Babu Tale Amjia Juu Mrisho Mpoto Kisa Diamond

Meneja wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Babu Tale amejikuta akimtolea Povu zito Msanii wa muziki Mrisho Mpoto Baada ya Msanii huyo kuhudhuria msiba wa Ruge Mutahaba.

Siku chache zilizopita Mrisho Mpoto alimtaka Diamond aweke tofauti zake pembeni na Marehemu Ruge na ahudhurie msiba Wake na Kupitia ukurasa wake wa Instagram, alimuandikia ujumbe mzito.

Siku ya jumamosi Ruge aliagwa na wasanii Mbali Mbali na viongozi wa serikali katika viwanja vya Karimjee Hall na Diamond na timu yake ya WCB walihudhuria hafla hiyo.

Baada ya Diamond kuhudhuria hafla hiyo Mrisho Mpoto alitumia ukurasa wake wa Instagram kumshukuru Diamond kwa kuenda kauli iliyomkera Babu Tale ambapo alimjia juu Diamond na kusema kuwa hakuenda kwenye msiba kwa sababu yeye alimwambia.

Siwezi Kuamini Msiba wa Ruge Mpaka Nione Mwili Wake :-Mrisho Mpoto

Msanii mkongwe wa nyimbo za asili nchini Mrisho Mpoto amefunguka alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika msiba wa Ruge Mutahaba uliopo nyumbani kwa wazazi wake  huku jijini Dar huko mikocheni .

Akiongea na waandishi wa habari Mrisho Mpoto anasema kuwa hakuna msanii mkubwa anaeonekana kwa sasa anaendesha gari na nyumb nzuri bila kupita mikononi kwa Ruge hata mmoja , hayupo Tanzania.

Hata hivyo Mrisho Mpoto anasema kuwa kamwe hawezi kukaa na kuamini kuwa Ruge amekufa mpaka pale atakapoona katika jeneza mwili wa Ruge ambae kwake ni kama kaka aliemshika mkono kumfanya ainuke.

Wasanii ni wengi sana na watu wa nyanja mbalimbali ambao wamekuwa wakitoa ushuhuda wa kile ambacho walifanyiwa na jasiri kiongozi huyo ambae mshumama wake umezima ghafla.

Ruge Aliniambia Nitembee Peku :-Mrisho

Msanii wa kughani mashairi nchini mrisho mpoto amefunguka na kutoa siri ya yeye uwa tofauti na wasanii wengine na kusema kuwa ile tabia ya utembea peu alifundishwa na mkurugenzi wa vipindi vya Clouds media Group bwana ruge mutahaba.

Mrisho anasema kuwa walikaa na ruge na kuongelea yeye kuwa na utofauti katika mashairi yake na jinsi gani anaweza kujitofautisha na wasanii wengine kama yeye.

Hata hivyo mrisho anasema “Ni Ruge ndio alinitengeneza mimi uwa tofauti na mashairi yangu, mwanzoni nilikuwa naimba tu lakini baadae aliamua kuni-brand na kunifanya wa tofauti.

Mrisho Mpoto- Wasanii Kuoa Nje Ya Nchi Kuna Tatizo na Wanahitaji Kufundwa

Mwanamuziki wa Muziki wa Asili  Mrisho Mpoto amefunguka kuhusu trend mpya ya mastaa mbali mbali wa Bongo fleva kuamua kwenda kuoa nje ya nchi.

Mrisho Mpoto amefunguka na kudai nyimbo yake inayofanya vizuri ya ‘Nimwage Radhi’ aliyomshirikisha Harmonize imetoka a na wasanii wanaoa nje ya nchi.

Kwenye mahojiano na Times Fm,  Mpoto alitoa kauli hiyo  pale alipoeleza kuwa awali alishauriwa na Harmonize video hiyo ikafanyike Nigeria au Afrika Kusini ila akakataa kutokana ujumbe wa wimbo huo ni kwa ajili ya Watanzania.

Kwa sababu wimbo mimi naongea na Watanzania, nilikuwa nimeguswa na jinsi vijana wetu wa Kitanzania wanavyokwenda kuoa nje ya Tanzania, kwa nini vijana wetu maarufu hawataki kuoa nyumbani?.

Nikaliona hilo, nikajua kuna tatizo hapa, hawa wanahitaji kufundwa, hawa kuna maneno wanatakiwa kuambiwa, waambie na mwenye maneno yake”.

Siku za hivi karibuni tumeshuhudia mastaa mbali mbali wakienda kuoa nje ya nchi kama vile Ali kiba aliyemuoa binti Amina kutoka Kenya, AY alimuoa Mwanamke kutoka Rwanda na hata Stamina alimuoa binti kutoka Rwanda.

 

Diamond Akiri Kumkubali Mrisho Mpoto Kwa Staili Yake Mpya

Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz amemvulia kofia  na kuonyesha kumkubali Msanii Mrisho Mpoto baada Ya staili yake aliyotumia kuimba wimbo alioshirikishwa na Harmonize unaoitwa Nimwage Radhi

Msanii Mrisho Mpoto ameshazoeleka kwa staili yake moja ya uimbaji aliyoitumia Kwenye nyimbo zake maarufu kama Mjomba, Zisonje na Njoo Uzichukue na nyinginezo.

Lakini Kwenye Wimbo Mpya alioshirikishwa na Harmonize ambao sasahivi unafanya vizuri sana Nimwage Radhi Mpoto amekuja kwa staili nyingine kabisa ya kuimba na kuwafurahisha watu wengi ikiwemo Diamond Platnumz.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond ameshindwa kujizuia na kumwagia sifa Mrisho Mpoto ambapo ameandika:

Kwa kweli Mrisho Mpoto nilikuwa nakuwaza sana, Kwa ufanisi wa serikali hii, ungewezaje kutupa vile vibao vyako vya #MJOMBA #WAITE Na Kadharika…. ila nimeamini kweli Mungu kakutunuku Kipaji na Ubunifu wa Sanaa, Sikutegemea kama UtaniSurprise namna hii… #NimwageRadhi Kali sana?? ….Mdogo angu Mmakonde @harmonize_tz naona Mwaka Huu unahasira nao sana….Kama Naiona hiyo #WasafiFestival Huu Mwaka Sjui hata tuanzie Mkoa gani???,” aliandika Diamond Instagram“.

Wimbo huo umekuwa ukifanya vizuri na kushika chati katika vituo mbali mbali vya habari na hata kushika nafasi za juu katika mtandao wa Youtube.

Katika Watanzania Mil54, Ay na Alikiba Hawajaona Mwanamke Tanzania:-Mrisho mpoto

Msanii wa mashairi Tanzania Mrisho Mpoto amefunguka na kutoa maoni yake kuhusu swala la wasanii kuona nje ya nchi huku wakiwa na mahusiano na wasichana  wa kitanzania na kuwaacha,

Mrisho Mpoto alipokuwa akiongea na Cloud e alisema kuwa wasichana wa kitanzania wanatakiwa wajitathmini sana kwa sababu katika wanawake wote  tanzania inakuwa changamoto sana kwa wasanii hawa kuamua kuona nje ya nchi wakati wasichana ni wengi tanzania.

mrisho mpoto anasema kuwa wasichanwengi wa bongo wamekuwa na tabia ya kuanika maungo yao wazi na hicho ni kitu ambacho wanaume wengi wamekuwa hawapendi kitu kama hico ingawa kwao wanaona kuwa ni kama dili.

Wanawake wanatakiwa wajifunze kitu kutokana na hili, Ay na Alikiba wote wameoa nje ya nchi. je ni kweli kuwa kati ya watanzania milion 54 hawajaona mwanamke wa kuoa hapa.hii ni changamoto wasichana waache kuanika hivyo vinanii.. vyao maana watashangaa na hata waliobaki wanawakosa.

Hata Mwasiti alipoulizwa kuhususwala hilo pia alisema kuwa wasichana wengi wa kitanzania wamekuwa wakiweka maungo yao wazi sana kiasi kwamba mtu akitaka kwnda kumtambulisha nyumbani anaazna kuwaza kwanza jinsi ya kuoneka kwao

 

Mrisho Mpoto Amtaka Steve Nyerere Apunguze Gubu Baada Ya Kukosa Tuzo

Msanii maarufu Bongo Mrisho Mpoto amemuoa juu msanii mwenzake wa Bongo movie Steve Nyerere kumtaka apunguze gubu na kukubali matokeo baada ya kukosa tuzo za SZIFF.

Tuzo za Sinema Zetu International Film Festival zilifanyika wikiendi iliyopita na kuleta gumzo baada ya wasanii waliokosa tuzo kama Steve Nyerere kuanza kulalamika.

Kwenye mahojiano aliyofanya siku chache zilizopita na Bongo 5 Steve Nyerere alilalamika yeye kukosa tuzo Lakini pia alidai pia kuna wasanii ambao angependa wapate tuzo lakini walikuwa kama vile Aunty Ezekiel, JB na wengineo.

Mrisho Mpoto amempa makavu na kumwambia aache kulalamika kwa sababu ameshindwa hilo ni gubu badala yake afanye juhudi ili Safari ijayo aweze kupata tuzo hizo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mrisho Mpoto ameandika mambo haya:

Steve Nyerere Mbona huna Jema ndugu? Uzalendo ni Hali ya Mtu kujitoa kufa na kupona Kwa maslahi ya wengi yenye Tija Kwa Taifa, nikakusikia kwenye vyombo vya habari unasema Uzalendo ni project yako, tena ukaenda Mbali zaidi ukasema nimedandia project yako kwa mbele, nikahisi tofauti kidogo: Kwakua kilikua kipindi cha jua kali kidogo.

Sasa hivi umeibuka na kuanza kuponda Tuzo za Sinema zetu ambazo ndiyo kwanza zinaanza ili kujaribu kurudisha Heshima ya filamu zetu ambazo wewe umechangia kufa kwake hauoni unakatisha tamaa watu wenye nia njema na Filamu? Ebu punguza gubu ndugu yangu angalau tuwe na kitu kimoja Chenye heshima cha kujivunia kwenye tasnia ya sanaa….ya uigizaji…

Zile Tuzo zilitolewa Kwa wenye Umiliki wa filamu na aliyewasilisha kwenye Mashindano na siyo anaeonekana sana kwenye Runinga…siyo lazima apewe unaemtaka wewe Stive. Najua kile kilikua kipindi cha jua, hiki cha mvua labda utanielewa kidogo…wadau na Mashabiki wa Bongo Movie msikatishwe tamaa”.

 

Mrisho Mpoto Amjia Juu Afande Sele Kisa Kesi Ya Lulu na Mauaji Ya Kanumba

Msanii wa Muziki Tanzania, Mrisho Mpoto ameshindwa kumvumilia msanii mwenzake Afande Sele na kumpa makavu baada ya Afande Sele kudai maiti ya Kanumba ifukuliwe na ichomwe moto kwa sababu ni mbakaji.

Baada ya kifungo cha Lulu siku mbili zilizopita wasanii mbali mbali walikuwa na maoni yao mmoja wapo kati ya watu hao ni mwanamuziki Afande Sele ambaye aliweka wazi hisia zake na kumjia juu Mama Kanumba kwa kitendo chake cha kufurahia Lulu kufungwa huku akisisitiza kuwa Kanumba ni mbakaji ambaye alikuwa anatembea na mtoto mdogo kama Lulu hivyo hastahili kupewa heshima bali ilitakiwa afukuliwe makaburini na kuchomwa moto.

Baada ya Kuongea maneno hayo ambayo yalionekana kutokumfurahisha Mrisho Mpoto alimjia juu Afande Sele na kufunga haya:

Afande Sele wewe ni kaka yangu na mwandishi ambary sijawahi kuacha kuheshimu maandishi yako…..Nimesoma mara 30 maandishi ulioandika kuhusu Kanumba naomba kujua ile barua uliomuandikia Marehemu Kanumba ulitaka imfikie au ulitaka wanaokuja nyuma yake wamfikishie? Ulitaka wanaokuja nyuma yake wajifunze kupitia waraka wako? Mbona nimepata kusikia marehemu halaumiwi kwa kuwa hana uwezo wa kujitetea? Umesema ulikuwepo Sinza kwenye msiba lakini hukutaka kusogea kuzika kwa sababu umesema we we sio mnafki kama Watanzania walioenda kuzik…ikiwa watu wote wangekataa ile maiti ingekuwaje? Nini hasa lengo la movies za kibongo kuziita maigizo yanayokwenda kwenye kanda? Una ugomvi na Bongo movie au uliandika ukiwa Una jazba kidogo? Mimi ndugu yako Mrisho Mpoto”.