Nikki Wa Pili Aandika Barua Ya Kumlilia Ruge

Msanii wa muziki wa Hip hop nchini Nickson Simon maarufu kama ‘Nikki wa pili’ amefunguka na kuweka wazi barua aliyomuandikia Mkurugenzi wa Clouds Media Ruge Mutahaba.

Siku chache zilizopita familia ya Clouds Media iliweka wazi kuwa Ruge yupo hoi hospitalini kutokana na maradhi ambayo yamekuwa yakimuandama kwa kipindi kirefu sasa.

Msanii Nikki wa Pili amefunguka mengi kuhusu Ruge na hata kutaja mambo mengine mengi ambayo amemfanyia ambayo mpaka leo yameweza kumpa mafanikio makubwa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nikki wa Pili aliandika maneno haya:

Muda wa kipindi kirefu sana katika maisha yangu ya shule nilikuwa naamini mim ni mtu wa kukaa nyuma, nisiye na uwezo wa kuzungumza mbele za watu, sikuwa nanyoosha mkono darasani hata kama najua jibu, nilio soma nao chuo wanajua nilivyo kuwa natoroka presentations.

Muda wa kipindi kirefu sana katika maisha yangu ya shule nilikuwa naamini mim ni mtu wa kukaa nyuma, nisiye na uwezo wa kuzungumza mbele za watu, sikuwa nanyoosha mkono darasani hata kama najua jibu, nilio soma nao chuo wanajua nilivyo kuwa natoroka presentations.

Akaniambia wewe ni public speaker mzuri, akaanza kunipa nafasi ya kuzungumza mbele za watu nilikuwa naona na kosea lakini kila niliposhuka alikuwa anaiambia umefanya vizuri sana ongeza hichi na hichi.

Leo nimekuwa naalikwa vyuoni, kwenye makongamano, semina,taasisi, kampeni mpaka makanisani, kama mzungumzaji au mtoa mada, na hata mitandaoni huwa naandika mawazo yangu bila woga, ingekuwaje nisingekutana na Ruge Mutahaba.

Mungu akupe wepesi urudi katika uzima wako, RG (genius)”.

Inaripotiwa Ruge yupo nchini Afrika Kusini akipatiwa matibabu kutokana na matatizo ya figo ambayo yanamsumbua kwa miezi kadhaa sasa.

 

RC Makonda Atangaza Kumaliza Bifu na Ruge na Uwepo Wake Fiesta

Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda ametangaza rasmi kumaliza Bifu lake na Mkurugenzi wa Clouds Fm Ruge Mutahaba na kutangaza kushiriki katika tamasha la Fiesta.

Siku ya jana kuna taarifa zilitoka kwamba Ruge Mutahaba anaumwa hoi na hivi sasa yupo nchini South Africa  kwa ajili ya matibabu.

Baada ya kuwepo Bifu la siku nyingi kati ya Makonda na Ruge hatimaye RC Makonda ameonekana kuweka tofauti zao pembeni na kuungana na Clouds Fm ili kukamilisha Fiesta.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Clouds Tv, RC Makonda ameelezea mahusiano yake kwa sasa na Boss wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba ambapo amesema wamekuwa karibu kama mtu na kaka yake.

Ruge ni kaka yangu, na nikwambie hivyo nilivyompata Keagan (mtoto wa RC makonda) ametunga wimbo maalumu kwa ajili ya Keagan. Unafahamu kama alivyokuwa India (Kwenye matibabu)  Mimi nilikuwa na wasiliana nae?. Unafahamu kuwa alishawahi kuja nyumbani kumuona mtoto?. Unafahamu kuwa alishawahi kuja nyumbani kwa ajili ya maombi? Ruge ana watoto… Fiesta nitakuwepo na itakuwa kubwa kuliko”.

Lakini pia Mhe. Paul Makonda amethibitisha kuwa hata yeye atahudhuria kwenye fainali ya Tamasha la Tigo Fiesta, itakayofanyika katika viwanja vya Leaders Jumamosi hii.

Clouds tv Yathibitisha Ruge Mutahaba Kuwa Mgonjwa, Anahitaji Mapumziko

Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu bila kutaka kuweka wazi swala hilo la bosi na mkurugenzi na kipenzi cha wasanii na wadau wengi wa sanaa nchini Ruge Mutahaba, hatimaye uongozi wa Clouds media umewka wazi kuwa bosi wao huyo ni kweli alikuwa mgonjwa kwa muda sasa lakini amekuwa akindelea vizuri na afya yake.

Ruge ambae amekuwa mchango na msimamzi na kuibua ndoto za vijana wengi sana nchini , alianza kuugu mwaka huu mwezi june hivyo kutakiwa na madaktari kwa maelezo ya matibabu kuwa hakupswa kufanya kazi muda mrefu zaidi ya kupumzika.

Akitoa taarifa hiyo,  bwana Joseph Kusaga anasema kuwa Ruge ambae badi abaendela na matibabu lakini pia anahitaji muda mwingi wa mapumzika akiwa nchini afrika ya kusini kwa sasa anaendela vizuri na anahitaji maombi ya wadau kufanikisha matibabu yake salama.

Kwa muda mashabii na watu mbalimbali walitaka kujua hali ya mpendwa wao na hata kama kuna kitu wanaweza kufanya kwa ajili ya mpendwa wao waweze kufanya kwa ajli ya afya yake.

 

Mange Ameanika Ukweli Wote Kuhusu Bifu la Diamond, Ruge na Kusaga

Mwanaharakati wa siasa mtandaoni mwanadada Mange Kimambi ameibuka na bomu jipya was huku safari hii akifunguka kuhusiana na mambo ambayo yanaendelea kati ya supastaa wa bongo fleva Diamond Platnumz na Wakurugenzi wa Clouds Fm Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba.

Wiki iliyopita Diamond na Clouds Fm waliingia katika vita kali ya maneno ambapo meneja wa Diamond, Salaam SK alimtolea maneno mazito Ruge kwa kudai ana njama za kutaka kumuangusha Diamond na kumshusha kimuziki.

Leo Mange amefunguka na kudai kuwa ukweli kuhusu bifu hili unaanzia kuwa msanii Diamond yuko chini ya Ruge akimaanisha kwamba meneja halisi wa Diamond ni Ruge na Babu Tale na Salaam SK ni watu waliowekwa ili kuzuga watu wasijue kuwa Diamond yuko chini ya Clouds Fm.

Lakini pia Mange amefunguka na kudai kuwa sasahivi Clouds kuna matatizo makubwa kwani Joseph Kusaga anataka kuiuza Clouds kwa kuwa anafungua redio yake nyingine:

Joseph Kusaga anataka kuwekeza pesa yake sehemu nyingine na hiyo sehemu ni kwa Diamond kwa sababu basilica Clouds kuna matatizo makubwa, na Ruge amekuwa dizaini anamsumbua Kusaga kuhusu umiliki ukweli ni kwamba hakuna Clouds Fm bila Ruge”.

Lakini pia Mange amefunguka kuhusu umiliki wa mali za Diamond ambazo amedai zinamilikiwa na Joseph Kusaga:

Jamani ni hivi hiyo Wasafi Radio na Wasafi Tv, Joseph Kusaga ndio mmiliki wa asilimia 80% na Diamond anamiliki 20%  All the investment ya Wasafi Radio na Wasafi Tv amefanya Joseph Kusaga na pia hiyo Wasafi online 95% inamilikiwa na Kusaga lakini pia Chibu perfume 100% inamilikiwa na Joseph Kusaga na Diamond Karanga 100% inamilikiwa na Johanna Kusaga mke wa Joseph Kusaga”.

Mange amesisitiza kuwa hili bifu linaloendelea hivi sasa kati ya Diamond na Ruge ni kwasababu wanajua kuwa boss mkuu Kusaga yupo upande wa Wasafi na hivyo wakiwchana na Ruge Babu Tale na Salaam watakuwa mameneja wa Diamond full time.

Meneja Wa Diamond Ahaidi ‘Kumuanika’ Ruge Endapo Atamuandama Tena Diamond

Sakata linaendelea kupamba mtoto kati ya meneja wa Diamond Platnumz Salaam SK na timu nzima ya WCB dhidi ya Ruge ambaye ni Mkurugenzi wa vipindi Clouds Media.

Kizazaa hiki kilianza wiki iliyopita kutoka kwa vijana watangazaji wa kipindi cha Shilawadu Qwisa na Soudy Brown ambao walidai kuwa wamepewa kichapo cha hali ya juu na mcheza shoo wa WCB Mose Iyobo.

Ambapo inasemekana kuwa walimfata Aunty Ezekiel ofisini kwa kwake kwenda kumfanyia mahojiano kuhusiana na suala la ugomvi wao na Tunda lakini kwa bahati mbaya hawakumkuta lakini badala yake walimkuta Mose Iyobo ambapo walidai baada ya kumuuliza maswali mawili matatu aliwageuzia kichapo na kuuanza kuwapiga na kutaka kuwagonga na gari hali iliyowasababishia majeraha.

Tangu siku hiyo kumekuwa na maneno mengi yanayoongelewa mtandaoni lakini hali ilikuwa inaonekana kama si shwari kati ya WCB na Clouds ambapo jana walitoleana povu zito ambapo Meneja wa Diamond anayejulikana kama Salaam Sk amedai kuwa kuna njama zinapangwa ili kumshusha Diamond kimuziki.

Diamond Platnumz na Uongozi Wake

Sallam Sk alifunguka na kudai kuwa Shilawadu hawakupigwa na Mose Iyobo kama walivyodai bali walimtumia Mose ili kumharibia Diamond kwenye jamii na timu nzima ya WCB hivyo akadai kuwa atamuanika Ruge na maovu yake yote ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika:

Kwa heshima ya bwana Joe Kusaga kukuombea msamaha leo Bwana Ruge Mutahaba naamua kukusitiri ila ukiendelea kuyafanya ambayo unayafanya basi ntayaanika maovu yako yote unayofanya kwenye Industry ya muziki. WCB haina tatizo na media yoyote na wala haina tatizo na Clouds media group ila huyu Ruge ndio mwenye matatizo #tumekataakuwakaa”.

Mpaka sasa sio Ruge wala Clouds waliotoa tamko lao rasmi kuhusu sakata hilo lakini kuna habari za chini chini zinazodai kuwa hii yote ni kiki tu iliyopangwa.

Nandy Amwaga Povu Baada ya Habari Kusambaa Kuwa Ameonekana Serengeti na Boss Ruge

Mwanamuziki wa Bongo fleva Nandy anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘kivuruge’ amejikuta katika wakati mgumu baada ya habari kusambaa mtandaoni kuwa ameonekana mbuga za wanyama Serengeti na Ruge.

Siku ya Jana habari zilianza kuenea mtandaoni msanii huyo ameonekana akiwa zero distance na mkurugenzi huyo wa Clouds Fm Ruge Mutahaba ambaye pia ni boss wake pale THT. Baadhi ya watu wanaofanya kazi huko Serengeti walituma ujumbe huu kuthibitisha kumuona Nandy na Boss Ruge:

Mwanamuziki Nandy ni kweli kabisa yupo Serengeti na Ruge nashangaa anavyobisha tena wapo Serengeti Serena waliingua Jumanne. Wapo room namba nane na akibisha tuseme hadi nguo alizovaa na alivyosuka mnafiki Mkubwa tena waliingia hapa mida ya saa nne”.

Baada ya habari hizo kuenea Kama moto wa kifuu Nandy kupitua ukurasa wake wa Instagram alikataa tuhuma hizo na kutoa povu Kali:

Mtu akifanya mziki wake kwa amani bila drama kuna watu wanakuwa hawatosheki kabisa….Hivi mimi ni kichaa mpaka kujiachia kama huyo msambaza habari anavyodai! Kwani suza kitoto. Msu force mambola la watu kusema natoka na boss wangu nalijua leo au ni geni mpaka nijiachie kwenda naye macamp au maclub na kupanda ndege kiufree kama mnavyodai?? Embu tuwe na pliiz kwaiyo mimi nimekuw wa kuja kiasi hicho na mshamba kiasi ya kwamba nikashindwa kufunga hata ushungi basi hata tungepishana kusafiri yeye akatangulia mimi nikafuata nyuma au mnadhani mimi mtoto sana tafadhali tupeane heshima kuna watu hatutaki drama za kitoto na msi force mambo”.