“Siwezi Kuachika Kirahisi “- Shamsa Ford

Muigizaji wa Bongo movie Shamsa Ford ameibuka na kudai kuwa hawezi kiachika na Mume Wake Chiddi Mapenzi kirahisi kama watu wengi wanavyofikiri.

Shamsa amefunguka na kusema kuwa anawashangaa wanaomtolea maneno ya kwamba ameachika kila anapoposti chochote kwenye mitandao ya kijamii.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Dimba, Shamsa alisema kuwa wanaosubiri ndoa yake ivunjike watasubiri sana, kwani yeye ni mwanamke anayejiamini na kutambua thamani ya mume wake.

Kila nikiposti kitu watu wanahusisha na mimi kuwa kwenye mgogoro na mume wangu Chid Mapenzi, nipende kuwaambia tu hakuna kitu kama hicho, bado tunapendana sana na tuna mikakati mingi ya kuhakikisha hakuna linalotuyumbisha”.

Shamsa amesema hayo kutokana na tetesi zilizosambaa kwenye Mitandao ya kijamii kuwa ameachana na mume Wake Chiddi Mapenzi kutokana na kuposti maneno yenye utata kuashiria Ndoa Yake kuvunjika.

“Vijana Kuweni Makini na Mitandao Ya Kijamii”- Shamsa Ford

Muigizaji wa Bongo movie Shamsa Ford ameibuka na kuwapa ushauri vijana wanaotumia mitandao ya kijamii ambapo amesema wanatakiwa kuwa Makini.

Shamsa Ford amewataka vijana kuwa Makini na Mitandao ya kijamii kwani endapo wakitumia vizuri basi itawajenga Lakini pia wakiitumia vibaya basi itawabomoa.

Lakini pia Shamsa amewataka vijana wasiige sana maisha ya mastaa mitandaoni kwani wengi wao hawaishi maisha yao halisi bali wanafeki ili waonekane wako juu mbele ya jamii.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Shamsa Ford aliandika maneno haya:

https://www.instagram.com/p/BsVVBdplIr9/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1ml10y2bkype2

 

Shamsa Ford Adhamiria Kuachana na Nguo Za Nusu Uchi

Muigizaji wa Bongo movie mrembo Shamsa Ford amefunguka na kuweka wazi kuwa moja ya mipango yake ya mwaka mpya wa 2019 ni kustaafu kabisa kuvaa vimini.

Shamsa amesema kuwa ameamua kuacha nguo za nusu uchi na kuanza kuvaa kwa stara zaidi na amedhamiria kuwabadili wanawake wengine kwa kuhakikisha anauza nguo za stara tu dukani kwake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Shamsa alisema anamshukuru Mungu kuuona mwaka huu akiwa mzima na kwa kuwa mwaka mpya unakuwa na mambo mapya, yeye ameamua kubadilika katika suala la mavazi.

Sina sababu tena ya kuendelea kutojistiri kwa sababu Mungu ameniokoa na kunistiri kwa kunipa mume, mwaka huu ni wa kuonesha kuwa mimi ni mama mwenye stara, naamini kwa kuwa na duka la madira na mitandio nitaweza kuwa mwanamke mwenye stara na hii ndiyo njia pekee ya kunipa mwisho mwema hapa duniani“.

 

Shamsa Ford Awamwagia Povu Wanaume Wanaonyanyasa Wake Zao

Muigizaji wa filamu za Bongo movie nchini Shamsa Ford ameibuka na kuwatolea Povu zito wanaume ambao wamekuwa na tabia za kunyanyasa Wake zao kwa kuwapiga.

Shamsa ametoa maneno makali ya kukemea wanaume ambao wanawafanyia vituko Wake zao Kama kuwapiga na kuwadhalilisha lakini pembeni wana michepuko wanayoithamini.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, ameandika maneno haya:

Wanawake ambao tuna mapenzi ya dhati ndio huwa tunaonewa sana. Wanawake ambao huwa tunaishi maisha ya uhalisia kutokana na mifuko ya waume zetu ndio tunaonewa na kuonekana kama washamba, lakini wale wanawake wachunaji ndio huwa wanapewa kipaumbele na kuthaminiwa sielewi wanaume huwa wanataka nini kutoka kwa wanawake.

Tunapigwa, tunasemwa vibaya, tunaonewa, tunabeba mzigo mkubwa lakini mwisho wa siku bado unafuta machozi na kusema Alhamdulilah. Nyie wanaume huwa mnataka nini?”.

Shamsa hataweza wazi Kama ujumbe huo umeilenga ndoa yake pia na mfanyabiashara Chid Mapenzi ya la ila ameambatanisha na picha akiwa amejeruhiwa jicho.

Shamsa Amjibu Babu Tale Kuhusu Passpoti za Kusafiria.

Baada ya kutangazwa kwa ofa ya wanakamati kwenda afria ya kusini na baadae kuonekana kama safari imeyeyuka hivi, Babu tale alikuja na sababu ya kuwa safari hiyo kwa wanakamati haiwezi kufankiwa kwa sababu wanakamati wengi hawana passpoti za kusafiria.

Baada ya kuongea hivi na Shamsa Ford ambae pia alikuwa moja ya wanakamati amemjibu babu tale na kumwambia kuwa hakuna ukweli wowote kuhusu wasanii kutokuwa na passpoti za kusafiria lakini wanachojua wao ni kwamba waliongea hivyo kama kiki tu na wala sio kitu kingine.

haiwezekanai bhana , msanii gani ambae hana passpoti, mimi mwenyewe ukiniambia kuwa nitembee nayo kila sehemu natembea nayo, ile ilikuwa ni kiki tu.hiyo ni kama kawaida yao kwa wasafi kla wanapoenda ni lazima wafanye kiki ya kuacha alama ya kuzungumziwa.na mimi nawapenda sana wale vijana wanajituma , kila wanapoondoka lazima waache gumzo.Ilikuwa ni kiki tu watanzania inabidi wazoee.

Hata hivyo Shamsa anasisitiza kuwa hata kama ingetokea wakatakiwa kwenda wala hasingeweza kwenda kwa sababu yeye na familia zile ni tofauti kabisa na hakuna mazoea yoyote.

“Bongo Movie Kwenda Kwenye Birthday Ya Tiffah Ilikuwa ni Kiki Tu”- Shamsa Ford

Msanii wa Bongo movie Shamsa Ford amefunguka na kupasua kuwa habari ya wasanii wa Bongo movie  kama Wema, Aunty, Shamsa, Faiza, Maimatha na Wolper Kwenda Kwenye party ya Tiffah ilikuwa ni kiki tu.

SIku chache zilizopita Kwenye 40 ya mtoto wa Zamaradi, Babu Tale aliwaalika Bongo Movie kwa ajili ya kwenda South Africa Kwenye party ya Tiffah South Africa Lakini mara moja Zari aliwapiga stop.

Baada ya mgogoro wasanii hao kila mmoja ameonekana kughaili Kwenda huku wengine wakidai kulikuwa hakuna Safari bali ilikuwa ni kiki tu.

Gazeti la Amani, liliamua kuwasaka baadhi ya mastaa waliokuwemo kwenye kamati hiyo ambapo kila mmoja aliongea la kwake kama ifuatavyo;

Faiza Ally alisema kuwa alijua wazi kuwa hatakwenda kwa sababu Zari ‘alishamblock’ siku nyingi kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Mimi baada ya kutangaziwa vile tu nilijua siwezi kwenda kwa sababu Zari alishaniblock siku nyingi, sasa huwezi kwenda kwa mtu ambaye alishakublock na alivyosema maneno yale ndio kabisaaa”.

Maimatha wa jesse alidai kuwa hawezi kwenda kwa sababu hakuipenda tabia ya Zari kuwaambia kuwa watakwenda kumchafulia nyumba.

Sikuipenda kabisa tabia ya Zari, yeye angeacha akaona kama kweli tutaenda au la lakini kabla hata siku hajizafika akajibu palepale, ya nini kwenda? Nimemshangaa maana hajui kama kwake tungeenda ingekuwa na faida sana hata kujitangaza kibiashara“.

Shamsa Ford yeye alidai kuwa anachojua lile tangazo la wao kwenda Sauz kwenye sherehe ya Tiffah ilikuwa ni kiki tu wala hakukuwa na ukweli wowote.

Unadhani mchezo kuwasafirisha watu wote wale, ile ilikuwa ni sehemu ya kiki tu, wala siendi mimi”.

 

Siamini Kama Zari Alisema Tutachafua Nyumba:-Shamsa Ford

Mwanadada kutoka bongo movies Shamsa Ford amefunguka na kusema kuwa pamoja na kwamba walipewa ofa ya kwenda afrika ya kusini kwa ajili ya kufurahia pamoja na familia ya Diamond katika siku ya kuzaliwa na mtoto wap tiffah na safari hiyo haijafanikiwa lakini haamini kama zari alisema kuhusu swala la kuchafua nyumba yake.

Hata hivyo shmasa amasma kuwa hata kama kungetokea safari ikakamilika lakini ukweli uatabaki kuwa hasingeweza kwenda kwa sababu  hajuani na familia hiyo hata kidogo hivyo wala asingeenda kokote.

mimi huwa siamini maneno ya kwenye mitandao, kwaio hata siamini kama hayo amneno Zari aliyasema kwa sababu sijamsikia akisema, ila binafsi hata kama atakuwa alisema au hajayasema  mimi ningealikwa wala nisingeenda kwa sababu sina ukaribu woowte na wale wanafamilia wote, hivyo wala nisngeenda.

Shamsa Ford Ajivunia Mapenzi ya Mumewe.

Mwanadada Shamsa ford ambae mara nyingi amekuwa akionekana kuwa tofauti na mawazo ya wasanii wengine au mashabiki amefunguka na kuonyesha ni jinis gani amekuwa akiringa na kujivunia sana mapenzi ya mume wake kuliko kitu kingine chochote.

Shamsa ford ambae anasema kuwa hata kama anachokiongea kinaweza kusababisha watu kumchukia wakati yeye akiamini kuwa ni ukweli , kwake wala hajali kwa sababu anajua kuwa akisapotiwa na kupendwa na mume wake basi kwake yeye inatosha sana.

Shamsa akiongea na moja ya gazeti la kampuni ya GPL, baada ya kuulizwa swala la yeye kutokea tofauti na wengine katika 40 ya mtoto wa zamarad shamsa anasema

mimi mungu kanijalia maneno kwaio mara nyingi huwa sijali kabisa,na isitoshe mimi chidi akinipenda na kukubali maamuzi yangu tu kwangu inatosha kabisa wala siwezi kumridhisha kila mtu.

Shamsa Ford Adai Hajali Kuchukiwa na Watu Ilimradi Anapendwa na Mumewe

Msanii wa filamu za kibongo Shamsa Ford amefunguka na kusema hajali kama watu  watamchukia kwa muonekano wake au hata kusema ukweli inapobidi ilimradi anapendwa na mume wake Chidi Mapenzi inatosha.

Shamsa amekuwa Kwenye headlines za mitandao ya kijamii tangu avae gauni lililokuwa fupi sana Kwenye arobaini ya mtoto wa Zamaradi Mketema wiki iliyopita.

Kwenye mahojiano na gazeti  Amani baada ya watu wengi kumshambulia kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kutokelezea na nguo fupi kwenye 40 ya mtoto wa Zamaradi, na kusema kuwa ni ngumu kumridhisha kila mtu kwenye maamuzi yako.

Mimi Mungu kanijalia maneno sijali kabisa na isitoshe Chidi akinipenda na akakubaliana na maamuzi yangu kwangu inatosha kabisa siwezi kumridhisha kila mtu”.

 

Zamaradi Amtumia Ujumbe Mzito Shamsa Ford

Mtangazaji na mdau mkubwa wa Bongo movie Zamaradi amemtumia ujumbe mzito msanii wa Bongo movie Shamsa Ford katika siku yake ya kuzaliwa.

Siku ya jana ilikuwa siku ya kuzaliwa ya Shamsa Ford wasanii mbali mbali walimtumia salamu za pongezi na mmoja kati ya watu hao ni Zamaradi ambaye ni rafiki wa karibu wa Shamsa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zamaradi alifunguka na kuelezea mapenzi yake mazito kwa Shamsa na hata kudai wana uhusiano zaidi ya urafiki ambapo alimtaka asimuite rafiki bali ndugu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Zamaradi aliandika;

https://www.instagram.com/p/Bl47YgNgT_n/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=6j5t59lks2z3

Shamsa Afunguka Kuhusu Nguo Aliyovaa kwa Zamaradi.

Mwanadada Shamsa ford amejikuta alitoa povu zito baada ya siku ya 40 ya king salah ambae ni mtoto wa zamaradi kutokana na maneno ya wwatu katika mitandao hasa page za udaku kumsema kuwa hakuendana na dress code ya  sherehe hiyo kutokana na kuvaa nguo fupi.

Page hizo zilipokuwa zikimtukana sana shansa walikuwa wakimtuhumu kwa kumwambia kuwa nguo hiyo haikuwa ya heshima kwa sababu watu wote waliokuwepo katika kamati walivaa nguo ndefu sasa kwanini yeye hamtie aibu rafiki yake kwa kvaa kinguo kifupi kama alichokuwa amekivaa.

Mnachoshindwa kuelewa kuwa hii ilikuwa ni party ya kumpongeza zama kutoka nje na mtoto na ndio maana kila mmoa alivaa vile anavyotakazama liashafanya shereh nyingi sana na zingine za kidini na alikuwa akialkia watu wake wa karibu na ndio maana hata yeye hukumuona kafunika kichwa.ila asanateni sana jamani kwa kuniongelea mmenibusti kidogo maana ningevaa mnavyotaka msingeniongelea kabisaa.

Mitandao ya kijamii hivi karibuni imekuwa ikimuandana mwanadada shamsa ford  kutona na maisha anayoishi huku wengine wakisema amefulia na wengine wakisema ameachana na mume wake.

Shamsa Ford Awatupia Madongo ‘Wanaume wa Dar’

Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali maarufu Shamsa Ford ameibuka na kuwatupia madongo wanaume wa Dar.

Shamsa amewasema vijana ambao wamekalia kuwa vibenten ambao wanategemewa kulelewa na wanawake wenye pesa kutoka na kukosa elimu ya kuweza kuwakwamua.

Shamsa alitokwa na povu hilo Kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo alidai mbali na kuwa vibenten bali wengi wao ni wambea na chawa:

Wanawake wenzangu tujitahidi sana kuwapa elimu ya kutosha watoto wetu wote haswa watoto wa kiume. Nimejikuta kuwa na huruma zaidi na watoto wa kiume kwasababu wa kwangu ni wa kiume. Huwa naumia sana nikiona mtoto wa kiume anavyoangaika kupata riziki”.

Lakini pia shamsa ameendelea kusema kuwa wazazi lazima wahakikishe wanawapa elimu watoto wao na yeye kama mzazi atahakikisha anatimiza hilo:

Mtoto wa kiume asipokuwa na elimu ya kutosha au ujuzi wowote mwisho wao huwa ni mbaya kuliko watoto wa kike. Sasa hivi vijana wengi ambao hawana kazi au hawakubahatika kusoma ndo WAMBEA,WAPAMBE,VIBENTEN MARA CHAWAAA.

Kuwa mwanaume ni heshima kubwa sana kama ukisimama kwenye misingi ya kiume..Nitauza vitumbua, madira hata kufagia barabara ilimradi mwanangu apate elimu”.

Shamsa ni mama wa mtoto mmoja wa kiume anayeitwa Terry.

“Irene Hana Marafiki Wa Kweli, Shamsa Ford ni Mnafki” Mwijaku Amchana Uwoya

Muigizaji wa Bongo movie maarufu kama Mwijaku amemwagia povu zito msanii mwenzake Irene Uwoya baada ya picha yake kusambaa siku ya jana.

Siku ya jana Irene aliposti picha iliyozua utata Kwenye mitandao ya kijamii na mara moja Mwijaku alimwandikia posti nzito ambayo alimsema sana kwa vazi lile hasa kwa sababu ni mke wa mtu.

Lakini Mwijaku hakuishia hapo kwani Kwenye mahojiano aliyofanya na Millard Ayo Tv, Mwijaku alionekana akiweka wazi Kuwa marafiki zake na a Uwoya wanaomsapoti kwa picha zile ni wanafiki wakubwa kwani wanamshauri vibaya wakijua wazi kabisa picha ile siyo nzuri:

Irene ni mtu mzima na mke wa mtu na hii ni ndoa yake ya pili kwa nini aposti picha kama ile? Nikajiuliza Marehemu Ndikumana angekuwepo wakati amemuoa angeweza kuposti kitu kama kile? Asingeweza kuposti Ndikumana alikuwa mkali ila kwa sababu mume wake Dogo Janja ni mdogo basi anamuonea.

Halafu na marafiki wanaomzunguka Irene ni wanafiki siku akija kufa atakuwa peke yake halafu na Shamsa Ford anaenda kumwambia hivyo hivyo umependeza ishi utakavyo! Tuongee ukweli Shamsa Ford ni mnafki na anampoteza mwenzake”.

Dogo Janja aliweka wazi kuwa hakukerwa na picha ile zaidi alimpa sapoti mke wake.

Shamsa Ford Aibuka Kumtetea Uwoya Baada Ya Picha Yake Ya Utata Kusambaa

Muigizaji wa Bongo movie Shamsa Ford ameibuka na kumkingia kifua Msanii mwenzake Irene Uwoya baada ya picha yake ya utata kusambaa mtandaoni.

Siku ya jana Irene Uwoya alitengeneza headlines baada ya kuweka picha kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha maungo yake nje ndani ya nguo ya kuogelea.

Watu walimjia juu Uwoya baada ya picha ile kusambaa ingawa mwenyewe alijitetea kuwa alikuwa yuko Beach na lile ni vazi la kuogelea hivyo haoni tatizo.

Shamsa amemtetea Uwoya na kuweka wazi kuwa haoni kama kuna kosa yeye kuvaaa vile hasa ukiangalia alikua mazingira ya baharini hivyo kuvaa vazi la baharini.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Shamsa maandiko ujumbe huu:

Picture zako zote nzuri mama umependeza sana, mimi nachojua mtu unavaa kutokana na location unayoenda, sasa sidhani kama Ir

Kuna wengine wanavaa en anaweza akavaa hivi halafu akaenda ofisini. Sasa mtu yupo beach mlitaka avae dira.

Mumewe amemsifia amependeza sasa nyie wapembeni mnasema amekosea mnajisumbua, kila mtu atahukumiwa kwa matendo yake binafsi na Mungu. Tusiishi kwa kuhukumiana maana wa peponi hawajulikani.

hadi dira beach lakini matendo yake ukiyashuhudia unaweza ukatoa mbio. Tatizo lako wewe dada Iren ni hilo umbo ndo limewakosesha amani watu.Ungekuwa na flatscreen maneno yasingewatoka hebu kafanye operation upunguze Gushepu“.

 

Mastaa Waendelee Kujisitiri Kama Mwezi Mtukufu-Shamsa Ford

Muigizaji wa Bongo movie Shamsa Ford amewataka wasanii wenzake kuendelea na kufanya mema waliyokuwa wanafanya kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda Shamsa alisema ndani ya mwezi wa Ramadhani watu mbalimbali hasa mastaa walikuwa wakiuhesh­imu kwa kufanya yaliyo mema, kuvaa kiheshima na kutoachia video na picha za ajabu mitandaoni hivyo hata sasa waendelee hivyo hivyo ili kuendelea kumtukuza Mungu zaidi.

Nawasihi mastaa waendeleze mema waliyokuwa waki­yafanya wakati wa Ramadhani, tusione wakiwa wanakaa nusu utupu au kufan­ya mambo mengine ya ajabu, wafanye ibada sana maana maisha yenyewe ni mafupi mno”.

Mwezi Huu wote ulikuwa ni mwezi mtukufu ambapo waislamu walikuwa wanafunga na kuomba kwa Imani zao na kufanya mema na hata mavazi yao yalikuwa yakujisitiri sana tofauti na siku za nyuma.

 

Shamsa Ford- Mara Nyingi Sipendelei Kujichanganya na Watu

Muigizaji wa Bongo movie Shamsa Ford amefunguka na kudai mara nyingi hupendelea kukaa mwenyewe kuliko kukaa na kujichanganya na watu wengine.

Shamsa amedai kuwa sababu pekee inayomfanya yeye kukaa mwenyewe ni kuamini kuwa akijua mwenyewe a anaweza kuipa akili yake muda mrefu wa kufikiria na kutafakari mambo mengi.

Shamsa alifunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers ambapo amekiri kuwa kuna wakati anapenda kukaa peke yake kabisa tena kwa muda mrefu ili kuweza kupata muda mwingi wa kujikwagua na kujitafakari wapi yupo sahihi na wapi amekosea ili awe mpya Tena.

Dawa yangu kubwa mimi kuna wakati napenda kukaa pekee yanagu najikwagua vizuri sana kuliko mtu anikwague kwasababu najua wapi niliteleza wapi nilikuwa sahihi”.