“Wanawake Lazima Tuwape Heshima Wanaume”- Rosa Ree

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayetamba kwa miondoko yake ya kuchana Rosary Robert maarufu kama Rosa Ree amefunguka na kusema kuwa ni vizuri kama Wanawake watawapa heshima wanaume.

Rosa Ree ameibuka na kusema kwamba ni vizuri Sana  kama Wanawake Wataanza kuwapa heshima wanaume heshima wanayostahili hasa kwa sababu ya mambo mengi ambayo wanayowafanyia.

Katika mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari, Rosa Ree amefunguka haya kuhusu heshima kwa wanaume:

Kiukweli inabidi tuwape heshima wanaume, wanajitahidi sana kutufanya tuwe na furaha sio kila siku kuwaimbia wanawake tu kwenye mapenzi, wanaume wanafanya mengi sana kwa ajili yetu ndio maana nimeandika wimbo huu kwa ajili yao”.

Rosa Ree ametoa Wimbo Wake Mpya wa ‘Asante Baba’ ambao ndani yake una ujumbe wa kushukuru wanaume.

Rosa Ree Atangaza Kuachana na Uongozi Wake

Mwanadada Rosa ree ameamua kutangaza na kusema ukweli kuwa kwa muda sasa amekuwa hafanyi kazi na uongozi wake aliokuwa akifanya nao kazi , uongozi ambao makao yake yalikuwa nchiki Afrika ya Kusini.

Rosa ree anasema kuwa yeye na uongozi wake wa Dimo wamekuwa hawafanyai kazi pamoja kwa sasa kutokana na sababu ambazo haziwezi kuzuilika kwa muda na ndio maana tangu mwaka 2018 October msanii huyo amekua akifanya kazi na watu wke wa awali.

Hata hivyo mwanadada huyo anasema kuwa inaishukuru kampuni hiyo kwa kufanya nayo kazi kwa kipindi walichokuwa pamoja ingawa pia kufanya kazi pekeyake kumemfanya kuwa imara zaidi.

Rosa anasema kuwa tangu ameachana na kampuni hiyo  mpaka sasa ameweza kutoa nyimbo mbili ya banjuka pamoja na asante baba ambazo pia zimekuwa zikifanya vizuri kwa sasa.

Rosa ree alitangaza kuwa katika mkataba na Dimo kwa miaka 3 ikiwa mkataba huo ungeanza kufanya kazi March 2018.

Rosa Ree Adai Bado Mdogo Mambo Ya Mapenzi Hataki

Msanii wa Bongo fleva anayefanya hip hop pia Rose Robert maarufu kama Rosa Ree ameibuka na kudai kuwa sababu inayomfanya asiharakishe kuingia kwenye mapenzi ni uamuzi.

Rosa Ree ameibuka na kudai kuwa anapokuwa hayupo kwenye mapenzi haimaanishi kuwa hakuna watu wanaomfuta kwa lengo la kumshawishi Lakini yeye mwenyewe ameamua kutulia kwenye sekta hiyo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, Rosa Ree amesema kuwa anaamini kuwa umri wake bado mdogo hivyo hana papara na mapenzi.

Mapenzi yapo, napenda familia yangu, nampenda Mwenyenzi Mungu, napenda pesa, mimi mdogo sana, am very young, yaani sio kwamba hawapo ambao hawatamani kuwa na Rosa Ree lakini hatuendani”.

Ingawa Rosa Ree ameshatajwa kuwahi kuwa kwneye mahusiano na wasanii Kama Young Dee na Bill Nas Lakini aliwahi kukataa na kusema kuwa wale ni washkaji zake tu.

Mapenzi yapo, Napenda pesa :-Rosa Ree

Mwanadada mwenye sifa za kipekee huku watu wakimsma sana kuhusu swala lake na kutokuwa na mahusiano amefunguka na kuelezea kwa nini kwa sasa hataki sana kujikita katika mahusinao kama mashabiki zake wanavyomuhoji huku wakitaka kuweka mahusinao yake hadharani.

Rosa ree anasema kuwa kitendo cha yeye kutokuwa katika mahusinao haimaanishi kuwa hakuna wanaomfuta kwa ajili ya kuwa nae katika mahusiano lakini kwake anaona mud wake bado kwa sababu anaamini kuwa yeye bado mdogo sana.

mapenzi yapo, napenda familia yangu, nampenda mwenyezi mungu na pia napenda sana pesamimi mdogo sana , am very young , yaani sio kwamba hawapo wanaotamani kuwa na rosa ree hapana lakini tu  hatuendani.

Mara nyingi mwanadada huyo amekuwa akisisitiza kuwa watu wasiomuenoa kama yuko tofauti kwa sababu ya swala la mapenzi tu kwa sababu hata yeye ana moyo wa kupenda na pia anaogopa kuumizwa.

Rosa Ree Ataja Sababu Za Kuonekana Kuwa Mgumu

Msanii wa muziki wa hip hop nchini anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘One way’ Rosemary Robert maarufu kama Rosa Ree amefungukia madai ya wadau wengi kuwa yeye ni mgumu.

Rosa Ree amesema kuwa watu wengi wanamuona mgumu kutokana na mavazi yake na jinsi alivyo lakini siyo kihivyo bali hapendi kujibebisha kama wafanyavyo wanawake wengine.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Rosa alisema kuna watu wengi wanamuona ana mambo ya kiume kwa sababu hajawahi kuonyesha mpenzi wake hadharani na hiyo ni sababu ya uhusiano wake wa kimapenzi kuwa binafsi zaidi.

Unajua wengi hawanielewi wanasema nina tabia za kiume lakini ukweli sipendi kujibebisha au kujilegeza na pia uhusiano wangu wa kimapenzi ni binafsi zaidi sipendi kuweka hadharani kabisa” .

 

Rosa Ree Akiri Kuacha Pombe Baada ya Kuona Haina Nafasi Katika Maisha Yake.

Mwanadada Rosa Ree anaetikisa kwa sasa katika anga za muziki wa hip-hop nchini amefunguka na kusema kuwa japokuwa hapo awali alikuwa akinywa sana pombe lakini alikuja kugundua kuwa hatakiwi kutawaliwa nayo hivyo aliamua kuachana  nayo.

Akiongea na EATV, rosa reee anasema “unajua pombe ukiipa nafasi kubwa ya kutawala maisha yako hautaweza kuiacha hata mara moja, ila wewe ukiitawala pombe unaweza kuiacha na ndio maana hata mimi niliweza “

Mbali na kuwa msanii wa hip-hop rosa ree amekuwa na muonekano wa tofauti sana na wasanii wengine wa kike hata anavyosema kuwa atumii kilevi inaweza kuwa ngumu baadahi ya watu kuamini kutokana na muonekano.

Rosa atoa ufafanuzi picha yake Dc Jokate Mwegelo

Mwanadada Rosa Ree amefunguka  na kuelezea kwa undani juu ya picha inayosambaa katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha yeye akiwa amepiga picha na mheshimiwa Dc Jokate Mwegelo miaka ya hapo nyuma.

Picha hiyo ambayo watu wengi walidhania kuwa kutakuwa kuna wimbo mpya katia ya wadada hao wawil, Rosa Ree amekanusha na kusema kuwa waiwli hao waliwahi kufukiria kufanya project moja ya nywele ambayo ilikuwa chini ya Jokate na kampuni yae ya Kidoti.

Rosa Ree anasema kuwa “actual sio ngoma , ilikuwa ni project ya nywele tulikuwa tunataka kufanya na nina kumbuka kipindi hicho nilikuwa the industry,tulikuwa tunaweka brand ya nywele na tulitaka kuweka brand ya rosa ree na kidoti kwa pamoja.”

Rosa Ree Asema Sababu ya Kufeli kwa Show Yao .

Wiki kadhaa zilizopita iliripotiwa  kuwa kulikuwa na show iliyofanyika nje ya nchi iliyomhusisha Rosa Ree na Aslay ambapo walilalamikiwa kwa sababu hakukuwa na mashabiki katika ukumbi waliofanyia show.

Inasemekana kuwa uwaja huo ulikuwa mtupu kabisa na haikuwa kawaidia kwa watu kutokutoka katika show za wasanii wa kitanzania kwa sababu nyimbo za huku zinapendwa sana na watu wa je .

Hata hivyo baada ya kuulizwa na XXL , rosa ree alijibu sababu kubwa ya kufeli kwa shoo hiyo ni kutokana na maanadalizi machache ya promoto na ukizingatia kuwa hawakuwahi kufanya kazi hawali na promota huyo.

akiongea na XXL,  anasema “show haikuwa poa na watu hawakuwa wengi kwa sababu promota hakujiandaa vizuri, yeye hakufanyaia matangazo nakumbuka baada ya kupata visa ndio alianza kutangaza show.watu waliojua kama kuna show walikuwa wachache, lakini mimi ni mfanya baishara najua kuna kupata na kukosa , ni promota wa kwanza kufanya nae kazi lakini aliwahikufanya kazi na Mh Temba nadahani aliamini kuwa show itakuwa poa  kwa sababu wasanii wote tulikuwa wakali.

Rosa Ree watolea Povu Wanaomsema Kuhusu Style Yake ya Kubinua Midomo.

Mwanadada anaefanya vizuri katika ku-rap Rosa ree amefunguka na kusema kuwa anakerwa sana na watu wanaokaa na kumsema vibaya kuhusu tabia yake ya kubinua midomo ilhali hakuna cha maana wanachomuongezea katika maisha yake na katika kile anachokifanya.

Rosa ree amesema kuwa hiyo ni style yake ya pekee yake katika nyimbo zake na inawezekana ndio inayowatofautisha na watu wengine.

hawanilipii bili pamoja na kubinua kwangu midomo na kutoa ulimi, sasa hivi nina super market , nimefanya kolabo na wasanii wengine  wa kimataifa, nafany vitu vikubwa mimi mwenyewe maneno ya watu hayajiandiki usoni wala hazilipi bili ila zingekuwa la ningejali.

Kujiamini na Kusimamia Ninachokiamini Kimenipa Mafanikio-Rosa Ree

MSanii wa Muziki wa Bongo fleva anayetamba kwa miondoko yake ya kipekee ya kurap amefunguka na kutoa siri yake iliyompa mafanikio mpaka leo yupo alipo kama Mwanamuziki.

Rosa Ree ambaye amewahi kufanya vizuri sana na wimbo wake ‘Way Up’ amefunguka na kuweka wazi siri ya mafanikio yake kwanza ni kujiamini halafu na kuamini anachokifanya.

Kwenye mahojiano na  Global Publishers, Rosa Ree alifunguka kuwa muda mwingi huko nyuma watu walikuwa wanamwambia kwamba anajifanya mnyamwezi kwa soko la Bongo hawezi kufika popote, lakini hakuwasikiliza kwa sababu alikuwa anawaza kwenda kimataifa.

Nisingejiamini na kusimamia kile nilichokiamini kiukweli nisingefika mahali nilipo leo, siku zote nilikuwa ninatazama soko la kimataifa, kwa hiyo hata maneno ya kunikatisha tamaa sikupenda kabisa kuyapa nafasi”.

Rosa Ree alizidi kupata mafanikio hivi karibuni baada ya kusaini dili la mamilioni na Recording Label  kutoka Afrika ya kusini ambayo ilimpatia nyumba mbili za kifahari.

Rosa Ree Afunguka Hakuna Mwanaume wa Kumhonga

Mwanadada anaefanya vizuri katika kiwanda cha muziki kwa upande wa rap ,Rosa ree amefunguka na kusema kuwa katika maisha haliyoishi mpaka kufikia sasa hivi aona kama kuna mwanaume anaeweza kumhonga hela nyingi za yee kuridhika nazo .

Mwanadada huyo ambae amekuwa akionekana na muonekano wa kiume kila siku na imekuwa ikisemekana kuwa hana mwanaume katika maisha yake ya kimahusiano anasema kuwa haoni kama mwanaume anaweza kumpa ela yoyote inayoweza kumridhisha.

Pia rosa ree anasema kuwa huwa hawaelewi sana wanaume wanapokuja na kumhonga kwa sababu anakuwa haelewi kama  ndio wanaonga au wanajaribu ” mimi sihongeki , kwaio hata mtu akinionga huwa nashindwa kuelewa ni kwamba annihonga au ananijaribu.”

Rosa Ree Azidi Kung’ara Nchini Afrika Ya Kusini

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na miondoko yake ya kipekee ya kuchana Rosary Robert Kimario maarufu kama Rosa Ree ameendelea kung’aa Zaidi Sauzi.

Rosa Ree ambaye mwezi uliopita alisaini mkataba mnono na kampuni ambayo inasimamia kazi zake ya  Afrika ya Kusini imeendelea kumsimamia kazi zake vyema na hata kumtangaza zaidi nchini humo.

Rosa amesemekana kuwa gumzo nchini humo kutokana na Media Tour anayefanya nchini humo ambapo mbali na kuzungumza Kizungu lakini kwa kiasi kikubwa amekuwa akizungumza Kiswahili, ili kuonyesha kwamba ni Mtanzania, lakini pia amefunguka kwamba kwa sasa kazi zake kwa kiasi kikubwa atakuwa anafanyia nchini humo kwa sababu menejimenti yake inatoka huko.

Kiukweli Sauz kwa sasa kumekuwa kama nyumbani, ninafanya ziara nyingi kila kukicha na menejimenti yangu imenitengenezea mazingira mazuri ya kufanya kazi. “Baada ya kumaliza tour kuna kitu kikubwa pia kinakuja, mashabiki wangu wakae mkao wa kula”.

 

Rosa Ree Azidi Kung’aa na Uongozi Mpya, Akabidhiwa Gari

Mwanadada rosa ree ambae hivi karibuni nyota yake inaonekana kung’aa sana kwa sasa amekabidhiwa gari jipya na uongozi wake mpya ambao umesaini mkataba mpya kwa sasa chini ya DIMO PRODUCTION .

Katika ukurasa wake wa instagram, Rosa ree aliweka picha akiwa katika gari jipya na kuandika maneno yaliyoonyesha kuwa gari hiyo amekabidhiwa na uongozi wake huo.

Rosa ree wiki chache zilizopita alisema amekabidhiwa nyumba yenye thamani ya zaidi ya milioni 400 na sasa amekabithiwa gari aina ya benzi atakalokuwa akitumia akiwa nchini Afrika ya Kusini.Kwa sasa Rosa ree yupo nchini afrika ya kusini kwa ajili ya kuutangaza muziki wake.

Alichokisema Nahrel Kuhusu Rosa Ree na lebel ya Afrika ya kusini

Mtayarishaji wa muziki kutoka katika kundi la Navy Kenzo nahrel amezungumzia msanii aliyewahi kumsaini katika lebel yake na kisa kuondoka na kuanza kufanya kazi zake mwenyewe Rosa Ree ambae kwa sasa anafanya vizuri sana ktika game kama rapper wa kike.

Nahrel amethibitisha kuwa msnaii huyo kwa sasa amepata dili nono la kusainiwa na moja ya lebel kubwa nchi afrika ya kusini inayojulikana  kama DIMO PRODUCTION ya nchini humo.

mimi nadhani tulichokifanya tumekifanya kwa uwezo wetu,tuliweza kutengeneza kitu ambacho kilionekana.we are proud kutengeneza wasanii kama yeye ambao leo hii wanaweza kuonekana kusainiwa na lebel nyingine ni dili kubwa sana na hata sisi tulivyoamua kuwasaini ilikuwa ni kwa ajili ya kuwasapoti.kwaio Rosa Ree anapopata dili lingine na mimi napata moyo wa kuendelea kusapoti wengine.ninaamini kuwa itamfikisha sehemu nyingine ambayo pengine mimi nisingeweza.

Rosa Ree alianza kufanya kazi na kundi hilo akiwa kama msani aliyesainiwa hapo na kutengenezwa katika kundi hilo mpaka pale iliposemekana kuwa kulitokea mtafarauku uliowafanya kushindwa kufanya kazi pamoja , lakini sasa hivi mambo yanaenda vizuri na kupata menejementi nyingine.

Mimi Napenda Sana Wanaume;-Rosa Ree

Mwanadada Rosa Ree amefunguka na kuwashangaa Baadhi ya mashabiki wanaokaa na kumuhukumu kuhusu swala la mahusiano kwa sababu amekuwa kimya na wala hataki kumuonyesha mtu anaetoka ane kimapenzi.

Rosa Ree anasema kuwa wapo baadh wanaomwita kuwa ni msagaji lakini amekuwa akishangaa swala hilo kwa sababu kwa upande wake aamini swala la Mapezi ya jinsia moja hivyo  wake si kitu cha kawaida.

Hata hivyo Rosa Ree anasema kuwa anaamini kuwa mwanamke ameumbwa kwa ajili ya mwanaume hivyo usagaji kwake sio dili.

hivi karibuni walisema natoka na MT . mara natoka na Billnass kisa tu tulisafiri tukaenda kutoa ngoma nje ya nchi, am just working guys, mimi sijui kuhusu hiyo idea ya wasichana kuwa wasagaji lakini ilishazoeleka kuwa ili msichana aweze kufanya mzuki wa hip-hop lazima awe mgumu kama mwanaume,wakikuona umevaa kama mwanamke wwanaanza kukuliza kwanii umevaa hivyo.

i dont believe in mapenzi ya jinsia moja,i love men men, nawapenda sana wanaume na ninaamini kuwa wanaume wameumbiwa sisi.

Rosa Ree Afunguka Kuhusu Kujiunga WCB

Msanii wa Bongo fleva Rosary Robert ‘Rosa Ree’ aliyejizolea umaarufu kutokana na  miondoko yake ya kuchana amefunguka juu ya mipango ya kusaini na Label maarufu nchini WCB.

Rosa Ree ambaye amekuwa akiulizwa mara kwa mara kama ana mpango wa kujiunga na label hiyo ameweka wazi kuwa hajwahi kufikiria kujiunga WCB.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Rosa Ree ambaye awali kabisa alikuwa katika label ya The Industry amesema  kuwa hawajawahi kuzungumza hilo ila ni watu ambao wamekuwa bega kwa bega na yeye katika muziki wake.

Hapana ilikuwa hamna, ndiyo timu mzima ya WCB wamekuwa wakinisapoti katika muziki wangu. Nafurahia hilo ila hatukuwahi kufikia hatua hiyo”.

Rosa Ree aliondoka The Industry, record label inayomilikiwa na Nahreel na Aikah wa Navy Kenzo mwaka jana oktoba na amekaa bila management kwa miezi kadhaa mpaka aliposainiwa mapema mwezi huu.