Nandy afungukia bifu lake na Ruby

Msanii wa Bongo fleva, Faustina Charles maarufu kama Nandy amesema japo watu wengi wamekuwa wakihoji kuhusu ukaribu wake na msanii wa zamani wa zao la Jumba la kuibua vipaji la THT (Tanzania House of Talent), Ruby kwa madai kuwa kwa sasa hawapikiki chungu kimoja kutokana na ushindani uliopo baina yao, ishu ambayo ameikataa na sio kweli kwani hana bifu na mwanadada huyo.
Kwenye mahojiano aliyofanya hivi karibuni alisema anawashangaa wanavyosema hapatani na Ruby kwa madai kuwa anahukiwa kwa sababu amemfunika mwenzake kimuziki

“Ukiniuliza mimi na Ruby nani anaimba vizuri, nitakujibu wote, yeye ana muziki wake nami nina muziki wangu sina ugomvi wala mazoea naye ila tukikutana tunasalimiana tu kama washkaji”,

Kumekuwa na tetesi mbalimbali za kuwepo kwa bifu kati ya warembo hawa wawili kutokana na ufanano wa muziki wanaofanya japo wamekuwa wakikana kwamba hawana tatizo na ni washkaji tu.

Aliyekuwa mpenzi wa Nandy afunguka kuhusu uhusiano wao wa sasa

Nandy kwa kweli ni mwanamke ambaye ameumbwa akaumbika. Kwa sababu hii ni wengi ambao wanatamani kuwa na uhusiano wa kimapenzi na yeye ila kwa hivi sasa mrembo huyo ametulia na kufocus kwenye muziki wake.

Hata hivyo aliyekuwa mpenzi wake hapo mbeleni Emmanuel Mathias ambaye anajulikana Kama MC Pilipili alifunguka kuelezea uhusiano wao wa sasa ni wa aina gani.

Akizungumza na Bongo 5 mchekeshaji huyo alidai kuwa bado anawasiliana na Nandy kuonyesha kuwa ingawa wameachana, bado wawili hao ni marafiki. Alisema,

“Mimi na Nandy bado tuna wasiliana vizuri tu, nimerudi kutoka Marekani nimemletea zawadi ya Perfume, hata hivyo yeye yupo Kenya amenicheki kunijulisha kuwa yupo huko na ninaona picha anazopost akiwa huko, unajua mimi na Nandy tumeachana sio kwa ubaya, ila tulifanya hivyo kwa sababu Nandy alikuwa anataka afanye kazi zake kwa uhuru zaidi,”

Aliongeza kuwa

” Kuachana na Nandy hapakuwa na kosa, sikutaka kumpa stress (mawazo)ni makubaliano yetu yalikuwa ni hayo, sio kwa ubaya ni kwa wema kabisa. Sikutaka kuzima ndoto zake kwani ningeshindwa kuwa mume wake ningekuwa nimezima ndoto zake za kufika hapo alipo.”

Nandy afutilia mbali fununu kuwa amekosana na Dully Sykes

Nandy ambaye ni msanii mpya kutoka Bongo ameanza kuwapa wengi wasiwasi kwani anaonekana kuwa anatalanta ambayo itampa umaarufu Afrika Mashariki.

Hata hivyo hapo awali ilikuwa inasemakana kuwa Nandy na Dully Sykes hawakuwa wanasikizana lakini akizungumza hivi karibuni kupitia Planet Bongo ya EA Radio Nandy alisema,

Nandy
Nandy

“Yupo sana proud na mimi kila tukikutana huwa ananisisitiza kuwa na heshima, kusikiliza wakubwa walionitangulia, kufanya kazi kwa bidii kwa sababu hustling yangu aliiona toka way back na ndoto zangu anazijua nyingi sana,”

Aliendelea kwa kuzungumzia issue ambayo mashabiki wengi wanadai kuwa anajaribu kuwa Kama Ruby ingawa alisema,

“Kwa hiyo kaniambia ndoto zako zimetimia, so usiachia hiyo chance kwako kwa kufanya lolote baya.”