Chuchu Hansy- Siwezi Kumchukia Ray

Msanii wa Bongo movie Chuchu Hansy amefunguka na kusema kuwa hawezi kumchukia msanii mwenzake Vicent Kigosi ‘Ray’ ambaye ni baba wa Mtoto wake.

Kwa Wiki kadhaa sasa kumekuwa na tetesi kuwa penzi la Ray na Chuchu Hansy limefika mwisho Baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa miaka mingi na kuzaa pamoja Mtoto mmoja.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Enews cha EATV, Chuchu amesema kuwa hawezi kumchukia Ray hata siku moja kwa sababu atabaki kuwa baba wa Watoto Wake hata kama wakiachana au wakiendelea kuwa wote.

Siwezi kabisa kuongelea mahusiano yangu na Ray kwa sababu hayo ni maisha yangu binafsi Lakini mimi na yeye tupo sawa kwa sababu tunalea mtoto kwa pamoja hivyo hamna shida”.

 

Chuchu Hansy Akana Mahusiano na Frank Baada Ya Kumwagana na Ray

Muigizaji wa Bongo movie Chuchu Hansy ambaye pia ni mzazi mwenzake na staa mkongwe Vicent Kigosi ‘Ray’ amekana kuwa kwenye mahusiano na Msanii mwingine Frank Mtao.

Wiki chache zilizopita Chuchu Hansy na Ray waliweka wazi kuwa baada ya mahusiano ya miaka mingi na Mtoto mmoja wameamua kutengana. Lakini muda mfupi Kupita kumekuwa na tetesi Chuchu Hansy yupo kwenye mahusiano na Frank.

Kwenye mahojiano aliyofanya Gazeti la  Ijumaa Wik­ienda, Chuchu alisema anachojua Frank ni mzazi mwenziye na walishamalizana muda mrefu kili­chobaki kati yake na yeye ni mtoto na si kitu kingine.

Unajua nashangaa hata hayo madai ya Frank na mimi yameibu­kia wapi kwa sababu yule mtu ana familia yake na mimi nina maisha yangu mengine kabisa, sijui kwa nini watu wanapenda kuingilia familia za watu, yule na mimi imebaki stori na ni kwa sababu ya mtoto“.

 

Povu La Chuchu Hansy Baada Ya Kuachana na Ray

Muigizaji wa Bongo movie Chuchu Hansy ameibuka na kumwaga povu zito kwa mashabiki ambao wamekuwa wakimuandama na kumponda kwenye mitandao ya kijamii.

Wiki iliyopita habari zilisambaa kwenye Mitandao ya kijamii kuwa Chuchu na baba Watoto Wake Msanii wa Bongo movie Vicent Kigosi ‘Ray’ wameachana.

Baada ya habari hizo kusambaaa Chuchu aliposti picha katika ukurasa wake wa Instagram iliyomuonyesha akiwa amevaa kibukta kigumu huku kikiacha sehemu kubwa ya mapaja yake na tumbo nje.

Baada ya picha hiyo mashabiki walimsema Chuchu kuwa anafanya hayo kwa sababu ameachna na Ray hivyo anataka kujionyesha huku  wengine wakimtolea maneno machafu.

Chuchu alishindwa kujizua na kumwaga povu zito kwa watu wote ambao walimsema na kuwataka waache kumpangia maisha ya kuishi kwani hawamsaidii kwa lolote wala kwa Chochote.

Chuchu Hansy Afungukia Tetesi Za Ray Kuwa Muathirika Wa Ukimwi

Muigizaji wa Bongo movie Chuchu Hansy amefunguka na kuongelea tetesi zilizowahi kukamata headlines kuwa Mzazi mwenzake na mpenzi wake Msanii Vicent Kigosi ‘Ray’ ni Muathirika wa Ukimwi.

Chuchu amefunguka na kudai kuwa alishawahi kukumbana na maneno mengi ya kejeli ikiwemo kusema kuwa amepewa ujauzito na mwanaume ambaye ni Muathirika wa Ukimwi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Chuchu amefungukia tetesi hizo:

Nilishtushwa sana na maneno hayo ila unajua siku zote mwisho wa ubaya ni aibu kwa sababu toka waseme nina Ukimwi kupitia kwa Ray mpaka leo hii bado wananiona nadunda na wala sina hata dalili yoyote ya kuumwa”.

Chuchu aliongeza kuwa maneno hayo yaliwachukiza sana ndipo mzazi mwenziye (Ray) alipowaumbua kwa kuweka picha yake (Chuchu) mtandaoni akimnyonyesha mwanaye Jaden kuthibitisha kuwa, wote ni wazima na hapo ndipo wambeya likawashuka.

Kuna watu wengine mpaka sasa wanaona hata aibu kunitazama, wamesahau kuwa haifai kabisa kumnyooshea mwenzako kidole”.

Kwa miaka mingi kulikuwa na tetesi za Ray kuwa mgumba baada ya kutofanikiwa kupata mtoto lakini tetesi hizo zilikuja kuisha baada ya Chuchu kujifungua mtoto wao Jaden.

Ray Atamani Kumpeleka Mtoto Wake Kusoma Majuu

Msanii mkongwe wa filamu za Bongo Movie Vicent Kigosi maarufu kama Ray ameibuka na kukiri kuwa anatamani sana mtoto wake Jaden aende akapate elimu katika nchi za nje.

Ray amefunguka kuwa yupo katika mapambano makubwa ya kufa na kupona ili kuhakikisha mtoto wake wa kipekee Jaden anaenda kupata elimu bora kabisa.

Katika mahojiano yake na Gazeti la Dimba, Ray alisema si kwamba Tanzania hakuna shule bora kwa hapa nyumbani lakini ndoto zake anatamani mwanawe asome nje ya Tanzania kama ambavyo amejiwekea toka awali.

Nilitamani sana mwanangu akasome nje na akikua kidogo tu atasoma moja ya shule bora kabisa, natamani abadilishe mazingira, natambua zipo shule bora sana hapa lakini si mbaya pia akazoee na mazingira mengine, napambana kuhakikisha namwekea akiba ya kutosha ili asipate tabu katika kupata elimu yake”.

Jadrn ni mtoto wa kwanza wa Ray aliyezaa na Msanii mwenzake wa Bongo movie mwanadada Chuchu Hansy.

Chuchu Hansy Afungukia Habari Za Mimba Yake Kuharibika

Msanii wa Bongo movie na mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Ray Vicent Kigosi, Chuchu Hansy amefunguka na kuongelea suala lake la mimba kuharibika.

Siku za hivi Karibuni Kumekuwa na tetesi kuwa Mrembo huyo Chuchu Hansy amekuwa katika kipindi kigumu mara baada ya mimba aliyokuwa amebeba kuchoropoka.

Chu­chu Hans ametoa povu baada ya kudaiwa kuwa alinasa ujauzito ukachoropoka akiwa nchi­ni Afrika Kusini alipokuwa na Ray kwa ajili ya matembezi ya kifamilia.

Kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti la Ijumaa Wikienda, Chuchu alisema anawashangaa wa­naomfuatilia kila kukicha. Alisema ni ajabu kuona watu wanamfuatilia kama ana mimba au la.

Kila kukicha watu wanapenda ku­fuatilia mambo yangu na sijui ni kwa nini maana hata kama nikizaa watoto kumi na Ray, ni sawa kwa sababu ni mwanaume na ananipenda na kujali, kwa hiyo hata kama imetoka nitabeba tena hivi karibuni“.

Ray na Chuchu Hansy tayari wana mtoto mmoja wa kiume anayeitwa Jaden.

 

Chuchu Awatolea Povu Wanaomponda Kuwa na Ray Katika Mwezi Mtukufu

Muigizaji wa Bongo movie Chuchu Hansy amekuwa mbogo kwa watu wote wanaomsema yeye kuwa na ukaribu na mpenzi wake Ray Kigosi katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani ili hali yeye ni binti wa Kiislamu.

Chuchu na Ray wamekuwa Kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa muda mrefu na wamejaliwa kupata mtoto mmoja lakini wawili hao hawajafunga ndoa ambapo ni kinyume maandiko ya dini ya kiislamu kukaa na mpenzi wako hasa kwa mwezi huu.

Kwenye mahojiano na Global Publishers kwa njia ya simu akiwa nchini Afrika Kusini na mzazi mwenziye huyo kwa ajili ya kushuti filamu, alisema kuwa kuishi na mzazi mwenziye huyo kwa ajili ya kazi haoni kama ni dhambi lakini anashangaa watu wanavyotoa hukumu mitandaoni kwamba anakosea.

Mimi ninachojua wa kumhukumu mtu ni Mungu pekee kwa sababu yeye ndiyo anajua ukweli wote na anajua kila kitu cha binadamu na si mtu mwingine, najua nilivyo huku na Ray watu wanasema sana tu lakini sijali“.

Johari Aipa Baraka Zote Ndoa Ya Ray na Chuchu Hansy

Muigizaji wa Bongo movie Johari Chagula ametoa baraka zake zote kwenye ndoa ya Ex wake Ray Vincent Kigosi na mama mtoto wake Chuchu Hansy.

Johari na Ray walikuwa kwenye Mahusiano ya kimapenzi kwa miaka mingi kipindi cha nyuma lakini ameibuka na kuweka wazi kwa hivi sasa hana kinyongo na wapendanao hao kuwa pamoja.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Johari amedai kuwa hakuna kitu kitakachomfurahisha kama mwigizaji mwenzake, Vincent Kigosi ‘Ray’ akimuoa mzazi mwenziye, Chuchu Hansy.

Ray na  chuchu Hansy

Lakini pia Johari ameweka wazi  kuwa Chuchu ni chaguo sahihi la Ray maana ni mwanamke ambaye amemzalia mtoto mzuri.

Kiukweli nitafurahi sana mkurugenzi mwenzangu (RJ Company) akimuoa Chuchu. Kwanza ni mwanamke wa chaguo lake na pia amemzalia kidume cha nguvu na kwenye harusi nitakuwa mstari wa mbele“.

Ray na  Chuchu Hansy wamejaaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume anayeitwa Jaden.

Chuchu Awapa Makavu Wote Waliomsema Ray Kama Tasa na Muathirika

Muigizaji wa Bongo movie Chuchu Hansy ambaye pia ni mzazi mwenza wa staa wa Bongo movie Ray Kigosi amewatolea uvivu watu wote waliokuwa wanamsema Ray kuwa ni tasa hana uwezo wa kuzaa na pia muathirika wa Ukimwi.

Ray na Chuchu wamezaa kwa pamoja mtoto wao wa kiume anayeitwa Jaden, lakini amedai kabla hawajazaa mtoto wao Ray alikuwa mtu ambaye alisemwa sana na watu.

Ray na mtoto wake Jaden

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Chuchu amefunguka haya:

Jaden Vincent Kigosi Asante Mungu najua umejua kumkomesha vibaya baba yako najua waja walikuwa wanaongea mengi juu ya ujio wako na kabla ya ujio wako walikuwa wanasema mengi hata mimba yako nilisemwa mengi leo nimetoa kidogo ya moyoni, Miungu watu walianza kusema juu ya Baba yako mara oooh Ray hazai angekuwa anazaa sahivi angekuwa na mtoto baadae wakahamia kwangu baada ya kuharibika sura nilivyokuwa na ujauzito mara mgonjwa wa Ukimwi na mengine mengi.

Nilivyozaa wakaendelea kumsingizia Ray hawezi kuzaa mtoto na sio wake sijui Kazaa na mzungu mara mwarabu rafiki wa Ray ilimradi kutapatapa yote haya nikayavumilia na yakapita”.

 

Nilishamwambia Wema Atakuja Kupata Mtoto- Chuchu Hansy

Muigizaji wa Bongo movie Chuchu Hansy ameonekana kumkingia kifua msanii mwenzake wa Bongo movie, Wema Sepetu kuhusu suala lake la kuzaa mtoto.

Kwa kipindi kirefu Wema amekuwa akiweka wazi hisia zake juu ya watoto na kusema kuwa anapenda kuwa na mtoto siku moja lakini pia ameweka wazi wakati mgumu ambao amekuwa akipata katika jitihada za kupata mtoto.

Kipindi cha nyuma Wema alishawahi kuweka wazi kuwa miaka ya nyuma alishawahi kutoa mimba ya aliyekuwa mpenzi wake kwa kipindi hiko msanii Marehemu Kanumba, lakini tangu aweke wazi taarifa hiyo amekuwa akisakamwa mtandaoni na maadui zake ambao kila siku akimposti mtoto basi watamsema kwa nini hazai na vitu vingine.

Sikh ya birthday ya mtoto wa Ray na Chuchu anayeitwa Jayden , Wema alimposti mtoto huyo kwenye ukurasa wake Instagram jambo lililozua balaa kwani mashabiki walimvamia na kuanza kumnanga na kumuita mgumba tasa na majina mengine.

Kitendo kile hakikukaa vizuri na Chichi ambaye kwenye mahojiano aliyofanya na Enews ya East Africa TV alifunguka yafuatayo:

Kusema kweli zile comments zilikuwa nyingi sana lakini nyingi zilikuwa ni za kumuumiza mtoto kawekwa pale badala ya kusema happy birthday Jaden mtu anamuandiki liukurasa kabaisa maneno ya kumuumiza sijui mgumba sijui tasa hayo nimaisha na ni kipindi tu wao sio Mungu kama walimsema Ray ni tasa lakini leo hii Mungu kawaonyesha kampa mtoto kwaiyo na Wema asubiri kwa sababu siyo tasa alishabeba mimba mara ya kwanza lakini nilishamwambia Wema wewe utakuja kupata mtoto lakini sio pale unapohitaji wewe pale Mungu atakapopenda upate”.

Chuchu Hansy Amedai Akiachana Na Ray Hataki Mwanaume Mwingine Tanzania

Muigizaji wa Bongo movie, Chuchu Hansy amefunguka na kudai kuwa endapo atakuja kuachana na mpenzi wake Ray Vincent Kigosi basi hataki mwanaume mwingine Tanzania.

Siku za hivi karibuni tetesi zimeenea kuwa Chuchu na Ray wameachana, wawili hao ambao miezi michache iliyopita walizaa mtoto wao wa kwanza wa kiume aitwae Jayden walisemekana kuwa kila mmoja kashika njia yake na kuenda kivyake taarifa zilizo thibitishwa na kutoonekana kwao pamoja wakipiga picha na kuweka kwenye mitandao ya kijamii kitu kilicho wafanya mashabiki zao waamini moja kwa moja kuwa wapendanao hawa wameachana.

Kwenye mahojiano waliofanyiwa na kituo cha televisheni cha East Africa kupitia kipindi cha Planet Bongo katika nyakati tofauti Chuchu na Ray wamekana tetesi hizo za wao kutengana. Huku Chuchu akisisitiza kuwa endapo ataachana na Ray hataki mwanaume mwingine Tanzania;

Kuachana kupo kwa sababu kila kitu Mwenyezi Mungu ndio anapanga, kwaiyo mimi siwezi kushindana na Mungu, basi kama ikitokea ndio itakuwa imefika mwisho wetu, Ila sidhani kama nitaweza kuwa na mwanaume mwingine hapa Tanzania, sidhani, yaani sidhani kama nitaingia kwenye mahusiano Tena, yaani nahisi nitakaa kwa muda mrefu sana bila mahusiano yoyote”.

Ray pia alikana tetesi hizo na kudai kuwa hana sababu yoyote ya kuachana na mpenzi wake Chuchu kwani ni mwanamke anayempenda sana.