Snura Mushi aeleza chanzo cha ajali mbaya aliyonusurika

Snura Mushi amekana habari zilizoenea kuhusu chanzo cha ajali mbaya aliyonusurika. Awali iliripotiwa kuwa mrembo huyo alipata ajali kwasababu alikua akiendesha gari lake kwa kasi.

Chanzo kilichokuwa eneo la tukio kilisema kuwa Snura alikuwa kwenye mwendo wa kasi na kushindwa kukata kona iliyopo maeneo ya Cocacola Mikocheni.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Snura alipinga kuwa ajali aliyopata ilisababishwa na yeye kuendesha gari lake kwa kasi.

Snura alieleza kuwa alipoteza mwelekeo kwani hakua anajua hio barabara vizuri, alisema ajali hio ilitokea kwasababu hakujua kuna kona kali mbele.

“Unajua ajali ilikuwa mbaya sana, nashukuru waliotuokoa, chanzo cha ajali ni kwamba ile barabara siijui vizuri kwa hiyo sikujua pale kama kuna kona kali ndiyo maana nikapoteza mwelekeo. Kupona au kutoka hivi salama kwenye ile ajali ni Mungu tu, maana gari liliacha njia na kupinduka, lakini mimi na mdogo wangu tulipata michubuko midogo tu mwilini na sasa hivi tunaendelea vizuri tu,” alisema Snura.

 

“Nilishalala njaa sana tu” Snura Mushi afunguka kuhusu maisha yake ya tabu

Ukiona vyaelea vimeundwa… Snura Mushi ametoka mbali kufika alipo sasa. Mwimbaji huyo amepitia yote ya maisha ikiwemo kulala njaa.

Snura amekana dhana iliyojengeka kwa akili ya watu wengi kuwa kila mwanamke mwenye mafanikio ya aina yoyote lazima atakuwa ameyapata kutoka kwa wanaume aliotembea nao kimapenzi.

Mwimbaji huyo amesema kuwa yeye alifanikiwa maishani mwake kwa jasho lake bila ya mwanaume yoyote kumsaidia.

Snura alieleza alivyotaabika alipotoka kwa wazazi wake na kuanza maisha ya kujitegemea, alisema kuwa ashawai lala njaa akiwa katika harakati ya kutafuta.

“Nilishalala njaa sana tu, tena wakati natoka kwa wazazi na kuanza maisha yangu binafsi ya kujitegemea, nilikuwa na wakati mgumu sana nakumbuka nilikuwa nashindia ugali na mbilimbi na nilikuwa jeuri sana japo nilikuwa na shida zangu kwa sababu maisha hayo hayakufanya nimtegemee mwanaume” alisema Snura.

 

Snura Mushi afurahishwa na wazito wa kimuziki kutoka Nigeria na Marekani wanaopenza wimbo wake ‘Chura’

Kuna watu waliokosoa Snura Mushi alipotoa wimbo wake ‘Chura’ – walisema kuwa wimbo huo hauzingatii maadili ya kijamii.

Ata hivyo kuna wale pia waliopenda wimbo huo, video yake unaonyesha Snura na wanawake wengine wakitingisha makalio zao.

wazito wa kimuziki kutoka Nigeria na Marekani ni miongoni mwa watu wanaopenda wimbo wake Snura. Akiongea kupitia kipindi cha Eight cha TVE, Snura alisema anafurahishwa na kuongezeka kwa idadi ya mashabiki.

“Nilishitushwa sana na producer Don Jazzy alivyo post video anaimba nyimbo yangu ya chura, nakumbuka aliposti pia hata video yake kwenye Instagram yake,Pia meneja wake Lil Wayne alipost pia nyimbo ya chura nilifurahi kuona watu wameielewa,” alisema Snura.

 

Snura akana kupangiwa nyumba na mwanaume wa Kiarabu

Inasemekana kuwa mwanamziki Snura amepangiwa nyumba mpya na mwanaume wa Kiarabua ambaye anaweza kuwa mpenzi wake hivi sasa.

Hata hivyo, akizungumza na waandishi wa Global Publishers amabao walimtembelea katika nyumba yake huko maeneo ya Tabata, Dar Snura alikana kwa kusema kuwa hana mawanume wa kiarabu ambaye amempangia nyumba.

Aliendelea kusema kuwa alihamia sehemu hiyo ili mwanae awache kuchoka akienda shule. Hivi ndivyo mazungumzo yao yalikuwa.

Snura
Snura

Wikienda: Snura mambo vipi? Mbona kimya sana kimuziki? Au ndiyo mambo ya ubuyu unaosemwa?

Snura: Yapi tena? Mimi mbona nipo najiandaa kutoa kazi? Siyo kila siku kusikika bila mpango. Mimi huwa nasikika kwa kazi ninayoitoa ninyi subirini mtanisikia.

Wikienda: Hata hivyo, tuna ubuyu hapa kuwa nyumba hii umepangishiwa na mwanaume wa Kiarabu ambaye amekuhamisha Mwananyamala kwa sababu alikuwa hapapendi, unalizungumziaje hilo?

Snura: Hahahahaha, mmenichekesha kweli, watu wanajua kuongea sana, mimi nimehama nyumba kwa sababu ya mtoto. Shule anayosoma mwanangu ipo huku Tabata. Mwananyamala ilikuwa ni mbali sana. Mwanangu alikuwa anachoka sana. Hayo mengine ya mwanaume wa Kiarabu ndiyo kwanza nayasikia kwenu.

Wikienda: Nasikia amekununulia na gari la kutembelea maana tunaliona hapa, tunasikia ana mpango wa kukupiga stop kuimba, je, ni kweli?

Snura: Gari nimenunua mwenyewe kwa jasho langu nikimaanisha kazi yangu, huyo Mwarabu mnayemkazania kama yupo hakuna la kufi cha kwani mwisho wa yote atajulikana tu na ataonekana, lakini nahisi labda wanayemzungumzia ni baba mtoto wangu, hahaha…

Snura Mushi aeleza kwa nini hatamani kabisa kuhusiana kimapenzi na mtu yeyote maarufu

Snura Mushi ni mama wa watoto wawili, alizaa mtoto wake wa pili Januari 2015. Msanii huyo hajawahi kuwa kwenye uhusiano uliodumu muda mrefu.

Ata hivyo Snura hataki kuhusiana kimapenzi na mtu yeyote maarufu, alisema kuwa amekuwa akifuatilia uhusiano wa kimapenzi wa mastaa wengi na kugundua kuwa huwa haudumu kutokana na mastaa kutokuwa waaminifu au mazingira ya kazi zao ambayo kwa wasanii wa kiume yanawafanya kuwa karibu na wanawake.

“Naomba niwe muwazi, kwa sasa sitamani kabisa kutoka kimapenzi na mtu maarufu au niseme tu staa kutokana na mimi kuwa mtu mwenye wivu sana, unajua mastaa wengi wa kiume huwa karibu sana na wanawake kwa mazingira ya kawaida ya kikazi, sasa mimi nikiona hivyo ninafahamu ninasalitiwa tu,” Snura aliambia Uwazi Showbiz.

 

Msanii anayevuma kwa nyimbo chafu Snura Mushi anataka kumrejea Mungu

Ata baada ya kurithi madrasa kutoka kwa babu yake, Snura Mushi aliupea dini kisogo na kuzama kwa mamba ya kidunia.

Msanii huyo amevuma kwa nyimbo zake chafu ambazo yeye hutingisha matako kama mtu aliye pagawa na pepo chafu kutoka kuzimu.

Snura ametamba na wimbo wake ‘Chura’ aliyo toa mwaka jana. Wimbo huo uliwashangaza wengi kutokana na uchafu ulio onyeshwa kwenye video yake.

Ata hivyo Snura sasa anataka kumrejea Mungu, alisema anaamini kwamba mambo ya kidunia yana mwisho wake.

Msanii huyo sasa anataka kuwa mlezi wa madrasa aliyoachiwa na marehemu babu yake iliyopo Yombo Vituka.

“Najitahidi kufanya kazi kwa bidii na maombi yangu kwa Mungu ni aniwezeshe niweze kumtumikia kabla siku yangu ya kufa maana natamani ifike siku niachane na masuala ya kidunia, nijielekeze kwenye dini,” alieleza Snura.