Mziwanda Akiri Kuwa Muziki wake Umeuliwa na Mapenzi.

Msanii Nuh mziwanda amefunguka leo alipokuwa akiongea na leo tena ya Couds Fm na kusema kuwa muziki wake kwa sasa umekufa na anakbali kuwa muziki huo kwa sasa umekufa kwa sababu ya  uzembe katika mapenzi.

Nuh mziwanda amefunguka na kusema kuwa pamoja na kwambaaliwahi kufanya vizuri sana lakini kitu kikubwa anachokiri kuwa kinampoteza katika ulimwengu wa muziki ni baada ya kuoa na kuna misukosuko mingi ilitokea na kufanya kuachana na mke wake ambae alikuwa pia ni mzazi mwenzake.

Nuh anasema kuwa baada ya hayo  yote aliona kabisa jinsi anavyoyumba na kumfanyya kuyumba na ndio maana hata alitoa wimbo wa natapatapa ambao ulikuwa ni storo ya kweli ya maisha yake halisi kwa muda huo.

Nuh aliwahi kuwa katika mahusiano na shiloleh na baadae kuachana na ndipo alipofunga ndoa na mwanamke mwingine ambae walizaa mtoto mmoja na kisha kushi ndwa kukaa pamoja na kuachana.

Nuh Mziwanda Alivunja Mahusiano Yangu na Prezzo- Amber Lulu

Msanii wa muziki wa Bongo fleva na video vixen maarufu Lulu Eugene ‘Amber Lulu’ amefunguka na kudai kuwa Msanii wenzake Nuh Mziwanda ndiye sababu kubwa ya Penzi lake na Prezzo kufa.

Amber Lulu na Prezzo walikuwa Kwenye Mahusiano ya muda mrefu lakini mapenzi yao yaliingia doa mara baada ya video iliyomuonyesha Nuh Mziwanda na Amber Lulu wakifanya yao kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Kwenye mahojiano aliyofanya  katika kipindi cha The Playlist cha Times FM, Amber amekiri kuwa kuna kipindi alikuwa karibu na Nuh Mziwanda na baadaye picha zake zilisambaa mitandaoni  wakiwa karibu wakijiachia kimahaba.

NUH NI MSHIKAJI TU ILA NDOA YANGU NA PREZZO ALIMAIND ILE KUKISIANA KISIANA NA NUH MZIWANDA JAPO NI MAKOSA TU KWAKUWA MIMI NI KIJANA NA YEYE YUPO MBALI MI NIPO HUKU MUDA MWINGINE NAHITAJI VITU VINGI LAKINI KUTELEZA KUPO  ILA NILIJITAHIDI SANA KUOMBA MSAMAHA SANA NIKAONA KAMA KANIKAZIA HIVI MWISHO WA SIKU NIKAONA NAOMBA MSAMAHA SANA KWAAJILI YA NINI NIKAONA FRESH TU KAMA UMEAMUA POA WACHA NIISHI MAISHA YANGU”.

Amber Lulu amesema hivi sasa ameamua kuwa Single ili apate muda wa kufanya kazi zake kwa uhuru bila kujali wanaume.

KWA SASA HIVI NIPO SINGLE SIHITAJI BOYFREND WALA MCHUMBA MUDA NINAOUPOTEZA KWAO NI BORA NIFANYE MAMBO YANGU ILA IKIFIKA MUDA NIKIMTAKA MTU NAMLIPA ARAFU TUNAMALIZANA FRESH SIHITAJI MUDA WA KUSUMBUANA WALA HUYO NUH HATA SIMTAKI YEYE MWENYEWE MAISHA YAKE YANAMSHINDA”.

Nuh Mziwanda Adai Na Yeye Alichangia Kununua Mjengo Wa Shilole

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Nuh Mziwanda ameibuka kuwa ana yeye pia aliweka mkono Kwenye kununua Mjengo mpya wa Shilole aliouanika Kwenye mitandao ya kijamii.

Ikiwa ni siku chache zimepita tangibly shilole aanikr Mjengo wenye thamani ya zaidi milioni 90 anaoujenga hivi sasa, aliyekuwa mpenzi wake Nuh Mziwanda amedai na yeye pia ana chake Kwenye Mjengo huo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Wasafi Tv, Mziwanda amedai pamoja na kwamba alishiriki kununua Mjengo huo wakati wa Mahusiano yao lakini amesem hawezi akaomba arudishiwe pesa sababu hawapo wote:

Ni kweli ule mjengo tulinunua wote Wakati tupo pamoja, nakumbuka tulikuwa na hela tukaenda mpaka kule tukamalizana na yule jamaa yaani mishe mishe zote tulikuwa wote tunanunua nyumba na kukamilisha kila kitu”.

Lakini pia Mziwanda amedai hawezi kumdai SHilole Pesa zake alizochangia Kwenye ule mjengo sababu yeye ni mwanaume:

Hapana siwezi kwa sababu yule mtoto wa kike ujue alafu mimi nilikuwa mwanaume kama Baba sasa nikianza kudai nilichangia hiki na kile inakuwa haileti picha nzuri yule ni mtoto wa kike muache atunzwe”.

Baada ya kuweka wazi mjengo wake Shilole aliweka wazi amejenga nyumba ile kwa nguvu zake bil msaada wa mwanaume yoyote na kusema ile sio nyumba ya mume wake Uchebe bali amejenga kwa ajili ya watoto wake.

Nuh Mziwanda- Sina Bifu na Diamond Ila Sina Ukaribu Naye Pia

Mwanamuziki wa Bongo fleva Nuh Mziwanda amefunguka na kudai jana bifu na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Nuh ambaye ameshafanya ngoma na Ali Kiba aliomshirikisha katika wimbo wake wa Jike Shupa amefunguka na kusema hata kama hajawahi kufanya ngoma na Diamond haimaanishi wana bifu.

Mziwanda alifunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na Dizzim Online pale alipotakiwa kujibu tetesi kama ana tatizo lolote na Diamond:

Mimi sina bifu na Msanii yoyote na wala sina bifu na Diamond wala sina ugomvi naye unajua yule mchizi sana na tulishawahi kufanya vitu vingi sana lakini muda nakumbuka Times hafanyi shoo zake tulikutana Dodoma tukafanya shoo yake kwaiyo ni mtu ambaye yuko Poa lakini hatuna mawasiliano wala ukaribu wowote.

Lakini pia Mziwanda ameweka wazi kuwa kama ikitokea nafasi ya kufanya kazi na Diamond basi atafuata taratibu za kwenda Kwenye uongozi wake na kuomba Kolabo.

Kutokana na Bifu lililopo kati ya Diamond na Ali Kiba, wasanii wanaofanya kazi na wasanii hao hujikuta wakichagua upande wa kuwa na hivyo Mziwanda baada ya kufanya Kolabo na Ali Kiba alidaiwa kuwa na bifu na Diamond.

 

Nuh Mziwanda Amtaka Diamond Aache Kudhalilisha Wanawake

Mwanamuziki wa Bongo fleva Nuh Mziwanda amemjia juu msanii mwenzake Diamond Platnumz na kumtaka aache vitendo vyake anavyofanya vinavyopelekea kudhalilisha wanawake.

Nih ameongelea kitendo cha Diamond kusabaza video Kwenye mitandao ya kijamii akiwa na wanawake wawili tofauti katika usiku mmoja kama udhalilishaji wa wanawake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Nuh Mziwanda amedai kitendo alichokifanya Diamond sio cha kiungwana kwani wanawake wote ni kama mama zetu hivyo tunapaswa kuwaheshimu.

Ni lazima tuwaheshimu wanawake maana ndio waliotuzaa na waliotuleta duniani kwaiyo automatically ni watu wa kuwaheshimu na hiyo ni nguvu ambayo Mwenyezi Mungu kaiweka kwaiyo huwezi ukarekodi vitu kama vile alafu ukaviweka Kwenye mitandao inakuwa inaleta picha mbaya kama vile dada zetu hawana thamani kitu ambacho sio cha kweli”.

Tangu kitendo hiko kitokee siku chache zilizopita tayari Diamond ameshachukuliwa hatua za kisheria na Waziri amehaidi atafikishwa mahakamani kwa kitendo hiko alichofanya.

Nuh Mziwanda Aonyesha Mjengo Wake Baada ya Tetesi Za Kufulia

Mwanamuziki wa Bongo fleva Nuh Mziwanda ameanika mjengo wake ambao unajengwa baada ya kugubikwa sana tetesi za kufulia hivi karibuni.

Nuh Mziwanda alikuwa Kwenye Mahusiano ya kimapenzi na msanii mwenzake Shilole kwa miaka kadhaa lakini baadae walikuja kuachana na Shilole kuolewa na mwanaume mwingine.

Lakini tangu Nuh ameachana na Shilole Kumekuwa na taarifa nyingi zinazodai kuwa amefulia vibaya mno kuanzi kimuziki mpaka kipesa kwani alikuwa anategemea mafanikio kutoka Shilole.

Nuh jana amewatolea povu watu wote ambao wamekuwa wakimponda na kusema amefulia baada ya kuuanika mjengo wake ambao unajengwa kuonyesha kwamba hajafulia.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nuh aliandika ujumbe huu:

 

Nuh Mziwanda ni Mwanaume Asiyejua Kutunza Siri

Msanii wa Bongo fleva Nuh Mziwanda amenyooshewa kidole na baadhi ya watu kwa tabia yake Kupenda kuimba kuhusu mahusiano yake ya kimapenzi na kuyaanika hadharani.

Nuh ni moja kati ya wale wasanii ambao wanapenda kuimba kuhusiana na uhalisia wa maisha yao lakini kwa upande wa Nuh yeye anapendelea kuimba kuhusiana na mahusiano yake ya kimapenzi hasa na wapenzi ambao ameshaachana nao.

Hili lilionekana na yeye alivyotoa wimbo wake wa ‘Jike shupa’ ambao alimuimbia aliyekuwa mpenzi wake Shilole baada ya kuachana ambapo kwenye wimbo huo alimtafuta video queen ambaye alikuwa anafanana na Shilole na kuonyesha baadhi ya mambo yaliyokuwa yanatokea kwenye Mahusiano yao kama vile Shilole kumpiga Nuh na kurudi nyumbani usiku akiwa amelewa sana.

Lakini pia hilo limeoneka tena kwenye video yake mpya ya wimbo wake wa Upofu ambapo inasemekana kamuimbia aliyekuwa mke wake Nawal ambaye lakini pia amezaa na urban mtoto mmoja anayeitwa Anya ambapo kwenye video hiyo pia ametafuta video queen anayefanana na Nawal.

Baada ya tuhuma hizo Nuh Mziwanda alifunguka haya alipofanya mahojiano na Enews ya East Africa Tv:

Napenda kuwa huru napenda kufanya vitu vyangu ili watu wajue kile kilishatokea kilishapita kulikoni unatembea mtu anaona una kitu moyoni kwaiyo inabidi ukubali matatizo yako ili uweze kuyamaliza yaishe ili uweze kuendelea kwaiyo siku zote mimi ni mkeweli siwezi kuficha kitu  mimi hata nikimsaliti mwanamke wangu nitamwambia ukweli siwezi kukaa na kitu moyoni mpaka washakaji zangu wanapenda kuniambia mimi mmbea”.

 

Nuh Mziwanda: Siwezi Kurudiana na Shilole

Mwanamuziki wa Bongo fleva Nuh Mziwanda amefunguka na kudai Kuwa habari zilizosambaa kuwa amerudiana na Shilole sio za kweli kwani hawezi tena kurudiana na aliyekuwa mpenzi wake hspo mwanzo.

Shilole na Nuh waliachana kipindi cha hapo nyuma ambapo baada ya kuachana waliingia katika vita ya kurushiana maneno mtandaoni ambapo Nuh alidai kuwa wakati wapenzi Shilole alikuwa anamnyanyasa kwa sababu yeye ndio aliyekuwa anatengeneza pesa kati yao lakini pia Shilole alimtuhumu kuwa Huh alikuwa ana michepuko ndio sababu ya yeye kumpiga.

Baada ya kuachana kila mmoja aliendelea na maisha yake binafsi huku Shilole akianzisha mahusiano na kijana anayeitwa Uchebe na Nuh Mziwanda alifunga ndoa na mrembo anayekwenda kwa jina la Nawal lakini baadae walikuja kuachana na Nawal kuolewa na mwanaume mwingine.

Kwenye mahojiano na Millard Ayo Tv, Nuh Mziwanda amekana tetesi za yeye kurudiana na Shilole na kudai kuwa hawezi kurudiana na Shilole tena bali anawatakia maisha mema yeye na mumewe Uchebe kwani penzi lao ni zilipendwa lakini pia amedai kuwa zile picha zilizosambazwa mtandaoni wakiwa wamelala kimahaba zilikuwa ni picha ya siku nyingi sana wakiwa wapenzi na sio yeye aliyezisambaza kama Shilole alivyomtuhumu kupitia ukurasa wake wa Instagram siku ya Jana.

Lakini Nuh pia alifunguka na kudai kuwa tetesi za Kuwa amerudiana na mama wa mtoto wake, Nawal sio za kweli bali wanapatana kwa sasa kwa ajili ya kumlea binti yao na sio mambo mengine ya kimapenzi amedai kwa sasa hana mpenzi yoyote.

 

 

 

Shilole Amtolea Povu Nuh Mziwanda na Kudai Anataka Kumgombanisha na Mpenzi Wake

Mwanamuziki wa Bongo fleva Shilole amemjia juu aliyekuwa mpenzi wake Nuhu Mziwanda na kudai kuwa anataka kumuharibia uhusiano wake na mpenzi wake Uchebe.

Siku ya Jana habari zilienea kuwa Shilole amerudiana na Nuhu Mziwanda na kumuacha mpenzi wake Uchebe. Siku chache zilizopita Uchebe na Shilole walitangaza kuwa wanatarajia kufunga ndoa hivi karibuni na kudai kuwa wanataka kufunga ndoa yao Ulaya. Pia Shilole alimpeleka Uchebe Nyumbani kwao Tabora, Igunga ili kumtambulisha kwa wazazi wao.

Hivyo Jana baada ya habari kusambaa kuwa Shilole kamuacha Uchebe na kurudiana na Nuh Mziwanda watu wengi walishangaa kwani ni juzi tu habari zilisambaa kuwa Nuh Mziwanda amerudiana na make wake Nawal ili wamlee mtoti wao.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Shilole amekataa vikali tetesi hizo za yeye kuachana na Uchebe na kurudiana na Nuh Mziwanda na hata kumnyooshea kidole Nuh na kudai kuwa yeye ndiye aliyesambaza habari hizo za uongo na ile picha ili mradi tu amgombanishe na mpenzi wake Uchebe.

Shilole ametoa tamko lifuatalo kutokana na tetesi hizo:

Ulizani utanikomoa kwa taarifa yako hiyo picha sio ya leo unaunga unga matukio ili kunigombanisha na mchumba wangu? Mashabiki zangu niwaambie tu hiyo staili ya nywele nadhani mnajua kuwa napenda kuitumia. Alipangalo Mwenyezi Mungu binadamu hawezi kulipangua”.

 

 

Hatimaye Nawal Kafuta tatoo Ya Nuh Mziwanda

Wasanii wengi wa bongo wamekuwa na desturi ya kuchora tatoo  kubwa za wapenzi wao katika miili yao  wanapokuwa katika mahaba lakini shida huwa inakuja pale wawili hao  wanapoachana , ndipo yule aliechora anapoanza kuangaika jinsi ya kuitoka michoro hiyo katika miili yao.

Nawal ambae alikuwa mwanamke wa ndoa wa msanii Nuh Mziwanda aliamua kuchora tatoo ya mpenzi wake huyo ikiwa ni kama ishara ya mapenzi kwa mwanaume  wake lakin baadae wawili hao walikuja kuachana ivyo deni linabaki kwa mwanadada Nawal jinsi gani anaweza kuondoa alama ile kubwa katika mwili wake.

Wengi walikuwa wakisubiri ili kuona itakuwaje kwa mwanadada huyo lakini hatimaye amefanikwa na kuamua kufuta tattoo iyo lakina ameibadilisha na kuiweka  katika mchoro mwingine usioeleweka zaidi.Mwanadada huyo alisema kuwa ipo siku mashabiki wataamka tu na kuona tatoo iyo imeondoka na kweli amekamilisha maneno yako.

Muonekana wa tatoo mkononi mwa Nawal

Nuh  Mziwanda na Nawal walianza mahusiano na mahusiano hayo yali-trend sana katika mitandao kwa sababu ilikuwa ndicho kipindi ambacho Nuh Mziwanda alikuwa ametoka katika penzi la manyanyaso la msanii wa kike SDhiloleh ambae anasifika kwa kutembea na vijana chini ya umri wake.Nawal na Nuh walifanikiwa kufunga ndoa ya kiislamu baada ya mwanadada huyo kupata ujauzito.

Walifanikiwa kupata mtoto mmoja lakini baadae waliachana na mtoto kubaki kwa mama kutokana na umri mdogo alionao mtoto.Wawili hao waliingia katika ugomvi mkubwa baadae kuhusu malezi ya mtoto wao.

Nuh mziwanda amekuwa kila siku akilalamika katika mitandao Ya kijamii kutokana na malezi anayopewa mtoto huyo na mamake kwa madai kuwa mama yake na mtoto ambae ni Nawal amekuwa akienda kwa mabwana wengine au kuonekana kuwa bar akiwa na mtoto huyo mida mibaya ambayo mtoto hapaswi kuwa katika maeneo hayo.

Hata hivyo kuna kipindi baada ya mwanadada huyo kuachana na Nuh Mziwanda alikiri kuwa ameshaolewa na mwanaume mwingine na amekubali kulea mtoto huyo wa Nuh Mziwanda.

Nuh Mziwanda Azidi Kumlilia Binti Yake Adai Mama Yake Anaenda Naye Kwa Wanaume Wengine

Msanii wa Bongo fleva Nuhu Mziwanda kwa mara nyingine ametumia mtandao wa kijamii kueleza majonzi yake kuhusiana na malezi ya binti yake Anya.

Nuhu Mziwanda na Mama wa mtoto wake ajulikanae kama Nawal walioana mapema mwaka huu lakini kwa Bahati mbaya ndoa hiyo haikudumu na hivyo kupelekea kuachana na Nawal kuolewa na mwanaume mwingine. Tangu wameachana wamekuwa wakikwaruzana kwenye mitandao ya kijamii kuhusu malezi ya mtoto huyo huku Nuhu akidai mzazi mwenzie anamkataza kumuona binti yake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nuhu amefunguka yafuatayo:

Nakumiss sana mwanangu Anya yaani Mungu anajua jinsi gani moyo wangu unaenda mbio nikikukumbuka au ukinijia akilini maana najua ungefurahi uwepo wangu karibu yako, Najua hauhisi Upendo kama uliokuwa unahisi ulipokuwa karibu yangu, ningependa nikukuze katika misingi yangu, sheria zangu na kanuni zangu kama baba ako. mama yako hakutendei haki kabisa na mimi natambua hilo anazunguka na wewe kwenye kumbi za starehe, anasafiri na wewe kwenda kwa wanaume wengine haukustahili haya mwanangu”.

Nuhu aliendelea kunung’unika lakini pia alitoa rai hiyo ili endapo akiwa mkubwa aelewe hakuwa kwenye maisha yake kwa sababu mama yake hakumruhusu.

Naandika hii ibaki kama kumbukumbu ukikua najua utaiona mwanangu maana wanawake wengi hupenda kupandikiza chuki kwa watoto ili wachukie baba zao, nimelia sana juu yako ila sasa namkabidhi Mungu hili suala na ninaamini atakulinda atakupa tabasamu sahihi japo upo mbali na mimi nakupenda Anyaghile wangu”.

Mpaka sasa Nawal hajajibu tuhuma hizi alizotupiwa na mzazi mwenzie. Kea sababu kila hadithi Ina pande mbili hatuwezi sana kutetea upande wa Nuhu bila kusikiliza na upande wa Nawal, lakini mpaka apo maoni yako ni nini?

Nuh Mziwanda aomba mashabiki wake ushauri kuhusu wanawake

Nuh Mziwanda hajafanikiwa kuwa kwenye uhusiano unaodumu; baada ya kuwachana na muimbaji Shilole staa huyo alimuoa kipusa Nawal ambaye alimzalia mtoto wa kike.

Nawal na Nuh hata hivyo walikorofishana kwa ndoa yao kwa kiwango kuwa walifikia maamuzi ya kuwachana na kila mmoja kuenda zake.

Nawal na Nuh

Nuh sasa ameshindwa namna ya kupata mwanamke ambaye atadumu kwenye uhusiono na yeye. Staa huyo hatimaye aliamua kuomba ushauri kwa mashabiki wake jinsi ya kupata mwanamke atakayemfaa katika maisha yake.

Nuh na mwanawe

“Nimejifunza mengi sana kwenye life style yangu ya kimapenzi na najitoaga sana ila siku ya mwisho naumizwa ‘je unahisi Mwanamke wa aina gani atanifaa na nitaweza kudumu nae?Leo Nawaachieni mashabiki wangu mmalize hili ? #BaoLaUshindi,” Nuh Mziwanda aliandika kwenye mtandao wa Instagram.

 

Nuh Mziwanda (ex wake Shilole): Sitaki mambo ya wanawake yaani staki hata kusikia

Nuh Mziwanda bado ako na uchungu tangu aachane na mke wake anayefahamika kwa jina la Nawal. Msanii huyo sasa anawachukia wanameke kwa dhati.

Akiongea katika kipindi cha 5seleKt kutoka EATV, Nuh Mziwanda alisema yeye sasa ni single boy baada ya kuachana na mke wake siku chache zilizopita.

Nuh Mziwanda

Nuh aliwahi kuwa na mahusiano na mwanamuziki Shilole kabla ya kuachana naye na kumoa mkewe Nawal ambaye alimzalia mtoto mmoja.

Nuh sasa amesema hataki mambo ya wanawake tena, alifunguka na kusema kuwa anatamani kukaa na mtoto wake ambaye kwa sasa anaichi na mkewe tangu waachane.

Nuh Mziwanda na mkewe

“Sasa hivi nipo ‘single boy’ sitaki mambo ya wanawake yaani staki hata kusikia. Nilitamani sana mtoto wangu ning’ekaa naye mimi ‘since’ yupo mdogo lakini nashindwa kufanya hivyo kwa sababu ya umri wake haujifikia kukaa na baba kwa hiyo nimemuachia mama yake kwa sasa lakini kama nikiona mwanangu wanamfanyia vitu ambavyo si sawa kwangu nitaenda kumchukua nikae naye mimi mwenyewe,” Nuh Mziwanda alisema.

 

Shilole aeleza kwanini hakujaliwa kumzalia mtoto ex wake Nuh Mziwanda

Staa wa Bongo Movies Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole ameeliza kwanini hakumpa mtoto ex wake Nuh Mziwanda.

Wawili hao, Shilole na Nuh, waliwapa watu sababu ya kuwazungumzia baada ya kuonekana katika mapozi ya kimapenzi.

Soma pia: Hawa watarudiana tu! Staa wa Bongo Movies na Bongo Fleva Shilole apatikana akiwa katika mapozi ya kimapenzi na ex wake

Nuh alimuoa Nawal na ata kuzaa naye mtoto wa kike baadaya ya uhusiano wake na Shilole kuvunjika. Ata hivyo Shilole na Nuh bado ni marafiki.

Alipoulizwa kwanini hakumpa mtoto Nuh kwenye kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio hivi karibuni, Shilole alisema kuwa hakujaaliwa tu kupata mtoto kwa uhusiano wake na Nuh. Alisema pia bado yupo single kwa sasa.

Shilole na Nuh Mziwanda