Miss Tanzania Afungukia Tetesi Za Bifu na Basila

Mashindano wa shindano la Miss Tanzania mwaka 2018/2019 Queen Elizabeth Makune amefungukia tetesi zinazosambaa kuwa huenda ana Bifu na Basila Mwanukuzi.

Queen Elizabeth anatajwa kuwa na Bifu na Mratibu wa shindano la Miss Tanzania Basila Mwanukuzi kisa kikitajwa na kamati yake kushindwa kupewa zawadi alizoshinda kwenye shindano hilo mwaka jana.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Mchanganyiko, Queen Elizabeth alisema, hana ugomvi wowote na Basila na maneno yanayoongelewa na watu yana lengo la kutaka  kuwagombanisha.

Ningeomba niweke wazi kuwa sina matatizo yoyote na mratibu wa shindano langu, Basila Mwanukuzi, tena ninampenda sana, nipo naye vizuri tu, ningependa maneno yanayoongelewa na watu yapuuzwe, tuangalie mambo ya maendeleo ili tuweze kufika mbali zaidi na kuitangaza nchi yetu”.

Queen Elizabeth aliiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss World mwaka jana Lakini alishindwa kufanya vizuri na moja ya sababu zilizotajwa ni maandalizi mabovu kutoka kwa kamati

Miss Tanzania 2018 Atangaza Kuibuka Kwenye Filamu na Muziki

Miss Tanzania mwaka 2018, Queen Elizabeth Makune ametangaza rasmi kwamba yupo tayari kuingia kwenye filamu za Bongo movie na muziki wa Bongo fleva.

Queen Elizabeth aliibuka kidedea kwenye mashindano ya Miss Tanzania miezi  michache iliyopita na kuenda kuiwakilisha Tanzania katika shindano la Miss world China.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers Miss Tanzania amejigamba kuwa atafanya chochote kwa kuwa ana uwezo katika kazi zote alizotaja alisema kuwa, hawezi kujifunga kwenye kitu kimoja na siku zote ana imani kwamba wanaofanikiwa wengi wanafanya vitu zaidi ya kimoja.

Mbali na kuwa Miss Tanzania kwa mwaka huu 2018, niseme tu kwamba mimi ni muigizaji mzuri na ninao uwezo pia wa kuimba. Kwa hiyo siwezi kusema nitafanya muziki au filamu, chochote kitakachokuja mbele yangu nitaanza nacho, hata ujasiriamali pia uko kwenye damu”.

Kuhusu kushindwa kufika mbali  kwenye mashindano ya Miss World yaliyofanyika hivi karibuni Sanya nchini China, mrembo huyo hakuwa tayari kuongea lolote akidai haukuwa muda muafaka.

Miss Tanzania Afunguka Haya Baada Ya Kurudi Kutoka Miss World

Miss Tanzania mwaka 2018/2019 Queen Elizabeth Makune amefunguka kwa Mara ya kwanza tangu arudi nchini kutokea nchini China kwenye mashindano ya Miss World.

Mashindano ya Miss World yalifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita huko Sanya nchini China ambapo mrembo kutoka Mexico Vanessa Ponce de Leon ndiye aliyetawazwa kuwa Miss World.

Ingawa Miss Tanzania hakufanya vizuri sana na kutoka katika hatua za mwanzoni za mashindano lakini watu wengi walionekana juhudi zake katika kutaka kushinda.

Siku ya Jumatatu Miss Tanzania alirudi nchini na kufanya mahojiano na Millard Ayo, ambapo amesema anawashukuru Watanzania kwa mchango wao, pia amejifunza mengi nchini China na anashukuru kwa matokeo aliyoyapata.

Nimejifunza vitu vingi sana ikiwemo tamaduni, vimenijenga mimi kama mrembo na safari yangu haijaishia hapo huu ni mwanzo tu“.

 

 

Jokate Amtaka Miss Tanzania Ajiandae na Matusi Ya Mitandaoni

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe na Aliyewahi kuwa mlimbwende wa Miss Tanzania Jokate Mwegelo amefunguka na kumuandaa kisaikolojia Miss Tanzania mwaka 2018 Queen Elizabeth na mitandao ya kijamii.

Siku ya Jumapili Tanzania ilipata Miss mpya wa kuliwakilisha Taifa Mrembo Queen Elizabeth na mara moja mitandao ya kijamii ilianza kutoa maoni yao kuhusu Mrembo huyo.

Jokate ameibuka na kumuelezea balaa la mitandao ya kijamii na namna inavyoweza kumbomoa au kumjenga ambapo cha muhimu ni uajasiri kwani watu watakuwa na maoni mengi juu yake.

Kwenye mahojiano na Global Publishers , Jokate alisema baada ya kushinda, Queen Elizabeth amekuwa staa mpya kwa hiyo ategemee kusikia mengi kutoka mitandaoni.

Kikubwa unatakiwa kuwa tayari kupokea kila kitakachokuja kwako. Kwa sababu wakati mwingine unaweza kutukanwa kiasi kwamba ukatamani uachane na mitandao hiyo. “Lakini unatakiwa kufahamu hiyo ni hali ambayo inawakuta wengi wetu. Kwa hiyo kuwa mvumilivu na kwa upande wako itumie mitandao kwa manufaa ya jina na kazi zako”.