Sauti Ya Ruby Yaacha Historia Tuzo Za SZIFF

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Hellen George maarufu kama Ruby ameacha historia ya aina yake kwenye tuzo za SZIFF Baada ya kupiga bonge la shoo.

Ruby ameweka historia Jumamosi ya Februari 23, 2019 kwenye kumbukumbu za wapenda burudani wengi, achana na namna waigizaji wachanga walivyowaangusha mastaa kwenye kipengele cha Muigizaji bora wa kike na wakiume, bali namna shoo kali kutoka kwa msanii Rubby alikonga nyoyo za mamia waliofika kuhudhuria hafla hiyo ya kipekee kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini.

Rubby ambaye alipanda kwenye jukwaa la SZIFF saa 4:50 hadi saa 5:13 usiku aliamsha shangwe la maana baada ya kutoa burudani ambayo haikuacha chembe yoyote ya shaka, achilia mbali vazi lake kali.

Mashabiki mbali mbali walishindwa kujizuia na kumimiminika stejini kwa ajili ya kumtunza ambapo anasemekana kupata pesa nyingi sana.

Lakini pia mastaa mbali mbali kama Jokate Mwegelo, Mama Diamond na wengineo wamempongeza Ruby na kuisifia sauti yake matata.

“Mimba Yangu Hainizuii Kupiga Kazi Kama Kawaida”-Ruby

Msanii wa muziki wa Bongo fleva ambaye Hivi sasa anafanya vyema na single yake ya ‘Alele’ Helen George ‘Ruby’ amefunguka na kuweka wazi kuwa pamoja na  kwamba ni mjamzito Lakini sio kikwazo kwake kwani anapiga kazi kama kawaida.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Ruby  amefunguka kuwa, kabla hajapata mimba alihisi labda akiipata atashindwa kufanya shughuli zake nyingine, lakini hali imekuwa tofauti kwani anapiga kazi kama kawaida.

Mwanzoni kabla sijapata mimba nilijua nikija kupata, basi sitaweza kufanya chochote, nilidhani labda nitakuwa nachoka sana, lakini namshukuru Mungu hali imekuwa tofauti kwani baada ya kuipata sasa hivi napiga kazi kama kawaida na nitaendelea hadi nitakapojifungua“.

Ruby anategemea kujifungua Mtoto Wake wa kwanza muda wowote kuanzia Hivi sasa ingawa Mpaka leo bado hajamuweka wazi nani baba wa Mtoto wake.

Shetta Athibitisha Kuwa Utovu Wa Nidhamu Wamfukuzisha Ruby ‘King Empire’

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Shetta ambaye pia ni mmoja wa viongozi Katika kampuni na Recording Label ya Kings Empire ameweka wazi sababu za kusimamishwa Msanii Ruby.

Kings Empire inasimamia wasanii Kama vile The Mafik, Aslay na wengineo wameweka wazi mmoja wa aliyekuwa Msanii wao Ruby hayupo tena na Label hiyo kutokana na kukosa nidhamu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Clouds FM, Shetta ameweka wazi kuwa  Ruby alisimamishwa na label hiyo baada ya kuonyesha utovu wa nidhamu.

Siwezi kusema sababu bali sisi ni familia kuna vitu vinatokea hata wachawi hugombana usiku wakiwanga, Hivyo kulitokea mpishano wa kauli kati yake na Meneja Kapasta kwenye group hivyo nikamwambia Ruby muheshimu kiongozi mara akanivamia na mimi hivyo nikamwambia #hambuso aandike barua ya kumsimamisha kwa muda kwa utovu wa nidhamu na angerudi tungezungumza lakini naona akaamua kufanya kazi zake yeye kama yeye“.

Skendo ya kuwa na kiburi na jeuri imekuwa ikimuandama Ruby kwa muda sasa ambapo watu kadhaa aliofanya nao kazi wameshawahi kumtuhumu kwa kuwa na tabia hizo ingawa mwenyewe ameshawahi kukataa taarifa hizo.

“Ruby Inabidi Ujifunze Kula na Kipofu”-Vanessa Mdee

Msabii wa muziki wa Bongo fleva Vanessa Mdee maarufu Kama Vee Money ameibuka na kumtaka Msanii mwenzake Ruby kujishusha kwa watu na kupunguza kiburi.

Kwa muda mrefu kumekuwa na tuhuma dhidi ya Ruby kuwa ni mgumu kufanya naye kazi kwani Ana kiburi kupitiliza kwaiyo inakuwa ngumu kwa wasanii wenzake na wadau kufanya naye kazi.

Siku ya jana Mange Kimambi alimchana Ruby kuhusu taarifa za kuwa mjeuri na kiburi mbele ya watu wanaomsaidia na kudai Ana kipaji sana lakini hafanikiwi kwa sababu watu wengi hawataki kufanya naye kazi kwa ajili ya kiburi chake.

Vanessa Mdee naye ameibuka na kumpa ushauri Ruby na kumtaka ajishushe anapokuwa na watu ili azidi kufanikiwa zaidi.

Kupitia Instagram, Vanessa Mdee amemuandikia maneno haya Ruby:

Leo nimekutana na Ruby na tumeongea sana kuhusu hii ishu yake, Nakupenda sana Ruby tupige kazi mama kula na kipofu, kuna muda mwingine jifunze kukaa kimya halafu acha muziki wako uongee zaidi fanya kwa manufaa yako na Mtoto wako”.

Ruby anatarajia kujifungua Mtoto Wake wa kwanza muda  wowote kuanzia sasa kwani hapo alipo ana  ujauzito wa miezi kadhaa.

Mange Amtaka Ruby Apunguze Kiburi Ili Afanikiwe

Mwanaharakati wa mambo ya siasa mtandaoni Mange Kimambi ameibuka na kumchana live mwanamuziki wa Bongo fleva Ruby na kumtaka aache kiburi.

Lwa muda mrefu kumekuwa na taarifa kwamba Ruby amekuwa hana maelewano mazuri na watu anaofanya nao kazi na kupelekea kuzidi kushuka kimuziki.

Mange amempa makavu Ruby na kumtaka apunguze kiburi kama anataka kufanikiwa kwani watu wengi wanashindwa kufanya naye kazi kutokana na jeuri na kiburi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mange amemuandikia Ruby ujumbe huu:

https://www.instagram.com/p/BqIdS2bA8qX/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=ww4uerb3oa9a

Utovu wa Nidhamu Wasabisha Empire Kumsimamisha Kazi Ruby.

Meneja wa kundi la The Mafik  na pia mkurugenzi wa  lebe l ya empire amefunguka  na kuthibitisha taarifa kuwa msanii Ruby amesimamishwa katika lebel hiyo huku sababu kubwa ikiwa ni utovu wa nidhamu,.

Meneja huyo anasema kuwa nidhamu imekuwa ikijumulisha vitu vingi hivyo hawezi kusema moja kwa moja ni upande gani hasa lakini hiyo ndio sababu kubwa.

tumemsimamisha ruby lakini sio kumfukuza , ila amesimamishwa kwa muda na sababu kubwa ni nidhamu tu hakuna kitu kingine.kuhusu nidhamu inakuwa na vitu vingi kwaio ina mambo mengi siwezi kusema kuwa ni kitu kimoja tu.

Ruby ambae hata hapo awali aliwahi kuripotiwa kushindwa kufanya kazi na THT na kusimama katika muziki kwa muda  mrefu sababu ilikuwa ni hiyo hiyo ya nidhamu lakini inaonekana kuwa ilishindikana.

Ruby aAjikita Katika Penzi Jipya na Msanii Mwenzie

Mwanadada Ruby mapenzi yamemkaba kooni na kushindwa kujizuia kufanya siri tena kwa kile alichamoa kukuifanya katika ukurasa wake wa instagram baada ya kutoa povu juu ya watu wanaomsema kuhusu mwili wake kuwa umekonda kila siku.

Ruby ambae alisema kuwa amechoka kila siku kusikia watu katika mitandao ya kijamii kuwa wanamsema mwili wake unazidi kupungua, huku akisema kuwa maneno hayo hajali ilimradi kusah (ambae alimtag) akiupenda kwake inatosha.

ooooooh mara kakonda mlishawahi kuninenepesha, nyie ni nani sasa kuusema mwili huu..mwili una wenyewe huu akiupenda @kusah   basi inatosha .ISIWE TABU TUKUTANE NGOME KONGWE.

Kwa maneno hayo uenda ikawa hii ni moja ya njia ambayo ruby ametumia kutuonyesha kuwa kwa sasa amejiweka hapo.

 

Mnasema Nimekonda Mlishawahi Kuniona Nimenenepa.:-Ruby

Mwanadada Ruby amefunguka na kuongelea picha zilizowahi kusambaa katika mtandaa wa instagram zikimuonyesha kuwa amekonda mpaka sehemu yake ya mbavu zikiwa zinaonekana na kusemwa sana ktika mtandao wa kijamii kuhusu kukonda kwake huko.

Hata hivyo Ruby amekanusha kuwepo kwa picha zake za aina hiyo na kusema kuwa picha hzio hazikuwa za kwake kwa sababu katika maisha yake hajawahi kunenepa mpka kufikia hatu ya watu kumwambia kuwa amekonda.Akiongea katika kipindi cha Friday Night Live, Ruby ameknausha kukonda huko huku akikanusha ia swala zima la yeye kutumia madawa ya kulevya.

Ile picha na sio hata ya Ruby, alafu mnasema kuwa nimekonda  kwani mlishawahi  kuniona nikiwa nimenenepa, haingii akilini kama vitu vya negative wanavyoongea wakati muda huo mimi kazi nafanya, na ninaangalia mbele kwenye kazi zangu.kazi yangu ndio inayoongea na wala sio mimi , mnaongelea mimi kuonekana kwa mbavu zangu mbona hamuongelei mimi kuonekana nikiwa na makalio makubwa.

Ile picha ilikuwa imepigwa kwa pembeni hata ukiangalia katika video yangu ya niwaze ndio utajua vizuri, wawe wanaleta show ili tunenepe.

 

Ruby Akana Kujihushisha Mambo ya Kishirikina.

Msanii wa bongo fleva Ruby amefunguka na kukanusha tetesi zinazosambaa juu yake kwamba amekuwa akitumia nguvu za giza kwa ajili ya kuu-push mziki wake ili uweze kufanya vizuri katika soko la muziki.Mwanadada huyo ambae hivi karibuni ametoa wimbo wake mpya wa Niwaze ambao amewashirikisha yhe mafik nasema kuwa tuhuma hizo sio kweli juu yake hata kidogo.

Mimi siko hivyo na wala siyajua hayo mambo kabisa , mimi nina bibi na babu yangu wako tanga hayo mengine siyajuai kabisaaa- alisema ruby alipokuwa akiongea na Papaso ya TBC.

Ruby anasema kuwa kwa anachokiamini yeye ni Mungu na ndio anaemsaidia katika muziki wake hayo mengine hayajuai na kupenda mashabii zake kumemfanya afanyye vizuri zaidi.

 

Ruby Afunguka Kuhusu Kushindwa Kufanya Show South Afrika.

Msanii wa muziki wa bongo fleva RUBY  ambae alikuwa kimya kwa miaka kadhaa kutokana na matatizo ya manejiment , lakini kwa sasa amerudi tena katika game amefunguka na kujibu tuhuma alizokuwa akizushiwa kwa muda mrefu kuhusu yeye kushindwa kufanya shoo nchini Afrika ya Kusini kwa madai ya kuwa alikuwa amelewa sana kutokana na vitu alivyokuwa akitumia na kumfanya abaki kulala tu hotelini.

Hata hivyo baada ya kuulizwa na eNews kuhusu habari hizo aliwajibu kwa hasira na kuhamaki na huku akisema kuwa habari hizo sio za kweli watu wanaongea vitu visivyokuwa na ukweli ndani yake

kuna sababu nyingi sana za kusafiri na mimi ukiona nimesafiri ujue nimeenda kupiga kazi , kiufupi ninaweza kusema kuwa watu wa south afrika ni watu peacefully sana , wakisema wanakipend kitu basi ujue wanakipenda kweli  na siwezi kusema ni show ngapi nimefanya nikiwa kule ila huwa naziweka katika ukurasa wangu wa instagram.

Ruby alikuwa kimya kwa muda mrefu lakini amerudi sasa na kutoa wimbo aliowashirikisha kundi la The Mafik.

 

Ruby Adai Wasanii Wengi Wanashindwa KujiBrand

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Ruby amefunguka na kusema sababu kubwa iliyonfanya akae kimya ni ilikua ni kwa dhumuni la kujitengezea au kujibrand kibiashara zaidi.

Msanii huyo ameweka wazi kuwa wasanii wengi wanafeli katika hilo kwani inapelekea wao kushindwa kujitengenezea soko lao binafsi la biashara.

Kama tunavyojua tofauti na zamani hivi sasa muziki ni biashara zamani muziki ulikuwa ni burudani tu lakini sasa watu wanaishi na kuendesha maisha yao kwa kutegemea muziki.

Kwenye Interview na Bongo 5, Ruby alifunguka na kutaka sababu za ukimya wake ambapo aliweka wazi kuwa ni katika kujitengeneza na kumuweka kibiashara zaidi.

Kwa sababu napenda vitu vizuri na vyenye kukaa kwenye biashara yangu muda mrefu kwa sababu nilikuwa natengeneza soko langu binafsi.

Watu wamekosa ile akili ya ziada ya kibiashara kwamba muziki si vile watu wanataka ila ni vile unautengeza kwa sababu ni kitu chanko kila mtu ana biashara yake”.

Baada ya ukimya mrefu tangu aondoke Clouds Fm, hatimaye ameachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Niwaze ambao amewashirikisha kundi la The Mafik.

 

Wasanii Wamekosa Akili ya Biashara;-Ruby

Mwanadada Ruby amefunguka na kusema kuwa kukaa kwake kimya hakukumaanisha kuwa alikuwa amefulia lakini pia alikuwa akijipanga jinsi ya kuja kurudi katika soko lake na sio kwamba angeiga kile walichokuwa wakifanya wengine.

Ruby anasema kuwa wasaii wengi hawana ile akili ya biashara na muziki wamekuwa wakifanya vitu kwa kuiga tu lakini kwake ni tofauti.

Nilikaa kimya ili kuutengeneza muziki wangu kwanza.wasanii wengi wamekosa ile akili ya baishara na kujua kwamba muziki sio vile watu wanavyoraka wewe uwe lakini ni vile wewe unavyoutengeneza kwa sababu kama mwenzio anauza maembe sio lazima na wewe uuze maembe unaweza kuuza kitu kingine tu au ukauza kile kwa maboresho zaidi.

Ruby ambae ametoa wimbo wake mpya unaitwa niwaze aliowashirikisha The Mafik anatoa sababu ya kuwashirkisha wasanii hawa na sio watu wengine akisema,

Niliwachagua the mafik kwa sababu ni wanaume wenye sauti za kupangilia na zinaweza kukaa kwenye muziki na kufanya muziki usikike vizuri.

Ruby Akiri Kuvutiwa na Jux

Mwanamuziki wa Bongo fleva Ruby amefunguka na kuelezea mapenzi yake kwa msanii mwenzake wa Bongo fleva Juma Jux Kwenye upande wa uimbaji wake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Clouds Fm, Ruby amekiri kuwa anavutiwa sana na uimbaji wa Jux hasa kwa sababu nyimbo zake nyingi zinawagusa wanawake huku akitaja wimbo unaoikonga sana nyoyo yake ni utaniua:

Kwa sababu nyimbo za Jux karibia zote zinawashika kwanza wanawake, halafu pia uimbaji wake ni RnB ambayo anaweza kuimba mwanaume au mwanamke, kwa hiyo nafikiri ule uliniingia zaidi”.

Jux ameonekana kama moja kati ya wasanii wa kiume ambao wanavutiwa sana na mabinti kwani kuna watu maarufu kadhaa waliokiri kuvutiwa na Jux ikiwemo Socialite maarufu kutoka Kenya anayejulikana kama Huddah na hata Amber Lulu.

Ruby amerudi kwa kasi ya ajabu Kwenye muziki na hivi sasa anafanya vizuri kwa wimbo wake wa One and only alioshirikishwa na Nedy Music.

Ruby Aiangukia Clouds FM Kwa Magoti na Kuomba Msamaha

Msanii wa Bongo fleva Ruby Africa amejishusha na kuiangukia kituo cha redio cha Clouds FM baada ya bifu lao la muda mrefu.

Msanii Ruby ambaye alijipstia umaatufu kwa mara ya kwanza alipokuwa chini ya THT (Tanzania House of Talent) aliingia kwenye mgogoro na uongozi wake huo na kusababisha kufarakana hali iliyopelekea Ruby kuendelea kuwa kimuziki kivyake.

Baada ya kutengana na kituo hicho Ruby alipotea kimuziki kwani hakuna nyimbo yake iliyovuma na baadae kuamua kupumzika kufanya sanaa kwa kipindi cha mwaka mzima wa 2017.

Baada ya kutangaza kurudi rasmi kwenye sanaa mwaka huu mwanzoni Ruby alifanya mahojiano na kipindi cha XXL ya Clouds FM kwa kipindi kirefu tangu afarakane nao na alianza kwa kuomba msamaha kwa kituo hiko na mashabiki zake alifunguka yafuatayo:

Ujumbe huu ni kwa yoyote, awe mwanakamati wa Clouds, team clouds au shabiki  wa nje napenda kuomba msamaha na kusema sorry to my fans, sorry to my management Clouds media na pia sorry to my country, Clouds nawapenda sana nisameheni nilikosea ninachohitaji ni support yenu, naamini kwamba ukiwa mjinga kwenye kila kitu ndio utapata kujua vitu vingi sana, nilikaa nikamuomba boss wangu Rugs samahani Mimi ni mdogo wewe ni Mkubwa kwaiyo kwa chochote Mimi nimekosea”.

Tangu alipogombana na uongozi huo wa Clouds Media Group nyimbo zake zilipigwa stop kupigwa na pia alikuwa haalikwi kwenye shoo za Clouds kama Fiesta lakinitangu ameomba msamaha nyimbo zake zimeanza kusikika Clouds.

Babu Tale Kamchana Ruby Kuwa Siku Akigundua Tatizo Lake Akajirekebisha Basi Heshima Yake Itarudi

Mdau mkongwe katika sanaa ya Bongo fleva Babu Tale na maarufu zaidi kwa kuwa meneja wa mwanamuziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz, amefunguka na kumchana msanii Ruby kuhusu tatizo alilonalo.

Ruby ambaye ni mwanamuziki wa Bongo fleva alifanya vizuri zaidi na vibao vyake mbali mbali siku za nyuma kidogo kwa kipindi cha mwaka mzima Ruby amekuwa kimya bila ya kutoa ngoma yoyote zaidi ya kuonekana kwenye mitandao ya kijamii jambo alilolieleza kuwa amechukua mapumziko kidogo.

Mziki wa Ruby ulianza kulega lega pale alipoamua kujitoa kwenye jumba la vipaji Tanzania (THT) ambapo sanaa yake mwanzoni kabisa aliianzia kwenye jumba hilo lakini mwishoni alipishana kidogo na mabosi zake huko THT  na kuamua kujiengua.

Siku ya Jana kuna video clip iliyomuonyesha Ruby akiimba wimbo wa dini wakusifu kwa hisia kali ambapo wasanii mbali mbali walikiri kuikubali sauti yake na kukikubali kipaji chake wakiwemo Kajala, Jacqueline Wolper, Shetta, na pia Babu Tale.

Babu Tale kupitia ukurasa wake wa Instagram aliiposti video hiyo na kuisindikiza na ujumbe uliomtaka Ruby kujua anasumbuliwa na ugonjwa gani kulitatua na kisha atapata heshima yake kwenye muziki anaofanya:

Fundi Sana we binti siku ukijua unaumwa nini na ukaamua upone basi ujue heshima ya wote wanao kuchukulia poa itarudi kwako Helena mama mimi nakuzimia unajua hilo mimi ni mmoja wa watetezi wako popote ulipo mama”.

Hii ndio video clip ya Ruby iliyozua gumzo siku ya Jana mtandaoni:

 

Ruby- Sihitaji Makalio Makubwa Ili Kuvutia Wanaume

Mwanamuziki wa Bongo fleva Ruby anayetamba na kibao chake cha ‘Nayule’ amerudi tena katika vichwa vya habari kuhusu makalio makubwa huku safari hii akidai kutu hatoweza kutumia madawa ya kichina kuongeza makalio ili tu avutie wanaume.

Wiki iliyopita Ruby aliwashangaza watu wengi pale alipotupia picha Instagram akiwa amefungasha bonge la wowowo hali iliozua utata kutokana na kuwa ukweli unaojulikana ni kuwa Ruby ni msichana mwenye umbo dogo kwaiyo hata makalio yake huwa ni madogo kwaiyo kitendo cha kuposti picha ambayo ghafla ilimuonyesha na msambwanda mkubwa ulishtua wengi.

Baada ya picha hizo kusambaa na kupata attention kubwa ya wanaume huku wengi wakimsifia  akiwa na wowowo kubwa Ruby amedai kuwa hatojiaribu kwa kufanya vitu vya ajabu ili kupata makalio makubwa ili tu apendwe na wanaume.

Kwenye interview aliyofanya na Enews ya East Africa Tv, Ruby ameongea haya kuhusiana na ishu hii;

Kwa kweli watu wengi walionesha muitikio mkubwa sana baada ya zile picha kutoka inaelekea wengi sana walivutiwa lakini kitu ambacho nimejifunza kwa mashabiki zangu ni kujikubali yaani siwezi kujibadilisha ili nikubalike na watu huyu mnaeniona ndio mimi siwezi kubadilika hasa eti tu ili nipendwe na mwananume hapana huyo sio mimi”.

Ruby ambaye ametoa nyimbo yake mpya baada ya kukaa kimya kwa muda karibia mwaka mzima ameoekana kupokelewa vizuri na watu kuikubali kazi yake mpya aliyoitoa baada ya hii kiki ya makalio.