Nandy Amtupia Lawana Billnass, Ni Baada ya Video Yao Chafu Kuvuja.

Mwanadada Nandy amemtupia lawama mpenzi wake Billnass kwa kuvuja kwa video chafu iliyokuwa ikiwaonyesha wakiwa pamoja faragha, na kuwaomba radhi mashabiki na watu wote waliopatwa na mshtuko kuhusu video hiyo ambayo imesambaa sana ktika mitandao ya kijamii.

Nandy amekubali kuwa ni kweli video hiyo iliuwa ni ya kwake na aliyewahi kuwa mpenzi wake Billnass na waliipiga mwaka 2016 kipindi wapo katika mahusiano lakini anashangaa kuona video hiyo ikiwa imevuja kwa sababu walikubaliana hata mahusiano yao yawe ya siri.

nilikuwa na mahusino na Bilnass 2016, nilikuwa na mahusiano na billnass na tulikubaliana kuwa mahusiano yetu yawe ya siri, sasa silewei kwa sababu gani kaamua kuvujisha ,nimesikitishwa sana , ni video ambayo ilikuwa imeshutiwa kwa snapchat.sasa silewei aliipataje hiyo video kwa sababu mpaka aipate ni mpaka nimrushie kutoka kwangu.Naomba radhi sana familia yangu, kanisani kwangu , mashabiki na serikali yangu kwakweli video imenichefua sana mpaka hapa ninapoongea nimechefuka sana, ila adhabu ya maumivu ninayoyapata  ni kutokana na kumuamini sana mwenzangu.-Aliongea nady alipokuwa akihojiwa na MCL digital.

Sitaki Ugomvi na Mtu: Nandy

Mwanadada mwenye wimbo uliovuma sana kwa hivi karibuni, Nandy amefunguka na kusema kuwa kuna watu wamekuwa wakimuingilia sana katika mabo yake lakini hapendi kuingi katika bifu na msanii mwenzake yoyote.

Mwanadada huyo ameongea hayo alipokuwa akiongea na Clouds  Tv kuwa yeye sio mtu mwenye asili ya ugomvi hivyo mara zote watu wamekuwa wakimuingilia katika mambo yake na amekuwa akikaa kimya

Mimi siku zote huwa sio mgimvi na mara kwa mara nimekuwa nikijiepousha kuingia katika ugomvi na watu.huwa napuuzia na kuwaonyesha watu kuwa wanachokifanya ni cha kijinga, huwa namuonyesha tu kuwa sifatilii kile anachokifanya au kuwa nimeshtuka na matendo yake.

Hivi karibuni kumekuwa na maneno yanayosambaa kuhusu yeye huku wengine wakimhukumu kutoka kimapenzi na bosi wake.

Kivuruge Ya Nandy Ilirudiwa Mara ya Pili.

Wimbo wa kivurge umekuwa ukifanya vizuri kila kona kwa audio na hata baadae baada ya kutolewa kwa video yake.Lakini inasemekana kuwa wimbo huo ulirudia mara ya pili na Nandy na kuufanyia haki zaidi kuliko mara ya kwanza.

Akijibu kuusu swala hilo, alikuwa mlimiki wa wimbo huo ambae pia ni msanii akijulikana kama Jay Melody anaetamba na wimbo wake wa Goroka amesema kuwa ni kweli wimbo huo aliuimba yeye lakini nany aliupenda zaidi hivyo akataka kuuchukua na ndipo waliofanya makubaliano na kuuchukua.

Nandy alinifuata baada ya kusikia nimeutoa na akaomba kuurudia na ndipo nilipokutana na uongozi wake na tukaweka makubaliano mazuri nikampatia, mimi ndie nilieutunga na hakuna hata kipande kilichobadilika-Aliongea Jay Melody.

Alpotafutwa nandy kuthibitisha hilo nae alikubali na kusema kweli aliupenda wimbo huo na kufanya makubaliana na aliyekuwa anaumiliki.

Ni kweli wimbo huo uliimbwa na jay melody lakini kuna makubaliano tuliyafikia ndipo nikaurudia na mimi.

 

Ruby Ajisifu Kuwa Nandy Mamuwezi Katika Muziki

Ruby ni moja ya wasanii waliokuja na kufanya vizuri sana katika tasnia ya muziki lakini ndoto zake zilizimika baada ya kukosana na menejimenti yake na kushindwa kuendelea na muziki kwa kipindi cha muda mrefu kidogo , lakini moja ya wasanii wa kike wenye kipaji cha kuimba na anaweza kufanya vizuri kama atapewa nafasi nyingine ya kufanya muziki.

Hivi karibuni msanii Ruby amekuja na nyimbo yake mpya iliyokwenda kwa jina la ‘are  you ready’, ambayo ni ya kwanza tangu kukaa kwake kimya kwa kipindi kirefu kidogo.

Aliipoulizwa kuhusu kimya chake cha muda mrefu Ruby aliibu kuwa sababu  moja wapo ya kukaa kimya ni kumpa nafasi msanii mwenzie Nandy ili aweze kujulikana katika muziki kwa sababu endapo na yeye angeendelea kufanya kazi basi Nandy asingeweza kufanya vizuri katika muziki kama ilivyo sasa.

Ruby anasema kuwa ujio wa Nandy haukuksumbua sana kwa sababu ana amini kuwa Nandy ni msanii mzuri lakini hakutaka kuanza kujishindanisha nae,lakini pia anasema kuwa watu wengi wamekuwa wakisema kuwa ujio  wa Nandy ulikuwa ni wa kuziba pengo aliloliacha lakini ukweli ni kwamba yeye na Nandy wote wanafanya muziki wa aina moja lakini bado kuna tofauti kubwa kati yao hasa upande wa TONE  na SCALES zao katika muziki wanaoimba.

Hata hivyo Ruby ameomba kutokushindwanishwa na mtu yoote kwa sababu hapendi kushindana na mtu katikamaisha yake zaidi ya yeye mwenyewe tu, na hata kama wanafanya muziki wa aina moja  haimaanishi kuwa wanafanana hata kidogo.

Ruby anatangaza kurudi tena katika muziki na kusema kuwa wakati yupo kimya alikuwa akiumia sana pale alipokuwa akiona mashabiki zake wanalalamika na kumuomba arudi na kwamba walikuwa wakim-miss sana.

Nandy Amwaga Povu Baada ya Habari Kusambaa Kuwa Ameonekana Serengeti na Boss Ruge

Mwanamuziki wa Bongo fleva Nandy anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘kivuruge’ amejikuta katika wakati mgumu baada ya habari kusambaa mtandaoni kuwa ameonekana mbuga za wanyama Serengeti na Ruge.

Siku ya Jana habari zilianza kuenea mtandaoni msanii huyo ameonekana akiwa zero distance na mkurugenzi huyo wa Clouds Fm Ruge Mutahaba ambaye pia ni boss wake pale THT. Baadhi ya watu wanaofanya kazi huko Serengeti walituma ujumbe huu kuthibitisha kumuona Nandy na Boss Ruge:

Mwanamuziki Nandy ni kweli kabisa yupo Serengeti na Ruge nashangaa anavyobisha tena wapo Serengeti Serena waliingua Jumanne. Wapo room namba nane na akibisha tuseme hadi nguo alizovaa na alivyosuka mnafiki Mkubwa tena waliingia hapa mida ya saa nne”.

Baada ya habari hizo kuenea Kama moto wa kifuu Nandy kupitua ukurasa wake wa Instagram alikataa tuhuma hizo na kutoa povu Kali:

Mtu akifanya mziki wake kwa amani bila drama kuna watu wanakuwa hawatosheki kabisa….Hivi mimi ni kichaa mpaka kujiachia kama huyo msambaza habari anavyodai! Kwani suza kitoto. Msu force mambola la watu kusema natoka na boss wangu nalijua leo au ni geni mpaka nijiachie kwenda naye macamp au maclub na kupanda ndege kiufree kama mnavyodai?? Embu tuwe na pliiz kwaiyo mimi nimekuw wa kuja kiasi hicho na mshamba kiasi ya kwamba nikashindwa kufunga hata ushungi basi hata tungepishana kusafiri yeye akatangulia mimi nikafuata nyuma au mnadhani mimi mtoto sana tafadhali tupeane heshima kuna watu hatutaki drama za kitoto na msi force mambo”.

 

Dkt.Tulia Akson Ashindwa Kuficha Hisia Zake Kwa Kivuruge

Naibu spika wa  bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Akson ameshindwa kuficha hisia zake kwa  kuonyesha kuwa wimbo mpya wa Nandy wa kivuruge umekuwa gumzo mtaani na yeye ameupenda na kuupokea vizuri wimbo huo.

Dkt.Tulia amemsifia Nandy na kumwambia kuwa jitihada alizonazo katika muziki atafika mbali ukizingatia yeye ni msanii mchanga lakini ameweza kufanya muziki vizuri na watu wakamkubali.dkt tulia bado amemsifia nandy na kumwambia kuwa amefanya vizuri katika wimbo wa kivuruge kwa kitendo cha kuelezea malalamiko ya mwanamke anaeteswa na  mwanaume.

Kwa jitihahada hizi ninatumaini utrafika mbali sana, uvumilivu na nidhamu ni vitu vya kuzingatia sana kwenda  kwenye mafanikio yako.Wimbo wa kivuruge tumeupokea kwa mikono miwili. –  Aliandika dkt tulia katika ukurasa wake wa instagram.

Wimbo wa kivuruge ulitoka kama zawadi kwa mashabiki wa Nandy baada ya kushindwa tuzo huko nchini Nigeria, ambapo ulianza na audio na baadae kufuatwa na video.Ikiwa leo ni siku ya tisa tangu kutoka kwa video hiyo ilishatizamwa zaidi ya mara  600,000.

Nandy: Bora Nitembee na Bill Nas Kuliko Dogo Janja

Mwanamuziki wa Bongo fleva nchini Nandy anayefanya vizuri kwa hivi sasa na wimbo wake wa ‘Kivuruge’ amefunguka na kudai kuwa yupo radhi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii mwenzie Bill Nas kuliko Dogo Janja.

Kutokana na urembo wake na mafanikio yake katika mziki huu wa Bongo fleva mashabiki wengi wamekuwa wakitaka kujua ni nani ambaye ana uhusiano na Nandy kwani amekuwa akificha sana nani ni mpenzi wake.

Kuna habari zilizosambaa sana kwa muda mrefu sasa kuwa Nandy ana uhusiano wa kimapenzi na msanii mwenzake ambaye na yeye anafanya vizuri Bill Nas lakini mara kwa mara wamekuwa wote wawili wakikataa tuhuma hizo huku wakisisitiza kuwa nimarafiki wa kawaida tu.

Lakini siku za hivi karibuni pia habari zilisambaa kuwa Nandy ana uhusiano pia na msanii mwingine wa Bongo fleva Dogo Janja ambaye ameimba naye nyimbo siku za nyuma kidogo.

Kwenye mahojiano na LilOmmy Nandy amefunguka na kudai kuwa ni bora awe na Bill Nas kuliko na Dogo Janja;

Hapana wimbo wangu wa Kivuruge sijamuimbia Dogo Janja alafu isitoshe hii nyimvo sijatunga mimi wala sijaiandika kuna mtu aliiandika nikaisikia nikaipenda ndio nikainunua lakini hainihusu mimi alafu isitoshe Dogo Janja ni rafiki yangu yaani hata sijawahi kumfikiria kiivyo yaani bora hata Billnas naweza nikakaa nikamuamgalia nikaona kwa mbali nikaona kama  ninaweza kutembea naye Lakini Dogo janja siwezi kupoteza muda wangu hata kumfikiria”.

 

Nandy: Fedha Sio Kigezo Cha Mimi Kuwa na Uhusiano na Mwanaume

Mwanamuziki wa Bongo fleva Faustina Charles ‘Nandy’ anayetamba na wimbo wake wa ‘kivuruge’ amefunguka na kudai kuwa ili yeye kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume sio lazima awe tajiri.

Wasanii wengi wa kike nchini wamewekwa kwenye kundi la wapenda pesa yaani ili umpate staa yoyote wa kike nchini ni lazima use na mkwanja mrefu. Wengi huita mapedeshee au madanga au sponsor ambapo baadhi baadhi ya wasanii wa like iwe ni wa Bongo movie au bingo fleva wanajulikana kwa kuwa na uhusiano na watu wanaojiweza kifedha tu.

Nandy alipofanya mahojiano na gazeti la Risasi vibes aliulizwa endapo kasumba hiyo mastaa wa kike kupenda wanaume wenye hela ina ukweli wowote alidai kuwa anachopenda yeye ni mwanaume mcha Mungu na mchapakazi haijalidhi kama hiyo kazi inamuingizia kipato kikubwa au la;

Kusema ukweli fedha peke yake sio kigezo cha mwanaume kuwa na mimi, muhimu mtu awe na hofu ya Mungu asiwe wa kujibweteka awe ni mtu wa kujishughulisha kwakazi yoyote ile tutapambana wote kutafuta maisha hadi mambo yatakapokuwa vizuri na kujivunia kwa pamoja kama wapenzi”.

Ingawa Nandy amekiri kuwa hawezi kuzungumza kwa niaba ya wanawake wote kwenye sanaa kuhusu nini matakwa yao lakini ameweka wazi kuwa wapo wanawake wa hivyo sehemu yoyote.

Nandy amekuwa katika vichwa vya habari kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki mwenzake Billnass ingawa wote wawili wamendelea kukana na kudai kuwa ni marafiki wa kawaida tu.

Nandy:Niliongea Kiswahili Kuoyesha Uzalendo,Naongea Kingereza Kupita Maelezo

Kumekuwa na maneno ya kumponda mwanadada Nandy anaefanya vizuri katika nyimbo zake kuwa alishindwa kuongea kiingerza baada ya kuhojiwa kwa lugha hiyo  alipokuwa nchini Nigeria wiki iliyopita ambapo aliweza kufanya shoo katika utoaji wa tuzo za AFRIMA na alibahatika kupata tuzo pia.Nandy mwenyewe ameamua kufunguka na kuwaelezea watu kuwa kitendo chake cha yeye kuongea kiswahili katika utoaji wa tuzo hizo alifanya makusudi na sio kwamba hajui kingerza kama wanavyosema.

Nandy anasema kuwa alifanya hivyo ili kuonyesha uzalendo wa nchi yake, lakini pia alifanya hivyo ili watu waweze kuvutiwa na kuhoji  na kutafuta ni nini alichokiongea. Lakini pia hata yule aliyemuhoji alitumia lugha yake kwanza ndio akaongea na kiingerza kwaio yeye kuongea  kiswahili  haikuwa mbaya  kwa sababu alitaka kukitangaza na kuwafanya watu wake wanaomsapoti  pia waelewe.

Nilihitaji watanzania waliokuwa wananianglia kwa sabau ilikuwa ikionyeshwa afrika nzima.wanielewe zaidi kwaio nilileta uzalendo kwanza.Lakini pia nilitaka lugha yetu isambae zaidi kwa sabau watu waliuliza hivi ameongea nini pale, kwaio ataingia ata-google na atatafuta niliongea nini kuliko ningeongea kiingerza ningeahisisha.-Alifunguka Nandy

Nilitaka kuwashukuru ma-fans wangu wote, na nina amini walielewa kwa sabau nilivyomaliza pale walipiga makofi,na pia hata nilivyoongea kiswahili yule dada pale aliniambi ai want you toi teach me swahili, so nikasema yes kumbe umependa eeh, yes i will. -Aliongeza Nandy.

Wasanii wengi wamekuwa wakitia aibu wanapokwenda katika nchi za ugenini kwa kutaka kuongea kiingereza  wakati mwingine hata kiingerza kinakuwa kigumu kwao kuongea, Nandy anaweza kuwa ni moja ya wasanii walioonyesha mfano mzuri kwa kutaka kutangaza utamaduni wao nje ya nchi kwa kuogea lugha yake ya taifa.

Akiendelea kuongelea experience aliyoipta kutoka katika tuzo hizo anasema kuwa imemfanya kuwa huru na ujasiri kuwa kumbe anapendwa na watu wengi Afrika, lakini pia imemuongezea faida kwasababu amekutana na wasanii mbalimbali na kupanga kufanya nao kolabo, na katika hao wasanii wawili aliowataja ni pamoja na Wizkid na Yemi Alade.

Kumalizia Nandy alisema kwa kujigamba kuwa anaongea kiingerza kupita maelezo.

Nandy Na Alikiba Kutwaa Tuzo Za AFRIMA Nigeria.

Usiku wa kuamkia leo Tanzania iliibuka kidedea tena ikiwakilishwa na wasanii wawili Alikiba na Nandy ambao wameweza kuiwakilisha vyema Tanzania katika mashindano ya tuzo za musiki zilizokuwa zikifanyika nchini Nigeria zinazojulikana kama  ALL AFRICA MUSIC AWARDS 2017 (AFRIMA).

Staa wa hit song ya wasikudanganye Nandy ameshinda tuzo moja ya  msanii bora wa kike kwa upande wa Afrika Mashariki huku msanii wa kiume kutoka Tanzania tena Alikiba akiwa ametwaa tuzo mbili yaani katika kipengele cha  Best Artist or Group  in African RnB  and Soul  akiwa na rapper MI na  kolabo bora ya africa  ikiwa ni wimbo wa Aje.

kutoka katika ukurasa wa AFRIMA

Lakini pia nandy ambae alikuwa huko siku chache kabla alionekana kuwa mwenye furaha huku akishukuru kwa mapokezi makubwa aliyoyakuta kitu ambacho hakutegemea kama na yeye anaweza kuwa na fanbase kubwa mpaka nchini tofauti na Tanzania ambapo alitegemewa kuperfom katika jukwaa hilo.

Msanii Nandy akionesha tuzo yake baada ya kuipokea

Ray C Alinidhalilisha Sana Kwa Maneno Yake- Nandy

Mwanamuziki kutoka Jumba la sanaa la Vipaji THT, Nandy ameibuka na kudai kuwa alivunjika moyo kwa maneno ya udhalilishaji aliyoambiwa na msanii mwenzake Rehema Chalamila au maarufu kama Ray C.

Wiki chache zilizopita wasanii hawa wawili waliingia katika vita kali ya maneno mtandaoni baada ya  Nandy kutumia/ kuimba nyimbo za Ray C katika tamasha la Fiesta ambapo hakulipwa kwenda kuimba. Ray C alimjia juu Nandy na kumwambia asitumie nyimbo zake kuingiza pesa kwani na yeye ni mwanamuziki hivyo anaweza kuimba nyimbo zake mwenyewe, jambo ambalo halikumpendeza Nandy ambaye alidai kuwa Ray C alikuwa na taarifa kuwa ataimba nyimbo zake kwani walikuwa wote THT kwenye mazoezi.

Nandy alipohojiwa na Dizzim Online, alisisitiza ya kuwa maneno yale aliyoyaongea mtandaoni yalimdhalilisha sana kama msanii

Sikuwahi kufikiria kama Ray C angeweza kupaniki kama alivyo paniki kwani hata mimi alinishangaza, baada ya yeye kuandika vile kwenye instagram, management yangu ilinipigia ili initulize kwa sababu kusema ukweli nilipaniki na nilijisikia vibaya sana pale watu walivyo nifata na kuanza kunitukana kwamba niimbe vinyimbo vyangu viwili na mambo mengine kitu kilichonidhalilisha sana pia kwa sababu nilivyoimba ile nyimbo sikuimba kwa ubaya ilikuwa ni kwa nia nzuri tu ya kuburudisha mashabiki zangu”.

Tangu ishu hii itokee Nandy amekuwa mtu wa kuizungumzia sana akionyesha kuwa hakufurahishwa hata kidogo tofauti na Ray C ambaye hajawahi kuongelea suala hili hata mara moja

Mnaukosea Heshima Mziki Wangu Mkinifananisha na Ruby -Nandy

Mwanamuziki wa bongo fleva, Nandy amefunguka na kudai kuwa amechoshwa na kufananishwa na mwanamuziki mwenzie Ruby.

Kwa muda mrefu sasa Ruby na Nandy wamekuwa kwenye aina ya ushindani ambao unatokana na watu kuwafananisha kutokana na aina ya muziki wanaofanya.

Kwenye mahojiano na Extra Showbiz, Nandy amesema kwa muda mrefu mashabiki wake wamekuwa wakimfananisha na mwanamuziki mwenzake Ruby hivyo amewataka wanao mfananisha na Ruby waache mara moja kwani miziki yao Ina ladha zilizo tofauti sana pia.

Namheshimu Ruby ni mwanamuziki mzuri, lakini kumfananisha na mimi ni kunikosea heshima mziki wangu ladha ya mziki wangu ni tofauti kabisa na Ruby kutokana na utofauti wangu wa mziki ninaofanya na pia kama unaufahamu mziki wa Ruby anaofanya utagundua ni mziki tofauti”.

Alisema Nandy ambaye hakufafanua kwa undani zaidi alimaanisha nini kwa kusema hayo. Ingawa kila mmoja amesema kuwa hana bifu na mwenzake lakini inasemekana ni kama paka na chui yaani hawaivi katika chungu kimoja hata kidogo.

Ruby: Nimechoka Kusikia Habari za Nandy Kila Siku

Msanii wa Bongo fleva Ruby amechoshwa na kile alichodai ni kuulizwa habari za Nandy kila siku anapohojiwa.

Ruby na Mwanamuziki mwenziye Nandy wanasemekana kuwa wana bifu la chinichini kwa kile kinachodaiwa wamegombania bwana, ingawa wawili hao wameziki kukana kuwa kila mmoja hana tatizo na mwenziye lakini habari chini ya kapeti zinadai kuwa wawili hao ni panya na paka (hawapatani).

Ruby alifunguka hayo kwenye kwenye mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni na stesheni moja ya redio na kudai kuwa amechoshwa na watangazaji wa media mbali mbali badala ya kumuuliza maswali ya maana kila siku wamekalia kumuuliza habari za Nandy ambazo kwa sasa zimeshamchosha na ni kitu kinachotengeneza ugomvi baina yao hata kama hakuna ugomvi.

Nachukia sana swali la kufananishwa na Nandy Kwa sababu honestly I am tired of that question! ni kama vile watangazaji wanashindwa ni maswali gani ya kuuliza , maswali ni yale yale nimeshayajibu sana ! I love Nandy she is a good artist, she is a good singer but don’t ask me too much questions about her, it’s like mnataka kutengeneza ugomvi sasa nashindwa kuelewa hata watu wa media mnatengeneza ugomvi sasa kwasababu swali lilishajibiwa mara Mia moja sasa kwa nini lijirudie kila siku?”.

Nandy na yeye alipoulizwa mara ya mwisho kama ana ugomvi na Ruby alikana kata kata ingawa wambea wa mjini wanadai eti kuwa wawili hao walikuwa marafiki walipokuwa wote THT lakini Ruby alipoondoka tu Nandy akajiweka kwa jamaa/ sponsor wa Ruby hivyo kusababisha ugomvi (habari hazijathibitishwa)

Nimejaribu Kumtumia Meseji Lakini Hajajibu, Nandy Aongelea Nia Yake Ya Kumuomba Msamaha Ray C

Mwanamuziki wa Bongo fleva mrembo Nandy ameongelea nia yake ya kutaka kumtafuta Ray C ili waweze kumaliza tofauti zao licha ya Ray C kumuwekea ugumu.

Mwanzoni mwa wiki hii Ray C hakumkopesha Nandy kwani alimjia juu kwa kitendo chake cha kuimba nyimbo zake bila ruhusa yake kwenye tamasha linaloendelea la fiesta. Ray C aliweka wazi kukerwa na kitendo hicho hasa kwa sababu yeye mwenye nyimbo hakualikwa kwenda kushiriki tamasha hilo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Millard Ayo, Nandy amefunguka ya moyoni kuhusu ishu hiyo name meseji aliyomtumia Rayc lakini hajaijibu:

Kiufupi ni kwamba tu niliposti clip ya nyimbo ya Mez B ambayo amemshirikisha dada angu Ray C ambayo tuliimba mimi na Ben pol na tulifanya hivyo kwasababu ilikuwa ni season ya kukumbuka malegend wa bongo fleva kwaiyo haikua kwa nia mbaya sasa nilishangaa kwa nini alichukulia vibaya mimi kuimba ile nyimbo yake hadi kupelekea mashabiki zake kunitukana sana lakini sikuishia hapo niliandika kama kumuelewesha na kumtaka radhi kwenye Instagram pia nilimwandikia meseji ya kawaida private nikamuuliza kwa nini kaamua kunifanyia hivi? Na ni siku gani nilishawahi kukutana naye sikumsalimia? Nikamwambia mbona mi nilikusapoti kukutangazia nyimbo yako ilipotoka lakini hata asante hukutoa! Lakini nilikuja kugundua hata mwaka jana nilivyoimba nyimbo yake hakupenda ingawa alikuwepo kwenye mazoezi na hata mashairi mengine mwenyewe alinisaidia”.

Nandy alimalizia kwa kudai kuwa amemsamehe Ray C na atachukua ushauri wake wa kuimba nyimbo zake mwenyewe kwani hata fiesta kupata kazi ni kutokana na watu kuvutiwa na  nyimbo zake mwenyewe na siyo nyimbo za Ray C au msanii mwingine yeyote.

Sitaki Unafki Amesema Ray C Baada Ya Nandy Kuimba Nyimbo Zake Bila Ruhusa

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva Rehema Chalamila amemjia juu msanii mwenzake Nandy baada ya kutumia nyimbo zake bila ruhusa.

Ray c alionekana kukasirishwa na kitendo cha Nandy kutumia nyimbo zake kwenye tamasha linaloendelea la Fiesta licha ya yeye kutokualikwa kushiriki tamasha hilo. Ray C aliyepumzika kimuziki kwa miaka mingi kutokana na kuingia kwenye utumiaji wa madawa ya kulevya amerudi na kibao chake ‘Unanimaliza’ kinachofanya vizuri hivi sasa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ray C alimfungukia Nandy yafuatayo:

Jamani hii tabia sio nzuri kabisaa! Sijafa bado!  Kama mnaona umuhimu wa sauti yangu kwenye shoo zenu muwe mnaniitaga basi! Sina Kansa ya koo ya kushindwa kuziimba hizo nyimbo Nandy hii ni Mara ya mwisho ukipanda Fanya kazi zako! Hii ni mara ya pili ujue, Mashabiki zangu hamuwatendei haki ujue! I don’t like it sipendi, Maana hata tukigongana salamu saa nyingine hamna kwaiyo sitaki mazoea! Niliimba tusitafutiane visa tena pisha sio tena presha, sitaki unafki na wewe Tena, mna nini lakini? Kila mtu apate riziki kwa jasho lake”.

Baada ya kuona povu la Ray c na mashabiki kumjia juu Nandy kwa kitendo alichofanya Nandy aliomba radhi;

Dada angu Ray c, kama wote tulivyosema kabla ya kuimba juzi, mimi ni mmoja wa wasanii wanaokukubali kama msanii uliyetufungulia njia ya mziki wetu ulipo, sitaacha kukuheshimu na kukukubali  kwa hilo  wewe na wengine wengi tu. Siamini kukusifia na kukuenzi ni lazima uwe umekufa hapana nafanya jambo hili zuri kwa moyo wangu mzuri Kama ulivyomuenzi Mama mwanahela kwa nyimbo zake. Heshima yangu kimuziki kwako itabaki siku zote kama nilivyoimba nyimbo za wasanii Kama king kiki, mwasiti, Yemi Alade na Recho”.

Ray C alionekana kukerwa na kitendo cha Nandy kulipwa kushiriki tamasha la fiesta na kutumia nyimbo zake wakati yeye mwenye nyimbo hajalipwa kushiriki tamasha hata moja.

Billnas -“Nandy Ana Sifa Zaidi Ya 60% Za Mwanamke Wa Kuoa”

Ikiwa ni  muda sasa tangu kuwepo kwa  tetesi za wasanii wa Bongo Fleva Nandy na Billnass kusemekana kuwa wapo katika mahusiano ya kimapenzi, Billnass nae ameamua kusema yaliyopo moyoni kuhusu mrembo huyo ambae amekuwa akifanya vizuri katika muziki wa Bongo Fleva.

Msanii huyo wa kiume alipokuwa katika mahojiano na BongoSwaggz alisema kuwa katika mipango yake ya kimaisha kwa sasa bado hana mpango wa kuoa ingawa atategemea kuoa hapo baadae, lakini bado alisema kuwa hata muda wa yeye kuoa ukifika bado kuna vigezo ambavyo anavizingatia hivyo muda ukifika laziamataangalia vile vigezo vya kumfanya aoe.

Billnass ambae amekuwa akifanya vizuri katika game la muziki kwa muda mrefu sasa huku nyimbo zake nyimbo zake karibia zote zikipokelewa vizuri na mashabiki,kwa sasa Billnass anatamba na vibao vyake vya  ‘mazoea’ na ‘sina jambo’ ambayo imetolewa hivi karibuni.”sijakaa nikafikiria  kwa sababu na mimi nina vigezo vyangu  ambavyo nataka , najua namtaka  .Najua namtaka mwanamke wa aina gani .Kwanza swala la kuoa kwangu linapita mbali,sio kwamba ninafikiria sana” ameongea Bilinass

Hata hivyo alipoulizwa kuhusu msanii  mwenzie wa kike wa Bongo Fleva  ambae kwa muda sasa kumekuwa na tetesi kuwa wapo katika mahusiano naye na wamekuwa wakionekana baadhi ya sehemu pamoja msanii Billnass anasema kuwa Nandy ni mmoja wa wanawake anaowapa zaidi ya 60% kwamba anasifa na vigezo ambae yeye anavihitaji  kwa mwanamke wa kuoa.

Nandy ni mwanadada ambae anafanya vizuri sana kwa sasa katika game akiwa ni msanii chipukizi aliechukua nafasi kubwa sana hasa mwaka 2016, lakini bado anaendelea kufanya vizuri kutokana na nyimbo zake kupendwa na mashabiki pia,Nandy kwa muda sasa amekuwa  akifanya vizuri na nyimbo zake kama ‘nagusagusa’ , ‘one day ‘na huo mpya wa ‘wasikudanganye’,pia amepata bahati ya kuwepo katika tamasha la Cokestudio kwa mwaka 2017.Lakini pia Nandy ni mjasiriamali ambae ana Lebel yake ya ushonaji wa nguo inayojulikana kama Nandy African Print. Kwa sifa za kujituma na kufanya kazi inawezekani ndipo aslimia 60 ya billnass inapokuja kwa nandy.