Mh Makonda Aongeza Muda wa Kupiga Matamasha Usiku.

Ikiwa ni zaidi ya mwaa sasa tangu mh paul makonda alipotangaza kuwa muda wa kupiga matamasha na shoo mbalimbali jijini dar es asalaam itakuwa mwisho saa sita, lakini sasa imebadilika baada ya Mh huyo kusikia kilio cha wasanii na kuamua kuwaongezea muda tena.

Paul Makonda aliamua kufanya hivyo kwa ajili ya usalama wa raia na mali zao lakini ameshaona kuwa usalama na ulinzi umeimarika lakini pia kaungalia na kujalai kazi za wasanii pia.akiongea katika eneo ya wazi alipokuwa katika siku ya kazimisha kuzaliwa kwa msani Diamond Platinumz jijini katika mtaana wa Tandale, Mh Paul Makonda ameongeza na kusema kuwa kwa siku za wikiend kutaongezea mpaka saa nane .

Habari hizo zimepokelewa kwa shangwe  na wasanii wote kutokana na kilio hicho kuwepo kwa muda mrefu hasa kutokana na kwamba muda uliokuwepo haukuwa unatosha kutoa burudani kwa mashabiki wao.

Mh.Makonda Awatoa Wananchi Hofu Kuhusu Hali ya Ommy Dimpoz

Mkuu wa mkoa wa Dar Es salam Paul Makonda amefunguka na kuwatoa hofu wananchi na mashabiki wa Ommy Dimpoz kwa muda mrefu baada ya kusambaa kwa taarifa kuwa msanii huyo yuko mahutiuti hospitali nje ya nchi akiwa katika chumba cha watu wasiojiweza.

Katika ukurasa wake wa instagram Paul Makonda amsema kuwa ameongea na msanii huyo na kwamba amemwambia anaendelea vizuri na hivi karibuni atarudi kuendelea nae na mazoezi.

Jana saa 8 usiku nilipata nafasi ya kuongea narafiki yangu Ommy Dimpoz,nilifurahi sana na kupiga stori na ndugu yangu  hsa baadaya kujua kuwa anendelea vizuri na soon tutarudi GYM.

Kumekuwa na post nyingi sana za wasanii na watu wa karibu walioguswa na habari za Ommy Dimpoz kusambaa kuwa yuko katika chumba  cha ICU kwa muda sasa kutokna na hali yake kubadilika.

Hata hivyo meneja wake alikanusha na kusema kuwa msanii huyo alikwenda hospitalini hapo kwa ajili ya kufanya chck-up inayotakiwa kufanya kila baada ya muda, hii inaweza kutokana na picha ya hospiali aliyokuwa ameweka ommy katika mtandao wa snapchat.

 

Wanaokuombea Mema Wako Wachache-Ujumbe Wa Makonda kwa Lulu.

Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salam Paul Makonda amemuandikia ujumbe mzito msanii lulu michael katika siku ya kumbukumbu wa kuzaliwa amabyo kwa upande wak hatoweza kuisherekea kutokana na kuwepo gerezani akitumikia kifungo chale cha miaka miwili baada ya kukutwa na hukumua ya kuua bila kukusudia.

Katika siku hii ambayo ndugu wa lulu waliamua kusherekea siku hiyo  wakitoa zawadi na misaada katika hospitali ya Muhimbili kama moja ya kumuombea msanii huyo , Paul Makonda aliamua kutuma ujumbe huo hata kama hatoweza kuuona kwa sasa ila unaweza kumfikia.

kumbe wanaokuombea mema wako wachache ila wenye nyusoza huzuni wako wengi sana   japo hawamaanishi.kwa  kuwa mungu ametenda watakuja tena na nyuso zao za furaha  japo hazina uhusiano na mioyo yao.kwa kifupi hii ndio dunia ambayo mungu amkuongezea mwaka mwingine wa kuishi.Happy birthday mwanangu @elizabethlulumichael

Lulu alifungwa baaada ya kukutwa na hatia ya kusababisha kifo cha marehemu Kanumba ambae alikuwa ni mpenzi wake.

RC Paul Makonda Amwagia Misifa Lukuki Wema Sepetu

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameshindwa kujizuia na kumwagia Misifa Lukuki msanii wa Bongo movie Wema Sepetu baada ya kujishindia tuzo ya muigizaji bora wa kike katika tuzo za SZIFF.

Tangu Wema ashinde tuzo hiyo siku ya jumapili Kumekuwa na maneno maneno mengi hasa kutoka kwa wasanii wenzake wa Bongo movie ambao wameona kuwa hajastahili kushinda tuzo hiyo.

Paul Makonda amemwagia sifa hizo Lukuki Wema na kuwajia juu wale wote wanaoziponda tuzo hizo zilizoandaliwa na Azamu Tv na kudai watu hao hawana hata uwezo wa kuandaa tuzo za kuku.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Paul Makonda alimwagia Wema sifa hizi:

Naomba picha uliopokea Tunzo kwa sababu nimesikia maneno maneno kwa watu wasioweza hata kuandaa tuzo za kuku. Hongera Azamu Tv mmefanya kuliko hata matatajio ya watu. Endeleeni kufanya vyema ili mwakani mpokee tuzo tena na wale wenye kukosa endeleeni kukosa ili mwakani mkose tena. Huu ndio Utamaduni unaofanya wenye kufanikiwa wachukiwe na wenye kuchukia kujifariji kwa maneno bila kuweka bidii katika kazi”.

 

Wema Azidi Kumwaga Sifa Kwa RC Makonda

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu amezidi kumwagia sifa na kuonyesha kumkubali sana mkuu wa moja wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda.

Wema Sepetu na RC Makonda walisemekana kuwa kwenye bifu hii ilikuwa mwaka jana baada ya Makonda kumtaja Wema kwenye listi ya watu wanaotumia madawa ya kulevya na kisha Wema kufiki uamuzi wa kuhama Chama na kuhamia Chadema.

Mwaka jana mwishoni kabisa disemba Wema alitangaza kurudi CCM na siku chache tu baada ya kurudi CCM Wema alionekana pamoja na RC Makonda wako pamoja wakipiga stori na hata kupiga picha na kuziweka mtandaoni.

Tangu hapo Wema kaheuka shabiki namba moja kwa Makonda yaani humwambii kitu kuhusu Makonda na jana usiku kupitia ukurasa wake wa Instagram alimuweka Makonda na kumuandikia ujumbe uliopita gumzo:

And he keeps doing what he does best….My RC…. Mtumishi wa Mungu….Hujalazimishwa Kupenda lakini….Gudnyt world”.

 

“Uoga ni uzembe” Babu Tale amtaje anayemlaumu kwa kupotea kwa Roma Mkatoliki

Msanii Roma Mkatoliki na wenzake wamepotea bila ya yeyote kujua nani aliwateke, wamepelekwa wapi na nia yao ni ipi.

Wasanii wengi wamehofia usalama wa Roma na wenzake kwasababu hata polisi hawajui nani aliwateka. Watu wengi kwenye mitandao ya kijamii wanahusisha kitendo hiki na masuala ya siasa yanayoendelea nchini hivi sasa.

Roma Mkatoliki

Babu Tale, meneja wa Diamond, ameweka wazi kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ndiye anafaa kulaumiwa kwa kupotea kwa Roma.

Babu Tale amemtaka Makonda awaeleze Watanzania kule Roma alipo, anasema kuwa yeye ndiye kiongozi wa kamati ya usalama Dar es Salaam kwahivyo anafaa ajue Roma alipo.

Paul Makonda

Uoga ni uzembe me nazani mwenye jukumu la kujua Roma yupo wapi ni Mkuu wa koa sababu yeye ndio kiongozi wa kamati ya usalama ya mkoa sasa ikiwa tumezunguka vituo vyote vya polisi na mwenzetu atumuoni nani wa kumfuata kumwambia tunamtaka mwenzetu kama sio @paulmakonda me naanza hili bila uoga mkuu wa mkoa naomba utusaidie kutuambia mnzetu @roma2030 alipo. Tukutane Tongwe mida hii me nipo kwa foleni wakuu #uogauzembe#freeroma,” Babu Tale aliandika kwa Instagram.

 

Diamond akutana na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika ofisi ya Wasafi kuzungumzia wizi wa kazi za wasanii

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda alikua mgeni wake Diamond Platnumz jana Aprili 4. Makonde alialikwa katika ofisi ya Wasafi na staa huyo wa muziki.

Afisa huyo wa police alifanya kikao na wadau wakuu wa Wafasi, walizungumzia wizi wa kazi za wasanii na mambo kadha wa kadha zikiwemo changamoto mbalimbali.

Tazama kikao hicho kati ya Wafasi na Paul Makonda kwenye video hapo chini:

Paul Makonda asema vijana wengi wameacha madawa ya kulevya tangu awachukulie watu maharufu hatua

Paul Makonda anaonekana kuwa mtu anayefuraha nyingi baada ya kufanya vijana waache kutumia madawa ya kulevya. Katika sherehe zilizofanyika hivi majuzi, Paul Makonda alisikika akisema kuwa vijana wengi wameacha madawa kupitia jitihada alizofanya kwa kushirikiana na Watendaji wengine wa Serikali.

Soma:“Mkome kunihusisha na watu wasio jua kitu chochote kuhusu maisha yangu” Wema Sepetu awaonya mashabiki
Mh Makonda huyu amesema kuwa jambo hilo linawafurahisha wazazi wengi walikuwa wanahofia watoto wao kupotea kwa kutumia madawa haya. Ingawa si wote wamebadilika, Makonda anaendelea kujitia moyo kuwa siku itafika na pia wao watanaswa na mkono wa serikali kuwanyosha.

Mwezi uliopita Paul Makonda aliwapeana amri kuwa Wema Sepetu, Romy Jones, TID na wengine wakamatwe kwa kushukiwa kuwa walikuwa wanahuika na mauzaji na matumiaji ya dawa za kulevya.

Lakini kwa sasa Paul Makonda amemsifu TID kwa kusema kuwa anaendelea vizuri na pia afya yake inaendelea kuwa nzuri. Hivi sasa anvutia kisura na ikiwa amejitolea kuachan madawa kabisa, basi mwezi ijayo atakuwa mtu wa maana tena

Mwanamuziki mashuhuri Temba amsifia Paul Makonda kwa kazi anayoitenda ya kupigana na dawa za kulevya

Mwanamuziki mashuhuri Temba ametokea kumsifia  Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwa kazi anayoifanya kupigana na madawa ya kulevya.

Paul Makonda amekua ofisini kwa mwaka mmoja na tayari amefanya mabadaliko makubwa ambayo yametambulika Tanzania na nchi zinazo karibia kama Kenya.

Kuamua kwake kulenga wanamuziki san asana lilishtua wengi lakini kweli matokeo yake inaonekana. Hilo ndilo jambo limefurahisha Temba ambaye alizungumzia jambo hilo kwenye Millard Ayo.

“Kwanza nianze kwa kumpongeza Makonda pia kitu ambacho kilinifurahisha kwenye huu mwaka mmoja wa RC Makonda ni kuona jinsi alivyokuwa anazunguka kwa wananchi kwa ajili ya kutafuta kero za Wananchi, pia kingine ni kuhusu hii ishu ya Dawa za Kulevya nampongeza sana Makonda wewe ni shujaa ishu ya Dawa za Kulevya si mchezo” Temba alisema.