Q-Chillah Atoa Shukrani Zake kwa Mh.Rais

Msanii mkongw wa muziki wa bongo fleva q-chillah amefunguka na kusema kuwa moja ya watu anaowashukuru sana mabao hawakutaka yeye aachane na muziki ni mh rais ambae aliwatuma watu na kwenda kuongea nae ili asiweze kuacha muziki.

Chillah anasema kuwa hapo ndipo alipomini kuwa muziki wake una mchango mkubwa sana na mpaka kufikia hatua ya mh raisi kutuma wajumbe kwenda kumuomba yeye hasiache muziki kwake ni jambo kubwa sana.

Chillah ambae alikuwa ametangaza kuachana na muziki kutokana na athari kubwa alizowahi kuzipata za kutumia madawa ya kulevya kutokana na muziki huo huo anasema kuwa kwake yeye hiyo ilikuwa ni heshima kubwa sana.

Baada ya interview nilipata meseji na simu nyingi sana kutoka kwa watu mbalimbali,na nilifarijika zaidi nilipoona Mh. Rais ametuwa watu wake waje kuongea na mimi  nisache muziki taifa bado linanihtaji.

Kutangaza Kuacha Muziki Haikuwa Kiki:-Q-Chillah

Msanii mkongwe wa muziki, Q-chillah mefunguka na kuongelea swala lake la kutangaza kuacha muziki na baadae kurudi tena katika muziki kuwa sio kiki kama watu wanavyosema kwamba alitaa kufanya hivyo ili kutengeneza attention kwa mashabiki wake bali alikuwa ameamua kuachana na muziki ili kufanya kitu kingne na sio muziki tena.

Q-Chillah anasema kuwa kilicokuja kutokea ni baada ya kupokea simu kutoka nje na kuongea na moja ya watu waliwahi kuupenda sana muziki wake na kumwambia kuwa amekuwa akiona na kukijua kipaji chake siku nyingi hivyo haoni sababu ya yeye kuacha muziki bali anaomba kufanya nae kazi.

Q-chillah anasema kuwawat wengi wamekuwa wakija na kumsema kuwa alichofanya ilikuwa ni kiki lakini ukweli ni kwamba alikuwa akiona  jinsi ambavyo muziki wake ukimuendea pabaya,

kama niliweza kuomba ridhaa ya  watu wakati nataka kufanya muziki  ndio maana hata wakati nataka kuacha ilinibidi kuomba ridhaa ya kuacha haikuwa rahisi  rahisi kama inavyodhaniwa lakini pia haikuwa kiki kama watu wanavyofikiria.-Aliongea Q-chillah alipokuwa akiongea na waandishi wa habari wa Clouds tv 360.

 

Kabula Amwagia Sifa Kiba Q Chillah Amuita Dhahabu

Muigizaji wa Bongo movie aliyewahi kutamba katika filamu ya Jumba la dhahabu Jini Kabula amefunguka na kuonyesha kuumizwa na Kitendo Cha Q Chief kutangaza kuacha mziki.

Mwezi uliopita msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Q Chillah aliweka wazi kuwa anataka kuachana na muziki baada ya kukata tamaa baada ya kushindwa kurudi kwenye chati kama zamani.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Kabula ameamua kutoa ushauri juu ya maamuzi aliyoyafanya Q Chillah kuhusiana na kuachana na muziki.

Wee unaanzaje kumuacha mtu kama huyu apotee kizembe ifike mahali Taifa lipaze sauti kwa vijana nguvu kazi Chilla ni dhahabu ya Tanzania alipotangaza kuacha mziki roho ilipasuka nikasema No bado anauwezo mkubwa wa kuipeperusha bendera ya Taifa letu.

Wewe ni dhahabu kaka na dhahabu haiwezi ngaa bila kupita kwenye moto huwezi kuwa shujaa mpaka ukutane na mengi ya kukuumiza moyo na kukukatisha tamaa lazima udharauliwe ukataliwe na wakati mwingine kunenewa maneno ya uwongo ila ukiweza kutobowa hakuna anaweza kukushusha chini tena.

Sisi ni mashujaa wa Taifa ata tukiondoka leo tutaacha histolia ktk vizazi vijavyo acha ya zamani yaende simama ukainuliwe kaka…Watanzania tunakupenda tuko pamoja Maisha na mziki Go chilla”.

Bushoke Amkingia Kifua Q-Chillah

Msanii wa muziki wa kitambo kidogo, bushoke amefunguka na kumtetea rafiki yake ambae pia ni msanii mwenzake q-chillah na kusema kuwa sio kweli kuwa alishawahi kuja kulala kwake kwa sababu ya kuishiwa au kuwa na maisha magumu kama watu wamekuwa wakizusha kwa sababu kwa jinsi anavyomju rafiki yake huyo ana uwezo wa kulala sehemu yoyote kwa kuamua.

Akiongea na eNews, bushoke anakanusha taarifa za kuwa Q-chillah alipoachana na mwanamke wake aliamua kwenda kukaa kwake kama kujiifadhi kutokana na kuwa hakuna na sehemu maalum ya kukaa kwa kipindi icho ivyo aliamua kumpa hifadhi .

Q-chief hajawahi kuja kukaa kwangu na ikitokea anakaa kwangu basi ujue kaja kupiga stori tu  na sio kwamba ana shida ya kulala.kuna watu wa kawaida ambao hawawezi kukosa sehmu ya kulaa, q-chillah hawezi kukosa sehemu ya kulala,ni maamuzi tu ya leo akalale wapi na anaweza hata akaenda kulala anapopataka  maana anaweza kwenda kulala hata Nairobi. 

 

Q-Chillah Atangaza Kuendelea Na Muziki Aweka Kando Mawazo Ya Kuacha

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva aliyewahi kutamba na kibao chake ‘Ulinikataa’ miaka ya nyuma Q Chillah ameweka pembeni mipango yake na ya kuacha muziki na kuendelea kupambana.

Wiki iliyopita Q Chillah aliwashtua watu wengi pale alipofanya Interview na kutangaza kuachana na muziki kwa kila alichodai kuwa amekuwa akifeli kwa kila wimbo anaotoa kwa hivi sasa.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha XXL cha Clouds Fm, Q Chillah amedai baada ya kupata ushauri wa watu wengi tangu atangaze kuachana na muziki ameamua kuendelea kupambana:

Kinachonitafuna mimi ni mimi mwenyewe, maisha yangu ya nyuma yananihukumu. Lakini I don’t want to be a prisoner of my past”

Tangu nimetangaza kuacha muziki, nimeona mapenzi ya watanzania, nimeona mahaba yao, mpaka nimejiuliza tatizo sio support ya watanzania, labda ni mimi, au sikupata msaada niliohitaji ili kufanikisha maendeleo ya kazi yangu”.

Wiki iliyopita Q Chillah aliweka wazi kutoakana na kuhangaaika na muziki alijikita akiingia Kwenye matumizi ya madawa ya kulevya yaliyosababisha mpaka kukimbiwa na mke wake.

Mzee wa Upako Ampigia Simu Q-Chief ,Ni Baada ya Kusikia Anaacha Muziki.

Mwanamuziki Q-Chillah hivi karibuni alitangaza rasmi kuacha muziki na kusema kuwa mambo mengi yamemtafuna na kumfanya ashuke sana kimuziki ikiwa  ni pamoja na athari mbaya ya matumizi ya madawa ya kulevya.

Hata hivyo baada ya kuongea hivyo watu wengi waliguswa na historia na maamuzi yake na wengi wamekuwa wakimpigia simu, kati ya hao pia yupo Mzee wa upako ambae alimpigia sim u na kuongea nae ili kumsaidia.

Nimepokea simu kutoka kwa mze wa upako, antony lusekelo usiku wa saa tisa unaweza kuona ni jinsi gani watu wameumia na hili anasema ameguswa sana na aliposikia alitaka kama kulia hivi. na pia nimepigiwa simu na maustadhi wakubwa sana.-Alisema Q-Chillah akiwa anaongea na clouds Tv.

Hata hivyo anasema kuwa amefikia maamuzi hay kwa kuamua yeye mwenyewe na hana kinyongo na mtu lakini tangu ametangaza kuacha muziki anaona kuwa watu walikuwa na mapenzi makubwa sana na yeye kuliko laivyokuwa akidhani.

 

Nuru The Light Aguswa na Matatizo Ya Q-Chillah

Mwanamuziki wa Bongo fleva mwenye makazi  yake  nchini Sweden aliyetamba na kibao chake cha Mhogo mtamu, Nuru The Light amefunguka kuguswa na kuimizwa na majanga yaliyomkuta Q challah.

Mwanzoni mwa wiki hii Q chief alifanya Interview na Bongo 5 na kufunguka mazito kuhusu maisha yake ikiwemo jinsi madawa ya kulevya yalivyo muharibia maisha yake na kusababisha kuacha mziki na kukimbiwa na mke wake.

Nuru The Light ni moja kati ya watu walioguswa na janga hilo lililomkuta Q chillah na kuwataka watu wampe sapoti kwani nafasi bado ipo ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika ujumbe huu:

Naandika this with heavy heart.Jana usiku sana nimeona interview mbili tofauti na Q Chief maisha yake kwasasa na Changamoto anazopitia. HE Spoke Very open na kwa unyenyekevu kuhusu kuacha MZIKI. INDUSTRY YA MZIKI INA SIRI NYINGI NA CHANGAMOTO NYINGI SANA. INDUSTRY hii INA watu wazuri na Wabaya Pia.

Q imeniuma kuwa unajiona huwezi au unakosea wakati you are The Real talent kwani Industry yetu inawatu wanaoweza kukufanya uonekane huwezi au uangamie kabisa na nimesikitishwa kuwa They took one of The best.Umekiri ulikosea kwa kutumia madawa na kuacha tuna wasanii wakubwa kwenye kila tasnia ndani na nje wanaotumia na walitumia na bado wanafanya shughuli zao vizuri tu.Your misstake should not define you or Your talent.

Q bado nafasi yako ipo na bado uwezo unao.Nyie ndio mliopigania huu MZIKI sasa kwanini Leo hii msile yale matunda.Kuanzisha kitu na kukipigania na kuonwa kizuri sio kazi ndogo kabisa naomba mjivunie hilo wasanii wa zamani na hata wajinga pumbavu mashabiki wakiwatukana kwa kutumia maneno YA umefulia,zilipendwa dont ever feel that kwani kazi mloifanya ni kubwa mnaijua kuliko anybody else.Ningependa ujue kutoka kwangu mie that I love you, I appreciate you, Respect you vilevile natambua nafasi yako kwenye MZIKI wa Bongoflava.

My People Q anatuhitaji sisi more than ever let US support kazi yake mpya Saratani akiitoa cause inawezekana kuwa his last“.

 

 

Q-chillah Afunguka Kukimbiwa na Mke , Kuacha Muziki kwa Sababu ya Madawa.

Siku kama moja iliyopita msanii Q-chillah alifumnguka na kutangaza rasmi kuwa ameamua kuach muziki huku akiwa na sema kuwa sababu kubwa ni familia yake ambayo kwa sasa anaona kuwa inamuhitaji sana kuwa nao karibu.

Q-Chillah ambae ameka katika game kwa muda wa miaka 14 katika game la muziki anasema kuwa imefika sehemu inaidi kuwapisha watu wengine kwa sababu kuna watu ambao inad=bidi waendeleze  gurudumu.

q-chillah anakiri kuwa ni kwa sababu ya marafiki wabaya ambao alikutana nao na walikuwa hawataki kumuona akiwa katika mafanikio na ndio maana aliweza kuingia katika madawa ya kulevya na hata kupata skendo mbaya katika mitandao ya kijamii.

Q-Chillaha anasema kuwa sababu kubwa ambayo anahisi ilimpelekeka hayo yoet ni baada ya yeye kukosa malezi mazuri kutoka kwa baba na mama yake na ndio maana hata inawezekana kabisa kuwa hakuwa na misingi ya kumfanya asimame katika kile alichokuwa anakiamini sana.

Q-Chillah anasema hakupaswa kuwa msanii hata mara moja zaidi ya kuwa mcheza mpira au daktari kutokana na historia ya wazazi wake, lakini kwa sababu alilelewa na uncles, aunties na grandma ndio maana amekuwa hivyo mpka kufikia hatua ya kujiingiza kwa marafiki wababy waliompeleka katika mada wa ya kulevya.

Q-chillah anasema kuwa swala ya yeye kuingia katika madawa ya kulevya lilimuathiri sana yeye lakini hasa familia yake kutokana na maswali mengi waliokuwa wakikutana nayo ndugu zake , mke wake na hata watoto wake waliokuwa wakienda shule na hii ilimpelekea kutaka kutoka kabisa katika tatizo hilo.

Q-Chillah anasema kuwa mke wake alimkimbia na kumuacha kwa sababu ya kutumia madawa ya kulevya.

 

Q-Chillah Aelezea Jinsi Alivyotaka Kujiua, Ametangaza Rasmi Kuacha Muziki.

mwanamuziki mkongwe wa bongo fleva amefunguka mengi alupokuwa akiongea na dizzim online  baada ya waandishi wa habari baada ya tetesi kusambaa kuwa msanii huyo ameamua kuacha muziki na kuamaua kufanya vitu vingine.

q chillah amefunguka na kuelezea wakati mgumu aliowah kuupitia kipindi cha nyumba hasa baada ya kujiingiza katika madaw aya kulevya mabapo ilimchukua muda mrefu mpaka kurudi katika game na kusema kuwa maamuazi makubwa ya kauachana na madawa yalikuja baada ya kuona kuwa kuna kuwa na hukumu kubwa sana kwa familia yake wanapokuatana na jamii inayowazunguka.

q-chillaha nasema kuwa alikuwa akihumia sana anaposikia watoto wakimuuliza maswali magumu sana ambayo walikuwa wakiyasikia wakiwa shule au mtaani na hiyo ndio ilimfanya kuomba msaada na kuamua kuacahana na vitu hivyo kabisa .

Hata hivyo q-chillah anasema kuwa kuna kipindi alitaka kujiua akiamini kuwa hiyo ndio njia sahihi ya yeye kupambana na matatizo yake lakini alipanza kusali na kuingia katika toba aliomba kuondolewa mawazo hayo huku mawazo yake mengi yalikuwa yakimpeleka kuokoka kwa sababu muda mwingi alikuwa akisikiliza nyimbo za dini kutokana na anguko la kiimanai alilokuwa nalo.

Q-Chillah anasema kuwa anafurahi kuona wasanii wengine wakifanikiwa na kwenda nje ya nchi wakarudi na tuzo na kuamini kuwa hicho ndicho kitu kikubwa mabacho walikuwa wakikitafuta kwa muda mrefu na kimefanikiwa lakini anaamua kuchukua maamuzi ya kuacha muziki huku akiamiani kuwa inawezekana muda wake wa kuendesha gurudumu hilo umekwisha na kuwapisha wengine kuendelea nalo.

Q-Chillah anasema kuwa alitaka kutoa wimbo wake wa mwisho lakini roho nyingine inamtaka kuacha kutoa nyimbo hio lakini kitu kikubwa anachoamini ni kwamba  ameamua kuacha muziki lakini anataka kuacha kwa kuaga kwa heshima maana asipofanya hivyo ni kama anaogopa .

Q-chillah anakubali kusema kuwa anacaha muziki lakini inauma sana yeye kuacha muziki na ndugu na watu wake wa karibu wengi hawakukubaliana nae na hata yeye mwenyewe hajui anakwenda kufanya nini lakini anatamani sana kuendelea ila anaona kuwa ni bora kuacha muziki.

Q-Chillah: Sina Tatizo na Papi Kocha Wala Baba.

Msanii mkongwe wa bongo fleva nchini Q-Chief amefunguka na kusema kuwa hana ugomvi wala matatizo yoyote na wasanii Papii Kocha na baba yake lakini kuna baadhi ya watu wametaka kuwaonyesha umma kuwa wao ni maadui au kuna kitu wanataka kuwafanyaia ili waonekana kama hawapo sawa.

Maneno hayo ameyasema Q-Chillah siku chache baada ya kumalizika kwa show ya kuwakaribisha wasaii hao wawili Papii na baba yake Mzee Nguza baada ya kuwa nje ya game la muziki kwa muda mrefu kutokana na wao  kuwa gerezani.

Q-chillah anasema kuwa alipata ruhusa na barak zote kutoka kwa mc na hata wasanii wenye show yao lakini kitu cha ajabu alishangaa kuona mic inazimwa na akashindwa kuendelea na show yake kwa uda huo.

wakati mimi nina perfom wimbo wangu wa kwanza wa nikilala naota katika show yao nilipata baraka zote kutoka kwa mc na hata papii na baba pia,so kwenye kazi unapoona watu wana muitiko mzuri na wewe inabidi ujiongeze.na kutokana na mapezni yao na mimi ilibidi kufanya kazi yangu kama vile ninavyokuwa nafanya sehemu nyingine, kwa sababu natumia nguvu nyisa sana katika kazi zangu lakini kitu cha ajabu ile napanda tena jukwaani naona kipaza sauti kimezimwa.

Sitaki kuweka kuwa nilikuwa na tofauti nao lakini nilikuja kuzijua baada ya kuziangalia zile video vizuri baadae nilipokuwa na watuwangu wa karibu ndipo hata mke wangu aliponiuliza kimetokea nini.lengo langu lilikuwa ni kuroa burudani tu na kumfariji rafiki yangu ambae alikuwa nje ya ulimwengu wetu kwa muda mrefu, 

Hata hivyo Q-Chillah anasema kuwa kama kutokea kwa tatizo la kuzimwa kwa kipaza sauti basi ilo sio tatizo la Papii Kocha au baba ila lilikuwa ni tatizo la fundi mitambo aliyekuwepo kwa muda ule.

Sio tatioz la papi wala mzee wangu nguza kwa sababu wao waka hawaitaji stress sasa hivi,litakuwa ni kosa la wale waliokuwa wanashughilika na mitambo kule nyuma maana ndio anashugulika na vyombo vyote.

Q-Chillah Afunguka Kupotea Kwa Siku Tatu Bila Mawasiliano.

Siku chache zilizopita msanii mkongwe wa muziki nchi Q-chillah alisemekana kutoweka nyumbani kwake na ndugu na watu wake wa karibu kushindwa kumfika kimawasilianao hivyo kuwatia wasiwasi watu wake wa karibuni kwa muda wa siku tatu hivyo kudhani kuwa msanii huyo ametekwa na kufanywa vitu vibaya.

Q-chillah amefunguka na kusema kuwa kupotea kwake kwa kutatanisha kulitokana na kukosa mawasiliano sehemu aaliyokuwepo ambapo alikuwa ametoka na rafiki yake kwenda kwenye mazungumzo.

Akizungumza na risasi vibes Q-chillaha anasema kuwa amesikitishwa sana na huzuni aliyowaachia watu wake wa karibu baaada ya kutokupatikana kwake kwa sabab hakutegemea kama itatokea icho kilichotokea kwa sababu ni kitu ambacho hakupanga kufanya hivyo lakini yeye yuko salama wala hakupoatwa na tatizo lolote baya.

nimeumia sana sikujua kama hayo mambo yatakuwa makubwa hivyo,kunarafiki yangu mmoja alikuwa hapa Dar akaniambia kuwa alikuwa na mazungumzo na mimi.

sikumkatalia na tulipanga kuwa tutaenda kufanyia mazungumzo yeti mkoani Morogoro,tukaenda  hadi sehemo moja Morogoro inaitwa Matombo.kufika nikakuta kule kna views nzuri za mimi kuweza kuja kufanya video zangu za mbeleni.basi tukazidi kuzonga lakini sikujua kuwa huko tunakoenda mawasiliano yanazidi kukatika kabisa,simu yangu ikakata netiweki na tayari tulikuwa tulishafika mbali sana.

ilinichukua siku mbili kule , siku ya tatu narudi   lakini simu yangu bado ilikuwa ikisumbua netiweki , nikashughulikia tatizo ili nakuja kuiwasha nakuta meseji nyingi sana  kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki zangu.

Familia ya Q-chillah iliapta wasiwasi kutokana na matukio mengi yanayowatokea wasanii ya kuwa wanatekwa na kwenda pasipojulikana na kuumiza hata wengine kuuwawa.Hata hivyo Q-chillaha anaomba radhi kwa watu wote waliokuwa na hofu ju yake na kuwahakikishia kuwa yeye yuko salama kabisa.

Q-Chillah Aingilia Ugomvi Wa T. I.D na Chid Benz.

Msanii mkongwe wa Bongo Fleva Q-Chillah ameingilia ugomvi unaoendelea kati ya msanii Chid Benz na msanii mwenzyie T.I.D.Wawili hao walijikuta wakiwa katika marubano mazito baada ya msanii T.I.D  kumtuhumu Chid Benz kuwa hafai kusaidiwa,  na tabia yake ya utumiaji wa madawa ya kulevya haiwezi kuisha. Wiki  iliyopita T.I.D alipokuwa anahojiwa katika eNews ya Clouds tv alisema kuwa  ili Chid Benz  aweze kusaidika basi inabidi apelekwe dentention akiwa amefungwa pingu akitulia afunguliwe  akaendelee na muziki wake.

Katika kujibu maneno ya T.I.D , Chid Benz alisema kuwa maneno aliyoyasema T.I.D  ni unafiki kwa sababu yeye anachojua T.I.D ni rafiki yake na kama ameweza kuongea maneno hayo basi T.I.D  ni mnafiki.Kwa mujibu wa Chid Benz yeye ni T.I.D ni marafiki walishafikia hatua ya kushare mpaka magari na T.I.D alikuwa akilala nyumbani kwao .

Akiwa kama rafiki wa karibu wa wasanii wote wawili ,msanii Q-Chillah  ameamua kuongea kuhusu ugomvi huo na kusema “Chid na T.I.D wapo kwenye same situation,wote wanahitaji msaada,tofauti ya Chid na T.I.D ni kwamba Chid anafanya open sana  alafu T.I.D haonekani,kwaiyo wote waache kurushiana maneno wanahitaji msaada”

“Hayo wanayoyafanya ni mambo ya kike,kurudishana maneno ya kwenye khanga” ameongezea Q-Chillah

Katika mahojiano hayo yaliyofanywa na kituo cha Clouds Tv kipindi cha eNews , Q-Chillah amesema kuwa hata alipojitolea kumsaidia kuna baadhi ya watu walisema na yeye anarudi kulekule “Nilijitoa kumsaidia  Chid Benz,lakini baadhi ya watu wakasema na mimi narudi kulekule, nilimsaidia kwa sababu nilihisi kuna siku na yeye atanisaidia mimi. nilijitolea kama kaka,kama rafiki, na ipo siku na yeye atasaidia wengine ”

Kwa muda sasa kumekuwa na kurushiana kwa maneno kati ya wasanii hao   huku T.I.D akionekana kama kuponda Chid Benz, hata hivyo kwa muda sasa Chid amerudi katika game la musiki na kutoa wimbo wake aliomshirikisha Q-Chillah unaojulikana kwa jina la “Muda” ambao pia umekuwa ukifanya vizuri katika vituo mbalimbali  vya Tv na Radio.