Rapa Wakazi Kupita Njia za Nandy

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kuchana (Rap) Wakazi ameweka wazi nia yake ya kufanya remix ya ngoma ya Msanii wa Bongo fleva Nandy.

Wakazi ameweka wazi kuwa yupo mbioni kutoa remix ya wimbo wa Nandy unaokwenda kwa jina la Aibu ambao unafanya vizuri kwa sasa kwenye chati mbalimbali za redio.

Siku za nyuma Utakumbuka Wakazi alifanya hivyo pia kwenye wimbo, Sijutii wa muimbaji Ruby ambaye anatajwa kuwa hasimu mkubwa na Nandy kimuziki kwa sasa. Pia Wakazi aliwahi kufanya refix ya wimbo wa msanii kutokea nchini Nigeria, Wizkid unaokwenda kwa jina laOjuelegba na kuipa jina la Natokea Dar .

Sina Urafiki Wowote na Billnas- Nandy

Msanii  wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vyema na ngoma yake. Mpya ya ‘Aibu’ amefunguka na kuweka wazi kuwa hivi sasa hana Mahusiano yoyote na aliyekuwa mpenzi wake Msanii mwenzake Bill Nas.

Nandy na Billnas waliwahi kuwa wapenzi miaka ya nyuma wakaja kuachana lakini walipata fedheha mapema mwaka huu baada ya video yao chafu ya Kitandani kuvuja Kwenye mitandao ya kijamii.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Nandy aliulizwa kuhusu urafiki wake na Billnas na kama waliacha kuongea baada ya video yao kuvuja Nandy alifunguka:

Hatuna ushikaji kiukweli tangu kipindi kile tatizo lilipotokea, hatujawahi kuwasiliana hata kwenye simu, ila nakumbuka mara ya mwisho tulionana central kituo cha Polisi, kwa hiyo sidhani kama kuna kitu chochote cha kuongea, japo najua tukikutana lazima tutapiga stori, tutacheka na kufurahi pia“.

Lakini pia Nandy amesema kwa sasa hivi amepata mpenzi mwingine na kama Mungu akijalia, hivi karibuni atafunga ndoa.

Nandy Atangaza Ndoa na Mpenzi Wake Mpya

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Faustina Charles ‘Nandy’ amefunguka na kusema hivi sasa amepata mpenzi mpya na endapo Mungu atajaalia basi ndoa itafungwa hivi karibuni.

Kwenye mahojiano na Risasi Vibes, Nandy amesema kwamba kwa sasa hana ukaribu wa aina yoyote ile na msanii mwenzake, William Lyimo ‘Billnas’ ambaye pia amewahi kuwa mpenzi wake, baada ya matatizo yaliyowahi kutokea ya kuvuja kwa video yao chafu.

Nandy amesema kwa sasa hivi amepata mpenzi mwingine na kama Mungu akijalia, hivi karibuni atafunga ndoa.

Shemeji yenu yupo, tusubiri ndoa tu kama Mungu akijalia lakini siwezi  kutaja ni lini kwa sababu naweza nikataja halafu isifanyike, kwa hiyo sasa hivi namuomba tu Mungu iweze kutimia”.

Nandy amefunguka pia kuwa kwa sasa hana urafiki wowote na Billnas tangu sakata lao la video chafu lakini wakikutana wanapiga stori kawaida tu.

Nafurahi Kuona Wasanii wa Kike Tukiwa na Ushindani.

Msanii wa kike kwenye anga za bongo fleva Nandy amefunguka na kusema kuwa amekuwa akifurahishwa sana na kasi ya wasanii wenzake wa kike kwa sasa kutokana na kuwa na ushindani sana sio kama hapo mwanzo walivyokuwa wakisemwa kuwa wasanii wa kike wamekuwa wakibweteka.

Nandy anasema kuwa tofauti na ilivyokuwa hapo awali kuwa katika muziki kulikuwa kumetawaliwa na wanaume tu, sasa hivi kuna ongezeko kuba la wasanii wa kike na kumekuwa na ushindani sana kitu kinachotoa matumaini kuwa wanawake wameamka na kutambua kuwa hata wao wanaweza.

Nafurahi sana kuona wasanii wa kike wakishindana vipaji na wanaume  katika muziki ,kwangu nifaraja kubwa na kama tutaendelea hivi basi tutafika mbali.

 

Nafurahi Kuona Wasanii Wa Kike Tukiwa na Ushindani-Nandy

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vyema na ngoma yake mpya ya ‘Aibu’ Faustina Charles maarufu kama Nandy amefunguka na kusema anapenda ushindani wa wasanii wa kike.

Nandy ameweka wazi kati ya vitu vinavyo mfurahisha Kwenye muziki huu wa Bongo fleva ni pale ambapo wasanii wa kike wa sasa wanavyoongeza kasi ya ushindani kwenye gemu.

Kutokana na kuwa na ongezeko kubwa la wasanii wa kike tofauti na miaka ya nyuma ambapo sanaa ilikuwa imetawaliwa na wasanii wa kiume na wasanii wa kike walikuwa wa kuhesabika.

Kwenye Interview aliyofanya na Gazeti la Dimba, Nandy amefunguka na kukiri kumekuwapo na ongezeko kubwa la ushindani kati ya wasanii wa kiume na wa kike, hali inayoongeza ladha ya muziki wao.

Nafurahi sana nikiona mwanamke mwenzangu anashindana kipaji na mwanamume, kwangu ni faraja kubwa, kwani tukiendelea hivi tutafika mbali”.

 

Nandy Atangaza Kuukacha Mziki Ukifika Mwaka 2020

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Faustine  Charles maarufu kama Nandy amefunguka na kuweka wazi kuwa ukifika mwaka 2020 ataachana kabisa na muziki.

Nandy ambaye aliingia kwenye muziki rasmi kuanzia mwaka 2016 Kupitia Nyumba ya vipaji THT na kutoa ngoma kali ambazo zimemuweka Kwenye ramani kama Msanii bora wa kike Tanzania ametangaza kuachana na muziki hapo baadae.

Kwenye mahojiano aliyofanya gazeti la Risasi Jumamosi, Nandy alisema ndoto yake ni kuwa mfanyabiashara mkubwa Bongo kwani ndiyo yalikuwa malengo yake pindi tu alipoanza kufanya muziki.

Wakati naanza kufanya muziki nilijiwekea malengo kwamba baada ya miaka mitano niache muziki ili niendeleze biashara zangu, hivyo namshukuru Mungu kwa sababu mpaka sasa nimeshatumia miaka miwili ambayo ni mwaka 2016 na 2017. Kwa hiyo utakapofika mwaka 2020 nitaacha muziki, ila siyo kama nitakuwa sitoi nyimbo hapana nitakuwa natoa lakini kwa mwaka mara moja ili niwe napata muda mzuri wa kusimamia biashara zangu”.

Hivi sasa Nandy anafanya vyema na wimbo wake wa ‘Aibu ambao pamoja na kwamba ni audio tu hauna video umeendelea kumuweka Kwenye ramani kama Msanii bora wa kike Kwenye Bongo fleva.

nady akiri video yake ya utupu ilimpa aibu.

mwanadada NaNdy anasema kuwa moja ya vitu vilivyowahi kumnyima amani na kumtia aibu ni ile video yake iliyosambaa ikimuonyesha yeye na Billnass wakiwa faragha na kusambaa sana katika mitandao ya kijamii .

Nandy ambae alikuwa katika mahusiano na msanii mwenzake Billnass  waliingia matatani siku za nyuma baada ya video hiyo kusambaa katika mitandao ya kijaimii kipindi ambacho Nandy alishakaaa sana kuhusu ukaribu wao na hata kusema kuwa hawakuwa na mahusiano yoyote.

hata hivyo  baada ya kusambaa kwa video hiyo wawili ho walitakiwa kuomba msamaha mbele ya umma kwa kosa hilo huku wakionywa na BASATA.

Nandy afunguka swala la kuacha muziki.

Moja ya wanamuziki wanafanya vizuri katika anga za bongo fleva Nandy amefunguka na kusema kuwa pamoja na kwamba amekuwa akifanya vizuri lakini alishawahi kujiwekea malengo katika hilo kuwa ndani ya miaka mitano basi tayari awe amekwisha fanikisha kila alichokuwa anataka kifanikiwe katika muziki.

Nandy anasema kuwa ndoto yake kubwa akiyonayo maishani ni kiwa mfanya biashara mkubwa sana lakini  haweiz kuacha sasa muziki kwa sababu alishasema atafanya muziki kwa mika ami5 na baada ya hapo ndipo ataendelea na biashara zake.

Mimi ndoto zangu ni kuwa mfanyabiashara mkubwa sana na hata wakati naanza kufanya muziki nilijiwekea malengo baada ya miaka mitano niache muziki na niendeleze biashara zangu na mpaka sasa nimeitumia miaka miwili (2016 na 2017) na mwaka 2020 ndiyo nitaacha muziki, Na sio kwamba nitakuwa sitoi ngoma hapana nitakuwa natoa sema kwa mwaka hata mara moja ha show naweza kuwa nafanya mara moja kwa mwaka ili nipate muda mzuri wa kusimamia biashara zangu” Ameyasema Hayo Nandy kuhusu kuachana na Muziki

Nandy Awahasa Wazazi Kupenda Kuhimiza Watoto Kuvaa Vitu vya Asili

Mwanadada Nandy ambae amekuwa moja ya wasanii wanaovaa sana nguo za sili na urembo wa sili kama vitenge na mabangili amefunguka na kusema kuwa kwa upande wake amekuwa aktika mazingira hayo na ndio maana inampa moyo kuendelea kufanya.

Nandy anasema kuwa wazazi wana nafasi kubwa sana ya kuwahimiza watoto wao kupenda vitu vya asili kama watakuwa wakiwakuza katika misingi ya kuvipenda kuliko kuwanunulia vitu tofauti na vile vya asili,

Akitolea mfano wake anasema kuwa tangu akiwa mtoto mama yake amekuwa akivaa mabatiki na vitenge na hata wao wamekuwa wakishonewa nguo hizo na ndio maana amekuwa akiona na kupenda kufanya hivyo.

Mneno hayo ya nandy yanakuja ikiwa ni kuelekea kilele cha tamasha la Urithi Festival linalotegemewa kufanyika mkoani Dodoma mwezi huu.

Mimi napenda sana kuvaa vitu vya asili na ndio maana mmekuwa mkiniona nashona shona,nimekuwa nikiona tangu nikiwa mdogo mamangu amekuwa akitushonea nguo kwaio nimekuwa nakiona na nikakipenda sana.

Nandy Awatolea Povu Wanaomsema Anabebwa Kimuziki.

Mwanadada Nandy amefnguka na kusema kuwa kuna baadhi ya watu wamekuwa wakimtuhumu na kumwambia kuwa amekuwa akibebwa katika muziki na baadhi ya watu na wala sio kipaji chake, Nandy ameonekana kuchukizwa na maneno hayo.

Nandy akiongea na bongo 5 anasema kuwa anashangazwa  sana na  watu wanaongea hivyo  kwa sababu kwa upande wake anajua kabisa kuwa amekuwa akifanya kazi na akitoa ngoma kila mara na nzuri zaidi ni kwamba zimekuwa zikipigwa katika station mbalimbali.

Hayo maneno yao hayanipi tabu yoyote kwa sababu kila siku nasikia kuhusu kubebwa kubebwa lakini nyimbo zangu zimekuwa zikipigwa radioni na zimekuwa zikihit kila kona kwa mfano sasa hivi ninogeshe ina viewers zaidi ya milion 5 kwaio siona kama nabebwa.

Hata hivyo Nandy anasema kuwa haogopi kuongelewa kwa sababu hiyo ni kawaida kwake kama star.

Nandy Awashukia Wanaosema Anabebwa Kwenye Muziki

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Faustina Charles maarufu kama Nandy amewatolea povu zito watu ambao wamekuwa wakimtuhumu Nandy kwa kubebwa Kwenye Muziki.

Nandy amefunguka kuzungumzia kelele ambazo zipo kwenye mitandao ya kijamii kwamba anabebwa kwenye muziki wake na sio kipaji chake ambacho kimemfikisha sehemu aliyofikia.

Kwenye Interview aliyofanya na Bongo 5, Nandy amedai anashangazwa na tuhuma za kubebwa kimuziki Wakati anaimba nyimbo na zinapigwa kila kona  na zinashika chati kama kawaida:

Hayo maneno ya watu hayanipi tabu yoyote kwa sababu each and everyday nasikia kuhusu kubebwa kubebwa lakini nyimbo zangu zinahit redioni na zinapigwa mpaka mikoani na zinatrend Kwenye chati kwa mfano kama sasahivi ‘ninogeshe’ ina viewers milioni 5 kwaiyo suala la kubebwa halipo”.

Lakini pia Nandy amedai yeye kama staa kuongelewa ni jambo la kawaida kwani ukiwa msanii halafu ukaona hakuna hata mtu mmoja anakuongelea basi wewe sio staa.

Tuhuma Za Nandy kubebwa zilianza kutokana na Nandy kuimba nyimbo nyingi za wasanii wa zamani Lakini pia Nandy amewahi kukiri kuandikiwa nyimbo zake nyingi anazoimba.

Nandy Kumuanika Aliyevujisha Video Yake na Billnass.

Kwa muda sasa tangu kulipotokea sakata la video liyokuwa ikimuonyesha Nandy na mpezi wake Billnass wakiwa faragha ambapo baada ya kuvuja na kusambaa sana, mwanadada huyo alionekana kuathirika sana lakini mambo yalikuja kuwa sawa kutokana na kuwaomba msamaha mashabiki na kupewa onyo na TCRA NA BASATA pia,

Sasa mwanadada huyo baada ya ukimya mrefu ameibuka na kusema kuwa muda wote huo alikuwa kimya kutafuata ni anni aliyafeanya kazi ya kusambaa video hiyo aktika mitandao na amefanikiwa kufanya hivuo.

Nandy anasema kuwa sasa hivi atakuwa na amani kwa sababu anataka kurudisha pia heshima yake kwa mashabiki aliokuwa nao kwa sababu kitendo kile kilimuahribia sifa yake kwa mashabiki wake.

Nandy Alamba Dili Nono na Kampuni Ya Mtandao Wa Simu

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vyema na kibao chake cha ‘Ninogeshe’ Faustina Mfinanga maarufu kama Nandy amelamba Dili nono na kampuni ya Halotel.

Nandy amechaguliwa na mtandao wa simu wa Halotel kuwa balozi wao mpya kupiti promotion yao mpya ulioizindua uitwayo, Ninogesha.

Akizungumza katika hafla fupi ya kusaini mkataba na msanii huyo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda amesema kampuni imemchagua Nandy kwa sababu ana uwezo wa kuwa na mchango chanya utakaosaidia kukuza mauzo ya bidhaa na huduma, pamoja na kuimarisha jina la kampuni.

Nandy ni msanii anayekonga nyoyo za mashabiki wake kupitia wimbo wake unaovuma kwa jina la ‘Ninogeshe’ na kumpa umaarufu unamfanya afahamike kwa watu wa rika zote. Unampa umaarufu ambao utasaidia kuiwakilisha vema kampuni ya Halotel“.

Nandy amesema hiyo ni fursa kubwa na ya kipekee kwake kuwa miongoni mwa familia ya kampuni hiyo na kupewa jukumu la kuiwakilisha ipasavyo kwa wateja wake na watanzania kwa ujumla kutokana na huduma bora za mawasiliano inazotoa.

Nandy Aelezea Mfumo wa Familia Anayoitamani.

Mwanadada Nandy amefunguka na kusema kuwa anatamani sana kuwa na familia kubwa na nzuri huku akitaja vigezo vyake vya kuwa na familia hiyo kuwa anataka familia inayomcha Mungu sana na yenye watoto watatu na yenye kujituma kutafuta pesa.

Nandy anasema kuwa anatamani sana kuwa na familia ya kumcha Mungu sana, wenye kutafuta pesa na kupata watoto wasiopungua watoto “kila mmoja anatamani kuwa na familia anayoipanga  mwenyewe kwa uapnde wangu natamani sana kuwa na familia nitakavyopenda na yenye hofu ya mungu, lakini pia ikipendeza nipate watoto wengi. “

Pamoja na kwamba hajasema ni lini ataingia katika ndoa lakini Nandy anaamini kuwa muda wake utafiki na kuingia katika familia na atatiiza malengo yake.

 

Nandy Ashinda Tuzo Nyingine Nchini Kenya.

Mwanadada kutoka Tanzania Nandy ameshida tuzo nchini kenya kutoka Maranatha Awards nchini humo.Tuzo hizo ni tuzo maalum zinazotolewa nchini humo kwa ajili ya wasanii wa injili.

katika tuzo hizo, Nandy ameshinda tuzo hiyo katika kipengele cha Best  Worship Song Cover kupitia wimbo wa Angel benard wa nikumbushe.

Kupitia wimbo huohuo , Angel Benard nae ameshinda tuzo nchini marekani , hivyo hii inaonyesha ni jinsi gani wimbo huo umekuwa na nguvu kubwa.

Nandy Avua Nguo Jukwaani kwa Mzuka wa Mashabiki.

Mwanadada Nandy amejikuta akivua nguoa na kubaki na nguo za ndani baada ya kupanda jukwaani na kuimba nyimbo zilizowapandisha mzuka mashabiki wake na kuanza kumshangilia kwa nguvvu na kujikita akianza kurusha kiatu na kufikia kuvua nguo.

Mambo hayo yametokea alipokuwa akifanya show huko mkoani Tarime maeneo ya Nyamongo ambapo alipoanza kuimba na mashabiki zake kumshangilia kwa mzuka sana ndipo alipojikuta akianza kuvua kitu kimoja na kukirusha na hata baada kuvua nguo ya juu na kubaki na nguo ya ndani.

Hata baada ya kumaliza sho, katika ukurasa wake wa instagram nandy alionyesha jinsi gani alifurahia show hiyo na kuandika kuwa ‘Juhudui huzidi kipaji, asanteni sana watu wa nyamongo”