Master J Apasua Kuwa Shaa Ameacha Mziki na Kugeukia Kilimo

Mtayarishaji wa Muziki maarufu na Mkongwe Katika tasnia ya Bongo fleva Master J ameweka wazi kuwa msanii wa Bongo fleva Sarah Kaisi maarufu kama Shaa ameachana na Mziki na kugeukia kilimo.

Master J ambaye amekuwa Kwenye Mahusiano ya kimapenzi na Shaa kwa miaka mingi amesema ukimya wa Shaa Kwenye muziki ni kutokana na maamuziki ya kuweka sanaa pembeni.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Master J amedai Shaa ameamua kuacha muziki na kufanya kilimo kinachomuingizia kipato kikubwa zaidi na sasa yupo mkoani Mbeya.

Shaa ni mfanyabiashara sasa hivi yupo busy na kulima kule Mbeya naona inalipa zaidi nimejaribu kumshawishi arudi Kwenye muziki lakini ananiambia subiri apige kazi apate pesa ndio atarudi tena kwenye  muziki”.

Lakini pia Master J ameweka wazi kuwa yeye na Shaa bado wapo wote Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi.

Shaa Ampa Shavu Adam Juma, Asema Hakuna Producer Kama Yeye.

Msanii mkongwe wa bongo movies nchini Shaa ambae ni msanii wa siku nyingi  amefunguka katika page zake za mitandao ya kijamii na kumsifia director wa siku nyingi wa nyimbo za bongo Adam Juma na kusema kuwa pamoja na uwepo wa ma-producer wengi nchini lakini kwake yeye Adam Juma ndio mtayarishaji bora kwa miaka yote.

                                                           

 Mtayarishaji maarufu wa nyimbo nchini ,Adam juma

Shaa amesema kuwa hata watu waseme kuwa amelogwa kwake iwe sawa tu lakini  anaamini kuwa hasingetokea kumjua hata Director maarufu wa sasa Justin Campos kama asingefanikishiwa yote hayo na Adam Juma.

call me pld school but adam juma will always be my go to video director and producer …nisingemjua justin campos if it werent for adam…love you bro!-Aliandika  sha katika ukurasa wake wa Twitter .

Na baadae alikuja kuongezea katika ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika tena”this is wher people will say umeniloga ..weeniloge tu #adamjuma want you to know that i appreciate mchango wako katika industry hii..and thank you for every seconf that you commit /commiteds to this industry.

Ni wasanii wachache sana wamekuwa wakishukuru na kuona mchango wa watu waliowatoa mbali kama shaa ambae amekuwa katika game kwa muda mrefu na bado akaona kabisa kuwa adam ni moja ya watu wasioweza kusahaulika katika kazi yake ya muziki.