Rose Anahitaji Maombi na Wala Sio Maneno :-Sayuni Mrita.

Sayuni Mrita muimbaji wa injili anayetamba sasa na Wimbo wa YESU AMEFANYA alipoulizwa kuhusu Rose Muhando ambaye ametajwa kukumbana na changamoto nyingi na watu kila mtu kusema lake, Sayuni amejibu

Muimbaji huyo anasema kuwa kinachotakiwa kwa sasa ni maombezi ya nguvu na yenye kumakinika sana kwa Rose Muhando na kuacha kufanya muzaha wa kumsema vibaya msanii huyo.
“Kwa upande wa dada yetu Rose Mhando, ndani yake Mungu alimuwekea hazina kubwa sana. Adui                nae alipopata mlango tu akaingia ili kuiharibu. Kwa bahati mbaya hakuna mtu aliyeweza                              kusimama kikamilifu katika nafasi kumsaidia.

Hivyo ni vyema tukaendelea kumuombea na kumsaidia kuliko kum-discuss na kumsema. Watu                  wengi hawajui shetani yuko kazini wakati wote, na ukishampa nafasi anakutawala na bila kupata                  msaada haraka waweza angamia kabisa”

Mchungaji Shillah Afungukia Swala la Rose Muhando

Mtumishi wa Mungu mchungaji Shillah amefunguka na kuongelea kile kinachoendelea kuongelewa katika mitandao ya kijamii kuhusu hali ya rose muhando ambae ni msanii wa injini nchini Tanzania ila kwa sasa yuko nchini Kenya .

Mwanadada huyo ambae aliripotiwa kuwa yu mgonjwa mautiuti na hata kabla ya hapo ailiwahi kusambaa video ikimuonyesha yuko kwa mchungaji akitolewa mapepo.

Mchungaji anasema kuwa watu wamekuwa wakimsema vibaya mchugaji aliyekuwa akimuombea rose muhando kwa madai kuwa hakufanya vizuri kwa sababu msanii mkubwa kama yule aliitaji usiri wa maombezi.

Mchungaji shillah anapinga hilo na kusema kuwa , watu wemgi wakubwa na maarufu wamekuwa wakiombewa  wanaonekana kwenye tv hata dunia nzima inakuwaje ishindikane kwa Rose Muhando.

Mchungaji anasema kuwa ni kweli kilichomkuta rose muhando ni pepo na wala sio vinginevyo.

Nilipofanya uchunguzi wangu wa kiroho niligundua kwamba , rose muhando kilichomkuta ni mapepo kweli sio uongo wala kiki na pia mimi nina mtetea mchungaji kwa sababu mimi ninapomtabiria mtu nikamrekodi kwanini akitokea staa nisikirushe? watu kama kina prophert joshua wanawatabiria maraisi na wanawaonyesha kwanini asiwe yeye , ile sio kiki.

Rose Muhando Hoi ICU-Kenya

Hali ya mwanamuziki wa injili Rose Muhando inasemekana kuwa mbaya huku ikisemwa kuwa hali yake wa sasa imekuwa ikiangaliwa na baadhi ya waimbaji wenzake ambao wamekuwa wakifanya siri juu ya afya ya mwanadada huyo.

Habari zinasema kuwa mwanadada huyo amekuwa akisumbuliwa na mkono ambao hapo awali katika baadhi ya picha na video zilizokuwa zikimuonyesha akiombewa kanisani zilimuonyesha kama mtu alievunjika mkono.

Hata hivyo inasemwa kuwa hata wenyeji wake ambao ni waimbaji wenzake wamekuwa wakifanya siri sana kuhusu kutoa taarifa ya kinachomsumbua ilhali mtu huyo yu mautiuti kitandani.

Hata baada ya gazeti la Risasi kupata habari hizo walianza kufatlia ukweli kwa kumuuliza kiongozi wa chama cha wanamuziki wa injili Tanzania, Bi Stella Joel na alisema kuwa hata wao wamesikia tu taarifa hizo lakini hakuna uhakika wowote na wanafatilia kwa karibu na watatoa taarifa.

Sheikh Afungukia Kinachomsibu Rose Muhando

Sheikh Abdulrazack aliyejizolea umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii kwa kuwa mlezi wa wasanii mbali mbali ametoa Siri ya nini hasa kinachomsibu Msanii wa nyimbo za Injili Rose Muhando.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Big Chawa wa Planet Bongo ya East Africa Radio, Sheikh Abdul Razak amesema kwamba mwanamuziki huyo atakuwa amemkosea Mungu kwa namna yoyote ile, hivyo njia sahihi ya yeye kumaliza matatizo yake ni kupiga goti na kuomba toba.

Akiendelea kuzungumzia hilo Sheikh Abdulrazak amesema kwamba binadamu yeyote ambaye kweli moyoni mwake ana Mungu, hawezi pitia anayopitia Rose Muhando, kwani hakuna uchawi unaoweza kupanda kwenye Mungu, hivyo ni vyema kwa yeye mwenyewe kuamua kumrudia Mungu.

Lazima uelewe kitu kimoja, mtu yeyote ambaye ndani yake kuna nafsi ya ufalme wa Mungu, hawezi kudhuriwa na wachawi, hawezi kudhuriwa na ushirikina, kuna mitihani Mungu atakupa, ni kujaingalia tu wapi alimuacha Mungu, wapi alimkosea Mungu, pale alipomkosea Mungu ndiyo funguo pekee ya yeye kurekebisha hayo yaliyoharinika, yeye mwenyewe Rose Muhando kuna sehemu kamkosea Mungu, hapo ndipo pa kutengeneza, yeye mwenyewe apige goti”.

 

Ray C Awataka Watu Wajitokeze Kumsaidia Zaidi Rose Muhando

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Rehema Chalamila maarufu kama Ray C ameibuka na kuwataka watanzania wote kuungana na kumsaidia Msanii mkongwe wa nyimbo za injili Rose Muhando.

Ray C ameweka wazi kuwa mpaka hivi sasa Rose Muhando yupo tu nchini Kenya ambapo makazi yake yapo lakini hana msaada wowote hivyo ameitaka serikali na wananchi kwa ujumla kujitokeza na kumsaidia Rose Muhando.

Kipitia ukurasa wake wa Instagram, Ray C ameandika maneno haya kutokana na maradhi yanayomsumbua msanii huyo wa nyimbo za injili:

https://www.instagram.com/p/BqpeRXTls6I/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=17h9a99f7xnox

Rose Muhando Atangaza Kurudi Uislamu

Mwanadada Rose Muhando ametangaza kurudi tena katika dini yake ya kiislamu baada ya kusema kuwa amegundua kuwa ule upendo aliwahi kuambiwa upo katika ukristo hauoni zaidi ya majonzi na maumivu kila siku.

Habari za Rose Muhando zimekuwa zikisambaa sana hapa karibuni kutokana  kuwa mwanadada huyo kwa sasa amekuwa akinekana kama amechanganyikiwa sana na kuwa amefirisika  na hata watoto wake hawana tena mahali pa kuishi.

Wakati ninaokoka niliambiwa maneno ya upendo sana na kwamba nitakutana na upendo lakini badalayake nimekuwa nikikutana na mahsuti tu kila siku, kwa mfano mtu anakuharika sehemu unashindwa kufika na unatoa taarifa lakini kesho yake unasikia kuwa anatangaza umemtapeli, wanashindwa kujua na kukumbuka hata jema moja kutoka kwangu.Nafikiria kurudi kwenye dini yangu ninaamini nitapata faraja.

Rose alikuwa moja ya wasanii wakubwa sana wa injili huku akisifia kila kona ya Tanzania na nje ya Tanzania kwa kazi zake, nyimbo zake zilikuwa zikipendwa na kila mtu bila kujali umri wala dini.

 

Emmanuel Mbasha Akerwa na Mchungaji Aliyemuombea Rose Muhando

Kuna video imesambaa ikimuonyesha Mwimbaji Mkongwe wa nyimbo za Gospel Rose Muhando akifanyiwa maombi ambapo kila mmoja amekua na maoni yake baada ya kuitazama. Hapo chini ni mtazamo wa Msanii wa Injili, Emmanuel Mbasha.
‘Nikiwa kama baba wa kiroho na mlezi mkuu wa waimbaji wote wa nyimbo za injili Tanzania, napenda kuweka wazi kuwa nimehuzunishwa sana na hii video ya maombezi ya muimbaji mwenzetu Rose Muhando.
Kwa unyenyekevu kabisa naweza kusema kuwa, maombi ni muhimu sana kwa watu wote, ila namna ya kuombea ikiwa mbaya inaweza kuharibu umuhimu wote wa maombi na kusababisha maombi yadharaurike au yamdharaulishe aliyeombewa.
Katika nia yangu ya ndani nimefurahishwa sana na kitendo cha Rose kuombewa, ila kero yangu kubwa imekuwa kwenye njia iliyotumika kumuombea. Rose Muhando ni star, na katika medani za mziki wa injili ni mtu anaetazamwa na watu wengi sana kama rol model wao, hivyo nadhani ilikuwa ni bora zaidi kuwa waangalifu katika kumuombea ili kulinda brand yake.
Biblia inasema, mwenye heshima apewe heshima, hivyo kwangu mimi sidhani kama mchungaji aliyemuombea Rose amempatia heshima anayostahili, maana binafsi sikuona haja ya kuwasha camera na kuanza kumuombea hadharani vile.
Hali hii inaweza kumtangaza sana muombeaji lakini kwa upande wa muombeaji inaweza kuzidisha tatizo na kusababisha adharaulike zaidi kwenye jamii inayomtazama. Watumishi wa Mungu mahitaji kuwa na hekima pamoja na kifua cha kutunza siri, na siyo kufanya mambo kwa mihemko huku mkitazama maslahi yenu.
Mimi nadhani ingekuwa bora sana endapo mchungaji angemuombea ofisini, na kama maombi yangeleta majibu naamini video ya shuhuda ambayo Rose Muhando ange ongea wakati akiwa na akili zake timamu ndiyo ingefaa kusambaa na kuendelea kumjengea heshima yeye pamoja na mtumishi aliyemuhudumia.
Kumbuka yule Akida (mkuu wa vikosi cha askari wa kirumi) alipohitaji maombi kwa Yesu, Biblia inasema Yesu alifunga safari kwenda nyumbani kwake ili kumuombea. Unadhani kwanini hakumwambia apelekwe amuombee hadharani kama alivyofanya kwa Batromayo? Hii ilikuwa ni hekima ya kulinda heshima ya muombewaji. Maana huwezi kumuombea Rais kama unavyoombea ombaomba au mpiga debe.
Kwa kweli nimeamua kuwa muwazi na kuziweka huzuni zangu hadharani ili waombeaji mjirekebishe. Siyo kila maombi yafanyike wakati caméra ziko on, kuna mengine ya kuzima camera na kuomba kwa staha ili kuendeleza uhai na kipawa’

Rose Muhando Kukufuliwa Tena Kwenye Muziki Wa Injili

Rose Muhando ni msanii wa kike wa injili aliyekuwa ameteka nyoyo za waamini wengi sana katika muziki wa injili, sio kwa upande wa kikristo tu lakini Rose alibeba mashabiki katika dini zote  hii yote ni kutokana na vile ambavyo msanii huyo alivyokuwa akifanya vizuri katika muziki wa injili.Imepita muda wa takribani miaka miwili au zaidi tangu msanii huyu wa kike awe kimya katika muziki wa injili, ingawa  kumekuwa na wasnii wengi wanochipukia na wamekuwa wakifanya vizuri lakini bdao kiu ya mashabiki kwa msanii Rose Muhando bado inaonekana.

Akiongea na waandishi wa habari, aliyekuwa meneja wa msanii huyo Alex Msama anasema kuwa ni kweli rose muhando alikuwa kimya kwa muda mrefu lakini hiyo yote ilisababishwa na yeye mwenyewe kwa sababu kuna kipindi alikuwa ameendekeza tabia ya utapeli kwa mashabiki zake na baadahi ya mameneja.Pia kulikuwa na kesi nyingi sana polisi zilikuwa zikimhusu, lakini kwa sasa anampngo wa kumrudisha tena kwa mashabiki ili aendelee kuwaburudisha mashabiki zake kwa sababu kwa sasa msanii huyo maebadilika kabisa na ana imani atafanya vizuri tena kama hapo awali.

  Rose alizidisha sana mambo yake ya utapeli ndio maana nikaacha kufanya nae kazi, na tangu hapo roseamepotea kabisa katika muziki wa injili,lakini nimethamilia kumrudisha hivi karibuni tu  mashabiki na wapenzi wake wakae mkao wa  kula maana rose ni msanii mzuri  sana na anajua kuimba vizuri.-Alisema meneja huyo

Hii itakuwa ni moja ya habari njema kwa mashabiki wa injili kwa sababu nyimbo za Rose Muhando zilikuwa zikipendwa na kuchezwa na watu wa kila rika na kila dini kutokana na uzuri wake.

Hili ndilo kosa ambalo lilisababisa kukamatwa kwa Rose Muhando

Msanii maarufu wa nyimbo za injili Rose Muhando anazuiliwa na polisi mkoani Singida baada ya kukamatwa  kwa kupata pesa kwa njia ya udanganyifu.

Kwaya ya AICT Singida ilimshtaki Rose Muhando kwa kuwalaghai Tsh. 800,000. Muhando alilipwa laki 800 kwa njia ya M-Pesa kwa makubaliano angeweza kufika kwenye uzinduzi wa kwaya ambao ulipangwa kufanyika November 8 mwaka jana lakini hakufanya hivyo.

Rose Muhando

Kwaya hio ingefaa kuongezea Muhando laki 150 ingine baada kufika kwenye uzinduzi huo. Mwimbaji huyo hata hivyo hakuweza kufika kwenye uzinduzi huo na pia hakurejesha laki 800 alizolipwa.

Jeshi la Polisi mkoani Singida linamzuia Rose Muhando kwa kituo cha polisi kwa mahojiano kufuatia tuhuma zinazomkabili.

\

Rose Muhando atoweka nyumbani kwake mjini Dodoma

Mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili Rose Muhando adaiwa kutoweka nyumbani kwake baada ya kutopea kwenye matumizi ya dawa ya kulevya.

Mwandani wa mwimbaji huyo aliwaambia wanahabari kwamba Muhando alikua akisakwa na uongozi wa Sober House ya Pederef ili waweze kumwokoa na matumiza ya mihadarati.

“Kuna kiongozi mmoja wa dini hapa Dodoma, ameamua kujitolea kumsaidia Rose baada ya kusikia hali yake ni mbaya. Ameamua kuwatafuta Pederef ili wamsake popote alipo na wakimpata wampeleke soba moja kwa moja na gharama zote yeye atazishughulikia,” Chanzo kilicho karibu na Muhando kilisema.

Mmliki wa Sober ya Pederef, Nuru Saleh, alidhibitisha madai hayo alipoulizwa na wanahabari. Saleh alisema kwamba alimtafuta Rose Muhando na kumrudisha katika soba yao iliyopo Dodoma na kuanza kumpatia tiba ya kuacha matumizi ya madawa ya kulevya.

“Ni kweli. Sisi ndiyo kazi yetu. Nimepewa hiyo kazi na kiongozi wa dini, naomba nisimtaje lakini tumeshaanza kumtafuta na tukimpata tu, tutampeleka kwenye soba yetu ya Dodoma,” Nuru alisema.