Soudy Brown na Maua Sama Waachiwa Kwa Dhamana

Mtangazaji wa Clouds Fm Soudy Brown na Msanii wa Bongo fleva Maua Sama wameachiwa kwa dhamana na jeshi la polisi baada ya kukaa rumande kwa wiki moja.

Soudy Brown na Maua Sama walishikiliwa na jeshi la polisi baada ya kuhusishwa na video waliyoisambaza Kwenye mitandao ya kijamii iliyoonyesha watu wakichezea na Kukanyagawpes

Soudy Brown, Maua Sama na Meneja wake Fadhili Kondo waliachiwa jana Septemba 25, jioni lakini wote wanatakiwa kesho kuripoti kituo cha kati (Central Police Station) saa 4 asubuhi.

Watatu hao jana walirudishwa mahabusu baada ya kupata dhamana ya kesi ya kwanza ya kuweka maudhui mitandao bila kibali kutoka kwa mamlaka husika, lakini waliendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa kile kilichodaiwa kuwa bado wanakosa lingine la kujibu, huku Mawakili wao wakizungumzia tukio la kukanyaga fedha ya Tanzania.

Wasanii ni Wanafiki Wanasubiri Kutoa Pole Badala Ya Kusaidia”- Steve Nyerere

Msanii wa Bongo movie na komedian maarufu Steve Nyerere amefunguka na kutaka Wasanii Wenzake waache unafiki na kupaaza sauti sasa ili Soudy Brown na Maua Sama waweze kuachwa huru.

Maua Sama na Soudy Brown wamewekwa  ndani tangu siku ya Ijumaa mpaka leo hawajapata dhamana baada ya kuposti video clip iliyowaonyesha kundi la watu wakicheza wimbo wa Iokote wa Maua Sama huku wakirusha pesa na kuzikanyaga.

Steve Nyerere amewatolea povu wasanii Wenzake na kuwataka wajitoe kuwasaidia wasanii wenzao katika kipindi hiki cha shida badala ya kukaa kimya halafu kuja kutoa pole wakija kutoka hapo baadae.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Steve Nyerere amemwaga povu hili:

Sisi wasanii ni waoga na wanafiki, limeanza kuhusishwa sijui kuna ugomvi na RC Makonda hawa wamekosea, sio wakitoka ndio tuanze kutoa pole, Ndio nilipanga kufanya hivi, Hapana muda ndio huu tuombe radhi kwa serikali vijana wetu wapewe dhamana”.

 

 

Wolper Awaombea Msamaha Soudy Brown na Maua Sama Wanaosota Rumande

Msanii wa filamu za Bongo Movie na mjasiriamali Mrembo Jacqueline Wolper ameibuka na kuwaombea msamaha mtangazaji wa Clouds Fm Soudy Brown na msanii wa Bongo fleva Maua Sama.

Maua na Soudy wamewekwa ndani tangu siku ya Jumapili mpaka leo hawajapata dhamana baada ya kuonekana kwenye video clips wakiwa wanakanyaga pesa.

Wolper amejikuta akiguswa na kitendo hicho cha kuwekwa ndani ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram, amesema anaomba viongozi wakubwa wa nchi wawaachie wasanii hao kwani walikuwa kwenye utafutaji na badala yake adhabu waliyoipata kwa siku hizi tatu liwe funzo kwa wengine.

 

Katika utafutaji Kuna mitihani Mingi Sana. Nachoweza kusema Nikuomba Tuu wakubwa muwasamehe vijana wenzetu Naamini katika Hili lililotokea Basi wengine wengi watajifunza kitu kupitia hili Naomba niwaombee masamaha wa Dhati kabisa Ndugu zetu Na wawe huru kuendelea Na majukumu yao inshallah. Maua & Soudy na wengine wore mliopo Ndani Juu ya hili sio sawa kutaja wote lakini hawa niwawakilishi poleni saanaa Jamani Ndani sio kuzuri“.

Mpaka sasa inadaiwa wawili hao bado wapo ndani bila dhamana.

Soudy Brown na Maua Sama Watiwa Mbaroni

Mtangazaji wa kipindi cha Shilawadu cha Clouds Tv, Soudy Brown na msanii wa Bongo fleva anayefanya vyema na ngoma yake ya ‘Iokote’ wamekuwa mbaroni mapema jana.

Soudy Brown na Maua Sama wanadaiwa kukamatwa na Polisi Kinondoni lakini mpaka jana jioni tayari walikuwa wameshahamishiwa Central Polisi.

Bongo 5 wanaripoti kuwa wawili hao walishikwa siku ya jana baada ya kupost video mtandaoni inayowaonekana watu wakicheza wimbo ‘Iokote’ wa Maua Sama huku wakiwa wanakanyaga hela.

Kamanda wa polisi kanda maalumu Dar, Mambosasa amefunguka na kuweka wazi kuwa Polisi inamshikiria mtangazaji Soudy Brown na mwanamuziki Maua Sama  kwa kosa la uharibifu wa mali. Inadaiwa wameonekana mtandaoni wakirusha hela na kuzikanyaga jambo ambalo ni kinyume na sheria.

“Nimepigwa Kama Mtoto na Uchebe Kisa Soudy Brown”- Shilole

Msanii wa Bongo fleva Shilole amefunguka na kuelezea kichapo kizito alichotembezewa na mumewe Uchebe ambapo amedai kisa na mkasa ni yeye kucheza mziki na Soudy Brown kwenye sherehe.

Siku ya jana kwenye kipindi cha XXL, Soudy Brown alifunguka kuwa alipokea taarifa kuwa Shilole alipokea kichapo kizito kutoka kwa mumewe Uchebe baada ya kurudi nyumbani usiku wa manane akitokea kwenye party Tabata.

Kupitia kwenye ‘You Heard’ Alitafutwa na kuulizwa kuhusu tetesi za kupokea kichapo hicho usiku usiku Shilole alikiri na kufunguka haya:

Tena Soudy niache kabisa wewe ndio umefanya mpaka mimi nagombana na Mume wangu eti Uchebe ana sema wewe bwana angu kweli? Umeshawahi kunitongoza wewe? Eti kisa siku ile kule Tabata tulivyokuwa tumekaa meza moja eti kakasirika, tulivyokuwa tunacheza mziki kwaiyo ina maana mimi nisicheze na mashabiki eti! MImi sitaki kuhusu kuongea mambo mengi nikaonekana mkorofi wa ajabu”.

 Lakini pia Shilole alikiri kupigwa kama mtoto na Uchebe kiasi kuwa walifunga mtaa hadi kupelekea Shilole kwenda kulala kwa marafiki zake:

Yaani Uchebe amenipiga kama mtoto mdogo lakini haina noma mimi mwanamke na dunia nzima inajua mimi mwanamke kuna mambo mimi nitakuja kusema mazito alafu ndo nitakapodai Talaka yangu”.

Baada ya sakata hilo Shilole alienda kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuweka ujumbe huu:

 

 

Ruby afunguka kwa nini alimtema Soudy Brown wa Cloud FM

Ruby alikua mpenzi wa Soudy Brown (mtangazaji wa kipindi cha Shilawadu cha Clouds FM) kwa muda wa miaka mbili. Mrembo huyo amefunguka kuhusu mahusiano yake na mtangazaji huyo.

Ruby alisema kuwa Soudy Brown ndiye mwanaume pekee kutoka kwenye industry ya muziki ambaye yeye amewai kuingia kimapenzi naye.

Ruby

Mrembo huyo alifunguka na kusema kuwa aliamua kumwacha Soudy Brown kwa sababu aliona mtangazaji huyo hakuwa na msimamo.

“Nikisema nitoke na mastaa wenzangu sio kwamba hawanisumbui wananisumbua sana lakini nawajua tayari the way walivyo. Lakini vitu vingi ambavyo naona wanafanyiwa wasanii wenzangu na mimi kweli nikawe na msanii? Hapana siwasemi kwa sifa mbaya wasanii lakini mimi siwezi kuisha nao kutokana na tabia zao kwa sababu mimi ni mwepesi sana kuumia. Mimi mwanaume ambaye nimetoka naye kwenye mapenzi na yupo kwenye industry yetu only ni Soudy Brown, na nimeishi naye kwa mwaka mmoja na miezi sita,” Ruby aliuambia mtandao wa Spin Tanzania.

 

 

“Napatana na Zari aliyeniletea watoto hao wengine siwajui” Mamake Diamond amkana Hamisa Mobeto

Kulingana na umbeya mitaani, Diamond Platnumz amempa mimba Hamisa Mobeto – mrembo yule aliyekuwa kwa video ya ‘Salome’.

Mbeya Soudy Brown alimpigia simu mamake Diamond Sanura ‘Sandra’ Kasim kudhibitisha kama ni ukweli kuwa Hamisa Mobeto amebeba mtoto wa Diamond tumboni.

Hamisa Mobeto na Diamond

La kushangaza ni kuwa Sandra alimkana Hamisa Mobeto licha ya mrembo huyo kuonesha ukaribu zaidi na familia ya Diamond. Hamisa aliwai zua utata alipoonekana na mamake Diamond kwa picha.

Mamake Diamond aliambia Soudy Brown kuwa yeye anapatana tu na Zari ambaye amemletea wajukuu wala hana lolote na warembo wengi wote wanaohusishwa na Diamond.

Skila mahojiano kati ya Soudy Brown na mamake Diamond hapo chini:

https://www.youtube.com/watch?v=jnG2h6EG32E