“Naanzaje Labda Kutembea na Shetta”- Lynn

Videi vixen ambaye Hivi karibuni aligeukia gani ya  Bongo fleva, Irene Godfrey maarufu kama Official Lynn amefunguka na kudai hawezi hata siku moja kutembea na msanii mwenzake Nurdin Bilal ‘Shetta.

Lynn amesemameweka hayo Baada ya tetesi zilizowahi kusambaaa kwenye Mitandao ya kijamii kuwa wawili hao ni wapenzi kutokana na ukaribu ambao wamekuwa nao sasa.

Katika mahojiano yake na Gazeti la  Risasi Jumamosi, Lyyn alisema kuwa ukaribu wake na Shetta unatokana na kazi wanayoifanya kwa pamoja lakini alishangazwa na maneno kwamba wanatoka kimapenzi kitu ambacho siyo kweli.

Hivi naanzaje kutoka na Shetta jamani kwa hiyo kila mtu nitakayekuwa naye karibu ni bwana wangu? Shetta ni mshikaji wangu, siwezi kutoka naye na huku Afrika Kusini tumekuja kikazi wala siyo kula bata kama watu wanavyosema ila kwa kuwa wanapenda kutunga uongo waendelee tu kuamini, sina muda wa kuwalazimisha waelewe, napiga kazi tu”.

 

Shetta awapongeza Navy kenzo.

Msanii wa Bongo Fleva, Sheta amelipongeza Kundi la  Navy Kenzo kwa kuefanikiwa kushinda tuzo ya Sound City MVP.

Tuzo hizo ambazo zilitolewa usiku wa kuamkia jana Lagos nchini Nigeria, Navy Kenzo wameshinda kwenye kipengele cha Kundi Bora.

“Hongera sana kwenu Navy Kenzo You guyz make Us proud, Lets support Our Own,” ameeleza Shetta.

Navy Kenzo ndiye wasanii pekee kutoka Tanzania walioshinda tuzo hiyo kwa mwaka huu licha ya wingine kuteuliwa kushiriki.

Penzi la Shetta na Mama Qyla bye-bye

Mwanamuziki shetta anaetamba kwa sasa na wmbo wake wa bye -bye pamoja na mama wa watoto wake mama qyla wamemwagana mchana kweupe huku kila mmoja akifanya utaratibu wake kwa sasa .Taarifa hizo zimethibitishwa na Shetta mwenyewe na kufungua A-Z    na kusema kuwa kwa sasa kila mmoja ameamua kuendelea na maisha yake .

Shetta anasema kuwa maisha ya sasa watu jawapaswi kuchanganywa na kitu kimoja hivyo kama unaona kuwa kitu kinakuchanganya ni bora kuachana nacho na kufanya kitu kingine cha maana ambacho unaona kuwa kinaweza kuwa cha maana zaidi, hivyo walipokaa na kuona kuwa hawawezi kuwa pamoja waliamua kila mtu kuchukua ustaarabu wake.

Kwa sasa hivi  niko peke yangu,  mama Qyla nilishaachana nae siku nying kwa sasa niko  peke yangu tu,  nashukuru kuwa mwanangu nimekuwa nikimuona kla wakati na hilo ndilo jambo la kumshukuru Mungu.

Siwezi Kuongea na Diamond Labda Biashara tu :-Shetta

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Shetta ambae ni  mkurugenzi wa Kings Empire lakini pia meneja ya The Mafik amefunguka na kusema kuwa kwa hali ilivyo sasa kati yake na Diamond hawawezi kuongea kitu chochote zaidi ya biashara tu .

Akitoa sababu kwanini hawakuweza kuendeleza ushikaji kati yake na diamond ilihali walikuwa marafiki wakubwa na hata familia zao zilikuwa karibu sana na kufanikiwa kufanya kazi pamoja shetta ansema kuwa kamwe hawawezi kuwa marafiki tena labda mahusiano ya kibiashara tu.

hakuna tatizo kati yetu ila sema tu ndo hivyo kwa sasa kila mtu yuko na mishe zake tu za kimasiha na hata kama tutaongea itakuwa ni mazungumzo ya kibiashara lakini sio ushikaji tena.

 

Mange Kimambi Ampokea Shetta Kwa Mikono Miwili

Mwanamama maarufu kwenye mitandao ya kijamii Mange Kimambi amefunguka na kusema yupo tayari kuolewa na staa wa Bongo fleva Shetta Baada ya kuweka wazi hisia zake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Shettta aliweka wazi kuwa anamkubali sana Mange Kimambi na hata kudai kuwa angependa kama angeweza kuwa Mpenzi Wake na hatimaye kufunga naye ndoa.

Mange amemjibu Shetta na kusema kuwa yupo tayari kufunga naye ndoa na kwa pamoja waweze kulea watoto wao.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mange amemuandikia Shetta Ujumbe huu:

https://www.instagram.com/p/BrQ5ZsigamT/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1xb5kl9rsf6ch

Shetta Atangaza Ndoa na Mange Kimambi

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Shetta ameibuka na kukiri mapenzi yake kwa Mange Kimambi na kudai yuko tayari hata kufunga naye ndoa kwani anampenda sana.

Shetta ameweka wazi mapenzi yake kwa Mange ambaye Hivi karibuni aliwahi kuposti katika ukurasa wake wa Instagram na kusema wazi kuwa anamkubali.

Kwenye mahojiano aliyofanya na mtandao wa Bongo 5, Shetta amefunguka haya kuhusu mahusiano yake na Mange Kimambi:

Mange ni my girlfriend wangu mpya na labda naona kama naweza kuona kwamba naweza kukaa pale maana ananikosha sana kwa picha zake anazoposti.

Halafu pia nina mpango wa kumuoa na kumuweka ndani yule Dada maana ni mzuri hasa maziwa yake yaani mi hoi”.

Shetta anafanya vizuri na ngoma yake ya ‘Hatufanani’ aliyowashirikisha wasanii Kama  Mr. Blue na Juma Jux.

Shetta Athibitisha Kuwa Utovu Wa Nidhamu Wamfukuzisha Ruby ‘King Empire’

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Shetta ambaye pia ni mmoja wa viongozi Katika kampuni na Recording Label ya Kings Empire ameweka wazi sababu za kusimamishwa Msanii Ruby.

Kings Empire inasimamia wasanii Kama vile The Mafik, Aslay na wengineo wameweka wazi mmoja wa aliyekuwa Msanii wao Ruby hayupo tena na Label hiyo kutokana na kukosa nidhamu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Clouds FM, Shetta ameweka wazi kuwa  Ruby alisimamishwa na label hiyo baada ya kuonyesha utovu wa nidhamu.

Siwezi kusema sababu bali sisi ni familia kuna vitu vinatokea hata wachawi hugombana usiku wakiwanga, Hivyo kulitokea mpishano wa kauli kati yake na Meneja Kapasta kwenye group hivyo nikamwambia Ruby muheshimu kiongozi mara akanivamia na mimi hivyo nikamwambia #hambuso aandike barua ya kumsimamisha kwa muda kwa utovu wa nidhamu na angerudi tungezungumza lakini naona akaamua kufanya kazi zake yeye kama yeye“.

Skendo ya kuwa na kiburi na jeuri imekuwa ikimuandama Ruby kwa muda sasa ambapo watu kadhaa aliofanya nao kazi wameshawahi kumtuhumu kwa kuwa na tabia hizo ingawa mwenyewe ameshawahi kukataa taarifa hizo.

Shett afaunguka Utajiri wa Gari lake Kufanana na Kiwanda

Msanii wa bongo fleva shetta amefunguka na kusema kuwa kwa kiwango cha pesa aliamua kukiweka katika ununuzi wa gari lake jipya kama angekuwa anataka kufungua kiwanda basi angeweza kufanya hivyo siku nyingi.

Maneno ya Shetta ayanakuja baada ya kufanya mjadaka katika EATV katka FNL kuhusu swala la Fid q kuingia na gari lake mpya katika vituo hivyo ili watu waweze kuona gari lakini ikiwa ni kama hatua ya kuwaamisha watu kuwa hata yeye amekuwa na mafanikio lakini hana majivumo.

Fid q alisema kwamba moja ya wasanii wa zamani sana lakini wamekuwa hawana mafanikio katika muziki wanaofanya, lakini kwa kuwjaibu wapinzani wake aliamua kufanya hivyo.

Hii gari kuingia ndani ni kwa ajili ya bwana fareed kulionyesha ua , mbona mimi nina gari ya milion 150 lakini sijaingia nalo ndani.mimi gri yangu bwana hata muulize fid q anajua , ningeamua kufanya biashara kwa sasa ningelkuwa nina miliki kiwanda cha pampers huko kinaitwa Kaila pampers.

Baadhi ya wasanii wamekuwa na mafanikio lakini hawataki kuwaonyesha mashabiki au watu kuwa wako hiyo , swala linakuja pale kunapotokea ushindani baina ya wasanii ndipo unaona kila mtu anaibuka na lake.

Shetta Akiri Wimbo Wake Kufanana na Aibu ya Nandy

Msanii wa kizazi kipya Shetta amefunguka na kukirikuwa ni kweli wimbo wake huo mpya ambao amemshirikisha Jux umekuwa  ukifafa sana na wimbo wa mwanadada Nandy wa aibu.Shetta anasema kuwa wimbo huo ni moja kati ya nyimbo kali sana alizozienda hivyo hakuona kama ni makosa ilhali aliomba ruhusa ya kutuia beat hilo.

Akiongea na kujibu swala hilo Sheta anasema , aliuenda sana wimbo huo na ndio alipouomba producer Maneck na pia mwenye wimbo ambae ni Nandy na walikubali na ndipo alipotumia beat hilo.

Shetta anasema kuwa watu wengine wamekuwa wakishambulia bila hata kujua chanzo chake wakati yeye kwa mapenzi na wimbo huo alitaka hata kuimba remix yake.

Shetta Afunguka Sababu ya Ruby Kutolewa Katika Uongozi Wao

Kuna habari nyingi sana zilisambaa katika mitandao ya kijamii kuwa mwanadada Ruby amefukuzwa katika uongozi wake mpya kwa sababu ya utovu wa nidhamu na wasanii wengi waliongelea swala hilo huku wakimtaka mwanadada huyo kutulia na kufanya kazi na watu.

katika baadhi ya sababu za kufukuzwa kwa Ruby katika uongozi wake mpya ilisemekana kuwa shetta alikuwa sababu. na kwa mujibu wa Ruby kwa maneno yake ya chini chini alikuwa akimlalamikia msanii mwenzake huy.

Sasa basi akiongea na Clouds Media , Shetta anaelezea hali ilivyokuwa mpaka kufanya ruby kufukuzwa katika uongoiz wao mpya , anasema “siwezi kusema kuwa mimi ndio sababu lakini sisi ni wanafamilia na tunakwaruzana maana hata wachawi pia wanagombana wanapokuwa wanawanga, kulitokea mpishan wa kauli kati yak na meneja, na nilimwambia kuwa yule ni kiongozi anahitaji heshima, lakini ruby alinvamia mimi, kwaio nikamwambia chambuso amuandikie barua ya kumsimamsiha kwa muda kwa utovu wa nidhamu.”

Hata hivyo Shetta anasema kuwa barua hiyo iliuwa ya muda na walitegema kuwa muda ukifika basi atarudi kwa ajili ya mazungumzo alkini wameshagaa ameamua kufanya kazi zake mwenyewe.

Ruby aliwahi kutajwa sana kuwa ni msanii anaekosana na viongozi wake mara nyingi kutokana na swala hilo la nidhamu, wasanii wengi wakubwa wamewahi kuongelea swala lake wakitaka ajirekebishe.

Shetta Adai Mtoto Wake Amezaliwa Staa

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Nurdin Bila maarufu kama Shetta ameibuka na kudai Mtoto Wake Qayla ana ustaa wa kipekee ni tofauti na watoto wa mastaa wengine ambao wametengenezwa kuwa mastaa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Enews cha EATV, Shetta amesema umaarufu ambao mtoto wake anao mpaka sasa hajahusika hata kidogo kuutengeneza kwa maana hajawahi kutumia muda wake mwingi kumtangaza wala kumfanyia mtoto wake kitu chochote ambacho kingefanya jamii imfahamu au kufatilia kile anachokifanya.

Kwa kweli umaarufu wa mwanangu Qayllah hata mimi mwenyewe unanishangaza kwa maana kila siku zinavyozidi kwenda nashangaa anafanya vitu ambavyo vinafanya watu wazidi kumpenda, yaani mpaka sasa naona kama anataka kuzidi jina la Shetta sasa maana watu wananiita baba Qayllah badala ya jina langu”.

Hivi sasa Shetta na mke Wake Leila  wana watoto wawili ambao wote ni wa kike ambao ni Qayla na Qamrah.

Shetta Aomba Mazingiraya Kisiwa cha Mbudya Yaboreshwe.

Imeripotiwa kuwa kisiwa cha Mbudya ni moja ya sehemu kuwa sana ambayo wasanii na watu maarufu mbalimbli kwa sasa wamekuwa wakienda kwa ajili ya kustarehe lakini kumekuwa na mazingira ya kuhatarisha sana maisha ya watu wanaokwenda huko.

Inasemekana kuwa watu wengi wamesababishia vifo katika kisiwa hicho kutokana na  mazingira yake kuwa hatarishi sana.

Moja ya wasanii wa bongo fleva shetta amefunguka na kusema kuwa kwa sababu mbudya ni sehemu inayopendwa sana na watu kwa sasa basi ni bora serikali inagalia jinsi ya kupaboresha au hata wale wamiliki wa maeneo hayo wapaangalia tena kwa kutunga sheria zitakazosaidia watumiaji na kuweka misingi bora ya maeneo hayo.

Haya yanakuja  baada ya moja ya wadau wakubwa katka muziki PANCHO kupoteza maisha siku za karibuni akiwa katika kisiwa hicho na hata hivyo baadhi ya watu waliowahi kufika eneo hilo wanasema eneo hilo bado ni hatarishi sana kutokana nakusababisha vifo mara nyingi ingawa vipo ambavyo haviripotiwi.

Shetta- Sijafulia Naingiza Milioni 1 Kwa Siku

Staa wa muziki wa Bongo fleva Nurdin Bilal Ali maarufu kama Shetta amefunguka na kudai kuwa hajafulia kama watu wengi wanavyodai kwani anafanya biashara inayompa kipato kikubwa tu.

Shetta alishawahi kufanya vizuri siku za nyuma na ngoma kali kama Nidanganye na Mdananda, amesema sababu tu hasikiki Kwenye muziki kwa hivi sasa haimaanishi kama amefulia.

Shetta amesema ana biashara ndogo ndogo ambazo zinamuingizia kipato kikubwa kwani hivi sasa ana vibanda vya kukaanga chipsi kama vitani ambavyo vinamuingizia kipato cha kutosha.

Mimi nafanya bishara, nina biashara ndogondogo ambazo nazikusanya pia, ujue mimi ni mmoja kati ya watu ambao wana vibanda vya chips vingi, kwa siku kila kimoja kinatoa laki na nusu au laki mbili, imagine una vibanda vya chips vitano ambavyo kila siku vinakupa laki 2, kwa hiyo nakusanaya milioni kila siku”.

Lakini pia Shetta amesema bado anaingiza pesa pia kwa njia ya muziki kwani anasimamia wasanii ambao ni The Mafik Band.

Shetta Ataja Sababu Ya Kutofautiana na Diamond

Staa wa muziki wa Bongo fleva Shetta amefunguka na kuweka wazi sababu hasa za yeye kutofautiana na msanii mwenzake Diamond Platnumz.

Shetta na Diamond mbali na kufanya kazi wote na kutengeneza hits mbali mbali Lakini pia walikuwa ni marafiki wa karibu lakini siku za hivi karibuni wamekuwa hawaonekani pamoja.

Kwenye mahojiano na Wasafi Tv, Shetta amefunguka na kusema hakuna bifu kati yake na Diamond kama watu wengi wanavyodhani bali wametangana kwa sababu za kibiashara:

Sidhani kama kuna bifu lakini mimi nafikiri biashara sababu mwanzo tulikuwa tunaishi kama washikaji lakini ikimbukwe sote ni wanamuziki ili kutafuta inabidi kila mtu apambane.

Siri ya biashara kila mmoja anataka kufanikiwa, kila mmoja anataka kuwa namba moja na kuna series za mafanikio. Automatic wewe kama mwanamuziki na sifaidiki na wewe kwa njia moja au nyingine, siwezi kukupa njia zangu na wewe huwezi kunipa njia zako lakini haiwezi kuwa kama tatizo”.

Wasanii hao wameshafanya ngoma kali kama vile Nifanganye na kerewa.