Msanii maarufu wa bongo aweka picha ambayo imezua utata mitandoni kusheherekea siku ya kuzaliwa ya Rayvanny

Diamond Platnumz amekuwa mada ya wiki huu baada ya Hamisa Mobetto kufunua jina la mtoto wake, Abdul Naseeb.

Kwa kufanya hivi, Diamond Platnumz alimbumburushia Mobetto matusi huku akimuita ‘bitch’ na kuwafanya mashabiki wake kumponda kwa kitendo hiki.

Hata hivyo, Diamond Platnumz ameonekana kuendelea kumponda Hamisa kwa kumuwekea picha za kuudhi mitandaoni. Akimsheherekea Rayvanny Leo, Mkali huyo wa Wasafi aliweka picha huku akionekana akimbusu Zari na Vanny akioneka kwenye background.

Kwenye picha hiyo, Simba aliandika;

Jus wanted to wish the guy at the back happy birthday…please tag him!!!

Lakini, mashabiki wake wameonyesha kutoridhika.

Rayvanny azindua video ya wimbo wake mpya – Mbeleko

Msanii kutoka Wasafi Records Rayvanny ameachai video yake mpya wiki kadhaa baada ya kuachia wimbo wake wa Mbeleko.

Kulingana na views ambazo amezipata kupitia YouTube kuna uhakika kuwa mashabiki wake wameupokea vizuri Kama nyimbo zake za hapo mbeleni.

Mbeleko ambayo imepata umaarufu Afrika Mashariki ni wimbo ambao wengi wameweza kuuelewa na video yake pia inavutia kwenye macho.

Video hiyo ambayo imeongozwa na Joowezy imeachiliwa wiki hii baada ya Rayvanny na Khaligraph Jones kutoka kenya kuachia wimbo wao mpya.

Itazame hapa chini;

Ni bora Nikose Vyote Lakini Sio Wewe Mwanangu’ Rayvanny kwa mwanaye JayDanny

Msanii Rayvanny ambaye sasa ni baba,amemwandikia ujumbe mwanaye JayDanny.

Kupitia Instagram yake Ray anasema,’Mungu Akukukuze Mwanangu, Katika Mema na Mafanikio Katika Maisha Yako.Wewe Nifuraha Yangu Na pia Wewe Ndio sababu Ya Mimi kumwaga Jasho Nakufanya Kazi kwa Bidii Kila Siku. Ni bora Nikose Vyote Lakini Sio Wewe Mwanangu. I LOVE YOU SON @jaydanvanny ‘

Wakati huo huo mtoto Jay amekaribishwa rasmi kwenye Kundi la Wasafi na Diamond Platnumz,’Nikubalieni kumtambulisha rasmi star wetu mpya JayDanny,Mwana wa Ray Vanny. Karibu ulimwenguni!’

 

 

‘Allow me to introduce to you our brand new @wcb_wasafi Mega Star! JayDanny!!!! Mwana wa RayVanny!!!!! Welcome to the World Prince!! @jaydanvanny Cc @rayvanny ameandika Diamond.

Mpenzi wa Rayvanny arudisha mwili wake wiki kadhaa baada ya kujifungua mtoto wa Kiume

Fahyma ambaye ni mpenzi na mama ya mtoto wa Rayvanny amekuwa akiwaekea mashabiki wake picha huku akionesha umbo lake ambalo limerudi wiki kadhaa baada ya kujifungua mtoto wake wa kwanza, Jaydan.

Mrembo huyu ambaye amejitambulisha kama teen mom amewapa wengi nafasi ya kufikiria kuwa bado hajafikisha miaka 20 na ikiwa ni ukweli basi inaonekana kuwa ameharakisha maisha yake.

Hata hivyo Rayvanny bado anampenda kulingana na mambo ambayo huyaweka kwenye mtandao wake wa Instagram. Tukiyaacha hayo, picha ambazo Fahyma ameziweka zinamuonesha kama amevalia nguo za kuogelea na kwa kweli amependeza sana.

Zitazame hapa.

Rayvanny aweka picha akiwa na mwanae, huu ndio ujumbe aliomwandikia

Msanii kutoka label ya Wasafi records Rayvanny sasa hivi ni baba ya mtoto mmoja wa kiume, Jayden. Jayden ambaye alizaliwa na Fahyma mwezi wa Aprili mwaka huu amewaletea wazazi wake furaha na Rayvanny hawezi ficha mapenzi aliyonayo kwa mtoto huyu.

Kupitia mtandao wake wa Instagram Rayvanny aliweka picha akiwa na mtoto wake huku akiandika kusema,

Mimi na pacha wangu @jaydanvanny

Japo bado Fahyma na Rayvanny hawaonyesha uso wa Jaydan wengi wana imani kuwa mtoto huyu anafanana na babake kwani rangi yao pia inafanan. Lakini mashabiki wao wanangojea Arobaini ya Jaden kuona kama watamuonyesha mtoto huyu.

Hata hivyo, tazama picha hiyo hapa:

Rayvanny akiwa na mwanae

” Nina Mimba ya Rayvanny” Reality TV staa wa Kenya akiri

Watoto ni baraka kutoka kwa mungu na kila mmoja huja na sahani yake. Basi, Rayvanny anawatarajia watoto wawili mwaka huu kutoka kwa mpenzi wake Fahyma na mwanamke mmoja kutoka Kenya aitwaye Mishi Dorah.

Kulingana na ubuyu mjini Rayvanny na Mishi Dorah walikutana Instagram na kulingana na Mishi wakati huo Rayvanny alikuwa anamtaka awe kama Video vixen wake.

Mishi Dorah

Lakini baada ya kujuana miezi kadhaa wawili hawa walianza kuingiana kimapenzi na hivyo ndivyo Mishi alivyopata mimba.

Mishi ambaye ana watoto wawili alisimulia Rayvanny alivyokuwa akimsihi amzalie na hivi sasa ametambua kuwa ana mimba ya muimbaji huyu ambaye amekuwa akimkana mitandaoni.

Kwa kweli hakuna anayejua kilichotokea kati ya wawili hawa na yupi anasema ukweli au uongo. Hata hivyo ikiwa Mishi ana mimba basi Rayvanny atabarikiwa na watoto wawili mwaka huu