Mr Nice Amuanikia Mtoto Wake wa Kike kwa Mara ya Kwanza

 

Msanii wa muziki wa siku nyingi Mr Nice kwa mara ya kwanza ameamua kuweka picha ya mtoto wake wa kwanza katika kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Mr Nice alshindwa kujiuzuia kuonyesha hisia zake baada ya kuweka picha hizo alianza kupokea maswali ya mashabiki zake ambao walikuwa wakimuuliza kuwa binti huyo ni nani na ndipo alipoamua kuwajibu kuwa huyo ni mtoto wake wa kwanza.

Mtoto huyo na Mr nice hawajawahi kuonekana  pamoja kwa mara nyngi zaidi ya kuweka picha wakiwa pamoja miaa kadhaa iliyopita wakiwa wote.

 

Binti huyo mwenye miaka zaidi ya 18 anahisia wa kuishi nchi Kenya au Uganda ambako msanii huyo amekuwa akifanya kazi huko mara nyingi.

Mr Nice Ajibu Tetesi za Kukwama Kampala

Kulisambaa kwa taarifa kuwa msanii mr nice amekwama jijini kampala kwa sababu tu meneja wa abtexpromotion alishindwa kumlipa pesa yake kama walivyokuwa wamekubaliana ambapo Mr nice alitakiwa kufanya show katika moja ya kumbi kubwa jijini humu.

Hata hivyo baada ya hapo taarifa zilisema kuwa tangu mwezi june mr nice amekwama nchini humo kutokana na hali yake kuwa mbaya na kwamba alikuwa amefikia moja ya hotel kubwa jijini humo.

Hata hivyo msanii huyoa ankanusha taarifa hizo na kusema kuwa pamoja na kwamba Abtex promotion ilishindwa kumlipa lakini sio kweli kuwa alikwama na kushindwa kujikimu akiwa nchini humo na hata kuaki kwake ni kwa ajili yakazi zake za kawaida zinazoendelea.

Kuna uvumi kuwa mr nice amekwama kampala, inawezekana kweli kukwama katika eneo langu.Abtex hawakunilipa hata asilimia moja, na nilipata mateso sana lakini Mr. Nice ni jina kubwa nikajitenga kwenye hali hiyo mwenyewe.

 

Wolper Amwaga Povu Baada Ya Tetesi Za Kutoka na Mr. Nice

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Jacqueline Wolper amemwaga povu baada ya tetesi kusambaa anatoka kimapenzi na msanii mkongwe wa Bongo fleva Mr. Nice.

Siku chache zilizopita Wolper na Mr. Nice walionekana pamoja wakila bata Kwenye club moja Nairobi nchini Kenya huku wakionyesha kuwa na ukaribu fulani.

Kwenye video ambayo iliwekwa Mtandaoni na Jacqueline Wolper iliwaonyesha wawili hao wakila bata yaani Wolper akivuta shisha huku Mr. Nice akinywa pombe ambapo watu mbalimbali walidai huenda wanatoka kimapenzi.

Baada ya Tetesi hizo za Mahusiano gazeti la Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Wolper kwa njia ya simu akiwa nchini Kenya na kumuuliza kuhusu ukaribu wake na Nice ambapo alisema ni wa kawaida tu na wako karibu kwa sababu bosi wao ni mmoja.

Watu wajue sisi tupo kikazi zaidi kwani kuonekana na mtu ni lazima awe mpenzi wako? Si lazima, huyu ni kaka yangu na bosi wetu ni mmoja, projekti yetu ikiwa tayari tutaitangaza itajulikana tu lakini kwa sasa bado ni mapema kuitangaza”.

 

Mr Nice Hana Msanii Bora Katika Muziki Zaidi Yake.

Msanii wa siuku nyingi ambae alikuwa mkali wa style ya takeu nchini, mr nice amefunguka na kusema kuwa katika mzuikiwa bongo hakuna msaniii anayemkubali zaidi yake mwenyewe tu.mr nic anasema kuwa tangu muziki uanze yeyye ndio msanii bora na hana mpinzani katika hilo.

Mr Nice anasema kuwa pamoja na kwamba mwanadada kama Jay Dee ni mkongwe mwenzake na ndio maana anamheshimu na pia Profesa Jay lakini pia Chamelion ni rafiki yake sana hawezi kumuacha lakini hao wengine hana ona wa kumtaja zaidi ya jina lake.

Lady Jay Dee ni legendari mwenzangu, ni wanamuziki wenzangu na hivyo hivyo kwa Profesa Jay.

Jose chamelion ni msanii mwenzangu ambae ninaweza kuvua viatu vynagu nikamwambia vaa viatu vyangu jose.,dah huyu mtu , unajua  mimi huwa simkubali msanii mwengine yeyote na hata ukiniambia nitaje list ya top five nitataja jina la Mr Nice tu.

Mr. Nice Amefungukia Tetesi Za Kuwa Muathirika Wa Ukimwi

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva Mr. Nice aliyewahi kutamba kipindi cha nyuma na nyimbo zake kama Kikulacho na nyinginzo amefunguka na kuwatolea povu zito watu wote wanaosambaza habari kuwa yeye ni muathirika wa virusi vya Ukimwi.

Kwa kipindi kirefu Mr. Nice alikuwa yuko kukua kwenye gemu ya Bongo fleva na alipokuja kuibuka alizua maneno mengi hasa kwa sababu ya muonekano wake kubadilika na kukongoroka na kukonda mwili hali iliyopelekea taarifa kuenea kuwa ni muathirika wa virusi vya Ukimwi.

Mr. Nice amefunguka kuhusu tuhuma hizo Kwenye mahojiano aliyofanya na Enews ya East Africa Tv anbapo amekataa kata kata tuhuma hizo:

Kwanza wanaoninyoshea vidole kuwa nimeathirika wataathirika wao mimi niko sawa sawa kabisa tatizo ni kwamba watu hawajui maisha ninayoishi wamekuwa wangapi na ngoma lakini mimi bado nipo nadunda nachotaka kuwaambia ni kwamba tuhushimiane nimeenda kusemwa nimeathirika tangu 2002 sasa mpaka leo si ningekuwa nimekufa”.

Mr. Nice pia amefunguka na kusema anajua watu wanaomsema ameathirika pia wanamsaidia kuepuka kupigwa mizinga maana hata wanawake akikutana naye hawampigi mizinga kama zamani.

Mr. Nice Achekelea Nyimbo za Wasanii Wenzake Kufungiwa

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Bongo fleva aliyetamba na Takeu Style miaka hiyo Mr. Nice amekuwa tofauti kidogo na watu wengine waliokasirika nyimbo 15 kufungiwa na BASATA kwani yeye amefurahia anawaunga mkono.

Wiki iliyopita nyimbo 15 za wasanii mbali mbali kama Diamond, Ney wa Mitego, Roma, na wengineo walifungiwa nyimbo zao kwa kisingizio kuwa zimekosa maadili ya Kitanzania huku Roma Mkatoliki akiambulia kufungiwa miezi Sita ya kufanya kazi.

Mr. Nice amejitokeza na kuipongeza serikali kwa hatua hiyo iliyochukua kwani amedai ni kweli nyimbo hizo hazina maadili yanayoendana na mila na desturi za Kitanzania.

Mr. Nice amefunguka hayo alipokuwa anafanya mahojiano na Planet Bongo ya East Africa redio amesema jambo hilo ni la busara kabisa kwa sababu nyimbo hizo zikiendelea kupigwa zitaharibu vijana kwa kukosa maadili:

Unajua vijana, watoto wadogo ndio wanapenda sana muziki kwa sasa, mimi kama msanii nikiimba kitu ambacho hakina maana, mantiki, adabu ni vibaya. Serikali inaona ni ajira yako lakini isifike mahali ukachafua watu wengine ni afadhali wewe samaki mmoja uliyeoza ukatupwa wengine wakaendelea kuchanua sio wote waonekane wameoza”.

Baada ya BASATA kutoa orodha hiyo ya nyimbo zilizopaswa kufungiwa na TCRA kuziweka wazi Kumekuwa na mjadala mkubwa juu ya suala hili na wasanii wengine wengi wamekemea kitendo hiki wasanii kama Fid Q, Stamina, Nikki wa pili na wengineo wengi.

Young Dee- Nimeiga Wimbo Wa Mr. Nice Kwa Heshima

Msanii wa Bongo fleva Young Dee ameibuka na kudai kuwa kitendo cha yeye kuiga wimbo msanii mkongwe wa Bongo fleva Lucas Mkenda maarufu kama Mr.Nice Ilikuwa ni kwa sababu ya heshima aliyonayo kwenye mziki wake na wala sio wizi.

Baada ya Young Dee kutoa wimbo wake mpya unaoenda kwa jina la Kiben10 ambao ndani yake ameweka kionjo cha wimbo wa Mr.Nice bila ruhusa, ndipo pale jasho lilimtoka kwani Mr. Nice alipousikia wimbo huo alimjia juu Young Dee kwenye mitandao ya kijamii na kudiriki kumuita mwizi wa kazi zake na kutishia kumchukulia hatua za kisheria.

Young Dee amemjibu Mr. Nice na amejitetea kuwa yeye kuimba wimbo wake haikuwa kwa nia mbaya bali alifnya vile kwa sababu alikuwa shabiki Mkubwa wa wimbo wa Mr. Nice.

Kwenye mahojiano aliyofanya na East Africa Tv kupitua kipindi Chao cha Enews Young Dee alifunguka:

Naomba niseme kuwa sikuwa na nia mbaya bali nia yangu ilikuwa ni kumpa heshima maana hawa ni kaka yangu aliyenitangulia katika gemu alafu ana mchango mkubwa kwenye mziki wetu wa Bongo fleva kwaiyo lengi langi lilikuwq ni kumuonyesha heshima aliyoiweka kwenye mziki wetu wa Bongo fleva kiasi ya kwamba miaka mingi baada ya wimbo huo kuhit lakini bado Una ladha ya kipekee kabisa”.

Mr. Nice Hakuna Msanii Mkali Zaidi Yangu Duniani

Msanii mkali na mkongwe aliyetamba miaka ya nyuma kwa nyimbo zake kama kikulacho, rafiki yangu na Fagilia na nyinginezo nyingi zilizosindikizwa kwa staili yake ya kipekee ya Takeu Style.

Tangu miaka hiyo mpaka leo hii kuna mambo mengi yaliyotokea lakini hasa lililochukua nafasi kubwa ni tetesi zilizokuwa zinaenea. Moja kati ya tetesi zilizoenea kwa kasi ni ugonjwa aliokuwa nao Mr. Nice ambapo wengi walizusha kuwa anaumwa ukimwi na amefulia hana mbele wala nyuma.

Siku za hivi karibuni Mr. Nice amerudi tena ghafla kwenye vyombo vya habari ambapo ni juzi tu alisikika kurudi kwenye bifu tena na aliyekuwa hasimu wake Mkubwa miaka ya nyuma msanii nwenzake Dudubaya lakini pia alitawala vichwa vya habari baada yaya kuingia kwenye sintofahamu na Young Dee.

Kwenye mahojiano na LilOmmy Mr. Nice amefunguka hayo yote na kusisitiza kuwa anaamini hakuna msanii mkubwa duniani kama yeye mwenyewe:

Kwangu mimi hakuna msanii yoyote ninaye mkubali zaidi yangu mimi mwenyewe yaani Mr. Nice ndiye Msanii ninayemkubali na kumheshimu sana  na ninapenda kusema kwa nini najiheshimu mwenyewe, ni kwa sababu naamini ni lazima ujipende wewe kabla haujampenda mwenzio kwaiyo kwa wasanii wenzangu wote sioni wa zaidi yangu kwaiyo nimimikwanza halafu wao ndio wanafata”.

Lakini Mr. Nice amefunguka na kudai kuwa tetesi za yeye kufulia sio za kweli kabisa kwani anaishi maisha mazuri na pia anasaidia watu wengi wasiojiweza lakini pia anamuangalia Mama yake mzazi ambapo anaamini mama take anaishi maisha mazuri kuliko mama wengi duniani.

Mr. Nice Amjia Juu Young Dee Baada ya Kuimuibia Wimbo Wake Wa ‘King’asti’

Msanii mkongwe wa Bongo fleva aliyetamba kwa staili yake ya ‘Takeu style’ ameibuka na kumtolea povu zito msanii mwenzake Young Dee baada ya kusample wimbo wake wa ‘King’asti’.

Mr. Nice amezidi kukaa kwenye headlines kwa wiki hii kuanzia kurudi upya kwa bifu lake na aliyekuwa hasimu wake mkubwa Dudubaya mpaka kuingia kwenye vita ya maneno na Paka rapa Young Dee baada ya Young Dee ku-sample wimbo wake ulio-hit miaka ya nyuma ulioenda kwa jina la ‘king’asti’.

Young Dee ametoa wimbo wake mpya unaoitwa ‘kiben-10’ na amemshirikisha Dayna Nyange ambapo kwenye wimbo huo kuna kionjo na mashairi machache kutoka kwenye wimbo huo wa Mr. Nice ambao amechukua bila ruhusa ya mwenye wimbo huo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mr. Nice amemtolea Young Dee povu zito:

Nadhani ni wizi na ni aibu kuchukua kazi ya mtu na kuirudia tena kwa manufaa yako binafsi bila hata kuomba ridhaa yoyote kutoka kwa mwenye kazi yake, ni wizi ambao serikali na jamii nzima imekuwa ikipiga vita every day na ni kosa kubwa kabisa kisheria…..Huyo msanii anayeitwa sijui Young Dee mwelezeni asije kutafuta huruma yangu hapo baadae kwa maana haitakuwepo”.

 

Mr Nice Atupa Jiwe Gizani,Yasemekana Alimlenga H.Baba

Moja ya wasanii wakongwe nchini aliyevuma sana hapo awali kwa style yake ya kucheza ikijulikana kama takeu ambayo ilipendwa sana na watoto Lucas Mkenda maarufu kama Mr.Nice amerusha jiwe gizani na kumponda moja ya wasanii wenzake wakongwe ambae pia kwa sasa yupo kimya.

Akiongea na East Africa alipokuwa akitambulisha wimbo wake mpya hivi karibuni , Mr. Nice anasema kuwa kuna baadhi ya wasanii katika game walikuwa wakisafiria nyota yake katika muziki huku wakiiga anavyoimba hadi kucheza lakini cha ajabu ni kwamba sasa hivi wamefulia na wameshindwa kuinuka tena.

Watu walikuja kwenye game, wakataka kutumia style yangu ya takeu na kuitumia kabisa  na bado wakashindwa, wakaingia bongo movies na huko nako pia kukawashinda.

Hata hivyo maneno hayo yanasemekana kutupiwa msanii mwenzie mkongwe h.baba kutokana na wasifu huo kumfanania kabisa msanii huo kwa sababu kwa kipindi cha style ya takeu ambapo Mr.Nice ndie aliekuwa mwanzilishi lakini h.baba nae alikuja na kuimba huku akicheza style hiyo hiyo.

H.Baba pia aliingia katika tasnia ya filamu na kufanya vizuri pia ingawa kwa sasa haijulikana msanii huyo yuko wapi kutokana na ukimya wake kwa muda mrefu.

Hata hivyo Mr.Nice alipoulizwa kuhusu kwanini amekuwa akitumia muda mrefu kuweka makazi yake nchini kenya , msanii huyo alisema kuwa amegundua kuwa kenya amekuwa na mashabiki wengi sana na kazi zake zinapendwa sana nchini kenya kulikio huko,Mr.Nice ametambulisha wimbo wake mpya baada ya kukaa kimya katika game kwa muda mrefu sana.

Mr Nice:Walichokifanya Irene Na Dogo Janja Sio Mfano Wa Kuigwa

Anafahamika tangu zamani kutokana na kazi nzuri aliyoifanya miaka ya nyuma, Lucas Mkenda  maarufu kama Mr .Nice ni msanii mkongwe wa muziki Tanzania ambae alikuwa akifanya vizuri na kuitambulisha vyema Tanzania nje ya Tanzania kwa style yake ya kucheza iliyojulikana kama Takeu style.Style ambayo ilikuwa ikichezwa mpaka na watoto wadogo.Ni wapi msanii huyo  alikuwa hajulikana, kila mtaa kila wakati utasikia nyimbo za msanii  Mr.Nice zikipigwa.

Akiongelea kurudi kwake katika muziki na jinsi wasanii wengine wanavyofanya style yao ya kutumia kiki ili kuweza ku-boost nyimbo zao ziweze kuvuma na kufanya vizuri Mr,Nice anasema kuwa kiki sio nzuri katika muziki kwa sababu unakuta mashabiki wanakuwa wanaamini na kusapoti kitu ulichotaka kukifanya kwa nguvu kubwa alafu baadae inakuja kujulikana kuwa ni kiki tu, akitolea mfano wa ndoa ya Irene Uwoya na DogJ janja iliyofanyika hivi karibuni anasema kuwa watu hao sio mfano wa kuigwa kwa kiki  walioifanya ya kuwafanya mashabiki waamini wamefunga ndoa kumbe sio kweli.

Swala la kiki kwangu halijakaa vizuri kabisa na ninaomba watu wote kwenye jamii walikemee, kwa nguvu zote kwa mfano hii kiki iliyotokea hivi karibuni ya  Irene Uwoya na Dogo Janja kwamba wameoana kumbe hata sio kweli ni kiki tu wala sio jambo zuri.unatumia nguvu nyingi sana kuwaaminisha mashabiki wako kuwa  mmeoana alafu kirahisi tu inakuja kugundulika kuwa sio kweli.Ukweli ni kwamba huo sio mfano mzuri wa kuigwa hata kidogo.

Hata hivyo katika mahojiano na gazeti moja pendwa hapa nchini Mr. Nice aliongezea kwa kumpa ushauri Aslay ambae amekuwa akitoa nyimbo kila kukicha na kumwambia kuwa yeye mwenyewe ndio  anaua soko lake la muziki kwa sababu hawapi muda mashabiki zake kusikilza nyimbo zake kila siku anatoa nyimbo mpya hivyo mashabiki wanakosa muda wa kusikiliza.Ni bora kutulia kuliko kufanya vitu kwa pupa maana haujui kilichokuangusha ni nini.

Lakini pia akiongelea swala ya yeye kuoa , Mr. Nice anasema kuwa kwa sasa hana mpango wa kuoa amejikita kulea familia yake yenye watoto watatu.

Mr. Nice akana kuibiwa katika sherehe ya kuapishwa kwa gavana wa Nairobi (Picha)

Mr. Nice alikua miongoni mwa wasanii na watu mashuhuri ambao walihuduria hafla ya kuapishwa kwa gavana mpya wa jimbo la Nairobi – Mike Mbuvi Sonko.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na makamo wake William Ruto pia walihudhuria sherehe hio ambayo iliandaliwa jana Agosti 21 jijini Nairobi.

Mr. Nice na Bahati wakiwa kwa hafla ya kuapishwa kwa gavana Sonko

Awali kulikuwa na repoti kwenye mtandao kuwa Mr. Nice aliibiwa baadhi ya vitu alipokuwa akitangamana na mashabiki katika hafla hio. Hata hivyo Mr. Nice amekana madai kuwa aliibiwa.

“Waandishi vilaza mnapenda kurukia sana hata msilolijua mimi katika show ya kuapishwa Sonko leo sijaibiwa na mtu yoyote. Kifupi ni kwamba mashabiki waling’ang’ana kucheza na mimi na bahati mbaya wakajikuta wamekata cheni zangu na pia leseni yangu ikadondoka nilikuwa nayo kwa mfuko wa koti la suti,” Mr. Nice aliandika kwa Facebook.

  

Mr. Nice awashangaza watu kwa kutokea kwenye video mpya ya Harmonize

Msanii Lucas Mkenda maarufu kama Mr. Nice anatrend kwenye mitandao ya kijamii kwa ajili ya kuonekana kwake kwenye video mpya ya Harmonize.

Staa huyo aliyevuma zamani alihamia Kenya kwani hakua anapata kiki Tanzania. Hata hivyo kutokea kwa Mr. Nice kwenye wimbo mpya wa Harmonize – ‘Sifa’ kumedhibitisha kuwa nyota huyo wa zamani bado anafanya kazi na wasanii wa Tanzania.

Wimbo huo wa Harmonize unaangazia maisha ya Mr. Nice alipopata pesa na kuwa mtu maarufu na maisha yake alipofilisika.

Tazama video hio hapo chini: