Chid Benz Amshauri Ney wa Mitego Kufanya Aina Nyingine ya Muziki

Msanii mkongwe wa muziki ambae amekuwa akikumbwa sana na kashfa za matumizi ya madawa ya kulevya na kuwa anachezea kichapo cha kulala ndani kila iitwapo leo kutokana na kukamatwa kwa tuhuma hizo hizo kila siku ingawa yeye mwenye amekuwa akikanusha kuwa kwa sasa ameshaacha matumizi ya madawa hayo Chid Benz amefunguka na kumtaka msani mwenzie Ney wa Mitego kuachana muziki anaofanya sasa ka kutafuta aina nyingine ya muziki  wa kufanya.

Chid Benz ameamua kumchana Ney wa Mitego na kumwambia kuwa muda wake wa kufanya mzuiki guo ulishahisha na sasa styke ya muziki anayoifanya anatakiwa kuwaachia wakina Billnass wafanye na yeye kukaa pembeni kufanya muziki huo.

kwa sisi wakongwe ni lazima tujue kuwa inafika muda na wakati wetu unapita,na sasa kiki inabidi tuwaachie  madogo kina #billnass  huku kina juma nature, afande sele na  nimshauri tu @naythetrueboy  kufanya aina nyingine ya muziki.

Nay wa Mitego ambae ni msanii wa hip-hop amekuwa ni mmoja wa wasanii walioingia katika list ya wasanii ambao wanatakiwa kubadlisha aina ya muziki na kuacha kuimba nyimbo za matusi kama ambavyo nyimbo zake za awali zilivyokuwa.

Mimi Naimba Hip hop hata Kama Wakikataa- Nay wa Mitego

Mwanamuziki wa Bongo Fleva Nay wa Mitego ameibuka na kujitamba kua yeye ni mwanamuziki wa Hip hop na kuwa anapendwa sana na mashabiki kwa ajili ya staili yake ya kipekee ya kurap ambayo iko tofauti na wasanii wengine.

Nay aliyasema hayo kwenye mahojiano aliyoyafanya kwenye kituo kimoja cha redio ambapo alisema kuwa kuna baadhi ya wasanii wenzake wa hip hop wamekuwa wakidai haimbi hip hop lakini amesema huo wote ni wivu kutoka kwa wasanii hao kutokana na mafanikio anayoyapata kuwashinda wenzake.

Nay amedai kuwa kama kweli angekuwa haimbi hip hop basi asingepata mashabiki wengi na kupendwa kuliko hao wasanii wengine wanavyopendwa. Ny ambaye anasifika kwa staili ya ya kuimba na kusema ukweli juu ya mambo mbalimbali hasa siasa au hata kuongelea wasanii wenzake na kazi zao.

Nay ambaye kwa sasa natamba na nyimbo yake mpya inayoenda kwa jina la ‘Makuzi’ ambayo amefanya kwa staili ya kuimba ambayo huenda ndio sababu wasanii wenzake wamemtoa kwenye kundi la kurap kwani nyimbo yake nyingine ya ‘Acheze’ imeimbwa pia lakini ngoma kama ‘Wapo’ na ‘Moto’ alizotoa mwaka huu aefanya kwa staili ya kurap.

Hata hivyo Nay amedai kuwa wasanii wenzake hao wakisema haimbi hip hop hakumuumizi kwani yeye anaangalia maslahi na kama anachofanya kinamuingizia kipato basi haina shida wasanii wenzake waseme nini kwani muziki kwake ni biashara.

“Gombaneni, roganeni mpaka muuane” Huu ndio ujumbe Nay aliowaandikia Ommy Dimpoz, King Kiba na Diamond Platnumz

Rapa wa bongo Nay wa Mitego hatimaye ameingilia vita mpya ya Ommy Dimpoz, Diamond Platnumz na King Kiba kwa kutoa maoni yake.

Kupitia mtandao wa Instagram Nay alifunguka kwa kusema kuwa hakuna anayemuunga mkono lakini jambo linalomkasirisha ni kuwahusisha wazazi kwenye vita hivi vyao vya utoto. Aliandika kusema;

Gombaneni, roganeni mpaka muuane, napenda kusikia changamoto kwenye gemu, ila tusiwaingize wazazi wetu tafadhali, tukananeni matusi yote wenyewe kwa wenyewe ikibidi piganeni kabisa atakaye kufa tutazika na itakuwa historia kama Big na Pac.

Akaendelea kwa kuongeza kuwa;

“Ila kuwaingiza wazazi ni ujinga, sipo upande wowote si kwa Kiba, Dimpoz wala Diamond, endeleeni na vita yenu kama wanawake mmechukuliana mabwana, ila suala la wazazi mnavuka mipaka,”

Young Killer amjibu Nay Wa Mtego baada ya kumdiss

Nay Wa Mtego ni msanii ambaye anajulikana kuwachana wasanii wenzake kupitia mziki wake. Hapo mbeleni ameskika akiwachana akina Wema Sepetu, Ommy Dimpoz na wengi kupitia nyimbo zake.

Nay wa Mitego

Hivi karibuni aliachia wimbo mpya ‘moto’ ambapo aliskika akimwambia Young Killer “Young Killer chali, safari ya Mwanza inanukia, usiwadharau waliokufanya ukatoba” kitu ambacho kimemfanya Killer kumjibu Nay.

Kupitia mtandao wa Instagram Young Killer aliandika, “Nasikia kuna mtu kanidiss” kuonyesha kuwa alikuwa ameupokea ujumbe wa Nay. Hata hivyo jambo hili halikumshtua rapper huyu kwani alimjibu Young Killer kwa kuandika ” #Ney True Boya,” kupitia mtandao wake wa Instagram.

Hata hivyo, hakuna anayejua kinachoendelea kati ya wawili hawa.

 

Kuna nini? Rich Mavoko na Nay wa Mitego wakijibizana mitandaoni

Kuna dalili za Rich Mavoko na Nay Wa Mitego kuanza beef baada ya majibizano yao mitandaoni ya kijamii hivi karibuni.

Hii ilianza baada ya Mavoko kuposti picha na maneno ya kuwajulisha mashabiki wake kuwa anatarajia kuachia nyimbo mpya hivi karibuni kwa kuandika.

Haya Mkimaliza Mambo Zenu Za Siasa Mtupe Tarehe Na Sisi Tufumue Hiii ? #Showme

Lakini baada ya masaa kadha Nay wa Mitego alirepost picha hiyo ya Mavoko na kumchana kwa kumwambia kuwa ngoma yake mpya WAPO ndio inapaswa kutiliwa maanani na wananchi. Aliandika kusema,

Haya Mkimaliza Mambo Zenu Za Siasa Mtupe Tarehe Na Sisi Tufumue Hiii ? #ShowmeNAOMBA MUENDELEE KUSUBILI, MAY BE MPAKA MWAKANI 2018, NDO MTAANZA KUJISHUGHULISHA NA MASWALA YA KUWAIMBIA WANA NCHI. MWAMBIENI NA BABA YENU PIA AWE MPOLE KWASASA ALEE WATOTO. KAZI TULIYO NAYO IKIENDA SAWA TUTA WARUHUSU MUENDELEE KUBURUDISHA WANA NCHI. TUNATAKA MAMBO YAENDA SAWA KWANZA✊?.
Wimbo wetu wa TAIFA ni #Wapo LINK ON MY BIO☝?️

Nay Wa Mitego anahofia maisha yake Sasa

Rapper Nay Wa Mitego ameewacha wengi wakimhofia maisha yake baada ya ujumbe aliouandika kwenye mtandao wake wa Instagram. Ujumbe huu umekuja wiki moja baada ya rapper huyo aliwekwa ndani na jeshi la polisi baada ya kuachia wimbo wake mpya ‘Wapo’.

Kulingana na ubuyu mitandaoni, wimbo huu ukikuwa ukichana serikali ya Magufuli hata hivyo Rais wa Tanzania Magufuli alitoa amri msanii huyo kuachiwa kwa kwa kusema wimbo wake haukuwa na matatizo yoyote.

Hata hivyo, Nay wa Mitego sasa hivi anasema kuwa anahofia maisha yake kwani anahisi kwamba kuna watu wanaotaka kumpoteza. Kupitia Instagram aliandika kusema

“Usalama wa maisha yangu umekua mdogo kwasasa, Wanapanga kunipoteza ikibidi nisiwepo kabisa kwenye hii dunia. Nipo tayari kwa chochote wanacho panga kufanya Coz sijajipanga kupambana nao, Mimi ni mwana muziki si vingine. Kwa chochote kitachotokea familia yangu itakua na chakuongea. Siwezi kuhama nchi wala kukimbia nitafia hapa hapa. Na siko tayari kupindisha chochote.! nyie Ndo mtanilinda. Sina Mlinzi na sitarajii kua na mlinzi. OnlyGod??#Wapo,”

Haijulikani ni nini kilichomfanya kuhisi hivyo, lakini tunafuatilia kusikia atachokisema hivi karibuni.

Mambo Nay wa Mitego na Waziri Mwakyembe walizungumzia baada ya kukutana

Hivi leo Nay wa Mitego alikutana na waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Dr. Harrison Mwakyembe ambapo walizungumzia mambo mbalimbali.

Nay amekuwa akizungumziwa kwa muda sasa na ni baada ya kukamatwa na polisi kwa ajili ya wimbo wake wapo ambao ulionekana kukashifu serikali ya Magufuli.

Alikuja kuachiliwa baadaye kwa maagizo ya waziri Mwakyembe na leo walikutana kuongelea mambo tofauti ikiwemo mambo wanafaa kuongeza kwenye wimbo huo.

Nape Moses aandika ujumbe huu baada ya Nay wa Mitego kuachiliwa

Nay Wa Mitego sasa hivi yuko huru baada ya kuachiliwa siku kadhaa baada ya kushikwa na serikali ya Magufuli. Mashabiki wake walikuwa mkondo wa kwanza kumkaribisha msanii huyu na pia alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Moses naye pia aliandika ujumbe wake kupitia account yake ya Twitter.

Nape Moses aliandika ujumbe wenye ulisihi viongozi kutumia busara na siyo nguvu katika kufanya maamuzi wakati wanapomuona mtu amefanya kosa ilikurahisisha kumkosoa.

Aliambatanisha picha ya Nay wa mitego alipoandika ujumbe huo kuonyesha kuwa hakufurahishwa na kitendo ambacho walichomfanyia mwanamziki huyu.

Ata hivyo wanamziki wengi walisita kuandika kitu chochote kupitia mitandao yao ya kijamii huku wakihofia kukamatwa. Huu umekuwa kama mtindo ambao serekali ya Magufuli imeanza kuiga na wengi wanonelea kuwa wamekosa busara na kuwafanya wengi kuogopa.