Queen Darleen Adaiwa Kuchomoa Kwa Tanasha

Dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’ amedaiwa kuwa hana shobo na Mpenzi mpya wa kaka yake Tanasha Donna.

Wiki iliyopita Diamond alimtambulisha Mpenzi Wake Tanasha kwa Familia yake nzima ambapo alikuwepo Mama Yake, Dada yake Esma na Ndugu wengine Lakini Queen Darleen hakuwepo katika tukio hilo.

Gazeti la Ijumaa Wikienda linaripoti kuwa Queen hakuwepo kwenye ‘mnuso’ huo kwa sababu ‘haziivi’ kivile na Tanasha. “Unajua Queen yeye katika wanawake wote wa Diamond, hakuna mwanamke ambaye anamkubali zaidi kama anavyomkubali Zari.

Yeye chaguo lake ni Zari na si mwanamke mwingine. Ndio maana unaona hana taimu na Tanasha, Esma na mama yake wao hawana shida, wanaunga mkono mwanamke yeyote ambaye Mondi atawatambulisha”.

Baada ya tetesi hizo, Gazeti hilo lilimtafuta Queen Darleen ambaye aliulizwa sababu za kutoonekana na wifi yake kama wanafamilia wengine alijibu:

Queen alianza kwa kuhoji kuna ulazima gani kuwepo

Kwani Tanasha ni mtu wa kawaida tu. “.

 

 

Queen Darleen Amwaga Chozi Kisa Mama Yake

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika Kundi la WCB, Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’ amejikuta akibubujikwa na machozi baada ya kumuongelea mama yake.

Sakata hilo lilitokea Wiki iliyopita kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha Wasafi Tv, ambapo  Queen Darleen aliulizwa mtu gani ambaye angependa sana kumuona kwa mwaka 2019.

Queen Darleen aliingia kilio huku akisema ombi  lake pekee kwa mwaka 2019 ni kuongea na mama yake mzazi ambaye hayupo naye kwa sasa hali iliyopelekea wasanii wenzake aliokuwa nao kuanza kumfariji.

Kumekuwa na tetesi kuwa Mama yake mzazi na Queen Darleen yupo kizuizini nchini China ambapo amekamatwa na madawa ya kulevya tangu mwaka jana Mwanzoni.

Queen Darleen wala familia yake hawajawahi kukubali tetesi hizo ambazo zimeshawahi kutengeneza headlines kwenye social media Lakini pia hakuweka wazi mama yake alipo kwa sasa.

Queen Darleen Aanika Tabia Yake Mbaya

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika Kundi la WCB, Mwanahawa Abdul maaruufu kama Queen Darleen amefunguka na kuanika tabia yake mbaya.

First Lady wa WCB amefunguka na kuweka wazi kuwa, alipokuwa mdogo alikuwa chau­roho kwani alipenda sana kukomba chakula akiwa anakula na watu wengi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Queen Dar­leen alisema alifikia hatua ya kuonekana na tabia hiyo kwani kila al­ipokuwa anakula kwenye sahani au sinia na wen­zake, alikuwa akikomba chakula na kujikusanyia upande wake.

Nilikuwa na tabia mbaya sana, yaani tukiwa tunakula wengi kwenye sinia halafu nione kama wananizidi spidi, naanza kukomba chakula, najiku­sanyia upande wangu yaani nilikuwa mroho kupitiliza, ila mama yangu aliikome­sha hiyo tabia kwa sababu ilikuwa ikitia aibu mbele za watu”.

Queen Darleen alifunguka maisha hayo aliyokulia uswahilini ‘Tandale’ pamoja na kaka yake staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

“Bwana Angu Anajiheshimu Siwezi Kumuanika Mitandaoni”- Queen Darleen

Msanii wa muziki wa Bongo fleva na First Lady wa WCB, Queen Darleen ameibuka na kusema kuwa kamwe hataweza kumuanika Mpenzi Wake kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu anajiheshimu.

Kwa muda mrefu kumekuwa na masaki juu ya mahusiano binafsi ya Queen Darleen kwani ameshawahi kutoa kauli ambazo zilizua utata ikiwemo kuwa yeye hajawahi kuwa na boyfriend na ni bikra wakati ana mtoto.

Lakini Kwenye mahojiano yake na Bongo 5, Queen Darleen anaweka wazi kuwa ana Bwana lakini hawezi kumuweka kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu jamaa huyo hapendi mambo hayo.

Simuweki wazi mwanaume wangu kwa sababu yeye mambo ya mitandao ya kijamii hapendi ni mstaarabu sana, anajiheshimu, Muislamu safi halafu ni muelewa sana kwa sababu haya mavazi yangu hana tatizo nayo kwa sababu amenikuta katika mazingira haya”.

Lakini pia Queen Darleen aliweka wazi kuwa mwanaume aliyewahi kumuweka kwenye ukurasa wake wa Instagram na kumtambulisha Kama Mpenzi Wake alikuwa ni mshkaji Wake tu.

Watanzania Wanapenda Sana Mapenzi Kuliko Kula- Queen Darleen

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB, Queen Darleen ameibuka na kuweka wazi sababu za kupendelea kuimba nyimbo za mapenzi.

Queen Darleen amesema anapenda sana kuimba nyimbo za mapenzi kwa sababu Watanzania wanapenda sana mapenzi kuliko kula kwaiyo nyimbo za mapenzi zimekuwa na soko zaidi Bongo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Queen Darleen ameweka wazi kuwa wasanii wengi Bongo soko lao lipo kwenye nyimbo za mapenzi ndio maana hata ukiangalia nyimbo hizo ndizo zinafanya vizuri zaidi.

Unajua Watanzania wanapenda sana Mapenzi kuliko kula kuliko hata kufanya kazi ndio maana nyimbo za mapenzi zinafanya vizuri zaidi kwenye Bongo fleva na ndio maana wakina Mbosso, Lavalva wanafanya vizuri na Diamond Mpaka leo yupo kwenye chati kisa nyimbo za mapenzi “.

Queen Darleen amesema anatamani Label ya WCB isaini Msanii wa kike ili yeye apate chagamoto ya kufanya kazi nzuri zaidi.

 

Sipendi Kusifiwa :-Queen Darleen

Watu wengi wanapenda kupokea sifa hasa pale wanapoonekna kupendeza hasa pale wanapokuwa wamevaa vizuri na kupendeza lakini kumbe hii iko tofauti kwa baadhi ya watu mmoja wapo akiwa ni Queen Darlen ambae yeye anasema kuwa hapendisana kusifiwa .

Queen Darlen anataka kuwa tofauti kabisa na watu wegine kutokana na msimamo wake huo huku akisema kuwa hapendie kabisa kusifiwa na amekuwa akichukia sana anpokuata na maoni ya kusifiwa katika ukurasa wake wa instagram.

mimi nachukia sana ninapona mtu ananisifia eti kwamba nimependeza, kwa sababu unaweza kukuta umependeza lakii mtu anakwambia ujapendeza au haujapendeza mtu anakwambia umependeza,  na mtu akiniambia isjapendeza nasikia raha hivyo hivyo , maana watu wa instagram wanafurahisha sana,

Kwa kutiia mkazo kabisa Queen darlen anasema kuwa yeye bado ni bikra.

Queen Darleen Adai Yeye ni Mkali Wa Mapenzi

Msanii wa muziki wa Bongo fleva na First Lady wa WCB, Queen Darleen ameibuka na kujitamba kuwa yeye ni mkali pale linapokuja Suala la mapenzi hakuna wa kumshinda.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Sam Misago Tv, Queen Darleen alianza kujisifia na kujimwagia sifa kemkem huku akidai kuwa yeye ni mtamu na romantic sana kwenye mapenzi.

Nakwambia Mimi ni mtamu halafu niko romantic sana kwenye Suala la mapenzi.

Halafu pia sinaga historia ya kuwa kwenye mapenzi na mwanaume kwa Wiki mbili wiki tatu halafu akiondokaga lazima tu arudi”.

Lakini pia pamoja na kujimwagia sifa kibao Queen Darleen alifunguka kuhusu mapenzi yake:

Kwenye mahusiano yangu kwanza mtu akinitongoza huwa nachukia sipendi kabisa kutongozwa na isitoshe huwa sisubiri mtu anitongoze maana kunakuwa na uongo mwingi mtu anakwambia anakupenda wakati anakutamani”.

Queen Darleen ameweka wazi kuwa hata yeye akivutiwa na mwanaume na alamtamani lazima apite naye na pia ana uhakika hakuna mwanaume anayeweza kumkataa kwa sababu yeye ni staa na pia Dada yake Diamond.

 

Queen Darleen Amwaga Povu Kuhusu Mavazi Yake Ya Ajabu

Mwanamuziki kutoka katika label ya WCB na Dada wa Staa wa Diamond Platnumz, Queen Darleen ameibuka na kuwamwagia Povu zito mashabiki ambao wamekuwa wakikosoa mavazi yake.

Queen Darleen amefunguka na kusema nguo anazovaa za kimitego zinazoacha sehemu kubwa ya mwili wake hazina madhara kwake na kwa mpen­zi wake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Darleen Risasi Jumamosi kuwa, mara nyingi anaona watu wanamse­ma kuhusu nguo anazovaa, lakini hawajui kwamba yeye kama mwanamuz­iki ndizo nguo anazo­paswa kuvaa.

Kinach­onishangaza ukivaa kibukta, utasikia watu wanakusema umekaa uchi, sasa sijui wa­nataka nikiwa ninapanda stejini nivae khanga? Maana hata huyo mpenzi wangu haongei chochote kuhusu mavazi yangu jamani”.

Kwa muda mrefu sasa Queen Darleen amekuwa akikosolewa sana na mashabiki zake kutokana na mavazi yake ya kimtego ambayo amekuwa akivaa na kujianika kwenye mitandao ya kijamii.

Queen Darleen Amuomba Msamaha Baba Yake Ili Kukwepa Laana

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva kutoka WCB, Mwanahamisi Abdul maarufu kama Queen Darleen amedaiwa kumuangukia kwa magoti Baba yake Mzee Abdul baada ya kuwa bifu la muda mrefu.

Sintofahamu kati ya Baba Diamond na mwanaye ilianza baada ya Queen Darleen kutoa kauli kuwa baba yake ni Diamond Platnumz na kudai Mzee Abdul sio Baba yake Tena.

Global Publishers wanaripoti ili kukwepa laana ya mzazi, hati­maye  Queen Darleen ametambua umuhimu wa wazazi na kuamua kumfuata na kumuomba msa­maha Baba yake.

Kwenye mahojiano na Global Publishers Baba Diamond amesema ni kweli awali ali­kuwa na ugomvi mkub­wa na Queen Darleen na ikafikia hatua mpaka ya kumtamkia maneno mazito kuwa hata akifa binti yake huyo asimzike ila anamshukuru Mungu kwamba mwanaye huyo ametambua makosa yake na kujirudi.

Haya ni mambo ya kawaida tu katika familia, ni kweli mimi na Queen Darleen tulikuwa na ugomvi mkubwa mpaka ikafikia hatua nikamtamkia maneno mabaya kwamba iki­tokea nimefariki dunia asije kunizika, jambo ambalo si zuri, lakini ameyatambua ma­kosa yake, akaja kuniomba msa­maha na mimi nikamsamehe kwa moyo mmoja”.

 

Mimi Kama bi Kidude , Tusipangiane Mavazi. _ Queen Darlen.

Msanii wa muziki nchini Tanzania, Queen Darleen amefunguka kuwa yeye kwenye muziki wake hajawahi kushuka kwenye muziki kama watu wengi wanavyodai kuwa wasanii wakike wanashindwa ku-maintain kwenye game.

Darleen amesema kuwa yeye hajawahi kushuka toka enzi hizo na kujifananisha na marehemu Bi. Kidude kuwa mzee wake utaendelea kuwa mzuri hata umri wake ukiendelea kumtupa mkono.

“Mimi sijui wao lakini mimi toka  hizo zama za kina Lady Jaydee, akina Ray C mpaka leo hii mimi bado nipo, nakwenda nao level za akina Nandy, yaani mimi nipo humo humo na sitoki yaani na wasitegee kutoka leo, kesho yaani mimi kama bi Kidude nakufa na muziki wangu,“amesema Queen Darleen kwenye mahojiano yake na Wasafi TV.

Kwa upande mwingine, Queen Darleen amezungumzia mavazi yake ambayo mashabiki wake wamekuwa wakimshambulia kuwa anavaa nusu utupu jambo ambalo ni kinyume na maadili ya Mtanzania.

“Kama mimi navaa najiona mwenyewe napendeza, niko fresh, lakini mtu anakuja anakwambia unavyovaa umevaa vibaya hujapendeza? My Friend pesa yangu ambayo nimenunulia nguo mimi unayoniambia sijapendeza, hiyo simu yako uliyoshika gharama yake hazilingani.. Tusipangiane mavazi wala maisha.“amesema Queen Darleeen.

Kuhusu muziki Queen Darleen ameahidi kuachia kazi yake mpya ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa na amewataka mashabiki wake wawe wavumilivu kwani WCB kuna mfumo wa namna ya kuachia ngoma.

“Sijawahi Kushuka Kwenye Muziki”-Queen Darleen

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB, Queen Darleen ameibuka na kudai kuwa yeye ni msanii wa kike ambaye hajawahi kushuka Kwenye chati.

Queen Darleen ambaye hivi sasa amesainiwa chini ya Label ya kaka yake Diamond Platnumz, WCB amedai pamoja na kwamba ni mkongwe lakini hajawahi kushuka na mpaka sasa anakimbiza na wasanii wapya kama Nandy na wengineo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Wasafi TV, Queen Darleen amesema kuwa yeye hajawahi kushuka toka enzi hizo na kujifananisha na marehemu Bi. Kidude kuwa mzee wake utaendelea kuwa mzuri hata umri wake ukiendelea kumtupa mkono.

Mimi sijui wao lakini mimi toka  hizo zama za kina Lady Jaydee, akina Ray C mpaka leo hii mimi bado nipo, nakwenda nao level za akina Nandy, yaani mimi nipo humo humo na sitoki yaani na wasitegee kutoka leo, kesho yaani mimi kama bi Kidude nakufa na muziki wangu”.

Lakini pia Darleen amewatolea povu zito mashabiki ambao wamekuwa wakiponda mavazi yake anayovaa:

Kama mimi navaa najiona mwenyewe napendeza, niko fresh, lakini mtu anakuja anakwambia unavyovaa umevaa vibaya hujapendeza? My Friend pesa yangu ambayo nimenunulia nguo mimi unayoniambia sijapendeza, hiyo simu yako uliyoshika gharama yake hazilingani.. Tusipangiane mavazi wala maisha”.

Licha ya Kuwa na Mtoto, Queen Darleen ni Bikra.

Haitakuwa mara ya kwanza kwa mwanadada Queen Darleen kukaa katika media na kutangza kuwa yeye bado bikra ukiachana na kuonekana kuwa yeye ni mcharuko mbele ya watu, hata hivyo wa habari za kutoka kwa watu wae wa karibu inasemekana kuwa mwanadada huyo ana mtoto mmoja mkubwa alyewahi kuzaa huko miaka ya nyuma.

Mwanadada huyo kutoka katika lebo kubwa kabisa nchini na inayofanya vizuri katika muziki yaani WCB , Queen Darleen amesema kuwa watu wanatakiwa kuamini kuwa yeye bado bikra na ametulia sana kulikoa hata vile wanavyomuona katika sehemu mbalimbali.

Queen Darleen anasema kuwa watu wengi wamekuwa wakimuona kama vile hana sifa za kuwa mwanamke bora, mwanadada huyo anajitetea na kusema kuwa anafaa kuolewa na mwanaume bora na kwamba anasifa zote za kuolewa sio mapepe kama wanavyofikiria.

Queen Darleen- Uongo na Usaliti ni Vitu Sivitaki Kwenye Mahusiano

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB, Queen Darleen amefunguka na kuanika vitu vieili ambavyo havifumbii macho kabisa anapokuwa Kwenye Mahusiano.

Queen Darleen ameweka wazi kuw anapokuwa Kwenye Mahusiano ya kimapenzi huwa hapendi kuwa na mwanaume ambaye ni msaliti au mwanaume ambaye ni muongo.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha Funiko Base ya Radio Five, Queen Darleen ameweka wazi endapo mwanaume akiwa na sifa hizo anamwaga:

Darleen kwenye mahusiano ni mtu ambaye hapendi uongo, hilo la kwanza, na akikaa na mtu anakaa na mtu lakini yule mtu akigundua kama amemsaliti hawezi kumsamehe.

Yaani umenisaliti na nina uhakika hata kama nakupenda vipi na tumeishi miaka mingapi mimi naachana na wewe kwa sababu imani yake Darleen atakapokusamehe basi utaendelea kuwa na mtu mwingine“.

Lakini pia Queen Darleen amekuwa mkimya sana juu ya Mahusiano Yake ingawa kulikuwa na tetesi kuwa anatoka na Mbosso lakini baadae ilikuja julikana kuwa sio kweli.

Mimi na Esma Muda Wote Tukikutana Tunapiga Umbea Tu;-Queen Darleen

Mwanadada mrembo pekee kutoka WCB amefunguka akiwa anaongea na dizzim online na kutoa msimamo wa mahusiano yake na dada yake ambae ni Esma Platinumz na kukanusha kuwa hawana mahusiano mazuri kama watu wanavyodai katika mitandao ya kijamii.

Akiongea na mwandishi Queen anasema kuwa yeye na Esma mara nyingi wakikutana wanapiga sana umbea kuhusu mambo ya mjini na wanaongea vizuri kama kawaida”mimi na esma wambea haswa, tukikutana muda wote sisi tunazungumzia vitu vya umbea tu. kwanza tukikaa na Esma dakika mbili lazima tugombane.”

Lakini pia Queen amezungumza kuhusu kutokuonekana kwa rich mavoko WCB na hata kutoa nyimbo kwa sasa na amesema “mavoko yupo na mavoko tunafanya nae kazi ofisini kama kawaida hakuna tatizo lolote lile.

Queen Darleen- Bado Nampenda Zari

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva kutoka label ya WCB Queen Darleen ambaye pia amejipatia umaarufu kwa kuwa dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, amefunguka na kusema bado anampenda aliyekuwa wifi yake Zari.

Zari alimwaga aliyekuwa mpenzi wake Diamond Platnumz mwezi uliopita lakini mpaka leo bado wanatengeneza headlines kwenye mitandao ya kijamii kwa kuongelewa.

Queen Darleen amefunguka kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers ambapo aliulizwa kuhusu mawifi zake kwa Diamond hasa kwa sababu Amekuwa hatabiriki yupo upande gani maana bado ana urafiki na Penny ambaye alikuwa mpenzi wa zamani wa kaka yake.

Queen Darleen ameongelea mapenzi yake kwa Zari huku akikiri kuwa bado anampenda sana wifi yake huyo:

Kwanza kabisa watu wajue mimi nampenda sana Zari Tena sanaa lakini kiukweli huko nyuma nilimpenda Wema kwa sababu ndiye alikuwa ni wifi kwa kipindi hiko lakini Penny amebaki kuwa rafiki yangu hadi sasa”.

Lakini pia Queen Darleen alifunguka kuhusu Hamisa ambapo amedai yeye na Hamisa hawana mazoea sana anachojua yeye yule ni mama wa mtoto wao Abdul na walikuwa wanaonana kwenye masherehe tu huko nyuma.

Queen Darleen amekiri kuwa hapendi sana kumfuatilia Diamond na maisha yake binafsi kwani yeye hajawahi kumfuatilia hata siku moja.

Queen Darleen – Mimi ni Bikra, Natongoza Mume wa Mtu

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka label ya WCB, Queen Darleen ameshangaza watu wengi baada ya kusema kuwa yeye ni mwanamke bikra kitu ambacho hakiwezekani kwani tayari ana mtoto.

Queen Darleen alifunguka hayo alipokuwa anafanya Interview na LilOmmy kwenye kipindi cha The playlist ambapo aliulizwa status ya Mahusiano yake ya kimapenzi maana haijulikani kwani Kumekuwa na tetesi anatoka na msanii Mbosso wa WCB.

Queen Darleen amefunguka kuwa yeye sio mtu wa kuona aibu yaani akikolea kwa mwanaume akiona hatongozwi basi mwenyewe hujiongeza na kutongoza huyo mwanaume bila uoga wowote na ameshatongoza wanaume wengi huku asilimia kubwa ni waume za watu.

Mimi bikra kwanza na kuhusu kumzaa mtoto wangu Rooney Mungu kanibariki tu”.

Lakini pia Queen Darleen aliwekwa kitimoto kuhusu tukio lililotokea ambapo Baba mtoto wake alizaa na rafiki yake watoto wawili lakini bado ameendelea kuwa na urafiki na huyo mke mwenzake ambapo alifunguka haya:

Unajua mimi ni mtu wa dini sana na ninaheshimu dini yangu na dini inaruhusu mwanaume kuoa hata wanawake wanne lakini sikubahatika kuolewa kwanini nimnunie yeye na kama nina uwezo wa kutembea na mwanaume wa mtu kwanini nishindwe kumruhusu mwanaume wangu awe na mtu mwingine”.