Ray C Aanika Majibu Yake Ya Ukimwi

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Rehema Chalamila maarufu kama Ray C ameamua kuanika majibu yake ya vipimo vya virusi vya Ukimwi alivyopima Hivi karibuni.

Ray C ambaye aliwahi kutamba na vibao vikali kama vile ‘Mapenzi matamu’ ‘Na wewe milele’ na vinginevyo ameweka wazi kuwa hana maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

Hivi sasa Ray C anaishi nchini Uingereza Lakini yupo nchini Marekani kwa ajili ya kufanya shoo ameanika majibu hayo Kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameandika:

https://www.instagram.com/p/BuCLNW7gcFM/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1dyvttiuc54cz

Ray C Afungukia Mipango Yake Ya Kufunga Ndoa na Mzungu Wake

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Rehema Chalamila maarufu kama Ray C ameweka wazi mipango yake ya kufunga ndoa na kuanzisha familia na mpenzi wake ambaye anaishi naye nchini Uingereza.

Kwenye mitandao ya kijamii kumekuwa na tetesi nyingi kuwa mwanadada huyo kwa sasa ana maisha mazuri mno huko London baada ya kuchumbiwa na m[enzi wake ambaye ni mzungu ambaye ana watoto wawili;

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Mchanganyiko, Ray C ameweka wazi mipango yake ya kufunga ndoa na kuanzisha familia ughaibuni na pia kuendeleza sanaa yake;

Mimi nipo na nina kazi (nyimbo) ambazo nilipozitoa zilifanya vizuri sana na zinaendelea kufanya poa sana. Kama watakumbuka mwaka juzi niliachia Wimbo wa Umezima, mwaka jana nikaachia Hatuachani na Rogaroga hivyo si kweli kwamba nipo kimya. Mwaka huu watege sikio maana mambo mazuri yanakuja.

Ni kweli muda mwingi niko nje ya nchi kwenye shughuli zangu binafsi, lakini nikipata shoo huwa ninafanya. Kwa mfano wiki hii nina shoo Houston (Texas, Marekani). Hivyo shoo zipo tu na zikija za huko Bongo wataniona tu.

Ukiona nipo London, ujue nipo kwa fiancee (mchumba) wangu (amechumbiwa na Mzungu, raia wa Uingereza). Ukweli ni kwamba sijaolewa, lakini nina mchumba ambaye tupo kwenye process (taratibu) za kufunga ndoa.

Natamani sana kumzalia mchumba wangu na nina mpango huo, sema acha niolewe kwanza kwani mtoto wa ndoa ana baraka zake”.

 

“Nibusu Shavuni, Vyovyote Vile, Nakupenda”- Ujumbe Wa Ray C Kwa Ruge

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Rehema Chalamila maarufu kama  Ray C amemtumia ujumbe mzito Mkurugenzi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba.

Ray C ameandika maneno yaliyowashangaza wengi huku yakiwaacha wengine vinywa wazi kwa ujumbe aliomwandikia Ruge  ambaye kwa wakati huu yupo nje ya nchi kwa matibabu.

Kupitia akaunti ya Ray C ya instagram ameandika:

Amka bwana, nashachoka kusubiri, msg zangu hujibu, simu hupokei, na stori kibao nataka kukwambia ingawa najua utanchamba lakini nishazoea kukwambia kila kitu changu kinachoendelea kwenye maisha yangu, tunagombanaga mpaka tunablokiana lakini tukionana tu tukaangaliana tunabaki kucheka tu.

Nishazoea kukwambia mambo yangu sababu we ndo msiri wangu, we ndo unanipaga makavu nikiharibu, Kuna muda mpaka nalia na ukiona nalia ndo unazidi kunipa makavu bila huruma.

Naondoka kwa hasira ingawa moyoni najua uliyoniambia ni kweli…. nakununiaaaaa ila haifiki wiki huyo nishakuja ofisini, Muda mwingine sina hata cha maana cha kukwambia ila nakuja tu ofisini kukuona unitanie nicheke!

Ray C umenimiss eeh…. Kama nywele hujazielewa unanipa live Ray nenda Katoe hizo nywele, Nikikuona tu napata amani ya moyo. Nikitoka tu studio wa kwanza kukutumia demo! ni wewe, wewe tu miaka yote tangu nimeanza muziki sababu naheshimu sikio lako na naliamini.

Mwezi wa ngapi sasa huu Ruge!Natuma msg, nakupigia, natamani kukuimbia japo kidogo upate nguvu sikupati..Ruge najua huko ulipo Unaumia sana,najua unataka kuamka na kufanya kazi zako. PLS WAKE UP babaa. Please!You are too strong babaa, Don’t give up Please..4 U

Nishike mkono, Nibusu shavuni, Vyovyote vile, Nakupenda. (Your favorite song )
#AmkaRuge”.

 

Ray C Amtumia Ujumbe Mzito Ruge Mutahaba

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva nchini Rehema Chalamila ‘Ray C’ ameibuka na kumtakia ujumbe mzito Mkurugenzi wa Clouds Media group na mdau mkubwa wa muziki wa Bongo fleva Ruge Mutahaba.

Miezi michache iliyopita Ruge alianza kuugua ingawa familia yake haijawahi kuweka wazi anaumwa nini lakini kumekuwa na tetesi kuwa ana ugonjwa wa figo.

Ray C ambaye aliwahi kuongozwa kimuziki na Ruge amemtumi ujumbe mzito wa kumlilia na kumtaka apone haraka ili aweze kurudi katika nafasi yake ya zamani.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ray c amemuandikia ujumbe huu Ruge:

https://www.instagram.com/p/BrodWomAsXt/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1jaz59t6pxypc

Ray C Awataka Watu Wajitokeze Kumsaidia Zaidi Rose Muhando

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Rehema Chalamila maarufu kama Ray C ameibuka na kuwataka watanzania wote kuungana na kumsaidia Msanii mkongwe wa nyimbo za injili Rose Muhando.

Ray C ameweka wazi kuwa mpaka hivi sasa Rose Muhando yupo tu nchini Kenya ambapo makazi yake yapo lakini hana msaada wowote hivyo ameitaka serikali na wananchi kwa ujumla kujitokeza na kumsaidia Rose Muhando.

Kipitia ukurasa wake wa Instagram, Ray C ameandika maneno haya kutokana na maradhi yanayomsumbua msanii huyo wa nyimbo za injili:

https://www.instagram.com/p/BqpeRXTls6I/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=17h9a99f7xnox

Ray C Amtumia Ujumbe Mzito Wema Sepetu

Msanii mkonwe wa muziki wa Bongo fleva Rehema Chalamila maarufu kama Ray C ameibuka na kumuandikia ujumbe mzito msanii wa Bongo movie Wema Sepetu ambaye amefungiwa kufanya sanaa ya maigizo kwa muda usiojulikana.

Siku chache Wema alijikuta katika upande mbaya wa sheria baada ya kuachia video iliyomuonyesha akipata wakati wa faragha na mpenzi wake baada y ahilo Wema aliomba msamaha lakini aliishia kufungiwa kufanya filamu kwa muda usiojulikana.

 

Baada ya sakata hilo Ray C ameibuka na kumpa ujumbe wa kumpa moyo katika kipindi hiki kigumu anachokuwa anapitia.

Kupitia ukurasa wake wa Instgram, Ray C amesndika;

Nakumbuka 2006 Mange alinipigia Simu akaniambia anakuja nyumbani na mshiriki mmoja atakaeperform wimbo wangu kwenye kipengele cha Vipaji kwenye mashindano ya urembo ya (Miss Indian Ocean)na inabidi tumvalishe kama mimi nikamwambia sawa!walipofika nyumbani Kwangu nilimwangalia wema juu mpaka chini na alivyo mrefu,nikamwambia Mange huyu anashinda Miss Tanzania,nakumbuka alikuwa mwembamba,mrembo na mwenye aibu and I was like Wow!!!!

Anyway kiufupi Nakupenda mpaka leo Wema,Maisha ni Kama milima!wewe bado ni mdogo sana na una nafasi ya kuwa utakacho!pamoja na yanayoendelea sasa bado moyo wangu una imani na wewe kuwa utasimama tena zaidi ya juzi jana na leo na Utakua.Never give up!

Dunia inaweza kukubadilikia kutoka kuwa kipenzi cha watu na kuwa Public enemy number one!Its normal!!!Its ok!ila kumbuka Familia yako ndio kila kitu!Please usihuzunike ukajiona wewe ndo mkosaji dunia nzima maana kila binadamu ana majanga yake ni Mungu tu ndio mkamilifu ingawa sio sababu ya kutufanya kurudia makosa over and over again!

Nakupenda na nina imani na wewe!Nakutakia kila la kheri katika maisha yako na natamani kumuona Wema Mpya.Lots of  love @wemasepetu ”.

 

Ray C Aanika Majibu Yake Ya Ukimwi

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Rehema Chalamila maarufu kama Ray C ameanika majibu yake ya kipimo cha virusi vya Ukimwi alichofanya siku za hivi karibuni.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Msanii huyo ameweka majibu ya kipimo hiko kinachoonyesha hana maambukizo ya gonjea hilo la Ukimwi.

https://www.instagram.com/p/BpCTiygHEE1/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=w5cqoijgcq

Lakini pia amewaasa na watu wengine waende kupima ili kupata kujua majibu ya afya zao kwa ujumla.

Baada ya kimya kirefu kutokana na athari za matumizi ya madawa ya kulevya, Ray C ambaye kwa hivi sasa anaishi nchini Kenya na kuonekana katika nchi za Ughaibuni na mpenzi wake mzungu ametoa wimbo mpya unaoitwa ‘My woman’.

“Mabifu Hayalipi Tanzania” Hamisa Mobetto Afungukia Bifu Lake na Ray C

Mwanamitindo na Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Hamisa Mobetto amefunguka na kuongelea bifu lake na msanii mkongwe wa Bongo fleva Rehema Chalamila Ray C.

Mobetto na Ray C waliingia kwenye sintofahamu siku za nyuma na kujikuta wanarushiana maneno ya kejeli na baadae mashabiki na wapambe wao kujikuta Kwenye vita ya maneno.

Lakini siku ya juzi Ray C alilimaliza bifu hilo baada ya kumposti Hamisa na nyimbo yake mpya na kusema amani itawale juu yao na kumtakia Mrembo mafanikio mema katika ulimwengu wa muziki.

Kwenye mahojiano na East Africa Television, Hamisa amefungukia bifu lake na Ray C na kuweka wazi kuwa hawezi kuwa na bifu na mtu maana kibongo Bongo mabifu ya wasanii hayalipi:

Unajua huyo dada sijawahi kumuona live yaani na Mwanzoni sikujua kama ananiongelea mimi man sikuwahi kumjibu lolote kuhusiana na hilo na binafsi napenda mziki wake kwaiyo kama ameposti video yangu nashukuru, Unajua nchi za wenzetu wakiwa na mabifu wanatengeneza pesa lakini huku kwetu hakuna faida”.

Lakini pia alipoulizwa kuhusu Tanzania Sweetheart Wema Sepetu, Hamisa amekataa kabisa kuliongelea na kusisitiza hana maelewano mzuri na Wema hivyo hawezi kusema chochote kuhusu yeye.

Ray C Amaliza Bifu Lake na Hamisa Mobetto

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Rehema Chalamila Maarufu kama Ray C ameonekana kumaliza bifu lake na Mwanamitindo Hamisa Mobetto baada ya kuposti video yake mpya.

Ray C na Mobetto wameahawahi kukwaruzana siku za nyuma ambapo Ray C alimponda Hamisa kwa mavazi yake ambayo alikuwa anauza Dukani kwake na kuyaita fake jambo lililopelekea mashabiki wa Hamisa kumvamia na kusababisha varangati.

Lakini Baada ya muda kupita Ray C ameonekana kumaliza bifu hilo baada ya kuposti video mpya ya Hamisa ya wimbo wake wa Madam hero na kuwataka mashabiki zake wakaangalie wimbo huo na kumsapoti Mobetto.

kuonyeshwa kuwa ameguswa na Kitendo hicho Hamisa alimshukuru Ray C na hata kutaniana kuhusu nguo za zilizowagom mbanisha.

 

Ray C Amuanika Mpenzi Wake Mpya Mzungu

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Rehema Chalamila maarufu kama Ray C amemuanika Kwenye mitandao ya kijamii mpenzi wake mpya.

Ray C ambaye ameshawahi kuwa Kwenye Mahusiano na Rapa Lord Eyes, ametumia ukurasa wake wa Instagram kumtambulisha  mpenzi wake huyo.

Mashabiki wengi wameonekana kufurahishwa na kitendo cha Ray C kumwanika mpenzi wake huyo wa sasa huku wengine wakionekana kumtaka achague wa hapa hapa nchini.

 

Kwa Hadhi yangu Siwezi Kutafuta Kiki kwa Mtoto mdogo :-Ray C

Mwanadada Ray c amefunguka na kusema kuwa kwa hdhi yake kubwa aliyonayo hawezi kukaa akanza kutafuta kiki kwa watoto wadogo ambao wanamtafuta katika mitando ya kijamii kama ambavyo watu wamekuwa wakimfikiria.

Ray c ambae aliwahi kuwa msanii mkubwa sana afrika mashariki amejikuta akiwa katika wakati mgumu baada ya kujiingiza katika mambo ya kuwa na TEAMS hasa baada ya kuanza kumshambulia mwanadada Hamisa mobeto na ndipo wafuasi wa hamisa walipoanza kumtukana na kumwambia kuwa amekuwa akitafuta kiki.

Ukiona nimeongea kitu katika mtandao ujue kabisa kuwa kitu icho kimenigusa sana,mimi siweiz kutafuta umaarufu kupitia mgongo wa watu.Mimi nina jina kubwa sana afrika mashariki , wala sihitaji kiki au kitu chochote kwa sabau hata nikipita mtaani wanajua kuwa yule Ray c kapita.

Ray c anasema kuwa kama asingekuwa na jina basi angesema kuwa anfanya hivyo ili kutafuta kiki lakini hana muda kwa sababu tayari anajulikana sana,  pia ansema kuwa hata hao wanaosema anatafuta kiki ni watoto wa juzi tu wakati yeye alishafanya mabo mengi sana ktika game la muziki.

Wabongo Mitandaoni Wanapenda Vitu vya Kijinga :-Ray C

Mwanamuziki mkongwe nchini Tanzania, Ray C amedai kwamba asilimia kubwa ya watanzania hawajui kuitumia mitandao ya kijamii ipasavyo ili iwaingizie fedha, na badala yake wanaitumia kwa kujadili mambo yasiyo na tija kwa mtu mwenyewe na taifa kwa ujumla.

Ray C ameeleza hayo wakati akizungumza na www.eatv.tv hii leo Agosti 23, 2018, na kusema watu wengi wamekuwa wakipoteza muda na fedha zao kuingia kwenye mitandao hiyo bila ya kufikiria ni jinsi gani itaweza kuwarudishia faida.

“Watu wengi mitandaoni wanapenda upuuzi, ukiweka kitu cha maana hakuna mtu ambaye ata ‘comment’ chochote katika hicho ulichokiweka, maana wanakichukulia poa lakini fanye kinyume chake hapo ndio utawajua walipo. Wenzetu Ulaya mitandao ya kijamii kama wakina Kim Kardishian na wengine wanatumia mitandao hiyo kuuza ‘product’ na kuonyesha kazi zao ili wapate pesa… 

lakini sisi ndio tumekuwa wakutoa pesa kwa kununua bando ili tukaharibu, tena sana sana Tanzania hatujui kutumia mitandao ili itunufaishe na badala yake tunatumia kwenye upuuzi”, amesema Ray C.

Mbali na hilo, Ray C amedai hasumbuki na maneno ambayo amekuwa akizungumziwa kwenye mitandaoo ya kijamii kwa kuwa ana wafahamu watanzania vizuri jinsi walivyo

Lulu Amuhamasisha Ray C Kumrudia Mungu

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Rehema Chalamila maarufu kama Ray C amefunguka na kuweka wazi jinsi video ya msanii wa Bongo movie Elizabeth Michael ‘Lulu’ ilivyomuhamasisha kurudi Kanisani.

Siku chache zilizopita kuna video iliyomuonyesha Lulu kwa mara ya kwanza hadharani kwa ridges yake tangu atoke jela Miezi michache iliyopita kwa msamaha wa Raisi.

Video hiyo ilimuonyesha Lulu akiwa mwenye afya tele kanisani akioenekana akiimba na kumsifu Mungu kwa hisia kali pamoja na waumini wenzake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ray C aliandika kuwa video hiyo imemfanya akumbuke kipindi cha nyuma wakati alipopitia kwenye matatizo ya kuugua kwani kipindi hicho alikuwa ni mcha Mungu na alikuwa hakosi kanisani tofauti na sasa.

Lulu nimeangalia hii video zaid ya mara kumi nahisi!mpaka machozi yamenilenga kwakweli!Sikumbuki lini nimeingia kanisani.’

Najiona mzima sasa na nasahau kuwa Mungu ni mkali! nimejifunza kitu kutoka kwako my dear! kikubwa sana. You Inspire Me”.

https://www.instagram.com/p/Blpj6psDs1Q/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=seqgtm1xok5m

Ray c Alizwa na Maisha ya Uokovu ya Lulu Michael.

Mwanadada Ray c amefunguka katika ukurasa wake wa instagram baada ya kuona video ya lulu michael inayosambaa katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha Lulu akiwa kanisani anaimba kwaya na kusema kuwa video hiyo imemkumbusha mbali sana hasa kipindi yeye alipokuwa hoi akiumwa alikuwa akimkumbuka sana mungu lakini baada ya kupona amemsahau Mungu kabisa.

Baada ya kuiona video hiyo Ray c aliandika “Lulu nimeangalia video hii zaidi ya mara kumi nahisi lakini mpaka machozi yamenilenga kabisa,sikumbuki ni lini nimeingia kanisani tena.najiona mzima sasa na kumsahau kabisa mungu wangu , najifunza kitu kutoka kwako my dear.you inspire me.

Video hiyo ya lulu iliyomuonyesha akiwa kanisani akiimba na kuabudu iliwafurahisha watu wengi ukizingatia kwamba kwa muda mrefu Lulu alikuwa haonkani katika mitandao ya kijamii.

Ray c Ampongeza Muna, Amwambia Ametua Mzigo.

Baada ya muna kuongea yaliyopo moyoni mwake kuhusu swala la marehemu mtoto wake Patrick   kusema wazi juu ya baba wa mtoto wake kuna watu waliongea mengi kila mtu akim-judge  Muna kwa lake huku wengine wakisema kuwa ameyafanya mapema sana mambo hayo alitakiwa kusubiri mpaka 40 ya mtoto huyo  ipite ndio aongee hayo.

Lakini wapo waliomtetea na kumuona kama alichokifanya labda kinaweza kumsaidia kukaa kwa amani lakini pia labda kingeweza kufunga midomo ya baadhi ya watu waliokuwa wakimhukumu bila kujua kwa nini yalitokea yaliyotokea.

Ray c ameguswa na maamuzi ya Muna na hivyo aliamua kuongea kuhusu swala hilo la kumpongeza kwa kumwambia kuwa aloichokifanya kimeweza kumuondolea mzigo wa maumivu yake aliyokuwa nayo kuhusu mtoto wake.

Una uhuru wa kuwa muwazi pale unapoona mambo fulani yamekuumiza au hayajakaa sawa,kuongea kuna kufanya nafsi yako inakaa sawa,safi muna ninaamini kuna kamzigi flani umekatua  kutoka kwenye moyo…good job.

Ray C na Hamisa Mobetto Ndani Ya Bifu Zito na Zari Aingizwa

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Rehema Chalamila maarufu kama Ray C amejikuta katikati ya bifu zito na mzazi mwenza wa Diamond Platnumz, Hamisa Mobetto.

Sintofahamu hiyo Ilianza siku mbili nyuma baada ya Ray C kuzisema nguo aina ya ‘Fendi’ feki ambazo zimekuwa zikiuzwa sana Hamisa ambaye ni mfanyabiashara ambapo Ray C alitoa kama maneno ya kejeli kuhusu nguo hizo ingawa hakutaja jina.

Basi Hamisa baada ya kuona kama Dongo lile katupiwa yeye basi moja kwa moja akaandika ujumbe ambao uliwakosoa watu ambao hawaonyeshi sapoti kwa biashara za wengine badala yake wanakuwa na wivu.

Baada ya sakata hilo na mashabiki wa Hamisa kumvamia Ray C basi aliweka wazi kuwa hakumtaja Hamisa jina kwa lile Dongo lakini baada ya kuona wanazidi ikabidi amvae Hamisa na kumsema kuhusu Zari na kudai yeye mwenyewe alimuumiza Zari kwa kitendo cha kuzaa na Diamond.