Nuh ataja sababu itakoyomfanya amchukue mtoto wake baada ya kuwachana na mke wake

Nuh ameweka wazi kuwa ameachana na mke wake lakini msanii huyu hakutaja sababu za kuachana.

Hata hivyo amemruhusua alikuwa mke wake kumlea mtoto wao wa kike aitwaye, Anyaghile. Lakini akizungumza na 5Selekt ya EATV hivi karibuni Nuh alisema kuwa aliyekuwa mke wake ashaolewa tena lakini ameapa kuwa hakuna kitakacho mfunga yeye kumchukua mwanawei wapo atafanyiwa vitu ambavyo si sawa.

“Mtoto still yupo na ningetamani sana kukaa naye tangu akiwa mdogo lakini nashindwa kufanya hivyo kwa sababu ya umri lakini nikiona mwanangu wanamfanyia vitu ambavyo si sawa nitaenda kumchukua na kukaa naye mimi mwenyewe,”

Aliongeza;

“Kwa hiyo nampa muda nione, nikienda nikakuta mwanangu amenenepa, ana furaha, yupo poa ataishi naye mpaka umri utakapofika lakini nikienda nikakuta mwanangu amepungua nambeba na kuondoka naye.”

Nuh Mziwanda akiri kubadili dini

Mkali wa Bongo Fleva Nuh Mziwanda amesema kuwa Sasa yeye ameirudia dini yake ya kwanza, Mkristo, baada kuachana na aliyekuwa mke wake.

Nuh alisema haya baada ya kuzungumza na XXL ya Clouds FM, huku aliendelea kusema ni kweli alikuwa kanisani Jumapili hii iliyopita na kukiri kuwa habari zinazoenea mitandaoni ni za kweli. Msanii huyu alisema;

“Nimerudi kwa Mungu wangu ili mambo yangu yaende vizuri maana tunafanya muziki wa dunia anatusamehe ila kurudi kwake pia ni jambo la kawaida sana.”

Aliendelea kwa kujibu tariffs zilizotolewa na aliyekuwa mke wake kuwa ameacha kumjali mtoto wake. Nuh alisema;

“Mara ya mwisho nilikuwa na Anyagile kwenye photoshoot ya ngoma yangu mpya jana kwa Mx Carter, inayotoka hivi karibuni sasa yeye anavyosema sijamuona mtoto muda mrefu sijui anamaanisha nini. Anaongea vibaya kwenye media sio vizuri, mimi na fan base yeye mwanamke anatakiwa ajue anaongea nini, ila muache aongee akikua ataacha, vile vile mimi sina tatizo naye kama kaolewa, yeye si ndio kaamau mimi bado kijana na kila mtu anafanya anachotaka mimi nimemrudia mungu huwezi jua atanipatia mke mwingine mwema”.

Nuh Mziwanda afanyiwa upasuaji wa shingo

Msanii wa Bongo Nuh Mziwanda ameandika ujumbe kuwashukuru madaktari wa hospitali ya Mwananyala kwa kumfanyia upasuaji wa shingo baada ya kupata maumivu makali shingoni.

Nuh Mziwanda anayejulikana kwa hit song yake ya Jike Shupa, aliweka picha huku akionekana na bandage shingoni na tabasamu usoni kwa upasuaji salama.

Ingawa bado hajafunguka kusema kilichotokea, Nuh aliandika ujumbe kusema,

“Thanks Jesus….thanks MY SUPER DR KIWALE BINGWA kabisa wa upasuaji ‘Na MWANANYAMARA HOSPITAL kwa surgery (Upasuaji)uliokua chini ya shingo yangu’ bila kusahau MAMA yangu na ndugu zangu waliokua pamoja na mimi.naomba Maombi yenu Mashabiki wangu nirudi katika hali yangu na Kazi ziendelee.Love you.”

Siku chache baada ya kuonyesha mtoto kwenye mtandao, Ndoa ya Nuh Mziwanda kukumbwa na matatizo

Nuh Mziwanda anaonekana mwenye furaha kwenye mitandaoni lakini ndoa yake sio shwari hata kamwe.

sababu moja kuu ni uvutano uliyopo kati ya mke wake na familia yake ambayo haikufurahia Nuh Mzinwanda kiuingia uislamuni ili kumuoa.

Mama yake Nuh ndio aliadhirika ata zaidi kwa sababu yeye anafuata mambo ya kanisa sana.

Stori hii ilibainika wazi wakati Soudy Brown alipata kuzungumza na mke wa Nay katika U heard Cluds FM.

“Nilimwambia mama unachelewa, mwambie aniache. Na anajua kuwa mimi sijaolewa na mwanawe, ila anajua nimezaa tu na mwanawe. Kwenye sherehe ya harusi hakuwepo, alikuwa kwenye msiba. Yule mama ni mzee wa Kanisa, alikuwa anataka niende kanisani nibadili dini ndio niolewe.” Mama Anya alisema.

Nuh Mziwanda azionyesha picha za mwanawe na mke wake

Wasanii wengi sasa hivi wameamua kuanza familia zao kwani hawana muda wa kungojea tena. Mmoja wao ni Nuh Mziwanda ambaye alibarikiwa na mtoto wa kike hivi karibuni na kama wasanii wengine ameweka picha ya mwanawake akiwa na mke wake.

Msanii huyu aliposti picha hizi katika mtandao wake wa Instagram akiziweka fikra zake wazi kupitia ujumbe aliomuandikia mtoto wake Anya na mamake. Mtindo huu pia tumeona na Diamond Platnumz na pia Rayvanny ambaye alibarikiwa na mtoto wa kiume hivi karibuni.

Nuh Mziwanda aliandika kusema…

Mungu pekee anajua jinsi gani moyo wangu na mihangaiko yangu inakulenga wewe Mwanangu #ANYAGHILE nasali sana Mungu akupe hekima ,busara ,upendo ,heshima kwa kila rika na upeo wa kujua baya na zuri ‘Nakupenda Mwanangu ANYA nipo kwa ajili yako kipenzi changu haijalishi nitaenda magharibi wala kusini katika hii dunia ? @iam_mrs_mziwanda #anameremeta video link on my bio @89studios #MariaStopesMwenge #DkSele

Tazama picha hizi hapa chini.