Nay wa mitego ;-Natamani kumuona Diamond Msibani.

Msanii Nay wa Mitego ambae pia alikuwa moja ya watu waliofika katika msiba wa Ruge amefunguka na kusema kuwa amekuwa akitamani sana kumuona Diamond Platinmz katika msiba wa bwana Ruge mutahaba lakini anashangaa kwanini msanii huyo hatokei.

Akiongea na waandishi wa habari, Nay wa mitego  anasem “Duniani Tunapita tu, leo hatunaye Bosi Ruge , kiukweli natamani sana kumuona Diamond hapa msibani, muda bado lakini tusubiri labda tutamuona”

Diamond amekuwa moja ya wasanii walioshangaza watu wengi hasa kutokana na ukweli kuwa hakuna alieyetegemea kutokumuona msibani ukizingatia kuwa hata yeye alipita mikononi mwa Ruge hata kama wawili hao wanasemwa kuwa na mfarakano hapo nyuma.

 

Nay wa Mitego Kugombea Ubunge 2020

Msanii Nay wa mitego amefunguk akushusu tetesi zake za kutaka kugombea ubunge mwaka 2020  kama amabvyo taaarifa hzio zimekuwa zikisamba katika mitandao ya kijamii kisa kuwa karibu na watu wake mitaani, huku baadhi ya watu wakisema kuwa kufanya  hivyo ni kujiwekakaribu na wananchi ilikuweka ku-win  mwaka 2020.

Hata hivyo nay wa mitego amefunguka na kukataa swala hilo huku akisema kuwa hawezi kufanya hivyo kwa sababu anaona kabisa kuwa yeye hawezi siasa ya tanzania.

Nay wa Mitego anasema kuwa kugombea ubunge hatoweza kwa sababu siasa ya tanzania imejaa uongo mwingi sana na hana haja ya kukaa na kudanganya wananchi wake pia.

Hata hivyo nay wa mitego ambae aliwahi kusimama jukwaani miaka iliyopita kunadi wagombea upande wa upinzani anasema kuwa amekuwa nandoto ya kuwa rais lakini rais asiyekuwa na mambo mengi zaidi ya kufanya vitendo tu na kunyoosha mambo kama anavyofanya sasa katika sanaa.

Sitamani Kuona Mtoto Wangu Akiimba Muziki :-Nay wa Mitego

Msanii Nay wa mitego amefunguka na kusema kuwa hatamani kuona mtoto wake hata mmoja akijiingiza katika swala la muziki kwa sababu hataki yale aliyoyapitia yeye katika muziki yawapate watoto wake pia.

Nay anasema kuwa ingawa hatoweza kukataa kama mtoto wake yoyote atajiingiza katika muziki  hivyo atamuunga mkono tu lakini hapendi iwe hivyo.

Natamani kuona siku moja wanangu wakipambana na maisha yao, wanakuwa na maisha na majina makubwa, ingawa ikitokea mmoja akijiingiza katika muziki ntamuunga mkono tu ingawa sitamani kuona hata mmoja wao akiijiingiza katika muziki.Na kwa sababu ya historia yangu sitamani mwanangu aje kuwa mwanamuziki.

Nay wa mitego ana watoto wawili wa kike na wa kiume.

 

Dudubaya Amtolea Povu Zito Nay Wa Mitego

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva nchini Godfrey Tumaini maarufu kama Dudubaya ameibuka na kumtolea Povu zito msanii mwenzake Nay wa Mitego.

Dudubaya amerudi kwa kasi ya ajabu kwenye headlines Baada ya kuwa kimya kwa miaka mingi tangu alipoacha kufanya muziki miaka michache iliyopita lakini tangu arudi kwenye ramani na Wasafi Festival Dudubaya amekuwa akitrend Sana.

Dudubaya ameibuka na kumjia juu msanii mwenzake Nay wa Mitego ambaye Hivi karibuni ametajwa kuwa na bifu na msanii mwenzake Diamond Platnumz ambaye hapo nyuma alikuwa mshkaji Wake pia.

Baada ya Nay wa Mitego kuwaponda wasanii wa Wasafi, Dudubaya amemtolea Povu hilo Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari:

Unamuona msanii kama Nay wa Mitego anasema wit wasanii wa Wasafi hawana amsha amsha hivi ana akili timamu? Nay wa Mitego alitumwa na Clouds kuandika wimbo wamepanda wameshuka kunitukana mimi na P-funk   Anawatukana malegendary waliozaa Bongo fleva”.

Lakini pia Dudubaya aliendelea kumtolea maneno Nay wa Mitego ikiwemo kudai kuwa amebuma na muziki wake umebuma:

Nilimwambia mdogo wangu Nay wa mitego siku zako zinakuja na chamoto utakiona, cha moto anakiona sasa amegombana na T. touch na sasa kila akitoa nyimbo inabuma na wale waliomwambia tunga wimbo uwaponde wakina Dudubaya siku hizi hawapigi nyimbo zake”.

 

Madongo ya Nay wa Mitego Yawaacha Mtegoni Mashabiki

Tangu kumekuwa na figizu za hapa na pale Katika mitandao ya kijamii msanii Nay wa Mitego amekuwa akitupa madongo gizani bila hata kuwa na uelekeo lakini swali linakuja kuwa madongo hayo yamekuwa yakimlenga nai haswa.

Msanii huyu ni moja ya wasanii ambao mara nyingi wamekuwa wakionywa sana juu ya nyimbo zake za kukosoa sana lakini pia muda  wote katika  mahojiano na watu amekuwa siku zote akitoa yale ya moyoni bila kuwaza yatamfikia mhusika au la.

Sasa basi tangu kumekuwa na figisu  juu ya matamasha matatu mabayo yote yameisha  wikiendi hii huku moja likihairishwa kabisa, msanii Nay wa Mitego bado anawatia mashabiki wake kigugumizi hasa kutoka na post zake katika mitandao huku wengi walisema kuwa atakuwa anatafuta bifu na WCB lakini wasafi wamekuwa wakimpotezea hivyo hawajali kile anachoongea.

ikumbukwe kuwa nay wa mitego na diamond waliwahi kuwa marafiki wa muda mrefu na hata kufanya kazi pamoja lakinu ghafla watu hawa walianza kuwa katika

 

 

Nay wa Mitego Atupa Jiwe Gizani,

Kutokana na vurugu za matamasha zinazoendelea wikiendhi hii katika mikoa mbalimbali ikiwepo wasafi testval, fiesta pamoja na ile show ya Alikiba huko Kahama , msanii ney wa  itego atoa kijembe na yake ya moyoni kuhusu matamasha hayo huku akisema kuwa wapo wanaoimba bure watachukuliwa kwa sababu tu huwa hawapati show.

Katika ukurasa wake huo , msanii huyo aliweka picha yake kama anaangalia simu huku akisema kuwa katika matamasha hayo anawaju wale wote ambao wapo kwa ajili ya kupata show hizo kwa sababu hawapatagi show za kulipwa.

Nay aliandika “nasubiri kuona list ikiendelea ..mmhhh mbona naona hawa hawana maajabu , waimba bure wote ninawaona hapa , hawapatagi hata show za bure hawa , nataka kuona wasanii heavy sio hawa wasiojulikana hata makwao hawa  kama wanaimba, msiniangushe wazeeeee

Wanangu wa Dar hakikishe mnajaa pale leaders , na wale wa Mtwara hakikisheni mnafika pale nangwanda na nyie wa Kahama  inabidi mkjae pale uwanja wa taifa.

Ney wa Mitego Afunguka Tetesi za Uchawi wa Kumwagia Maji Mashabiki

Nay wa mitego amekuwa akiwaacha mashabiki mdomo wazi siku za hivi karibuni baada ya kubuni mbinu kpya ya kuwamwagia maji mashabiki wake  anapokuwa jukwaani kwa nia ya kusema kuwa anawachangamsha mashabiki wake.

Hata hivyo Ney wa mitego amefunguka na kukanusha juu ya nguvu ya maji hayo kuwa ni ya kishirikina na kwamba amekuwa akifanya hivyo kwa ajili ya kuwachangamsha watu ambao wamekuwa wakija kwenye show zake na wala sio kama watu wanavyosema kuwa ni uchawi.

jamani mimi sio mshirikina na wala siawahi kujihusisha na mambo hayo , yale majin ni ya kawaida tu na wala hayana madhara yoyote kwa mtu yoyote  kwani ninaweza kumpa mtu akanywa, mimi nimekuwa nikiyatumia tu kwa ajili kuwachangamsha mashabiki wangu.

Nay anasema kuwa amekuwa akisumbuliwa na tetesi za kutumia uchawi anapokuwa jukwaanu lakini ukweli ni kwamna nyimbo zake zimekuwa zikigusa maisha ya kawaida ya jamii.

 

Nay wa Mitego Akanusha Kufungiwa , Asema Anatakiwa Kufanya Marekebisho

Baada ya uwa akiitwa BASATA kila siku na hata kupewa barua na baadae kutosema kitu chochote hadharani, msanii Nay wa mitego amefunguka na kuelezea kuhusus sababu za kuwa anaitwa BASATA mara kwa mara tangu wimbo wake mpya ulipotoka hivi karibuni.

Nay wa mitego anasema kuwa wimbo wake mpya haujafungiwa lakini kuna baadhi ya sehemu inabidi kurekebisha na kuutoa tena ukiwa hakuna baadhi ya vipande.

Nay wa mitego anasema kuwa “kikao kilikuwa ni kwa ajili ya wimbo wa alisema mabao haujafungiwa lakini siwezi kuongea mambo mengi sana kwa sababu kuna viongozi tulikuwa nao kwaio hao wataweza kuongea kile tulikuwa tunakiongea huko.”

Hata hivyo Nay wa mitego anasema kuwa kuteuliwa kwa baadhi ya wasanii kuwakilisha wasaii katika uongozi wa BASATA ni jambo zuri lakini hawezi kuliongelea kwaio bora wakae kimya waangalie jinsi wasanii hao pia watakavyoweza kufanya kazi.

Mara ya kwanza Nay wa mitego alipoitwa na BASATA aliwahi kuposti picha ambayo kidogo ilileta wasiwasi kwa mashabiki wakidhani kuwa wimbo wake mpya umefungiwa katika vituo vya habari.

Nay Wa Mitego Aitwa Tena Ndani Ya BASATA

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Emmanuel Elibariki maarufu kama Nay wa Mitego amefunguka na kukiri kuitwa tena BASATA kwa ajili ya mazungumzo.

Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limempatia Nay wa Mitego barua yenye ukarasa mmoja iliyokuwa ikielezea ajenda ya kukutana naye kuwa ni kujadili mwenendo ya kazi zake.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Nay wa Mitego amefungukia tetesi za kuitwa siku ya kesho katika ofisi hizo na kusema:

Ni kweli nimepokea barua na nitatekeleza wito. Waliniita Basata na nilipokwenda ndiyo nikapatiwa barua yenye ukurasa mmoja na nilipoifungua ndani kuisoma ndiyo nikakutana na maelezo ya kutakiwa kufika Basata Jumanne (kesho) ambapo tutakaa meza moja na uongozi wa Basata kujadili mwendendo na mstakabali wa kazi zangu za kimu-ziki”.

Nay wa Mitego alikaa kimya kwa muda wa mwezi mmoja baada ya kufungiwa kazi yake na BASATA na kuamua kurudi kwa kuachia Ngoma ya Alisema ambayo nayo imeonekana kuleta utata.

 

Haya ni Maneno ya Nay wa Mitego Baada ya Kukutana na BASATA

October 17 msanii Nay wa  Mitego aliitwa na Baraza la Sanaa Tanzania  na alifanikiwa kufika ofisni hapo na kupokea barua yake ingawa baada ya kutoka hakuna aliyejua Nay wa Mitego ameambiwa nini  na BASATA, kitu ambach watu wamekuwa wakitaka kujua ni kitu gani kimetokea,

hata hivyo baada ya muda kidogo katika ukurasa wake wa instagram Nay wa Mitego aliweka picha yenye kufunga na taswira nzito  huku akindika ujumbe uliosomeka hivi ”

unaweza kugungwa kila kitu, midomo, miguu,mikon na kazi pia kila kitu lakini kamwe huwezi kufunga mtazamo wa mtu itafungwa kwa sababu lakini mida ikitimia hakuna kinachoshindikana,.

Mara ya kwanza Nay wa mitego alisema kuwa aliwahi kupigiwa simu na BASATA na kumabiw kuwa wimbo wake  umekuwa moja ya nyimbo nzuri na za kuhamasisha jamii.

 

Nilimficha Mama Yangu Kuhusu Wimbo Wangu Mpya -Nay Wa Mitego

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Alisema’ Nay wa Mitego amefunguka na kuweka wazi kuwa alimficha mama yake kuhusu ngoma hiyo.

Wiki iliyopita Nay wa Mitego aliweka wazi kuwa mama yake mzazi ameshawahi kumtaka mwanaye aachane na muziki na kufanya biashara nyingine kutokana na kuhofia kitakachoweza kumpata kwa kuimba nyimbo zake za utata.

Katika Interview yake aliyofanya na Global Publishers, Nay ameweka wazi kuwa kutokana na kumuhofia mama yake Nay aliamua kumficha kuhusu kufanya ngoma hiyo.

Kiukweli nilifanya siri sikumueleza mama yangu kuhusu ule wimbo na mpaka natengeneza video yake sikumwambia lakini nilipokuwa studio nikawaza tu kwamba kuimba nyimbo za aina hii mama alishanikataza, huwa ananiambia niache kabisa kuimba kwa kuwa mimi nina watoto wananitegemea na familia kwa ujumla.

Kwa kuwa nimlificha aliisikia mtaani akanipigia simu na kuniambia niende nyumbani, nilienda pale na kumkuta akinisubiri kwa hamu sana ili kuniuulizia kwa nini nimerudia tena kuimba? Ikabidi nimueleweshe tu sikuwa na jinsi akanielewa,

Nilivyoutunga nikaishirikisha na menejimenti yangu nikaambiwa nimpe mwanasheria wangu aisikilize kwanza nikafanya hivyo alipoisikiliza akaniambia haina tatizo na vitu vichache tu nirekebishe nikafanya hivyo na hatimaye ikatoka”.

Nay wa Mitego ameshawahi kuingia matatizoni kwa aina yake ya uimbaji na ameshafungiwa nyimbo kadhaa na Basata.

Mama Yangu Hataki Kabisa Niimbe- Nay Wa Mitego

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Emanuel Elibariki maarufu kama Nay wa Mitego ameibuka na kuweka wazi kuwa Mama yake mzazi hataki kabisa aimbe kutokana na changamoto alizowahi kumbana nazo.

Nay wa Mitego ambaye anafanya vizuri na ngoma yake ya ‘Alisema’ amewafungukia Global Publishers kuwa mama yake mzazi amemtaka kuachana na muziki na kuangalia biashara nyingine.

Mama yangu hataki nifanye muziki na niendelee kuimba kwa sababu ya matatizo ninayokutana nayo katika kazi zangu kwa sababu mara ya mwisho nilipokamatwa baada ya kutoa Wimbo wa Wapo ndiyo alinikataza, aliniambia niachane na muziki nifanye shughuli nyingine maana nitakuja kufa siku si zangu.

Huu wimbo nimefanya kwa ajili ya wananchi wa Tanzania na mashabiki wa muziki wangu, nimefanya kwa ajili ya hali iliyopo kwa sasa, ninampenda sana mama yangu na huwa ninamsikiliza sana, lakini kwa Wimbo wa Alisema nilijua tu unaweza kuzua balaa (utata), lakini nilipokuwa nikiendelea na kukumbuka kauli ya mama wakati nimeingia studio na kurekodi ndiyo nikaambiwa hebu weka sawa mashairi yako na ndipo nikayapangilia na wimbo ukatoka kama mnavyousikia.

Kwa kuwa nilimuahidi mama kuwa sitafanya muziki anaonikataza, kwa hiyo kwenye huu wimbo najua yeye asingeukubali utoke ndiyo maana nikamwambia mama huu ni wa mwisho naapa”.

Nay Wa Mitego amesema ataacha kuimba nyimbo ambazo zinaikosoa serikali na zenye utata lakini ataendelea kuimba nyimbo za kawaida kwani muziki ndio unamuongizia kipato hivyo hawezi kuacha kabisa.

Nay wa Mitego Ashangwazwa na Simu ya BASATA.

Msanii nay wa mitego amezungumzia furaha yake hasa pale anapoona kuwa wimbo wake mpya uliotoka hivi karubuni kupedbwa na watu wengi hata kufikia hatua ya kupokea pongezi kutoka kwa wabungu na  viongozi mbalimbali.

Nay wa mitego anasema kuwa wimbo huo hakumlenga Mh Rais kama watu wengi wanavyosema bali aliamua kutumua tasfida kwa sababu ukiusikiliza kwa makini unakuta kuwa unalenga karibia  kila mtu ambae ni kiongozi katika jamii.

Kikubwa katika hayo, Nay anasema kuwa kitu kikubwa kilichomstua ni baada ya kupokea simu za viongozi wengi lakini pia alipokea simu kutoka BASATA na kama ilivyo ada amekuwa akijua kuwa kama ni  BASATA basi wimbo unaweza kufungiwa kwa muda owowte kutokana na kazi yao kubwa wanayoifanya.

Hata hivyo Nay anasema kuwa safari hii ilikuwa tofauti kwa sababu BASATA walipompigia walikuwa wanampa pongezi za wmbo wak huo.

Tangu nimeachia wimbo huo nimepokea smu nyingi kutoa kwa viongozi weng sana kutoka serikalini wakinipongeza lakini kilichonishtua ni simu kutoka  kwa kiongozi wa BASATA,  na aliniambi kuwa kwake yeye binafsi  hakupiga simu kuzungumiza BASATA bali alipiga simu kunipongeza kwa wimbo huo  kwa kweli nilifurahi sana lakini mpaka sasa sijapokea simu kutoka kwao.

Nay Akanusha Kumuimba Mh Rais Kweye Wimbo Wake Mpya.

Msanii Nay wa mitego amekanusha taarifa zinazoenea katika mitandao ya kijamii kuwa wimbo wake mpya wa alisema umekuwa ukimsifia na kumponda mh rais hasa pale aliposema zote kwa John.Nay wa mitego anasema kuwa kile alichokimba kinalenga jamii yote kwa ujumla bila kusema kuwa unakwenda moja kwa moja kwa mtu fulani.

Nay anasema kuwa John ni mtu yoyote ambae ni kiongozi anaeweza kulaumiwa na watu kwa kufanya mabaya lakini pia kwa kusifiwa na baadhi kutokana pia  na mazuri yake anayofanya katika jamii.

Kwa sasa hivi john ndio amekuwa akilaumiwa sana na nilitaka kuwakumbusha kuwa ukizungumzia mabaya yake unatakiwa kuzungumzia mazuri yake pia, kwa sababu kila binadamu anakuwa anatenda mazuri na mabaya.Sitaki kusema kuwa ni johngani kwa sababu mimi ni msanii kwaio nimekuwa nikitumia sanaa yangu kuweka mafumbo ili kufikisha ujumbe kwa jamii yangu na ukweli ninaujua mimi ambae nimeongelea swala hilo.

Huo ni wimbo wenye tasfiri nyingi sana, na kila ukiusikiliza unaweza kukaa na kujiuliza kuwa ni  mimi ninaongelewa hapa au vipi.Nimetumia tasfida kwa sababu ninataka watu watumie akili nyingi sana.

Fatma Karume Akiri Kumkubali Sana Nay Wa Mitego

Raisi wa Chama cha wanasheria Tanganyika (TLS) Fatma Karume amwfunguka na kukiri kuwa anamkubali sana Msanii wa Bongo fleva Nay wa Mitego.

Fatma Karume amefunguka na kuweka wazi kuwa anavutiwa sana na Nay wa Mitego kutokana na ubishi wake na msimamo alionao Kwenye sanaa yake anayofanya licha ya kukumbana na vikwazo kibao kila siku.

Katika Interview yake na kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Fatma Karume alimtaja Nay wa Mitego kama Msanii anayemkubali sana kibongo Bongo:

Kwenye gemu ya Bongo fleva nampenda sana Nay wa Mitego I really like that man, kwa sababu unajua binadamu ukisha kutandikwa lakini ukasema to hell ukarudia Tena ukasema Wapo, ni big respect kama unanisikiliza Nay I love you”.

Lakini Fatma amesema Nay ameonyesha ujasiri mkubwa baada ya kuoneakana akiendelea kutoa nyimbo ambazo anazoziamini licha kuingia matatizoni jambo ambalo pia amelitaja kama uonevu.

Nay Wa Mitego ameachia wimbo wake mpya wa ‘Alisema’ ambao umezua gumzo ambao ndani yake imeitaja serikali na sakata la Aqulina ambapo aliishia kuitwa BASATA siku ya jana.

Nipo Likizo ya Mapenzi:-Nay wa Mitego

Msanii Nay wa mitego amefunguka na kusema kuwa kwa sasa yupo single na wala hataki tea kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na mwanamke mpaka pale atakapopata mwanamke ambae anaweza kusema kuwa huyo anaweza kufunga nae ndoa .

unajua kuwa mimi nina watoto kwaio kwanza lazima niw na mtu ambae anajua kuwa mimi ninawapenda watoto wangu, lakini pia inabidi watoto wangu waenjoy kuwa na yeye lakini sipendi kutaja sifa za mwanamke ninayemtaka wasije wakajipanga na kujitengeneza.

kuna muda unaona kabisa kuwa watoto wanaitaji kuwa na mama lakini pia familia inakutaka uoe.

Hivi karibuni Nay aliachana na mpenzi wake ambae alikuwa pia ni msanii katika studio yake , Nini.hata hivyo nay alikiri kuwa yeye ndio alikuwa sababu ya kutokuelewana lakini mpenzi wake huyo hakutaka maelewano.