Petit Man Afungukia Kuvunjika Kwa Ndoa Yake na Esma

Mdau wa Sanaa ya Bongo fleva ambaye pia anasimamia wasanii wenye majina makubwa kama vile Country Boy, Petit Man wakuache ameibuka na kuongelea Ndoa Yake na Esma.

Petit Man aliyekuwa  kwenye ndoa na Dada wa staa wa Bongo fleva nchini Diamond Platnumz aitwaye  Esma Platnumz amefunguka kuhusu kuvunjika kwa Ndoa hiyo.

Baada ya kuishi kwenye ndoa kwa miaka minne na kufanikiwa kuzaa Mtoto mmoja ajulikanaye kama Taraj wawili hao walisemekana kuachana mapema mwaka huu.

Kwenye mitandao ya kijamii kuna skendo ilisambaa kuwa Petit hakuwa mwaminifu kwa mke wake hadi kupelekea kuzaa na mwanamke mwingine kipindi cha ndoa yao.

Katika mahojiano aliyofanya na Millard Ayo, Petit Man kwa mara ya kwanza ameweka wazi suala la kuachana Man Esma:

Kwenye mahusiano kuna makosa, kila Binadamu ameumbwa lakini ana mapungufu yake, Mimi na Esma tuliishi miaka mitano siwezi weka hadharani yaliyotokea yule ni Mke wangu tumezaa nae, matatizo yapo ni kawaida” .

Esma Ataja Sifa Za Mwanaume Anayetaka Kuwa Naye Baada Ya Kumwagana Na Petit

Dada wa Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Khan ‘Esma Platnumz’amefunguka na kutaja sifa za mwanaume anayetaka kuwa naye sasa baada ya kumwagana na mume wake Petit Man.

Siku ya jana Esma aliweka wazi kuwa yeye na Petit waliachana kipindi kirefu kidogo na kisa cha kuachana kikiwa ni Mumewe kuzidisha kuwa na michepuko.

Kwenye mahojiano na kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, Esma ameweka wazi kuwa yeye ndio alimuacha Petit na kabla hajamuacha alimfuata mama yake na kumwambia matatizo ya Mumewe na kukiri kuwa mama yake alimsema sana.

Lakini pia amesema hivi sasa anatafuta nyumba ya peke yake ili aweze kuanza maisha mapya peke yake na pia ametajwa sifa za mwanaume ambaye atapenda kuwa naye Kwenye Mahusiano kwa sasa:

Kwanza  mwanaume ambaye namuhitaji ni mwanaume gentleman anayejielewa, mwenye kazi yake nzuri, Awe sio mtu wa drama na Instagram yaani Awe yule mwanaume ambaye yuko straight tunapanga kufanya kitu fulani tunafanya yaani in short nataka mwanaume anayejielewaa kama mimi mwenyewe”.