Rosa Ree Atoboa Siri Ya Kuzidi Kufanikiwa

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vyema kabisa kwa staili yake ya kuchana mwanadada Rosary Robert ‘Rosa Ree’ ametaja siri ya mafanikio yake.

Rosa Ree ni moja ya msanii ambaye amepata umaarufu kutokana na staili yake ya kipekee kabisa ya kuchana inayomtofautisha na wasanii wote wa Bongo fleva.

Kwenye mahojiano yake na gazeti la Risasi Vibes, Rosa Ree alisema kuwa, siri hiyo ni namna ya uimbaji wake kwani haujakaa Kibongo sana na anajiweka ‘kimtoni’ zaidi ndiyo maana anafanikiwa.

Ukiwasikiliza wanamuziki wa kike wa Bongo, wengi wanavyorap ni ‘local’ ndiyo maana hata hawatusui kama mimi, kikubwa aina yangu ya uimbaji inanifanya kupata mashabiki wengi zaidi nje ya Bango”.

Rosa Ree anayeendelea kufanya vizuri na ngoma yake ya ‘Way up’ amezidi kupata mafanikio zaidi kwani wiki chache zilizopita alitangaza kupata uongozi mpya kutoka South Africa ambao umemzawadia mijengo miwili huku mmoja wa Bongo ukiwa na thamani ya milioni 400.

 

Rosa Ree Anunuliwa Mjengo Wa Milioni 400 na Uongozi Mpya (+picha)

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kurap Rosa Ree ameanika mijengo yake miwili aliyonunuliwa na uongozi wake mpya.

Siku ya jana Rosa Ree aliita waandishi wa habari Kwenye mjengo wake mpya wenye thamani ya shilingi milioni 400 ili kutambulisha uongozi wake mpya uliopo nchini Afrika ya Kusini unaoitwa Dimo Production South Africa.

Rosa Ree ametangaza kusaini mkataba wa miaka mitatu na record label ambayo imeweka wazi kuwa imeamua kumnunulia nyumba mbili moja nchini Tanzania na nyingine nchini South Africa.

Hizi ni baadhi ya picha za mjengo huo uliopo nchini South Africa:

.
.
.
.

Nahreel Afungukia Ishu Ya Rosa Ree Kuondoka The Industry

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka katika kundi la Navy Kenzo, Nahreel amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu msanii Rosa Ree kuondoka Kwenye label yake ya The Industry.

Msanii wa kike anayefanya vizuri kwa hivi sasa Rosa Ree alianza kujulikana baada ya kusainiwa chini ya label ya The Industry inayomilikiwa na Nahreel ambaye pia ni producer.

Rosa Ree alitangaza kuondoka kwenye label hiyo mapema mwaka jana baada ya kuwepo humo kwa muda mrefu huku akidai sababu pekee iliyomuondoa ni kuisha kwa mkataba wake na kusisitiza hana ubaya nao.

Lakini baadae Rosa Ree aliweka wazi kuwa kuna baadhi ya mambo ambayo yalifanyika ndani ya label hiyo ambayo hayakumfurahisha ikiwemo kukataa kumpa akaunti yake ya Youtube hali iliyoashiria kulikuwa na kabifu fulani.

NAhreel anefunguka kwa mara ya kwanza na kumuongelea Rosa Ree tangu alipoondoka The Industry ambapo kwenye kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv ameweka wazi hakukuwa na bifu baina yao bali mwenyewe aliomba kuondoka.

Rosa Ree watu wamemjua Kupitia The Industry na kama alivyosema yeye time ilivyofika alitaka kuondoka na sisi tukamuacha aende but hatuna tatizo Rosa”.

 

Rosa Ree Amekuja Na Mini Supermarket Yenye Thamani Ya Milioni 30

Mwanamuziki wa Bongo fleva Rose Kimario maarufu kama Rosa Ree ameingia Kwenye ulimwengu wa kibiashara baada ya kufungua mini supermarket yake mpya aliyoipa jina la Rosa Ree Mini Supermarket.

Risa Ree alitumia ukurasa wake wa Instagram kutangaza habari hiyo njema na kuandika maneno haya:

Rosa Ree amefanya Interview na Millard Ayo Tv na ameweka waiz kuwa imemgharimu zaidi ya milioni 30 kuwekeza Kwenye biashara ile

Ile ni Supermarket yangu na ninategemea kuifungua rasmi wiki ijayo hivi sasa tupo Kwenye maandalizi ya mwisho ni kitu ambacho nilipanga kufanya kwa muda mrefu sasa.

Kusema ukweli nimewekeza pesa nyingi lakini kwa haraka haraka nimewekeza zaidi ya milioni 30 na nina mpango wa kufungua supermarket kubwa zaidi ya ile”.

 

Rosa Ree Atoa Siri ya Mafanikio kwa Mwanamke.

Akiwa kama msanii wa kike amabe ilifika sehemu aliona kuwa anaweza kusimama peke yake katika muziki na hakuna wa kumuangusha, Rosa Ree amefunguka na kuelezea kwa makini kabisa ni jinsi gani mwanamke anapaswa kufanya ili kuweza kufanikiwa na ku-win ndoto zako.

Akiyaongea hayo  katika siku ya wanawake Duniani, yeye pia ni moja ya wanawake jasiri sana na walioweza kuamini kuwa aina ya muziki anaoufanya sio lazima kufanywa na mwanaume ndio uonekane kama umefanywa.

Rosa Ree anasema kuwa lazima mwanamke ajiamini sana ili kuweza kufanikiwa lakini pia inabdidi awe na bidii katika kutimiza ndoto yake.

Kwa wanawake wote wenye vuipaji, kikubwa ni kujiamini tu.unatakiwa kujiamini ili uweze kukamilisha ndoto.

pili kuwa na imani na kile kitu uanataka kukifanya,tatu ni kutia bidii , huwezi kuwa na ndoto alafu hautii bidid ili ifanikiwe  na kukamilisha malengo yako.

Mwanadada huyo amehaidi kutoa wimbo mpya siku ya tarehe 9 mwezi huu na kuwaomba mashabiki zake kuupokea vizuri.

Rosa Ree Awatolea Povu The Industry na Kusema Hawawezi Kumshusha

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayetamba kwa miondoko yake ya kurap na hata kupewa jina the rap Godess Rose Kimario ‘Rosa Ree’ amewatolea povu zito wale wote wanaotaka kumshusha hawataweza kushusha kipaji chake kikubwa.

Rosa Ree alipata umaarufu kwa mara ya kwanza baada ya kuwa chini ya uongozi wa The Industry ambao uko chini wa Nahreel na Aikah Navykenzo.

Tangu alipoondoka kwenye label hiyo na kuanza kufanya muziki kama Solo artist Miezi michache iliyopita siku zote amekuwa akisisitiza kuwa hana bifu wala ubaya na Navykenzo.

Lakini siku chache ziliopita Rosa Ree aliibuka na kuongelea mchezo mchafu aliofanyiwa na Uongozi wake wa zamani ambapo amedai wamefuta baadhi ya video za nyimbo zake YouTube ambazo zilikuwa kwenye kurasa yao lakini pia amesema nyingine wamezishusha wameziweka private jambo ambalo amedai limemrudisha nyuma.

Rosa Ree amefanya Interview na Enews ya East Africa Tv amekiri pamoja na kwamba kitendo hiko kimemrudisha nyuma lakini hakijamkatisha tamaa na hakiwezi kushusha kipaji chake:

Kusema ukweli walivyoshusha video zangu kuna thamani ambayo imeshuka kidogo na ninajikongoja kuweza kupita ile sehemu ambayo ilikuwa zinaweza kunifikisha lakini siamini kama video zikishushwa kwenye YouTube na kipaji changu kimeshushwa kwaiyo nina iyo imani kwamba bado kipaji changu kipo na bado uwezo wangu upo na nitaendelea kufanya vyema”.

Pia Rosa Ree aliulizwa kuhusu uhusiano wake na Navy Kenzo kwa sasa endapo kuna bifu lolote ambalo linapelekea wao kumfanyia hivyo yeye na alisema:

Sina mawasiliano yoyote na Navykenzo kwa muda mrefu Lakini naamini ni kwa sababu ya majukumu mimi niko busy na muziki wangu hivyo sijaweza kuwasiliana nao lakini na wao wamepata mtoto ambalo ni jukumu kubwa naamini hivyo siwezi kujiuliza kwa nini hatuwasiliani”.

 

Rosa Ree:Siwezi kufanya Kazi na Mtu Nisie-endana Nae.

Msanii wa muziki  wa kike wa Hip-Hop nchini Rosa Ree amesema kuwa kwa sasa  hawezi kufanya kazi na msanii yoyte ambae hawaendani nae kimuziki kwa sababu anapenda kufanya azi inayoeleweka na itakayowakonga mashabiki zake.

Rosa Ree ameyasema hayo baada ya kutoa wimbo wake unaojulikana kama marathoni ambao amemshirikisha billnass hivi karibuni na kukubali kuwa yeye na billnass wameweza kufanya kazi hiyo naikafanya vizuri kwa sababu kuna kitu cha kimuziki kinachowaunganisha na kuendana sana.

Bill nass kabisa nimshikaji wangu sana na nimoja ya wasanii wenye vibes sana,ni myu wangu wa karibu na tuna vibes  sana,as  a person yeye ni mtu poa sana.napenda sana watru ambao wapo Og,alafu kitu kingine ni kwamba siwei kufanya kazi namtu ambae sina vibes nae kabisa, mtu ambae hana positives vibes.

Rosa Ree na Billnas wametoa wimbo wao mpya hivi karibu na kuwafanya kuwa karibu zaidi, lakini kama ilivyo kawaida watu wengi wameanza kutilia mashaka uhusiano wa wawili hao lakini wao wameshakanusha taarifa hizo.

Rosa Ree Akanusha Kutoka Kimapenzi na Young Dee

Msanii wa muziki anaefanya vizuri kwenye hip-hop Rosa Ree amefunguka na kukanusha tetesi zinazosambaa kuhusu yeye kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii mwenzie Yound Dee kwa muda sasa.Rosa Ree amesema kuwa watu wamekuwa wakizusha mambo hasa wanapoona watu wamekuwa na ukaribu hata kama ni wa kibiashara na kikazi.

Rosa Ree amefunguka na kusema kuwa kwa muda sasa amekuwa singo bila kujiingiza katika mahusiano yoyote na ikitokea siku akiwa katika mahusinoa yaliyo serious basi  lazima atawatambulisha mwanaume  lakini sio kupitia katika kurasa za udaku kama inavyotokea saa hivi kwa young dee.

Niko singo siko kwenye mahusiano yoyote yale na mtu yoyote yule,na hata akija mtu na nikawa nae katika mahusiano ntamtambulisha tu kwenu kwa njia proper sio kwa kupitia udaku na sijawahi kutoka na Young Dee ni mwanangu tu nafanya nae kazi na tumekuwa watu wa karibu.

Wasanii wengi wamekuwa wakiambiwa au kuhisiwa kuwa wanatoka na wasanii wenzao lakini wanakuwa wanakanusha lakini ukweli wanaokuwa nao wenyewe na mbaya zaidi mambo yanapokuwa magumu ndio siri zinaanza kuvuja na kushindwa kuyatatua matatizo yao ingawa sio vizuri kuonyesha mahusiano yao katika mitandao.

 

Rosa Ree Afunguka ni Sababu Gani Zilimpelekea Kumtosa Fid-Q

Msanii wa kike anayetamba kwa staili ya peke yake ya kuimba na kurap Rosa Ree, amefunguka kuwa ni sababu gani iliyompelekea kumtosa mwanamuzi mkongwe  Fid-Q.

Rosa Ree anayetamba na wimbo wake mpya wa ‘Dow’ amekuwa katika vichwa vya habari hivi karibuni baada ya habari kutapakaa kuwa amehama label ya The Industry ingawa ameendelea kusisitiza kuwa hana shida nao lakini za chini ya kapeti zinadai mengine. Kumekuwa na tetesi nyingi kuwa mkali wa mashairi, Fid-q alipomtaka Rosa Ree wafanye kazi alikataa.

Kwenye mahojiano aliyoyafanya na Lilommy, Rosa Ree amefunguka yafuatayo kuhusiana na masuala hayo:

Naweza kusema wimbo wa Fid-Q ni moja Kati ya vitu ambavyo The Industry imeniangusha sana, nilitumiwa hiyo nyimbo na nikaandika mpaka verse lakini ikawa inatakiwa ipite kwanza kwa Nahreel sasa baada ya kufika huko sikujua nini kilitokea lakini sikurudishiwa tena kile kitu kilinishangaza kwa sababu Fid ni moja Kati ya wasanii wakubwa sana lakini sina tatizo naye ni kaka yangu tuko fresh”.

Pia Rosa Ree alifunguka kuwa hana muda wa kuwaza mapenzi kwa sasa kwaniyuko bize na kuzisaka pesa kwanza na kuboresha maisha yake.

Rosa Ree Kufuata Nyayo Za Diamond,Ni Baada Ya Kupata Dili Nono

Msanii anaefanya vizuri kwa sasa katika anga za muziki wa bongo , Rosa Ree amekuwa msanii wa kwanza wa kike lakini wa pili kutoka Tanzania kupata deal kubwa kutoka katika kampuni ya Belaire baada ya Diamond kupata dili hili week chache zilizopita.Kampuni iyo ambayo ina mabalozi wengine wakubwa duniani  kama Rick Ross  inaendelea kuona kazi nzuri wanazofanya wasanii wa Tanzania na kuamua kufanyanao kazi,

Akiongea na mwandishi wa habari msanii Rosa Ree amethibitisha kupata dili ilo na anasema kuwa anahisi ni kwa sababu ya muziki na kazi zake kufanya vizuri ndio maana ameweza kuchaguliwa lakini hajui nini kuliwasukuma kampuni iyo kumuangalia na kumchagua msanii kama yeye ambae ndio kwanza anaibuka na kuanza kufanya vizuri tofauti na Diamond ambae amekuwa katika industry ya muziki kwa muda mrefu kidogo.

To be honest mimi sijui kwa sababu na mimi nimechaguliwa hivyhivyo tu na wao wenyewe hata sikujichagua, au kujipendekeza nikasema labda nina quality sana , kwaio hata ukiniuliza sijui ni quality gani Belaire wanaangalia kuchagua wasanii  na sijui ni zipi waliangalia wakaona Rosa Ree anafaa” alifunguka Rosa Ree

Hata hivyo Rosa Ree anasema kuwa muda mwingine vile unavyojichukulia ndivyo na watu wanaokuangalia watakuchukulia pia kana unakaa kutokujiamini itakuwa hivyo kwa watu pia”lakini najua kwamba ukiweza kujichukulia mwenyewe kwa uzito fulani  na watu wanaweza kukuchukulia kwa uzito huohuo na kwa thamani hiyo na ukijikuta unafika katika viwangi vikubwa” aliongezea mwanadada huyo

Rosa Ree ni msanii chipukizi ambae alianza kazi chini ya lebel ya The industry, hata hivyo kutokana na juhudi zake kwa sasa anafanya kazi vizuri akiwa kama moja wa ma-rapper bora wa kike Tanzania mwenye style ya pekee katika uimbaji,kama ilivyo kwa Diamond, Rosa Ree pia amepata dili la kuwa msanii anatoka Tanzania wa kike atakae kuwa balozi wa kinywaji chenye brand  kubwa duniani cha Belaire.

Rosa Ree Afunguka Kuhusu Kuondoka Kwenye Label Ya The Industry

Mwanamuziki wa bongo fleva anayefanya miondoko ya rap, Rosa Ree amefunguka na kukubali kuwa tetesi zilizoenea kuwa yeye ameachana na label ya The Industry ni kweli.

Label ya The Industry ambayo inasimamiwa na wanamuziki kutoka Navy Kenzo Nahreel na Aika iliyokuwa inasimamia kazi za mwanadada Rosa Ree ambaye amepata umaarufu kutokana na staili yake tofauti na wasanii wengine ya kuimba kwa kurap huku watu wengi wakimfananisha na rapa maarufu kutoka Marekani mwanadada Nicki Minaj.

Kwenye mahojiano na Millard Ayo Tv, Rosa ree alifunguka zaidi kuhusiana na uamuzi wake wa kuondoka katika label hiyo;

Ni kweli kwa sasa sipo tena kwenye label ya The Industry ila sio kwamba nimeondoka au kuendelea ila ni mkataba umeisha at the moment na tuko salama kabisa ni vitu vya mkataba ni masuala ya biashara haituingilii kwenye urafiki au ufamilia tunaoweza kuwa nao kwaiyo tunaishi kama zamani tupo freshi na bado ni marafiki kwaiyo hamna kitu chochote kibaya kilichotokea kati yetu. Pia napenda kuwashukuru kwa mchango wao ambao wameweza kuweka kwenye mziki wangu kwani sio rahisi watu wakuamini kwaiyo ni kitu ambacho they really deserve credit for na walifanya kwa moyo mmoja kwaiyo nawashukuru kwa hilo “.

Baada ya Rosa Ree kuondoka The Industry hivi karibuni watu wengi walizusha kuwa ameondolewa kwa sababu ya mambo ya kiheshima na pi ailisemekana kuwa Rosa Ree alikuwa na ugomvi na First lady wa The Industry Aikah kitu ambacho wote wamekataa huku akisisitiza kuwa hana ugomvi nao bado ni marafiki kama zamani lakini tu mkataba wake umeisha ila kwa sasa Rosa Ree kasema anajisimamia mwenyewe.