Mwili Wa Ruge Mutahaba Kuzikwa Jumatatu Mkoani Bukoba

MWILI wa Mku­rugenzi wa Vipindi Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, unatara­jiwa kuwasili nchini kesho Ijumaa uki­tokea nchini Afrika Kusini.

Ruge alifariki dunia Jumanne jioni akiwa huko kwenye matibabu kwa muda na kwa sasa msiba upo nyumbani kwa baba yake, Miko­cheni jijini Dar.

Kwa mujibu wa Mse­maji wa Familia, Anick Kashasha, taratibu za kuaga mwili itakuwa ni Jumamosi.

Aliongeza kuwa Jumapili mwili huo utasafirishwa hadi Kizilu, Bukoba, kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika Jumatatu.

Watu mbalimbali jana walijitokeza kutoa pole kwa familia pale Mikocheni wakiongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na viongozi wengine wa serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda.

Pia wasanii wa Bongo Movie, Bongo Fleva na sanaa nyingine mbalimbali waliku­wepo kutoa pole kwa wafiwa na wengine walifanya hivyo kupitia mitandao ya kijamii.

Kwa upande wake Majaliwa alisema: “Historia ya Ruge kwa upande wa serikali ni kubwa, kuanzia awamu ya nne na ya tano kwa kuwatu­mikia kikamilifu Watanzania kwa kuwasaidia vijana wengi kielimu na msaada wake wa hali na mali.

“Ruge alikuwa balozi wa kutafsiri Philosophy ya uzal­endo na fursa, vifo ni mpan­go wa Mungu tumuombee, salamu hizi ni kwa niaba ya serikali, kwa muda huu Rais John Magufuli anatimiza itifaki atakuja kutoa pole, tumuombee ndugu yetu.”

Naye Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba alisema kuwa:

”Uthubutu na kujituma kwa Ruge ni darasa ambalo ameliacha kwa kila mmoja aliyekuwa akimfuatilia, ubunifu na juhudi ni alama itakayodumu.”

Kala Jeremiah ambaye ni msanii wa Bongo Fleva alisema: Kuondoka kwa Ruge kutabaki kwenye kumbuku­mbu kutokana na namna alivyokuwa akijitoa kwa ajili ya sanaa na kuwasimamia vijana.

“Nimefanya kazi na Ruge, alikuwa mshauri mzuri mfano ni mwaka 2015 ambapo alinishauri niyatoe mashairi ya Prof. Jay kwenye Wimbo wa Nchi ya Ahadi, aliona mbele kwa kuwa Profesor alikuwa ameingia kwenye siasa ninaamini atakumbukwa daima.”

Pia Shirikisho la Soka la Tanzania kupitia kwa Rais wake, Wallace Karia, jana walionyeshwa kuguswa na msiba huo pamoja na taa­sisi mbalimbali za Serikali. ambapo walituma salamu za rambirambi kwa wafiwa.

Jakaya Kikwete: “Nimelemewa, Huzuni, Majonzi, Taifa Limepoteza Mtu Mahiri”

Raisi Mstaafu wa awamu ya nne Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefunguka kuguswa na msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa vipindi Clouds Media Group Ruge Mutahaba.

Raisi Kikwete Kupitia ukurasa wake wa Twitter amefunguka hudhuni yake Baada ya kufariki Ruge na kuweka wazi kuwa katika kipindi kigumu cha maombolezo:

Nimelemewa! Nakosa maneno ya kuelezea huzuni na majonzi niliyonayo kwa kifo cha Ruge Mutahaba. Taifa limepoteza kijana wake mahiri, mbunifu na mzalendo wa kweli. Nimepoteza rafiki, mshirika mwaminifu na mtu ambaye amenisaidia kwa mengi ktk uongozi wangu na hata baada ya kustaafu”

“Moyo wangu uko pamoja na wazazi wake, ndugu zake na familia yake katika kipindi hiki kigumu. namuombea kwa mola ampe mapumziko mema peponi. Ameen.” 

 

Pascal Cassian Awataka Wasanii Kuacha Unafiki Msibani kwa Ruge

Msanii Pascal Cassian ambae kwa sasa yuko hospitali akipatiwa  matibabu hospitali amefunguka na kusema kuwa wasanii wengi sasa hivi wameonekana kuguswa sana na msiba wa Ruge wakati alipokuwa hai hakuna aletaka kujali hali yake kwa ujumla.

Pascal Cassian ambae kwa sasa ni mgonjwa na alisaidiwa sana na mh paul makonda anasema kuwa wasanii walikuwa kimya sana na walikuwa wapi kuonyesha kusikitishwa kwao na hali ya Ruge mpaka wameona sasa hivi hayupo ndio wameanza kujitokeza kufanya hayo wanayofanya.

katika ukurasa wake aliandika

Familia Ya Ruge Yaweka Wazi Ratiba Ya Mazishi

Ikiwa zimepita siku mbili tangu aliyekuwa Mkurugenzi wa vipindi Clouds Media Group, Ruge Mutahaba afariki dunia Familia yake imeweka wazi ratiba ya mazishi yake.

NDUGU Kashasha ambaye ni msemaji wa Familia ya Mutahaba amesema kama mambo yakienda kama yalivyopangwa, mwili wa #RugeMutahaba utawasili jijini Dar es salaam kutokea Afrika Kusini siku ya IJUMAA (March 1/2019).

Ikiwa hivyo wakazi wa Dar es Salaam watatoa heshima za mwisho na kumuaga mpendwa wetu siku ya JUMAMOSI (March 2/2019). .

Baada ya hapo: Familia imeamua kwamba Ruge atakwenda kuzikwa nyumbani kwao huko Bukoba siku ya JUMATATU (March 4/2019) (Jumapili mwili utasafirishwa kwenda Bukoba).

 

January Makamba Amuandikia Barua Ya Majonzi Ruge Mutahaba

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira na Muungano, Mheshimiwa January Makamba amemuandikia Barua ya wazi aliyekuwa Mkurugenzi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba.

January Makamba na Ruge walikuwa na urafiki wa karibu sana na kifo chake kimeonekana kumgusa kiutofauti na kuamua kumuandikia Barua iliyobeba ujumbe mzito sana.

Ndugu yangu Ruge, najua ndio umewasili huko upande wa pili na si ajabu una mambo mengi na bado unasalimiana na jamaa zetu wengi waliotangulia. Lakini naomba uchukue muda wako kidogo kunisikiliza. Nimeumia sana na nimelia peke yangu kwamba umetuacha namna hii. Sawa, umeitwa kwa wakati wako na sisi hatuna kauli kwenye suala la wakati wa kuitwa lakini nilitegemea, na sikuwa na shaka kabisa, kwamba tutakamilisha yale mawazo yako mengi mazuri uliyoniambia. Sikuwa na shaka kwasababu nilishuhudia pale Hospitali ya Kairuki kabla hujaenda India, ulivyorudi kutoka India, na siku nimekuona Afrika Kusini, ulivyokuwa unapigana kupona — hadi madaktari wa Afrika Kusini wakakupa jina “Ruge, The Fighter”. Jina sahihi kabisa lililotafsiri harakati za maisha yako.

Unajua nini? Nilikuwa nangoja urudi Dar nikwambie nilichogundua mara ya mwisho nilivyokuona hospitali. Lakini ngoja tu nikwambie kabla sijaja huko uliko. Ile kiu kubwa ya kupona niliyoiona kwenye macho yako haikuwa kwa ajili yako wewe, bali kwa ajili ya kutoiangusha familia yako nzima iliyosimamisha kila kitu kukuuguza na Watanzania wote waliokuwa wanakuombea. Ulipigana kupona, sio kwa ajili yako, bali kwa ajili yetu. Hukuamka kitandani lakini hukushindwa mapambano kwasababu umeamkia ndani ya mioyo ya Watanzania. Huku tuliko karibu watu wote tunakumbuka ulivyotugusa. Jamaa yangu, tunakuomboleza wakati huu, halafu tutabaki tunafurahia nuru yako katika maisha ya wengi kwa urefu wa uhai wetu. Umekimbia mbio njema, umemaliza safari yako vyema.

Majonzi yangu ni kwamba umeondoka kabla sijalipa kwa ukamilifu deni langu kwako. Deni la upendo na urafiki wa kweli. Ulinipa heshima kubwa ya kuwa msiri wako — kwa kuniamini na kunielezea wasiwasi wako, ndoto zako, matumaini yako, harakati zako, mipango yako. Ulinipa heshima ya kunipa fursa ya kubishana nawe kuhusu mawazo na fikra zako.

Majonzi yangu ni kwamba kuna vitu fulani vikubwa na vizuri tulivipanga — mimi na marafiki na wadogo zako, kwa ajili yako, kwa staili yako — mapema mwezi Machi, ambavyo naamini vingekupa tabasamu. Kama unaweza, hapo ulipolala, tupe ishara tufanyeje.

Nafarijika kidogo kwamba nilipata nafasi ya kukukumbatia kwa mara ya mwisho. Sikujua kwamba tunaagana. Ulinishika mkono kwa nguvu, hukutaka kuuachia, na ulitabasamu niliposema nakungoja Dar tukae pale THT, kama kawaida yetu, kujadili mawazo na mipango yako mingi.

Ingawa umeshawasili huko upande wa pili, familia yako na watu wengi watauaga mwili wako kwa heshima kubwa. Utajengewa kaburi. Nadhani litawekwa marumaru. Lakini tukitaka kukusalimia tena hatutakutafuta kaburini kwako. Tutakutafuta kwenye nyoyo za watu uliowagusa na kuwasaidia. Na ni wengi kweli. Kumbukumbu yako itabaki kwenye nyoyo zao na kwenye mafanikio yao. Watoto wako hawapo peke yao. Watalia sana, lakini ni kwa muda tu; kwasababu watafunikwa kwa upendo wetu sote na watafarijika, na watakuwa na fahari, kwa jinsi unavyosemwa na unavyokumbukwa.

Ndugu yangu, nisikuchoshe. Mengine tutaongea tutakapokutana tena kwasababu kwa hakika sisi sote, mmoja mmoja na kwa wakati wetu, kwa kadri ya mipango ya yeye aliyetuumba, tutakufuata huko. Miaka yote nimekujua, sijawahi kukuona umepumzika. Pumzika kwa amani kwa sasa — na milele.

Ndimi, rafiki yako,

January Makamba

27 Februari 2019”.

 

Mastaa Waguswa na Ugonjwa wa Ruge Mutahaba

Ni siku chache zimepita tangu taarifa zisambae kuhusu ugonjwa wa Mkurugenzi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba wasanii mbali mbali wameguswa na Suala hilo.

Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, wasanii hao wameguswa kwa kuweka mahojiano hayo huku wengine wakitumia nafasi hiyo kuomba Watanzania na wadau wa burudani kusaidia. Wasanii na watangazaji walioguswa na kuweka video na mahojiano hayo ni Madee, Roma Mkatoliki, Nikki wa Pili, Zamaradi Mketema, Fid Q na wengine wengi.

Katika akaunti zao wameweka;“Mbaki Mutahaba, ambaye ni mdogo wa #RugeMutahaba ameeleza kwamba ni wazi kwamba gharama za matibabu ya Ruge ni kubwa mno. Amesema Rais Dkt Magufuli na wengine walichangia lakini gharama hizo ni kubwa kuliko kawaida.

Gharama za matibabu kwa kule ni kubwa na kwa siku inaweza kufika million 5 mpaka 6, kuna number ambayo imeandikishwa kwa jina la mdogo wetu, Kemilembe Mutahaba 0752 222 210 hiyo ndiyo namba ambayo watu wanaweza kutuma sms za pole, faraja na hata wengine ambao wangetamani kutuma chochote”.

 

“Mume Wangu Angenishangaa Kama Nisingemsaidia Ruge”- Zamaradi

Mtangazaji na mdau mkubwa wa Bongo movie Zamaradi Mketema amefunguka na kuweka wazi sababu ya kuwa mstari wa mbele kuhamasisha michango kwa ajili ya matibabu ya baba Watoto Wake Ruge Mutahaba.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Zamaradi alisema kuwa angeonekana mtu wa ajabu na watu wangejiuliza endapo na yeye angekuwa nyuma kutohamasisha watu kuchangia matibabu ya Ruge ambaye pia ni baba wa watoto wake wawili.

Unajua watu wangekuwa kwenye mshangao endapo nisingefanya kitendo cha uungwana cha kuamua na mimi kuchangisha. Hata mume wangu angenishangaa, lakini pia ugonjwa siyo kitu cha kufanya mashindano hata kidogo maana yeyote anaweza kuumwa“.

Watoto wangu wanampenda baba yao na wanampenda baba anayewalea hivi sasa, lakini mimi kutoonesha kuguswa katika hili, hata watoto wangu wangenishangaa sana. Unajua suala la mgonjwa linamgusa kila mtu”.

Ruge alianza kuchangiwa fedha za matibabu mwanzoni mwa wiki hii baada ya familia yake kuomba kusaidiwa katika kipindi hiki ambacho jamaa huyo anaendelea na matibabu ya matatizo ya figo nchini Afrika Kusini.

Steve Nyerere Awataka Watu Waache Kuibua Mabaya Ya Ruge na Kumsaidia

Msanii wa Bongo movie na mdau wa mambo ya siasa Steve Nyerere ameibuka na jipya Safari hii aewataka watu wenye ubaya na Mkurugenzi wa CMG Ruge Mutahaba kuweka pembeni na kumsaidia katika kipindi hiki cha shida.

Kupitia ukurasa wa instagram wa Steve Nyerereamesema kuwa  Ruge aliweza kupaza sauti za wasanii bila kujali ana kipaji cha kuimba, utangazaji, riadha, taarabu, bendi na inabidi watu wakumbuke kuwa Ruge alisimama kutetea na kutoa nafasi kwa kila msanii.

Maisha yanavozidi kwenda kwa kasi ndipo unapogundua una rafiki SHETANI, maana wengi uvumilivu na neno msamaha kwao gumu, Mama aliniambia ukijua kusamehe BASI wewe ni MTU unayeweza kuishi popote, Ivi Nani kama RUGE, Upande wa Michezo hakuna narudia hakuna, Ruge alifungua milango kwa vijana, Aliweza kuwambia vijana mimi sina hela ya kukupa lakini kipaji chako ni hela zaidi ya kwangu mnayotaka kukupa, Ruge aliweza kumwambia kila msanii kauli mbiu jitambue wewe nani”

“Ruge aliweza kupaza sauti ya wasanii bila kujali una kipaji cha kuimba, Ama ngumi, Kwaya, Utangazaji, Riadha, Taarabu,Bendi nk, Ruge alisimama kutetea na kutoa nafasi kwa kila msanii mwenye kuonyesha nia, kwenye kazi yake, Sisemi Ruge kuwa hana mabaya hapana, bali nawaza mazuri yake maana naona yana Faida sana kwa binadamu mwenye kujua kusema neno asante, RUGE Ruge”

“Watanzania wapo milioni 57 ,Vijana peke yao wapo milioni 33 ,Kama aliweza kufungua njia hata ya Vijana milioni 10 tu huyu ni MTU wakumwambia Asante, Ruge, Maana hasinge weza watoa WOTE, Ntashangaa kuona hata watu waliokuwa na majina makubwa leo wakisema RUGE BORA AFE ,kwa kipi Tunasahau alitupa ndoano tukavue samaki na tukavua samaki”

“Badala ya kwenda kuuza samaki wale tulio vua, Tukala wenyewe sasa tunalaumu nini, mbona wakati tumeshiba samaki hakukuwa na tatizo, RUGE nawaza cha kukufanyia najiona nisipo jitoa kwako basi Sijatenda haki, Hakuna mkamilifu DUNIA HIIII, Tusameane kutokana na matatizo yetu, SASA ivi mimi nilizani tunaomba DUA au kuandaa kisomo kwa RUGE AMA MISA KWA RUGE, mimi nilidhani tunasimama kila mmoja KWA uwezo wetu kuangalia jinsi ya kumsaidia Ruge”

“Mimi nilidhani Tunafanya Tamasha ama kufanya kitu kikubwa kwa ajili ya RUGE, Sio muda wa kufukua makaburi huu ni muda wa kusema KAKA amka RUGE, kwa pamoja tunaweza sana Upendo ukiwa mkubwa hata mafanikio ya sanaa yataonekana, RUGE anamema sana kwako wewe msanii kuliko mabaya unayo nena leo”.

Majizo Aunda Kamati Ya Kusaidia Matibabu Ya Ruge

Mkurugenzi wa EFM na E-TV, Majizo ameunda kamati ambayo itaratibu namna ya kukusanya fedha za kusaidia mtibabu ya mkurugenzi wa vipindi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba ambaye yupo nchini Afrika Kusini kwa matibabu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Cloud360 cha Clouds Tv, Majizzo amesema kuwa kamati ya kuchangisha wa pesa za matibabu imeshaundwa na imeanza kukutana siku ya jana.

Lengo letu ni moja tu kuhakikisha Ruge anarudi mtaani kwani gemu bila yeye linakuwa halina ushindani, Watanzania tunapokuja kwenu tunaomba mtupokee kwani Ruge ni wetu sote sio wa Clouds tu”.

Lakini pia Majjizo amekanusha tetesi za yeye na Ruge kuwa na bifu na kusema kuwa ni mtu ambaye amekuwa kama kaka, rafiki na mshauri kwake kwani ana mchango mkubwa kwake katika kufungua vituo vyake vya habari.

Gharama za Matibabu ya Ruge ni Kubwa :-Familia

Familia ya aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi Clouds Media RUGE MUTAHABA, amefunguka na kusema kuwa matibabu ya mgonjwa huyo ambae yuko Afrika ya kusini imekuwa kubwa sana wa siku inaweza kufika kaisi cha shilingi milion 5 hadi 6 kiasi kwamba inakuwa ngumu kama familia kuweza kumudu swala hili peke yao

Kaka wa Ruge anasema kuwa wanashukuru kwa sababu watu mbalimbali wamekuwa wakijitahidi kwa ajili ya kumsaidia hasa kipindi wanaanza matibabu , lakini kuna nguvu ya ziada katika pesa inahitajika kwa ajili ya kupata pesa ya matibabu kwa ajili ya mgonjwa.

Gharama za matibabu kwa kule ni kubwa inaweza kufika mpaa milion 5 , au 6 kwa siku, pamoja na wamba hata Mh rais Magufuli aliwahi kutoa pesa kwa ajili ya matibabu lakini  gharama zimekuwa kubwa sana

“Nibusu Shavuni, Vyovyote Vile, Nakupenda”- Ujumbe Wa Ray C Kwa Ruge

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Rehema Chalamila maarufu kama  Ray C amemtumia ujumbe mzito Mkurugenzi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba.

Ray C ameandika maneno yaliyowashangaza wengi huku yakiwaacha wengine vinywa wazi kwa ujumbe aliomwandikia Ruge  ambaye kwa wakati huu yupo nje ya nchi kwa matibabu.

Kupitia akaunti ya Ray C ya instagram ameandika:

Amka bwana, nashachoka kusubiri, msg zangu hujibu, simu hupokei, na stori kibao nataka kukwambia ingawa najua utanchamba lakini nishazoea kukwambia kila kitu changu kinachoendelea kwenye maisha yangu, tunagombanaga mpaka tunablokiana lakini tukionana tu tukaangaliana tunabaki kucheka tu.

Nishazoea kukwambia mambo yangu sababu we ndo msiri wangu, we ndo unanipaga makavu nikiharibu, Kuna muda mpaka nalia na ukiona nalia ndo unazidi kunipa makavu bila huruma.

Naondoka kwa hasira ingawa moyoni najua uliyoniambia ni kweli…. nakununiaaaaa ila haifiki wiki huyo nishakuja ofisini, Muda mwingine sina hata cha maana cha kukwambia ila nakuja tu ofisini kukuona unitanie nicheke!

Ray C umenimiss eeh…. Kama nywele hujazielewa unanipa live Ray nenda Katoe hizo nywele, Nikikuona tu napata amani ya moyo. Nikitoka tu studio wa kwanza kukutumia demo! ni wewe, wewe tu miaka yote tangu nimeanza muziki sababu naheshimu sikio lako na naliamini.

Mwezi wa ngapi sasa huu Ruge!Natuma msg, nakupigia, natamani kukuimbia japo kidogo upate nguvu sikupati..Ruge najua huko ulipo Unaumia sana,najua unataka kuamka na kufanya kazi zako. PLS WAKE UP babaa. Please!You are too strong babaa, Don’t give up Please..4 U

Nishike mkono, Nibusu shavuni, Vyovyote vile, Nakupenda. (Your favorite song )
#AmkaRuge”.

 

Ray C Amtumia Ujumbe Mzito Ruge Mutahaba

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva nchini Rehema Chalamila ‘Ray C’ ameibuka na kumtakia ujumbe mzito Mkurugenzi wa Clouds Media group na mdau mkubwa wa muziki wa Bongo fleva Ruge Mutahaba.

Miezi michache iliyopita Ruge alianza kuugua ingawa familia yake haijawahi kuweka wazi anaumwa nini lakini kumekuwa na tetesi kuwa ana ugonjwa wa figo.

Ray C ambaye aliwahi kuongozwa kimuziki na Ruge amemtumi ujumbe mzito wa kumlilia na kumtaka apone haraka ili aweze kurudi katika nafasi yake ya zamani.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ray c amemuandikia ujumbe huu Ruge:

https://www.instagram.com/p/BrodWomAsXt/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1jaz59t6pxypc

Barakah The Prince Afunguka Mazito Kuhusu Ruge

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Barakah The Prince amefunguka mambo mazito sana kuhusu Mkurugenzi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba Baada ya kuugua.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Barakah The Prince amefunguka mazito juu ya mchango wa Ruge kwake na katika muziki Wake na kumtakia kheri:

https://www.instagram.com/p/Bqow-5Nh8fC/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=11rvm40wvfi6z

Alichoandika Gerson msigwa kuhusu Ruge

Mkurugebzi wa mawasiliano ya Ikulu bwana Gerson Msigwa amekuwa moja ya viongozi wa serikali walioguswa sana na ugonjwa unaomkabili sasa hivi boai na mkurugenzi wa uzalishaji wa vipindi bwana Ruge mutahaba ambae amekuwa mgonjwa sasa kwa muda mrefu.

Ruge ambae anasemwa kuwepo Afrika ya Kusini kwa matibabu na mapumziko ya muda mrefu amekuwa akitolewa dua na maombi ya watu wengi tangu kutangazwa kuumwa kwake huku kila mtu akimlilia kutoka na kuwa amegusa maisha na mafanikio ya watu wnegi sana.

Gerson anasema kuwa kama ambavyo Ruge amekuwa mstari wa mbele kupIgania maisha ya wengine basi sasa anamuombea kwa Mungu li aweze kupigania maisha yake kwa sasa, huku akisistiza kuwa ni jukumu la kila mtanzania kumuombea.

Mbasha Atangaza Kutenga Siku Maalumu Ya Kumuombea Ruge

Mwanamuziki wa nyimbo za injili nchini Emmanuel Mbasha amefunguka na kuweka wazi mipango yake ya kutenga siku maalumu ambayo ataitumia kwa ajili ya kumuombea Mkurugenzi wa Clouds Media Ruge Mutahaba.

Mbasha ametenga siku ya Ijumaa ya wiki hii Novemba 30 kufanya mkesha wa kufunga na kufungua  mwezi Desemba.

Lakini pia Mbasha amewataka Wasanii wenzake, waache mambo ya utimu na waungane katika maombi ili afya ya Ruge iweze kuimarika na arudi kwenye majukumu yake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mbasha ameandika ujumbe huu mrefu:

Ijumaa hii nitakuwa kwenye mkesha wa kufunga na kufungua mwezi, na katika mkesha huu nitakuwa na maombi maalum ya kumuombea Ruge Mutahaba ambaye yuko nchini Afrika kusini kwa matibabu. Huyu ndugu binafsi tunafahamiana vizuri sana, maana alikuwa mtu wa karibu sana kwangu. Najua wengi hawajui kuwa Ruge ndiye aliyekuwa meneja wetu aliyeisimamia albam yetu ya kwanza na ya pili wakati tunaimba na mke wangu, na hata baadhi ya nyimbo zetu ni yeye alisimamia kwa umakini mkubwa nikishirikiana nae kwa ukaribu sana, na kuzisimamia hadi zikavuma kila kona na kujulikana. Na kupitia usimamizi huu wa Ruge tulisaini mikataba mingi sana iliyokuwa ya faida. Hata katika ndoa yangu Ruge alipenda kunitia moyo na kuniambia kuwa “anafurahi kuona jinsi ninavyompenda mke wangu na kumsimamia vizuri, jambo ambalo ni gumu sana kufanywa na wanaume wengi wa kiafrika. Kwa kweli katika mambo yanayohusu tasnia ya muziki Tanzania kwa ujumla Ruge ana mchango mkubwa sana kwenye hii sanaa. Sio tu kwenye bongo fleva bali hata nyimbo za injili maana hadi leo hii ukitazama wanamuziki wengi wa nyimbo za injili ambao umaarufu wao umevuka ile mipaka ya kujulikana ndani ya kanisa tu, asilimia kubwa utakuta nyuma yao kuna support ya Ruge Mutahaba. Hivyo naamini hata katika ufalme wa Mungu huyu ni mtu wa faida sana. Na umuhimu wa wake umezidi kuonekana katika tukio la juzi la Fiesta, maana naamini kabisa endapo angekuwepo kila kitu kingeenda sawa. Nikiwa kama baba wa kiroho na mlezi mkuu wa waimbaji wote wa nyimbo za injili Tanzania, napenda kutoa rai kwa wasanii wote Tanzania, huu ni wakati muafaka wa kila mmoja kuweka pembeni tofauti zake za u team na tuungane kwa pamoja kumuombea dua njema ndugu yetu Ruge Mutahaba, na huu ndiyo moyo wa binadamu muungwana anaejua utu ni nini.
Ila kwa yule atakaefurahia matatizo yake hakika atakuwa mchawi hata kama hajawahi kupaa na ungo. Maana ugonjwa ni hali inayompata mtu yeyote, leo kwake kesho kwako.
Asanteni….Get well soon brother ruge”.