilikuwa na ndoto ya kufanya kazi naye siku moja, nashukuru Mungu leo imetimia, niwaombe mashabiki waingie kwa wingi kujionea kazi yangu mpya katika Mtandao wa Youtube niliyofanya naye inayoitwa Ntala Nawe”.

 

Monalisah Ashinda Tuzo Nyingine Nchini Marekani

Muigizaji Mkongwe wa Bongo movie Ivyonne Cherry maarufu kama Monalisah ameibuka kidedea baada ya kupokea tuzo kutoka katika tuzo za The African Film Festival (TAFF) zilizofanyika nchini Marekani.

Miezi michache iliyopita Monalisah alipokea tuzo nyingine kutoka katika tuzo ya The African Prestigious Awards (APA) 2017 kwenye kipengele cha Msanii Bora wa Kike barani Afrika. Tuzo hizo zilitolewa Accra nchini Ghana.

Mona amedai safari hii hakujua kama anaenda kupewa tuzo kwani alienda Kwenye hafla hiyo kama host.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Monalisah amefubguka haya:

Namshukuru Mungu sana kwa anayonitendea, sikujua lolote kuhusu Tuzo, nilialikwa kama Host wa usiku wa Tuzo na kushiriki Tamasha la Filamu. Kumbe TAFF walikuwa wana nia ya kunizawadia Tuzo hii Wow!.

Sijui niseme nini mtoto wa Natasha Mimi?watu wa nje wananielewa kiasi hiki kwa kitu ninachofanya kwa ajili ya nchi yangu?ni hisia ambazo siwezi kuelezea“.

 

Monalisa Kukutana Jukwaa Moja na Bofeda wa Nollywood

Mwanadada Monalisa nyota yake ya uigizaji inazidi kungaa na kuzidi kuifanyia vizuri nchi ya Tanzania baada kutegemea kukutana na msanii mkubwa kutoka nigeria katika jukwa moja nchini Marekani hivi karibuni.

Katika tamasha hilo linalotegemewa kuanza June 29 , monalisa atakuwa moja ya washiriki katika tamasha hilo la Afrika Film Festival na kukutana na bofeda kutoka Nigeria akiwa kama host wa tamasha hilo,

Monalisa atakutana na wasanii wengi kutoka nchi mbalimbali Afrika  huku yeye akiwa ndio msanii pekee kutoka tanzania, hii inaweza kutokana na umaridadi mkubwa alionao Monalisa lakini pia kutokana na kushinda tuzo ya african pestigious award mapema mwaka huu.

Monalisa Afungukia Bifu La Wema na Riyama

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Ivyonne Cherry maarufu kama Monalisa amefunguka na kuongelea bifu lililosemekana lili kuwepo kati ya waigizaji wawili wa Bongo movie ambao ni Wema Sepetu na Riyama Ally.

Wiki chache zilizopita Wema alichukua tuzo ya Muigizaji bora wa kike kwenye Bongo movie Kupitia Tuzo za SZIFF ambayo alishindanishwa na wasanii wengi kama Riyama.

Baada ya Riyama kukosa tuzo ile alifanya Interview na kituo kimoja cha redio na alimwaga machozi live  kabisa huku akidai kuwa yeye alistahili kupata tuzo ile na kuwataka SZIFF wamuombe radhi kwani kukosa kwake tuzo ni Kumdhalilisha.

Baada ya kuongea maneno hayo moja kwa moja ilivhukuliwa kuwa Riyama amejijengea bifu na Wema Sepetu kwani ni sawa na alisema kuwa Wema hakustahili kupata tuzo hiyo.

Lakini Riyama na Wema walizima tetesi hizo za kuwa na bifu baada ya kupiga picha pamoja wakiwa Airport walipoenda kumpokea Monalisa ambaye alikuwa ametoka kuchukua tuzo yake nchini Ghana.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Times Fm Monalisa alifunguka haya kuhusiana na maneno yaliyosemwa kati ya Wena na Riyama:

Kwanza niseme nilivyofika pale sikutegemea kuona watu lakini nilivyoshuka nikakutana na wasanii wenzangu, nilijisikia furaha sana..

Nilifurahi kuawaona, sidhani kama Riyama kamlalamikia Wema nyie tu ndio mnachukulia vibaya, Riyama alikuwa na malalamiko yake na mimi ninayafahamu toka siku ya kwanza”.