Ommy Dimpoz Uso kwa Uso na Steve Nyerere

Msanii wa maigizo ya bongo movies Steve Nyerere amekutaja uso kwa uso na msanii Ommy Dimpoz tangu ilipotokea mfarakano kati yao na kusababisha wawili hao kama kurushiana maneno katika mtandao wa kijamii.

Steve Nyerere aliwahi kusema maneno flani kuhusu hali ya kiafya aliokuwa nayo msanii huyo na hata Ommy aliporejea katika hali yake ilikuwa ngumu kwa Steve Nyerere kujitetea lakini alikiri na kuomba msamaha.

Hata hivyo wawili hao wameweza kukutana katika msiba wa Ruge Mutahaba na kuonekana wenye furaha na hakuna alieyekuwa na kinyongo na mwenzake kabisa

Moja ya wasanii aliowakuta pamoja alikuwa RIYAMA ALLY ambae alisema kuwa amefurahi kuona wawili hao wakiwa pamoja na kuwa wako sawa.

 

Steve Nyerere: Dudubaya Aombe Msamaha na Atengwe

Msanii wa Bongo movie Steve Nyerere ameibuka na kumtolea Povu zito Msanii wa Bongo fleva Godfrey Tumaini maarufu kama Dudubaya Baada ya kutoa maneno na Chafu dhidi ya Marehemu Ruge Mutahaba.

Steve Nyerere, amesema kama kuna msanii anamzungumzia vibaya marehemu Ruge Mutahaba kwa sasa jkama anavyofanya Rapa Dudu Baya basi anapaswa kutengwa kwani hakuna binadamu aliye mkamilifu.

Steve amesema Ruge amefungua milango kwa vijana wengi na kutoa fursa waweze kufanikiwa huku akiweka wazi kuwa atamkumbuka milele.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Steve ameongea haya:

 

Steve Nyerere Awataka Watu Waache Kuibua Mabaya Ya Ruge na Kumsaidia

Msanii wa Bongo movie na mdau wa mambo ya siasa Steve Nyerere ameibuka na jipya Safari hii aewataka watu wenye ubaya na Mkurugenzi wa CMG Ruge Mutahaba kuweka pembeni na kumsaidia katika kipindi hiki cha shida.

Kupitia ukurasa wa instagram wa Steve Nyerereamesema kuwa  Ruge aliweza kupaza sauti za wasanii bila kujali ana kipaji cha kuimba, utangazaji, riadha, taarabu, bendi na inabidi watu wakumbuke kuwa Ruge alisimama kutetea na kutoa nafasi kwa kila msanii.

Maisha yanavozidi kwenda kwa kasi ndipo unapogundua una rafiki SHETANI, maana wengi uvumilivu na neno msamaha kwao gumu, Mama aliniambia ukijua kusamehe BASI wewe ni MTU unayeweza kuishi popote, Ivi Nani kama RUGE, Upande wa Michezo hakuna narudia hakuna, Ruge alifungua milango kwa vijana, Aliweza kuwambia vijana mimi sina hela ya kukupa lakini kipaji chako ni hela zaidi ya kwangu mnayotaka kukupa, Ruge aliweza kumwambia kila msanii kauli mbiu jitambue wewe nani”

“Ruge aliweza kupaza sauti ya wasanii bila kujali una kipaji cha kuimba, Ama ngumi, Kwaya, Utangazaji, Riadha, Taarabu,Bendi nk, Ruge alisimama kutetea na kutoa nafasi kwa kila msanii mwenye kuonyesha nia, kwenye kazi yake, Sisemi Ruge kuwa hana mabaya hapana, bali nawaza mazuri yake maana naona yana Faida sana kwa binadamu mwenye kujua kusema neno asante, RUGE Ruge”

“Watanzania wapo milioni 57 ,Vijana peke yao wapo milioni 33 ,Kama aliweza kufungua njia hata ya Vijana milioni 10 tu huyu ni MTU wakumwambia Asante, Ruge, Maana hasinge weza watoa WOTE, Ntashangaa kuona hata watu waliokuwa na majina makubwa leo wakisema RUGE BORA AFE ,kwa kipi Tunasahau alitupa ndoano tukavue samaki na tukavua samaki”

“Badala ya kwenda kuuza samaki wale tulio vua, Tukala wenyewe sasa tunalaumu nini, mbona wakati tumeshiba samaki hakukuwa na tatizo, RUGE nawaza cha kukufanyia najiona nisipo jitoa kwako basi Sijatenda haki, Hakuna mkamilifu DUNIA HIIII, Tusameane kutokana na matatizo yetu, SASA ivi mimi nilizani tunaomba DUA au kuandaa kisomo kwa RUGE AMA MISA KWA RUGE, mimi nilidhani tunasimama kila mmoja KWA uwezo wetu kuangalia jinsi ya kumsaidia Ruge”

“Mimi nilidhani Tunafanya Tamasha ama kufanya kitu kikubwa kwa ajili ya RUGE, Sio muda wa kufukua makaburi huu ni muda wa kusema KAKA amka RUGE, kwa pamoja tunaweza sana Upendo ukiwa mkubwa hata mafanikio ya sanaa yataonekana, RUGE anamema sana kwako wewe msanii kuliko mabaya unayo nena leo”.

Wellu Sengo Amkingia Kifua Steve Nyerere

Muigizaji wa Bongo movie Wellu Sengo ameibuka na kumkingia kifua Baba Watoto Wake Steve Nyerere kwa kusema haoni tatizo kwa mambo yake anayoyafanya mitandaoni hasa kuropoka juu ya ishu za mastaa wenzake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Wellu alisema kuwa hawezi kupitia kila anachokifanya Steve mitandaoni ila kama kuna kitu anaona kina tatizo, huwa anamshauri.

Sioni sababu na siwezi kupitia kila kitu anachokifanya Steve mtandaoni. Unajua kila mtu ana hulka yake, labda na yeye ndivyo alivyo. Kwa hiyo mimi huwa naangalia vitu muhimu kama anakosea ndiyo tunakaa, tunashauriana“.

Stwvw Nyerere amekuwa akipingwa sana na mashabiki wengi wa Mitandao kutokana na misimamo yake ya kisiasa Lakini pia Hivi karibuni alipatwa na Skendo ya mwaka Baada ya kutoa kauli kuhusu Ommy Dimpoz kuwa hatoweza kuimba tena.

Maneno ya Mitandao Yamrudisha Nyuma Steve Msiba wa Godzilla

Maneno ambayo yamekuwa mengi katika mitandao ya kijamii kuhusu msanii Steve Nyerere kuwa akitumia sana misiba na kupata michango ambayo mwisho wa siku inakuwa ikimnufaisha mwenyewe  imekwamisha maswala mengi sana katika kufanikiwa katika mazishi ya wasanii wengi na hata huu wa msanii Godzilla.

Steve Nyerere kwa sasa amekuwa kimya na amekuwa kama muuzuliaji tu katika misiaba na kujiweka pembeni ilhali kulikuwa na haja ya kujihusisha na misiba ya wasanii wenzake kwa sababu amekuwa na ushawishi mkubwa katika kufanikisha mambo mbalimbali.

Msanii huyo alipopata taarifa za msiba wa Godzilla , hakutaka kujihusisha sana zaidi ya kuonyesha kuwa hata yeye ameguswa na msiba na kuamua kuweka post kaushiria pole yake kwa familia kumpoteza msanii huyo lakini bado  wapo walioamua kumshambulia msanii huyo na kumwambia kuwa amekuwa akijinufaisha na misiba.

Hata hivyo umuhimu wake unaonekana kwa sababu bado wapo wanaohitaji msaada wake katika misia ba hata huu wa Godzilla lakini amekuwa kimya na hataki kujihusisha na kitu chochote.

 

Steve Nyerere Apitia Kipindi Kigumu Sakata la Ommy Dimpoz

Msanii wa Bongo movie Steve Nyerere amejikuta katika kipindi kigumu Baada ya kusema kuwa Ommy Dimpoz hataweza kurejea na kuimba vizuri kama zamani kwa kuwa hali yake kiafya si nzuri,

Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amejikuta akikaliwa kooni baada ya mashabiki wa Dimpoz kumjia juu na kumtaka atengue kauli yake kwani haikuwa nzuri hasa kwa Ommy Dimpoz ambaye anaumwa.

Gazeti la Ijumaa, Ommy Dimpoz alisema kuwa alichokizungumza ni kwamba, Dimpoz atachukua muda kurejea katika gemu tofauti na jinsi watu walivyomtafsiri kwamba hataweza kuimba kamwe.

Narudia kauli yangu nilisema hivi, atachukua muda kurudi katika gemu, kwa sababu hakuna mtu ambaye hajamuonea huruma Dimpoz wakati anaumwa, wote tulihuzunika, kwanza ni kijana mdogo amepita katika misukosuko mikubwa sana ya kimaradhi kwa hiyo sisi wote kama vijana tulimuonea huruma, ilitupasa sisi kama wasanii wenzake tuungane naye katika kipindi kile alichokuwa anapitia, lakini tunaamini kabisa kwamba itamchukua muda kurudi kwenye gemu na ndiyo kauli niliyosema mimi.

“Ni sawasawa na kocha akuambie kwamba itakuchukua muda kurudi kucheza mpira, kwa hiyo hayo maneno yanayosambaa huko mitandaoni sijui Steve kafanya hivi, sijui kafanya vile hayaniumizi kichwa hata kidogo, sina mamlaka ya kusema kwamba hataimba milele, mimi ni nani?”.

 

Steve Nyerere Aomba Msamaha kwa Ommy Dimpoz

Msanii wa maigizo nchini Steve Nyerere , amefunguka na kuamua kufunguka kuhusu swala lililokuwa limezuka na kusambaa sana katika mitandao ya kijamii kuhusu ommy dimpoz.Steve Nyerere, amefunguka na kuomba msamaha kwa Ommy dimpoz hasa baada ya kauli yake aliyowahi kusema wakati msanii huyo akiwa hospitali akiwa anaumwa.

Steve alisikika akisema kuwa Ommy Dimpoz hawezi kuimba tena kutokana na malazi yanayomsumbua na kwamba hata kama aatapona lakini hawezi kurudi katika muziki kitu ambacho baada ya ommy kutoka aliweza kujibu maneno ya watu kama Steve kwa kutoa wimbo mpya .

Hata hivyo , Ommy alipoulizwa kuhusu kauli ya Steve hakuonekana kukwazika sana ingawa maneno katika mitandao ya kijamii yalizidi kufanya watu kuwa na tension kubwa sana.

hivyo Steve ameamua kuomba msamaha kwa msanii huyo kwa kisema kuwa wakati anasema hakukusuduai kile ambacho wengine wamekipokea zaidi ya kuwa mitandao wamekuwa wakizidisha chumvi.

Katika ukurasa wake wa instagram alielezea maengi kuhusu kauli hiyo lakini kitu cha mwisho kabisa alikubali kosa hilo na kukiri lakini pia aliomba msamaha kwa kusema

Nakiri kukosea kutokana na ile kauli yangu zidi ya Ommy Dimpoz.

Steve Nyerere Apangua Tuhuma za Kutabiri Kushuka kwa Ommy

Msanii Steve Nyerere amefunguka  baada ya kuandamwa sana katika mitandao ya kijamii kuhusu kauli yake ya kuwa  Ommy dimpoz hawezi kuimba tena kwa sababu ya upasuaji aliofanya nchi Afrika ya Kusini.

Msanii huyo ambae aliwahi kuojiwa akiwa kama moja ya watu wanaoshughulikia sana matatizo ya wasanii alisikika akisema kuwa Ommy hawezi tena kuimba kwa sababu koo lake halina tena uwezo huo kutokana na malazi  yanayomsumbua.

Hata hivyo msanii huyo amerudi kutoka katika matibabu hivi karibuni na kusema kuwa maneno hayo aliyasikia lakini anaamini kuwa hiyo ni moja ya changamoto anazop[itia kikubwa anamshukuru mungu kwa kuwa amefanya arudi tena katika kazi yake.

Hata hivyo steve anasema kuwa walimnukuu walinukuu vibaya kwa saabu yeye alisema kuwa Ommy hatoiweza kuimba kwa sasa mpaka pale atakapo-recover, kitu ambacho kiliibua hisia sana kwa mashabiki wa muziki nchini.

Hata hivyo msanii huyo pamoja na kutabiriwa mengi mabaya , bado ameweza kuimba tena .

Steve Nyerere Afungukia Sakata Lake na Ommy Dimpoz

Msanii wa Bongo movie ambaye ni maarufu kwa kuiga sauti za viongozi mbali mbali w serikali, Steve Nyerere amefunguka na kuongelea skendo inayomuandama hivi sasa dhidi ya Msanii wa Bongo movie Ommy Dimpoz.

Siku za nyuma kidogo Steve Nyerere alifanya mahojiano na kituo kimoja cha habari na kusema Ommy Dimpoz hawezi kuimba tena kwa sababu ya hali ya ugonjwa wake, huku akiwaomba Watanzania kumuombea na kuwa naye karibu ili apate faraja na kupona.

Baada ya sakata hilo Steve Nyerere ameibuka na kusema maneno hayo yanayosambazwa hayana ukweli kwani yeye hakusema hataweza kuimba kabisa bali alisema hataweza kuimba kwa wakati ule.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Millard Ayo, Steve Nyerere amefunguka haya:

Kwanza niseme kuwa yupo kwenye dunia ya kubadilisha maneno na ya kugombanisha watu, Mimi sipo huko…Unapomzungumzia Steve Nyerere unakuwa unazungumzia brand , mzigo mkubwa sana usikaone hivi”.

Siachagi kunukuu kitu nilichokisema, nilisema hatoweza kuimba tena kwa muda huu, Aki-recover sijui mnaelewa maana ya ku-recover”.

Ommy Dimpoz ameweka wazi kuwa ameshangazwa na kauli ya Steve Nyerere kuwa kutokana na ugonjwa Wake hatoweza kuimba hasa ukizingatia Steve hajawahi kumtafuta kumjulia hali kipindi chote alivyokuwa mgonjwa.

 

Wasanii 300 Kutembelea Ujenzi wa Reli ya Kisasa.

Wasanii 300 kutoka katika makundi ya sanaa wanatarajiwa  k kufanya ziara ya kuangalia ujenzi wa reli ya kisasa kutoka jijini Dar es salaam mpaka Morogoro.

Akiongeana waandishi wa habari kiongozi wa wasanii na mratibu wa safari hiyo bwana Steve Nyerere anasema kuwa safari hiyo itawahusisha wasanii wote wa muziki, bongo movies, wacheza mpira na kila kundi linalohusu sanaa na burudani.

Steve anasema kuwa safari hii ni moja ya matokeo chanya ya kikao chao kilichofanyika wiki iliyopita kati yao na mkuu wa mkoa huo.safari hiyo inategemea kuanza asubui na kupitia maeneo yote ambapo reli hiyo inapita.

Ommy Dimpoz Akiri Kushangazwa na Maneno Ya Steve Nyerere

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz amefunguka na kuweka wazi kuwa ameshangazwa na maneno ambayo Msanii Steve Nyerere alisema Juu yake.

Kwenye mahojiano aliyofanya siku za nyuma na chombo kimoja cha habari, Steve Nyerere aliibuka na kusema Dimpoz hawezi kuimba tena kwa sababu ya hali ya ugonjwa wake, huku akiwaomba Watanzania kumuombea na kuwa naye karibu ili apate faraja na kupona.

Ommy Dimpoz amemjia juu Stevw Nyerere juu ya kauli hiyo na kumtaka awe makini na maneno yake kwani hajawahi hata siku moja kumpigia simu na kumjulia hali hivyo asingeweza kujua afya yake.

Muda mwingine tunapaswa tuzitumie vizuri hizi kamera, kama kuna kitu huna uhakika ni vizuri usikizungumze, ungeweza hata kunitafuta kwanza, ila mimi sina tatizo nae, alijikwaa tu”.

 

Wakazi Amhoji Steve Nyerere Kama ni Msanii Au Mwanasiasa

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Wakazi Music amemjia juu msanii wa Bongo fleva na mwanaharakati wa mambo ya siasa Steve Nyerere kutokana na kauli alizotoa.

Sakata hilo limetokea siku chache zilizopita baada ya Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda kuanika wasanii katika mkutano Wake na wasanii wachache kujitokeza.

Wasanii wengi waliweka wazi kuwa hawakuenda kwenye mkutano huo kutoka na kwamba hawakupata mwaliko rasmi zaidi ya kuona matangazo kwenye Mitandao ya kijamii.

Stevw Nyerere ambaye alikuwa mratibu wa Shughuli hiyo amewajia juu wasanii ambao Hawakufika kwenye mkutano huo Mpaka kufikia hatua ya Kuwaita Madodoki.

Wakazi amemjia juu Steve Nyerere kwa kauli yake hiyo na kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika maneno haya:

https://www.instagram.com/p/BtYAjLZFFpb/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=17yqbv5ow4sx6

Kisa Steve Nyerere, Makonda Awashushua Wasanii.

Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda amewatolea povu wasanii wote ambao wamekuwa na tabia ya  kumsema vibaya Steve Nyerere na hata kumuita bwana mipango   na kwamba ni tapeli na kusahau kuwa wao ndio wamekuwa wakimtumia huyo huyo kuomba misaada kwake.

Paul Makonda anasema kuwa amekuwa akichukizwa sana na tabia ya baadhi ya wasannii kufanya na kuongea kashaf kwa steve nyerere wakati wasanii wengi sana wanapokuwa na shida wamekuwa wakimtumia msanii huyo ama daraja ya kutaka kufanikisha matatizo yao.

Akitolea mfano, mkuu wa mkoa anasema kuwa wapo waliowahi kukamatwa na wamekuwa na tabia ya kumuomba steve kuongea na mkuu wa mkoa ili wapate wepesi wa makosa yao.

Ikumbukwe kuwa steve nyerere amekuwa akiandamwa mara nyingi hasa kutokana na kujitoa kwake huku wengi wakisema amekuwa akifanya hivyo kwa ajili ya maslahi yake.

Steve Nyerere Amtaja JB Kuwa ‘Bodyguard’ Wake

Muigizaji wa Bongo movie ambaye amebobea kwenye kuingia sauti za viongozi mbali mbali wa siasa Steve Nyerere ameibuka na jipya hivi karibuni Baada ya kudai msanii mwenzake JB ni mlinzi wake.

Gazeti lab ijumaa linaripoti kuwa Tukio hilo lilijiri katika Hoteli ya Hyatt Regency, Posta jijini Dar kulipokuwa na hafla ya kuzindua taasisi ya kusaidia watu wenye ulemavu wa ngozi pamoja na bidhaa ya manukato ya De La Boss iliyoandaliwa na Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara.

Katikati ya hafla hiyo, Steve aliyekuwa ameongozana na JB alijigamba mbele ya watu kuwa kwa sasa analindwa naye jambo liliolofanya wengi kuangua vicheko.

Nina bodigadi huyu hapa (JB) na mimi nimekuwa mmojawapo kati ya wanaolindwa”.

Katika kuonyesha tukio hilo lilikuwa la utani Steve alionekana kumtaka JB amsogezee gari lake ili kumuiga Diamond ambaye alionekana na mabodyguard wawili na walionekana kumfungulia milango ya gari, JB aligoma na kila mmoja kuondoka kivyake.

Steve Awajibu Walimtaka Kupitia Michango ya Msiba wa Pasha wa Sultani

Jina la Mwigizaji Steve Nyerere limerudi kwenye headlines kwenye mitandao ya kijamii hii ni baada ya kupokea jumbe za utani za baadhi ya mashabiki kuhusiana na kifo cha Ibrahim Pasha kupitia tamthiliya ya Sultan inayooneshwa na Azam TV.

Kupitia caption aliyoiandika Steve Nyerere kwenye ukurasa wa instagram unaonyesha kuwa mashabiki wamemtaka aanzishe mchango kutokana na wengi kudai kuwa Misiba mingi ya wasanii, Steve huwa anakuwa katika mstari wa mbele wakidai kuhamasisha upatikanaji wa michango.

Pasha amefariki lakini kufariki kwa Pasha ni katika tamthilia ya Sultan, hivyo Steve ameamua kuwajibu wale wanaomtania kuwa aanze utaratibu wa kuratibu mazishi ya Pasha “Nimeona sms zenu kuhusu ibrahim pasha , Nimebaki nacheka TU mitandao hiii DOOO, Aya jibu lenu ni hili Wasaniii Wote tukutane lidas fyuuuuuuuuuuuuuuuuuuu Ila niacheni KIDOGO nipumue kaaaaaaaa”

Steve Nyerere Adai Kutishiwa Kuuawa na watu Wasiojulikana.

Msanii wa bongo movies Steve Nyerere amefunguka na kusema kuwa kuna watu wasiojulikana wamekuwa wakimtishai kumuu a hivi karibuni, na ni watu ambao wanaonekna kuyafatilia maisha yke na kuyajua kiundani  zaidi.

Steve Nyerere anasema kuwa amekuwa na maisa ya wasiwasi na kuwa kama yatima kwa sababu kuna watu wamekuwa wakija mpaka nyumbani wakimtafauta na hata kumtumia meseji za vitisho katika simu yake.

Steve Nyerere anasema kuwa amekuwa na maisha ya wasiwasi na wala hajui kesho yake lakini kitu kikubwa amekuwa akiwaza sana juu ya familia yake tena hasa watoto wake ambao bado wamekuwa wakimuhitaji sana.

Steve anasema kuwa amekuwa akiipenda sana Tanzania na anachoamini kuwa hata hao wanaofanya hivyo wanamjengea ujasiri wa kujiamini na kupambana pia.

Steve amekuwa moja ya msanii anaekumbana na upinzani hata kutoka kwa wasanii wenzake mara nyingi kutokana na sababu mbalimbali na hata kufikia hatau ya kuwa wakirushiana maneno katika mitandao ya kijamii.