Shamsa Ford afunguka kwa nini anatamani kuokoka lakini anashindwa

Muigizaji wa filamu za Bongo Shamsa Ford kwa Sasa anatamani sana kuzifuata nyayo za Mzee Yusuf kwa kuokoka na kuacha mambo ya dunia.

Mrembo huyu anadai kuwa siku za mwisho zimekaribia na ndio maana anaonelea kubadilisha mienendo Yale. Akizungumza na Risasi Jumamosi, Shamsa alisema kuwa,

Shamsa Ford

Nimejaribu kusali sala tano kila siku. Kuna wakati ninasahau lakini kuna siku ninasali zote, ninaamini taratibu nitakuwa kama Mzee Yusuf, ninamuomba sana Mungu.

Mume wa Shamsa Ford Kafunguka kwa mara ya kwanza baada ya kudaiwa kumpiga

Wiki kadhaa zilizopita, picha zilijitokeza kwenye mtandao za Shamsa Ford kama ameumia sana kwenye uso.

Sababu? Bado haijaweleka vizuri.

Mume wake Chidi Mapenzi ndio aliyekuwa mgeni maalum kwenye U Heard ya Soudy Brown na hivi ndivyo alivyosema.

”Siwezi kumpiga mke wangu. Wewe mwenyewe unanijua mimi siyo mgomvi. Nilitoka ofisini, nikamkuta mke wangu ameumia, nilipomuuliza nini tatizo, akanielezea. Nilipomuuliza unamjua mtu mwenyewe, akasema tumeyamaliza. Basi nikampeleka hospitali.” 

Shamsa Ford apasuliwa uso baada ya kupigwa ngumi

Shamsa Ford ‘Chausiku’, amepata jeraha usoni baada ya mwanaume ambaye hajulikani alimpiga ngumi huku akimuacha kama amepasuka na kuvuja damu. Kupitia Instagram Shamsa aliposti picha na kuonyesha mashabiki wake alivyofanywa na mtu huyo.

Jeraha lake limewaacha wengi wakisema kuwa litabaki maisha. Shamsa naye aliandika ujumbe kwa mashabiki zake kuwa alipigwa akiwa anaamua ugomvi. Inasemekana kuwa jamaa aliyempasua uso alikuwa akimtongoza mfanyikazi wa Shamsa kwa nguvu na ndipo muigizaji huyu aliingilia kumsaidia msichana wa wenyewe.

Shamsa Ford
Shamsa Ford

Hata hivyo inaonekana jamaa huyo alikuwa amejaa hasira baada msichana huyo kumkataa na baada ya Shamsa kuingilia, akamtolea hasira kwa kumpiga ngumi ya uso.

Ingawa Shamsa alikuwa akilalamika maumivu makali kichwani, hivi sasa anaendelea vizuri.