Christian Bella Awajia Juu Waliomposti Dimpoz Alipokuwa Mgonjwa Hoi Kitandani

Msanii maarufu wa muziki wa dansi nchini Christian Bella amewajia juu watu waliokuwa mstari wa mbele kumposti Ommy Dimpoz alipokuwa hoi kitandani lakini wakashindwa kumposti alipopona siku yake ya birthday.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Bella amesema alikuwepo wakati Dimpoz anaanza kuugua koo mpaka kufikia hatua ya kufanyiwa Upasuaji lakini amewalipua watu ambao walimposti Dimpoz wakati akiwa hoi kitandani na kumtakia apone haraka lakini alivyopona hawakufanya hivyo wala hawakuposti wimbo wake mpya aliouachia hivi karibuni.

Watu walikuwa na wasiwasi sana huenda chochote kikatokea kwa Dimpoz, walimposti sana wakimuombea apone, hadi wale ambao alikuwa haelewani nao walimposti. Baada ya hapo ikafika Birthday yake lakini hao watu hawakumposti, na hata juzi alivyotoa wimbo wake hawakumposti lakini angefariki wangemposti sana”

Ommy Dimpoz aliugua nusu ya kufa miezi Michache iliyopita mpaka kufikia hatua ya kupostiwa na kila Msanii akiwemo hasimu Wake namba moja Diamond Platnumz.

Steve Nyerere Apitia Kipindi Kigumu Sakata la Ommy Dimpoz

Msanii wa Bongo movie Steve Nyerere amejikuta katika kipindi kigumu Baada ya kusema kuwa Ommy Dimpoz hataweza kurejea na kuimba vizuri kama zamani kwa kuwa hali yake kiafya si nzuri,

Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amejikuta akikaliwa kooni baada ya mashabiki wa Dimpoz kumjia juu na kumtaka atengue kauli yake kwani haikuwa nzuri hasa kwa Ommy Dimpoz ambaye anaumwa.

Gazeti la Ijumaa, Ommy Dimpoz alisema kuwa alichokizungumza ni kwamba, Dimpoz atachukua muda kurejea katika gemu tofauti na jinsi watu walivyomtafsiri kwamba hataweza kuimba kamwe.

Narudia kauli yangu nilisema hivi, atachukua muda kurudi katika gemu, kwa sababu hakuna mtu ambaye hajamuonea huruma Dimpoz wakati anaumwa, wote tulihuzunika, kwanza ni kijana mdogo amepita katika misukosuko mikubwa sana ya kimaradhi kwa hiyo sisi wote kama vijana tulimuonea huruma, ilitupasa sisi kama wasanii wenzake tuungane naye katika kipindi kile alichokuwa anapitia, lakini tunaamini kabisa kwamba itamchukua muda kurudi kwenye gemu na ndiyo kauli niliyosema mimi.

“Ni sawasawa na kocha akuambie kwamba itakuchukua muda kurudi kucheza mpira, kwa hiyo hayo maneno yanayosambaa huko mitandaoni sijui Steve kafanya hivi, sijui kafanya vile hayaniumizi kichwa hata kidogo, sina mamlaka ya kusema kwamba hataimba milele, mimi ni nani?”.

 

Ommy Dimpoz Akerwa na Maisha ya Mitadao juu ya Ukaribu Wake na Alikiba

Msanii Ommy Dimpozi ambae amechukua sana vichwa vya habari katika vituo na kurasa mbalimbali hasa baada ya kutoka katika hali mbaya aliyokuwa nayo na sasa kurudi katika hali nzuri ya kuwafurahisha mashabiki wake ambao walikuwa na wasiwasi kutokana na hali mbaya ya kiafya aliyokuwa nayo ameongea  jinsi matumizi mabaya ya mitandao yanayomchafua roho.

hata hivyo, msanii huyo anasema kuwa watu wamekuwa hawajui kabisa matumizi ya mitandao ya kijamii kiasi kwamba hata wanakuwa wakikaa wakiuliza  juu ya ukaribu wake na Alikiba kwa sasa ilhali wasanii hawa kwa sasa wamekuwa wakifanya kazi pamoja.

Ommy anasema kuwa amekerwa sana na tabia ya baadhi ya mashabiki walipokuwa wakimtumia sms Dm na kumuuliza kwani hajamposti alikiba katika ukurasa wake kumpa pole baada ya kufiwa na baba yake.

Ommy anasema kuwa amekerwa na swala hilo kwa sababu watu wengine wamekuwa akitaka maisha ya watu kuwa kama matangazo wakati kila mtu ana uhuru wa kuwa na maisha yake Private.

 

RC Makonda Awachana Wabongo Kisa Ommy Dimpoz

Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda ameibuka na kuwajia juu Mashabiki wa muziki wa Bongo fleva ambao wamegoma kuonyesha sapoti kwa muziki wa Ommy Dimpoz Baada ya kuachia wimbo mpya.

RC Makonda akimtolea mfano msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz, amesema kuwa kuna watu kipindi msanii huyo anaugua, walikuwa wanatangaza amefariki dunia, leo amepona na ametoa wimbo wake mpya wa kumshukuru Mungu watu hao wamekaa kimya kama hawajui.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Makonda ameandika ujumbe huu mzito:

Ukitaka kujua watu walivyo wa Ajabu tazama leo, Ommy dimpo alikuwa mgonjwa sana na ikafika hatua ya watu kutangaza Amekufa. Leo amerejea tena akiwa na wimbo wa kumshukuru Mungu wamekaa kimya Kama vile siyo wao waliokuwa wana post kumwombea apone. Angefariki tungeona mitandao yote imechafuka RIP Ommy oooh umeenda bado tunakuhitaji. Unafiki huu sijuwi utaisha lini, tunapenda kutangaza msiba kuliko Uponyaji”.

 

Steve Nyerere Afungukia Sakata Lake na Ommy Dimpoz

Msanii wa Bongo movie ambaye ni maarufu kwa kuiga sauti za viongozi mbali mbali w serikali, Steve Nyerere amefunguka na kuongelea skendo inayomuandama hivi sasa dhidi ya Msanii wa Bongo movie Ommy Dimpoz.

Siku za nyuma kidogo Steve Nyerere alifanya mahojiano na kituo kimoja cha habari na kusema Ommy Dimpoz hawezi kuimba tena kwa sababu ya hali ya ugonjwa wake, huku akiwaomba Watanzania kumuombea na kuwa naye karibu ili apate faraja na kupona.

Baada ya sakata hilo Steve Nyerere ameibuka na kusema maneno hayo yanayosambazwa hayana ukweli kwani yeye hakusema hataweza kuimba kabisa bali alisema hataweza kuimba kwa wakati ule.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Millard Ayo, Steve Nyerere amefunguka haya:

Kwanza niseme kuwa yupo kwenye dunia ya kubadilisha maneno na ya kugombanisha watu, Mimi sipo huko…Unapomzungumzia Steve Nyerere unakuwa unazungumzia brand , mzigo mkubwa sana usikaone hivi”.

Siachagi kunukuu kitu nilichokisema, nilisema hatoweza kuimba tena kwa muda huu, Aki-recover sijui mnaelewa maana ya ku-recover”.

Ommy Dimpoz ameweka wazi kuwa ameshangazwa na kauli ya Steve Nyerere kuwa kutokana na ugonjwa Wake hatoweza kuimba hasa ukizingatia Steve hajawahi kumtafuta kumjulia hali kipindi chote alivyokuwa mgonjwa.

 

Ommy Dimpoz Akiri Kushangazwa na Maneno Ya Steve Nyerere

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz amefunguka na kuweka wazi kuwa ameshangazwa na maneno ambayo Msanii Steve Nyerere alisema Juu yake.

Kwenye mahojiano aliyofanya siku za nyuma na chombo kimoja cha habari, Steve Nyerere aliibuka na kusema Dimpoz hawezi kuimba tena kwa sababu ya hali ya ugonjwa wake, huku akiwaomba Watanzania kumuombea na kuwa naye karibu ili apate faraja na kupona.

Ommy Dimpoz amemjia juu Stevw Nyerere juu ya kauli hiyo na kumtaka awe makini na maneno yake kwani hajawahi hata siku moja kumpigia simu na kumjulia hali hivyo asingeweza kujua afya yake.

Muda mwingine tunapaswa tuzitumie vizuri hizi kamera, kama kuna kitu huna uhakika ni vizuri usikizungumze, ungeweza hata kunitafuta kwanza, ila mimi sina tatizo nae, alijikwaa tu”.

 

Ujerumani Waliniambia Nilibakiza Wiki Moja Kufa, Usaha Ulijaa Tumboni- Ommy Dimpoz

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz amefunguka na kuelezea Jinsi ugonjwa Wake ulivyotaka kumuua Wiki chache zilizopita.

Katika mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari, Ommy DImpoz amefunguka  kuhusu ugonjwa wake wa koo ulivyokuwa ukimsumbua na kusema alibakiza wiki moja tu angefariki dunia kwani madhara ya tatizo alilokuwa nalo yalikuwa makubwa na sumu ilikaribia kuingia kwenye maini.

Wakati sijafanyiwa upasuaji wa kwanza, madaktari waliniambia upasuaji utakuwa mkubwa, hivyo wakanikupa muda wa kukaa na kujitafakari tena na nikaongea na familia yangu pamoja na wasimamizi wangu na wao waliniambia tunaimani kuwa nitatoka salama na kunisihi kufanya upasuaji na nikafanya.

Upasuaji ulichukua saa sita mpaka kumi na moja. Madaktari walikata tumboni mpaka karibia na kifua, pia shingoni na sehemu zingine na walifanya hivyo ili kupandisha tumbo juu na vitu vingine ili kuhakikisha wananusuru maisha yangu.

Nilivyoenda Ujerumani, walivyonicheki wakagundua ‘usaha’ umezidi na unakaribia kuingia kwenye maini na nilibakiza wiki moja tu, ningechelewa basi habari ingekuwa imeisha. Walinifanyia upasuaji wa dharula na waliniambia ingechukua saa nne lakini ilichukua saa 8, nilikaa hospital wiki tatu, nashukuru imenisaidia na kwa sasa naendelea vizuri Alhamdulillah“.

Hivi sasa Ommy Dimpoz ambaye amerejea nchini siku chache zilizopita ameonekana kuendelea vizuri na hata kutoa wimbo wake mpya.

Ugonjwa Wangu ni Zaidi ya Ule wa Tekno ;-_Ommy

Msanii Ommy Dimpoz amefunguka alipokuwa akiongea na  Millard Ayo na kusema kuwa ugonjwa aliokuwa akiumwa yeye ni tofauti na ule wa Tekno kwa sababu pamoja na kwamba msani mwenzake huyo aliambiwa kuwa alikuwa na matatizo katika koo lakini hakufikia hatua ya kufanyiwa upasuajika kama yeye alivyokuwa amefikia.

Ommy anasema kuwa katika maisha yake alikuwa amezoea kuona na kusikia kuwa watu wanaingia ICU nakutoka na wengine walikuwa wanakufa endapo wanaingia huku, hata alipokuwa akiona katika TV alikuwa hanaona  ICU na kuiogopa sana kutokana na sifa zake lakini kitu cha kushangaza tangu aliapoanza kuumwa mpaka sasa anmejikuta ICU ameshaizoea.

Tatizo langu lilikuwa kubwa zaidi, sijui kama tekno alifikia huko kwenye maoperation kama mimi, nilikuwa naziona kwenye tv tu hizo Icu , nilikuwa naambiwa tu kuwa kuna ICU , Nikiambiwa mtu kaingia ICU nilikuwa naogopa na kuona kama kuna taarifa nyingine mbaya inaweza kuja lakini kwa sasa mpaka nimeshazizoea.

 

Mh.Makonda Akerwa na Tabia ya Watu Kuzushiana Vifo.

Mkuu wa Mkoa wa jijini Dar amefunguka na kusema kuwa watu wamekuwa na tabia ya kusema mambo ya uongo hasa maswala ya kuzushiana vifo kitu ambacho kinakuwa kinaleta kukatisha tamaa hasa kama mtu ni mgonjwa.

Makonda anasema kuwa  msanii Ommy dimpoz amekuwa akiugua kwa muda mrefu sana mpaka sasa amerudi kuwa mwenye afya lakini watu wengine wamekuwa wakitangaza kuwa msanii huyo amefariki Dunia.

Mh makonda anasema kuwa watu hao hao waliokuwa wakitangaza kuwa msanii huyo amekufa  sasa hivi wako kimya baada ya kugundua kuwa  msanii huyo kwa sasa tuo vizuri na anaimba wimbo wa kumsifa bwana.

Mh Makonda anasema  kuwa endapo ingetokea kweli msanii huyo angepoteza uhai wake basi kila mtu angeweka katikamtandao RIP na kuanza kulalamika kuwa msanii huyo ameondoka bado wanamuhitaji.

 

Ommy Ahaidi Kuoa Tanzania, Asema Hatoki nje Kama Wengine.

Ommy dimpoz ambae hana siku nyingi tangu amewasili kutoa Afrika ya Kusini ambapo alikuwa akipatiwa matibabu ya maradhi yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda mrefu sasa amefunguka na kusema kuwa hana mpango wa kuoa nje ya nchi kama wanavyofanya wasanii wengine.

Akijibu maneno ya waandishi wa habari, amefunguka na kusema kuwa ingawa amekuwa na mpango wa kuoa wanawake wanne, anategemea kuwa kuwa watatu wote wanatoka tanzania na kama kuna mmoja ataongezeka basi anaweza kutafuta kutoka nje.

Kumekuwa na malalamiko sana kuwa wasanii wengi wa Tanzania wa kiume wamekuwa wakienda kuoa nje ya nchi na kuacha wanawake wa tanzania wakilalamikia swala hilo.

Ninawaahidi dada zangu wa Tanzania kuwa nitaoa Tanzania, watatu tanzania na pengine mmoja kutoka nje , maana naona wenzangu wote wanatoka nje.

Ommy Dimpoz Arejea Nyumbani.

Baada ya kuugua kwa muda mrefu, msanii ommy dimpoz hatimaye ametua nyumbani na kuonekana kwa sasa hali yake inaendelea vizuri huku akishukuru wale wote waliokuwa waamuombea.

Ommy ambae amekuwa na hali mbaya kama walivyokuwa wakiripoti mara zingine anasema kuwa sasa yuko vizuri lakini pia anawashukuru sana wale waliokuwa wakizusha kuwa amekufa wakati walikuwa hawana taarifa kamili kuhusu hali yake.

Ommy dimpoz anaonekana mwenye afya na mwe nye furaha sio kama ilivyokuwa hapo awali akionekana akiwa kitandani na hali yake ikiwa mbaya,

Hata hivyo hii ni habari njema kwa mashabiki wa msanii huyo mpaka kufikia hatua ya kurudi nyumbani ina maana msanii huyo kwa sasa atakuwa mwenye afya iliyotengemea.

Hata hivyo haijafahamika kuwa msanii huyo atachukua muda gani mpaka kurudi katika hali ya kufanya muziki tena.

Ommy dimpoz alisema ‘lakini watu wanachojisahaku kuwa sisi binadamu owte tunapita na kila mtu atakufa na hata mimi pia ntakufa, kuhusu kuimbakwa sasa siwezi kuzungmzia.

Ommy Dimpoz Afunguka Baada Ya Kurejea Nchini

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz amerejea nchini Tanzania rasmi kutoka majuu alipokuwa kwa ajili ya matibabu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers,  katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam wakati akirejea nchini Ommy Dimpoz amesema haamini kama amerudi nyumbani licha ya watu mbalimbali kumzushia kuwa amekufa.

Hali kama unavyoiona mimi mwenyewe siamini naona nimefika nyumbani, kiukweli kuhusu uzushi wa kifo nishazoea kwa sababu ya kazi niliyoichagua inatufanya tuzoee hali kama hii. Lakini wanachojisahau duniani wote tunapita kila mtu atakufa na mimi nitakufa, kuhusu kuanza kuimba kwa sasa siwezi kuzungumzia chochote“.

Ommy Dimpoz alianza kuumwa mwaka jana Baada ya kuwekewa sumu na kusababisha kulazwa nchini Africa ya Kusini kwa miezi kadhaa ambapo alifanikiwa kutoka na kupona kabisa Lakini mwaka jana mwishoni ilisemekana kuwa amezidiwa tena na kutajwa kuwa nchini Ujerumani kwa ajili ya matibabu.

Ommy Dimpoz Aibukia Nchini Kenya

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz ameonekana nchini Kenya Baada ya kipindi cha muda kidogo ambacho hakuonekana.

Ommy Dimpoz amekuwa kimya kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii toka Decemba Mosi mwaka jana. Kuliibuka taarifa za yeye kuzidiwa na kupelekwa nchini Ujerumani kwaajili ya matibabu  tena lakini taarifa hizo zilitupiliwa mbali na watu wake wa karibu.

Baada ya kimya kirefu Ommy Dimpoz ameonekana nchini Kenya akiwa na msanii wa Kenya anayejulikana Kama Willy Paul Msafi.

Willy Paul ameposti picha inayomuonyesha akiwa na Ommy Dimpoz katika ukurasa wake wa Instagram na kusindikiza kwa maneno yaliyosomeka “Happy to see my Brother”.

https://www.instagram.com/p/Bs5lkk6gEuB/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1n9rmz0yf9jxe

Ommy Dimpoz na Willy Paul wamekutana Kenya, bado haijajulikana iwapo wawili hao wamekutana kwa lengo la kudumisha urafiki au ni kazi pekee.

Ommy Dimpoz ampiga mkwara Baba yake Mzazi.

Ommy Dimpoz amempiga mkwara mzito baba’ke, mzazi Faraji Nyembo kisa kikitajwa ni ugonjwa wake. Chanzo makini kutoka Sumbawanga anakoishi mzee huyo kilieleza kwamba Dimpoz alimtumia ujumbe baba yake huyo na kumpiga mkwara mzito kuwa kuanzia sasa asizungumzie kwenye vyombo vya habari au kwa watu baki kuhusu afya yake au mambo yoyote yanayomuhusu ili yabaki kuwa mambo ya kifamilia zaidi.
“Unajua baba Dimpoz ni muongeaji sana, huwa hapendi kuficha mambo sasa ile anavyozungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mwanaye huyo kumbe ilikuwa inamkera hivyo amempiga mkwara mzito kwamba kuanzia sasa asizungumze chochote kuhusu yeye. “Hii inatokana na kwamba Dimpoz hataki watu wajue kuhusu afya yake vile anavyoumwa kwa hiyo anaona baba yake kama anamuharibia wakati alitaka kuufanya ugonjwa huo kuwa siri, ndiyo maana amepata hasira,” kilisema chanzo .

Baada ya kupata habari hizo, gazeti la Risasi lilimsaka baba Dimpoz kwa njia ya simu ambapo alifunguka kuwa ni kweli amepata ujumbe huo mzito ambao umemuhuzunisha kwani hakutarajia ingekuwa hivyo. “Dimpoz amemtumia mtu ujumbe aniletee mimi kwamba kuanzia sasa siruhusiwi kuzungumza chochote kuhusiana na yeye hivyo nimenawa mikono kwa kweli sasa. “Nilikuwa namzungumzia kwa uzuri tu mwanangu na kumtetea kwa wale wanaomsema vibaya lakini kaona nilikuwa nafanya vibaya, nimekubaliana naye kwa kuwa hata hainisaidii kitu chochote katika maisha yangu,” alisema baba Dimpoz. .
Alipotafutwa Dimpoz kwa njia ya simu kwa kutumia mtandao wa kijamii wa WhatsApp kwa kuwa yupo Kenya, iliita bila kupokelewa.

Ommy Dimpoz Adaiwa Kumpa Maneno Makali Baba Yake

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz amedaiwa kumchimba mkwara mzito baba yake mzazi Faraji Nyembo.

Gazeti la Ijumaa linaripoti kuwa Ommy Dimpoz alimtumia ujumbe baba yake huyo na kumpiga mkwara mzito kuwa kuanzia sasa asizungumzie kuhusu afya yake au mambo yoyote yanayomuhusu.

Siku za nyuma kidogo kuna taarifa zilisambaa kuwa Ommy Dimpoz alizidiwa na kurudishwa tena nchini Ujerumani kwa ajili ya matibabu taarifa ambazo baba yake na Ommy alithibitisha.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi, Baba Dimpoz alifunguka kuwa ni kweli amepata ujumbe huo mzito ambao umemuhuzunisha kwani hakutarajia ingekuwa hivyo.

Dimpoz amemtumia mtu ujumbe aniletee mimi kwamba kuanzia sasa siruhusiwi kuzungumza chochote kuhusiana na yeye hivyo nimenawa mikono kwa kweli sasa.

Nilikuwa namzungumzia kwa uzuri tu mwanangu na kumtetea kwa wale wanaomsema vibaya lakini kaona nilikuwa nafanya vibaya, nimekubaliana naye kwa kuwa hata hainisaidii kitu chochote katika maisha yangu”.

Inasemekana kuwa Dimpoz hataki watu wajue kuhusu afya yake vile anavyoumwa kwa hiyo anaona baba yake kama anamuharibia wakati alitaka kuufanya ugonjwa huo kuwa siri, ndiyo maana amepata hasira.

Familia Ya Ommy Dimpoz Yafungukia Afya Yake Baada ya Kusafirishwa Nchini Ujerumani

Siku chache zilizopita kuna taarifa zilisambaa kuwa Staa wa Bongo fleva Ommy Dimpoz amezidiwa kwa Mara nyingine na kurudishwa nchini Ujerumani kwa ajili ya matibabu.

Global Publishers wanaripoti kuwa baada ya Ommy Dimpoz kufanyiwa upasuaji wa awali wa koo hadi tumboni  alipata tatizo la kujaa usaha ambalo ndilo lililomfanya azidiwe na familia ikalazimika kumpeleka Ujerumani baada ya kushauriwa kuwa kuna wataalam wazuri wa tatizo lake.

Gazeti la Ijumaa Wikienda lilimvutia waya baba mzazi wa Dimpoz aliyeko Sumbawanga mkaoni Rukwa ambapo alipopatikana alithibitisha mwanaye kuzidiwa hivi karibuni na kwamba amepelekwa nchini Ujerumani kwa matibabu zaidi.

Ni kweli walinijulisha kwamba mwanangu amezidiwa tena, wakampeleka Ujerumani kwa ajili ya matibabu zaidi kisha kufanyiwa operesheni kwa mara nyingine na nimekuwa nikiwasiliana nao kujua hali yake.

Kikubwa kabisa niwaombe Watanzania wenzangu tumuombee Dimpoz, bado anaumwa yupo hospitalini, tumuombee aweze kuwa na afya njema”.

Lakini pia Gazeti hilo lilimsaka Meneja wa Ommy, Seven Mosha ambaye alifunguka kuwa Dimpoz kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu nchini humo na kwamba hali aliyokuwa nayo awali na sasa, ni vitu viwili tofauti, afya yake imeimarika maradufu na sasa anaweza kuongea vizuri kwani sauti inatoka.

Kwa sasa kwa kweli tunamshukuru Mungu yupo vizuri. Alivyoenda kule na alivyo sasa kwa kweli tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu, amepata ahueni kubwa”.