Snura Akiri Kuwa Uvivu Ulimponza Sana

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Snura Mushi amefunguka na kuweka wazi Siri Yake ya utoto na kukiri kuwa alikuwa mvivu sana kiasi cha kusingizia ugonjwa akitumwa.

Snura anajulikana kama Msanii mchapakazi ambaye pia mama wa Watoto wawili ambao ameweka wazi kuwa anawalea Watoto Wake mwenyewe, Lakini ameweka wazi pia ameshawahi kuwa mvivu sana wakati mdogo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Snura alisema haku­wahi kupenda kutumwatumwa, alikuwa ni mvivu na kila al­ipoagizwa kufanya jambo alizua ugonjwa wa tumbo ili tu asifanye kazi husika.

Uvivu huu acheni tu, sasa hivi nikikumbuka najiona mjinga, nilimsumbua sana bibi yangu kwa kusingizia ugonjwa, kila nikiona sasa natumwa naibua ugonjwa ambao sikuwa nao, bibi alinionea huruma na ku­nitungia jina flani kwani niliumwa kila siku“.

Kwenye mahojiano aliyofanya Hivi karibuni Snura aliangua kilio na kuweka wazi kuwa baba Watoto Wake hamsaidii kabisa kulea Watoto Wake hivyo inampasa kufanya kila kitu.

Video iliyomuonyesha SNURA akilia yazua Gumzo

Mwanadada Snura Musih azua gumzo baada ya kuonekana akilia katika mahojiano huku sababu kubwa ya kulia ikiwa ni kulalamika kwae kuwa amekuwa na maisha magumu na kwamba wasanii wamekuw waizulumiwa lakini hakuna wa kuwasaidia .

Snura anasema kuwa watu wanaowadhulumu wamekuwa ni matajiri na wao maskini ndio kila siku wamekuwa wakipata shida ya kupambana na hali zao.

Hata baada ya kusambaa wa video hiyo katika mitandao ya kijamii watu wamemshambulia msanii huo kwa kumwambia kuwa wanamshangaa kinachomliza kwa sababu amekuwa akimlea mtu mzima ambae ni kiben ten chake  ambae ana uwezo wa kufanya kazi na kusaidiana katika familia.

Ikumbukwe kuwa snura ameuwa katika mahusiano na mwanaume huyo wanaemwita kibenten kwa muda mrefu sasa huku tetesi zikisema kuwa kijana huyo amekuwa akilelewa na msanii huyo

Snura Azungumzia Bifu lake na Shiloleh

Msanii wa muziki wa Bongo fleva, Snura Mushi ‘Snura’ amefunguka kuwa uhusiano wake na msanii mwenzake Shilole haujawahi kubadilika tangu mwanzo na hawakuwahi kuwa na tofauti kama wengi wanavyodai.

Snura amefunguka hayo wakati akizungumza na www.eatv.tv, ambapo amesema kuwa Shilole na yeye walikuwa na mpango wa kufanya kazi wakati ule ili kuonesha kuwa hawakuwa na tofauti lakini muda ulikosekana.

“Uhusiano wangu na Shilole haujawahi badilika, upo vilevile tangu tulipozaliwa na umesimama palepale kama picha la ‘bisimini'”, amesema Snura.

Akizungumzia mafanikio yake katika sanaa, Snura amesema kuwa anajivunia vitu vingi ambavyo amevipata kupitia muziki lakini hapendi kuonesha.

Nina vitu vingi vya kujivunia lakini siwezi kunadi mali zangu mtandaoni, mimi huwa na nadi kazi tu”, amesema Snura

Snura Amsifia Mpenzi Wake kwa Kujali Watoto Wake

Msanii wa Bongo Fleva, Snura Mushi amesema kuwa mpenzi wake, Minu Calypto amekuwa akijali sana watoto wake kuliko watu wanavyodhani.

Akizugumza na Clouds FM amesema ni kitu ambacho kimekuwa kikimpa furaha kwenye mahusiano yao.

“Anapenda familia yangu yaani anapenda watoto wangu na watoto wangu wanampenda sana. Tunaweza tukawa tunatoka na mtoto wangu wa mwisho akataka abaki nyumbani na mimi ndiyo nitoke,” amesema.

Snura Mushi na Minu Calypto ni wapenzi ambao pia wanafanya muziki. Wawili hao kwasasa wametoa ngoma yao ya pamoja inayokwenda kwa jina la Shoko.

Muziki wa Snura Watua Mikononi Mwa Snoop Dogg

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Snura Mushi maarufu kama Snu sexy amekula Shavu la haja  baada ya wimbo wake wa ‘Chura’ kurushwa na staa mkubwa duniani kutoka nchini Marekani rapper Snoop Dogg.

Snoop Dogg alirusha video ambayo inamuonyesha mwanadada akicheza wimbo wa Snura ‘Chura’ na kuonyesha kumvulia kofia.

Snoop ameiweka video hiyo Kwenye ukurasa wake wa Instagram ambao una mashabiki zaidi ya Milioni 28 na mpaka sasa video hiyo imetazamwa na watu zaidi ya Milioni mbili.

https://www.instagram.com/p/BpBbq6eBPdT/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1758b5ns6v14b

 

Snura ameonekana kupata shavu nono kwani watu wameonekana kuikubali video hiyo na wimbo na hat wapo ambao wanaulizia muziki ule ni wa wapi na Watanzania wameendelea kumtag Snura.

Snura Atabiriwa Kupotea Kimuziki Baada Ya Kubeba Ujauzito Wa Kibenten

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini Snura Mushi maarufu kama Malkia wa Uswazi amedaiwa kuwa anaweza akapotea kimuziki baada ya kubeba ujauzito wa kibenten chake.

Kumekuwa na tetesi nyingi Kwenye mitandao ya kijamii kuwa Snura amebeba ujauzito wa mpenzi wake kibenten ambaye pia ni msanii mwenzake Muna Calypto.

Hofu kubwa ya wadau ni kuwa huenda Snura akapoteza soko lake Kimuziki na kumtabiria kupoteza mashabiki endapo atazaa sahivi basi huyo atakuwa mtoto wake wa tatu.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha Enews ya East Africa Tv, Maneja wa Snura anayejulikana kama HK amedai hakuna tatizo lolote kama Snura ni mjamzito na wala hawezi kushuka Kimuziki:

Kwa jinsi ninavyomjua Snura ni mtu ambaye hajawahi kutoa ujauzito na wala hafikirii kufanya hivyo kwaiyo atazaa kama kawaida na suala kushuka Kimuziki sidhani na haiwezi kutokea kwa sababu yule ni mtoto wa kike na lazima atapata watu wa kuja kumsaidia baadae”.

Lakini pia Meneja huyo amesisitiza Snura akishazaa atarudi Kwenye chati kwani alizaa mtoto wake wa Pili na akarudi kama kawaida na kutoa nyimbo kali kama kawaida hivyo mashabiki wasubiri baada ya miezi

Msanii Snura Mushi na Mpenzi Wake Wapata Ajali Ya Gari

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayetamba kwa miondoko ya Mduara Snura Mushi ‘Snu Sexy’ pamoja na mpenzi wake Minu Calypto wamepata ajali ya gari siku ya jana mkoani Lindi walipokuwa anaelekea Kwenye shoo.

Taarifa za awali zinadai kuwa ajali hiyo ilitokea wakati Dereva wa gari la Snura alipokuwa anajaribu kulikwepa korongo na kusababisha gari hilo kupinduka.

Ndani ya gari hilo kulikuwa kuna watu watatno ambao ni Snura na Minu pamoja na madancer wawili wa Snura pamoja na Dereva wa gari hilo lakini kwa bahati nzuri kila mtu ni mzima zaidi ya majeraha machache.

Mpenzi wa Snura ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuhusu ajali hiyo:

https://www.instagram.com/p/BmRRmsnFpXz/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=rzkvn5quub6p

Nitapunguza Mauno kwenye Video Ila Sio Kwenyee Show;-Snura

mwanadada snura mushi amefunguka na kusema kuwa kwa sasa amepunguza kabisa kukatika mauno katika video zake na sio kwa sababau ya BASATA lakini tangu alipoanza kutolewa katika kinyanganyio cha kilimanjaro music awards amejifunza na sasa ameanza kupunguza ukali wa video zake.

Hata hivyo mwana dada huyo amesmea kuwa pamoja na kwamba mauno ya kwenye video yatapungu lakini haitapunguza mauno katika show zake kwa sababu anaamini kuwa watu wanaopatikana kule wanaendana na mambo ya show anayoifanya.

Akiongea na Dida katika mitikisiko ya pwani , Snura anasema kuwa video yake ya nimevurugwa ilikuwa ikifanya vizuri lakini ilikuja kufungiwa na kushindwa kuingia katika tuzo  za Kili , hicho kitu kilimuuma sana.

Tayari mimi sasa hivi nimeshabadilika sana kabla hata ya hayo mambo ya kili video yangu ilikuwa imefungiwa na hata wimbo wangu wa ushaharibu ukitoka watu watajua jinsi gani nimeweza kubadilika , kwenye video sio kwamba hakutakuwa na viuno ila nimepunguza.wimbo unaokuja sijakatika kama kwenye nimevurugwa wakati nafanya kule nilijua ni ubunifu na utundu wangu lakini  kumbe sio kweli na wala sikujua kama nitafungiwa.

ninajua nina mashabiki wengi wanaopenda sana viuno vyangu lakini kwenye show sitakuwa nakatika sana naomba wavumilie tu lakini wale tutakao kuwa tunakutana kwenye show nitakuwa najiachia kama kawaida.

 

Sina Bifu na Snura Ila Sio Rafiki Yangu- Nisha

Muigizaji wa Bongo movie Nisha aliyetoa nyimbo yake mpya ‘Bachela’ amefunguka kuhusu uhusiano wake na msanii wa Bongo fleva Snura na kusema hana bifu naye ila pia sio marafiki.

Ishu ya Snura na Nisha ilishika headlines sana wiki chache zilizopita baada ya Snura kuonekana ana uhusiano wa kimapenzi na Minu Calypto ambaye alikuwa ni mpenzi wa Nisha.

Taarifa zilienea na kudai kuwa Snura alimpindua NIsha kwa Minu ambaye alikuwa ni kiben 10 cha Nisha na hata maneno maneno yalisemwa Kwenye mitandao ya kijamii ingawa kila mmoja alisisitiza kuwa hana bifu na mwenzake.

Kwenye mahojiano aliyofanya hivi karibuni na Millard Ayo Tv, Nisha ameweka wazi kuwa hana bifu na Snura wala hawana urafiki ila ni watu tu ambao wanafanya wote sanaa zao:

Mimi na Snura hatuna urafiki ni wasanii tu lakini pia hatuna Uhasama wowote wala bifu kwa sababu mwisho wa siku maisha yanaendelea kwa sababu aliyekuwa naye nilishaahana naye kabla hata hawajaanza mahusiano kwaiyo moyo wangu mweupe kwake”.

 

Snura- Natamani Ningepata Nafasi Ya Kusoma Zaidi

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya mduara Snura Mushi ‘Snu sexy’ amefunguka na kusema majuto yake maisha ni ni kukosa elimu.

Snura ambaye amekiri kuwa aliishia elimu ya msingi na hakufanikiwa kabisa kukanyaga elimu ya sekondari kutokana na maisha kuwa magumu na wazazi wake kukosa uwezo wa kumsomesha na kumfikisha mbali kielimu.

Snura amelifungukia gazeti la Ijumaa Wikienda na kueleza jinsi anavyojikuta akizitolea macho sare za shule za sekondari kwani hakubahatika juzi ana kabisa:

Kiukweli nikaona wasichana wamevaa sare za sekondari huwa nazitolea macho sana natamani siku zirudi nyuma ili nami nipate elimu hiyo kwani maskini niliishia darasa la saba tu”.

Snura pia ametoa ushauri kwa wasichana ambao wamepata nafasi ya kusoma watumie nafasi hiyo kusoma kwa bidii na kuachana na mambo ambayo hayana faida kwani mtu kama yeye hakubahatika kabisa kupata nafasi hiyo ya kuendelea na masomo ya sekondari.

Snura ameweka wazi ugumu wa maisha aliyopitia kutokana na kukosa elimu ndio kitu kilichomfanya aweze kuhangaika sana ili wanaye waweze kusoma mpaka elimu ya juu.

Snura Apanga Kuwa Mwalimu wa Kwaya Mashuleni.

Msanii wa muziki wa bongo fleva nchini snura mushi amefunga na kusema kuwa kwa sasa hana anachowaza kuhusu sanaa zaidi ya kujiajiri mwenyewe kwa sababu anaona kuwa kazi ya kufanya muziki imekuwa ina makwazo ambayo hayatatuliki.

Snura anasema kuwa kwa sasa anafikiria tu kufanya kazi ya kujiajiri ambapo amepanga kwenda  kufundisha kwaya mashuleni na kusema kuwa anawashangaa sana BASATA  kwa kuufungia wimbo wake wa chura kwa sababu walishaakaa chini  wakauzungumzia wimbo huo na kuweza kufanya baadhi ya marekebisho na kuruhusu kupigwa kwa sababu alitoa baadhi ya vipande ambavyo vilikuwa vinatakiwa kutolewa.

kwa sasa najifikia kujiakiri mwenyewe zaidi na zaidi ndio maana najipanga niwe tu mwalimu wa kwaya shuleni kwa kuwa muziki wetu umekuwa mgumu sana kwa sababu mtu unafungiwa wimbo wako hata  kosa halijulikani.

wakati mwingine unawapelekea kazi kabisa wanaikagua lakini wanakuja kukugeuka baaadae kama ilivyokuwa kwangu huu wimbo wa chura niliubadilisha na wakaukagua kabisa  na wakaniruhusu niwaite waandishi  wa habari na kuwaambia mabdiliko hayo na ukaanza kupigwa kwenye vyombo vya habari lakini sasa hivi  nimefungiwa tena sijui hata kosa ni nini..

Snura ni mmoja wa wasanii ambao wamekumbwa na adhabu ya kufungiwa nyimbo zake baaada ya kuonekana kuwa nyimbo zake mbili zilikuwa hazina maadili na zinakiuka taratibu za maadili ya Tanzania.

 

Snura: Bado Sijajua BASATA Wanataka Kitu Gani

Mwanamuziki wa Bongo fleva Snura makali wa ‘Majanga’ amefunguka na kusema kuwa anawashangaa sana BASATA kwani mpaka sahivi hajajua wanataka nini au wanaangalia vigezo gani.

Wiki iliyopita TCRA walitangaza rasmi kuwa wamefungia nyimbo 15 zisipigwe kwenye vyombo vya habari kwa kile walichodai kuwa BASATA wamezipitia na kuagiza zifungiwe kwa kukiuka desturi na  maadili ya Kitanzania.

Snura ni moja kati ya wasanii waliofungiwa nyimbo mbili ambazo ni ‘Nimevurugwa’ na ‘Chura’  ambao ulizua gumzo tangu ulipokuwa unatoka mwanzoni kabisa ambapo ilidaiwa kuwa hauendani na maadili ya Kitanzania.

Snura amefanya Interview na Millard Ayo Tv lakini ameonyeshwa kushangazwa kuliko hata kukasirika kutokana na kitendo hiko ambapo amefunguka na kusema:

Kabla ya hapo sikupata taarifa yoyote kuwa nafungiwa nyimbo zangu kwa sababu wakati nafungiwa Chura nilitumiwa barua lakini safari hii sikuitwa wala sikuwa na taarifa yoyote ile kwaiyo kwa hilo nakuwa nashindwa kuwaelewa BASATA wanakuwa wanataka nini kutoka kwangu”.

Snura amedai alishawahi Kuitwa na BASATA ambapo walifanya kikao na kuamua kuwa video ya wimbo wa Chura ndio ulikuwa mbaya lakini audio ilikuwa nzuri hivyo aliambiwa abadilishe video na hatafungiwa nyimbo hiyo ambapo amedai alifanya video mpya ambayo waliikubali na kuipitisha.

Snura hajashangazwa Kuona Ngoma ya Chura kufungiwa.

Malkia wa ngoma za uswazi Tanzania Snura Mushi maarufu kama Snura Majanga amefunguka na kusema kuwa hajashangazwa hata kidogo kuona ngoma ya chura imegungiwa lakini anachoshangaa ni kwanini wimbo wake wa  nimevurugwa nao pia kufungiwa wakati ni wimbo wa siku nyingi.

Snura anayaongea hayo baada ya jana tarehe 28 February kutoka list ya nyimbo zaidi ya kumi kufungiwa na Baraza la Sanaa Tanzania BASATA kwa madai kuwa nyimbo hizo zimekosa maadili ya kusikilizwa na kuonekana katika vituo vya habari nchini.

Kufungiwa kwa nyimbo hizi ni muendelezo wa kazi ya BASATA  likiwa na nia ya kufungia na kukataza nyimbo zote na wasanii wote ambao wamekuwa wakitoa nyimbo au kuchapisha picha ambazo hazina maadili.

Snura anasema kuwa wimbo wa nimevurugwa ni wa zamani sana ukilinganisha na nyimbo yake ya chura na hata za wengine zilizofungiwa kwa sababu ni za hivi karibuni, hata hivyo nbado Snura anasema kuwa hajapata taarifa rasmi kutoka BASATA  kuhusu kufungiwa kwa nyimbo zake zaidi ya kuona taarifa hizo katika mitandao tu.

Wasanii wengine walofungiwa ni pamoja na Diamond, Ney wa mitego  Gigy money , Barnaba.

Snura Afungukia Kupora Bwana wa Nisha, Akubali Kuwa ni Mpenzi Wake.

Mwandada naesifika kwa kutoa mauno anapokuwa jukwaani snura majanga amefunguka na kukubali kuwa ni kweli mwanaume yule ambae picha zake zimevuja ni mpenzi wake lakini sio kweli kuwa mwanaume huyo amempra kutoka kwa nisha kama tetsi na taarifa zinazokuwa zikisambaa katika mitandao ya kijamii.

Snura ambae kwa muda mrefu alikuwa akikana kuwa hana mahusiano na mwanaume huyo , aliumbuka sana siku ya wapendanao baada ya baadhi ya watu kudaka picha zake zikimuonyesha yuko na mwanaume ambae watu walikuwa wakimtuhumu kuwa amempora kutoka kwa msanii mwenzake Nisha ambae pia kwa muda mrefu amekuwa akilia kuwa amekuwa akiibiwa mabwana kila kukicha.

Baada ya kuvuja kwa picha hizo Snura aliona ni bora kuweka bayana swala hilo kwa sababu amekuwa akiandamwa na kukosa amani ya kuwa na mwanaume huyo kwa sababu ya kusimangwa na marafiki na mashabiki zake katika mitandao.

Nisha alikubalikuwa ni kweli wapo katika mapenzi mazito na mwanaume huyo lakini sio kweli kuwa amemuiba mwanaume huyo bali mwanaume huyo aliingia nae katika mahusiano tayari alikuwa amekwisha achana na Nisha siku nyingi na ukweli ni kwamba ni nisha mwenyewe ndie aliwaunganisha wawili hao kwa sababu ya kufanya kazi pamoja.

Minihai sio mpezni wa nisha na hata sikumchukua kwake,kwani hadi naningia katika mahusiano na mwanaume huyo tayari alikuwa maeshaachana na Nisha siku nyingi na hata aliyetunganisha ni yeye mwenyewe Nisha kwa sababu alimpa Minihali namba yangu ya simu.

Snura alisema kuwa amekuwa akiwashanga watu ambao wanamsema katika mitandoa kwa kumtuhumu kuwa ameiba mwanaume wa nisha wakati ukweli ni kwamba aliyewaunganisha ni nisha mwenyewe na hata kuingia katika mapenzi iliwachukua muda mrefu kwa sababu walikuwa wakifanya kazi kwa pamoja na kujikuta wanazoea sana na kuingia katika mahusiano.

Siku za nyuma baada ya kuanza kwa tetesi hizo, msanii Snura aliwatolea povu zito kipindi cha shilawadu kwa kusambaza taarifa za uongo kuhusu mahusiano hayo lakini baada ya picha za Snura na mwanaume huyo kuvuja imemfanua Snura kufunguka na kusema ukweli.

 

Snura Ajibu Atuhuma za Kuiba Mwanaume Wa Nisha

Msanii wa muziki bongo Snura Mushi maefunguka na kudai kuwa hana mahusiano yoyote na wanaume anaejulikana kwa jina la Minu kama ambavyo imekuwa ikisambaa katika mitandao kuwa anatemeba na mwanaume huyo kisa tu amemu-wish mwanaume huyo kheri katika siku yake ya kuzaliwa.snura amesema kuwa kati yake na minu kumekuwa na urafiki tu tena sio wa muda mrefu kama ambavyo watu wamekuwa wakizusha.

Mwanaume huyo ambae alikuwa mwanaume wa Nisha Bebe, msanii wa bongo movies inasemekana kwa aliibiwa na Snura kutoka kwa Nisha .

Tetesi hizo zilianza kusambaa baaada ya Snura kuweka picha ya kijana huyo na kuandika anampenda sana sana huku akimtakia kheri kwa siku yake ya kuzaliwa ndipo watu walipoanza ku-judge na kusema kuwa mwanaume huyo ameibwa kutoka kwa Nisha kwa sababu ni siku chache tu katika ukurasa wa Nisha aliandika akionekana kulalamika kuwa akuna watu wamemuibia mwanaume aliyekuwa nae.

Snura alisema kuwa minu na yeye walijuana baada ya nisha mwenyewe kumpa namba yake ili wafanye kazi ya muziki pamoja kwa sababu mwanaume huyo ni mwandishi wa mashairi.

huyo Minu sio mpenzi wangu na wala hatuna muda mrefu tangu nimejuana nae , kuna siku alinitafuta baada ya kupewa namba yangu na  nisha kwa sababu alipewa alikuwa ameandika wimbo ambao aliona mimi ninafaa kuuimba.sasa nimemtakaia kheri ya kuzaliwa na kumwambia kuwa ninampenda basi imekuwa kosa.

Nisha amekuwa akilalamika kila kukicha kuwa kila mwanaume anaekuwa nae katika mahusiano anachukuliwa na mwanamke mwenzie na kuacha mpweke.

 

 

Snura Ajikuta Matatani Baada Ya Kutoa Maoni Kuhusu Faiza Ally.

Baada ya Faiza Ally kuweka picha yake ya utupu ikimuonyesha alivyokuwa leba kipindi anamzaa mtoto wake wa pili wa kiume, baadhi ya watu walishikwa na hasira na wengine waliona kuwa kitendo hicho ni kitendo cha kudharirisha wanawake.Moja ya wasanii wa bongo movies anaefanya vizuri na anaesifika kwa kukata viuno anaejulikana kama Snura Majanga alifunguka na kuongelea swala la Faiza kutuma picha hiyo ni kudharirisha wanawake waliokwend leba tayari.

najua wengi watasema mbona na yeye hana adabu ,ila ukichunguza utagundua sehemu yangu ya kiuno tu ndio inayoniweka matatani, sinaga mambo mengi ya ajabu na sitakuja kuwa nayo kamwe.faiza hii umepitiliza TUSITIRI WANAWAKE WENZIO.. mwanamke anapotaka kuzaa hata kama ni barabarani utafutwa nguo na kuziba …leba ni siri yetu kuna mengi tunayafanya kule ambayo hayapaswi kujulikana nje,ni wengi wanashoot hata video lakini huwa inabaki kumbukumbu yao,na sio kuweka hadharani kila mtu akaona, inakuwaga aibu hasa kwa sisi wanawake, tunadharirika na kupoteza heshima kabisa ya mama, tunadharauliwa sanakwa mtindo huo.hata ndugu zetu wakija hawaruhusiwi kuingia leba zaidi ya manesi na  madaktari  na kama ni private ataruhusiwa kuingia mumeo tu, hizi ndizo tamaduni zetu tusijikatae sana tukaendekeza uzungu, mengine tuwaachie wenyewe sisi tubaki kuwa sisi.#niliemkwazapole -Aliandika Snura katika ukurasa wake wa instagram.

Lakini baada ya posti hiyo ya snura nae faiza aliamua kumjibu na kumjia juu snura kwa kuandika,

Video yako ya Chura na picha ya mimi leba bora nani,na mauno kutwa kucha kuhamasisha ngono kupitia musiki kweli, hebu jiongeze bwana nimezaa hiyo ni natural  mama, wanangu watakuwawasomi hawatakuwa na mawazo ya kipuuzi hivyo, kama za kwako na wengne…so stupid of you kama wewe na mziki wako tu  #postiyamudamfupi @snuramushi. Aliandka Faiza kumjibu Snura.

Hata hivyo posti hiyo iliyokuwa ikimuonyesha faiza yupo leba ilifutwa dakika chache baada ya kuwekwa kutokana na sheria za mitandao  na watu wengi kuiripoti picha hiyo kuwa haina maadili.