Mpenzi Mpya wa Hamisa Amuumbua Tahiya.

Mwanaume anaesadikika kuwa na mpezi mpya wa Hamisa Mobeto amefunguka na kuonyeshwa kukerwa na tabiaya wanadada Tahiya ambae ni video queen na model kuwa amekuwa akitangaza kama bado wapo katika mahusiano ya kimapenzi wakati walishaachana siku nyingi.

Mwanaume huyo anasema kuwa anamuomba dada huyo kuacha kufanya hivyo anavyofanya kwa sababu wao tayari walishaachana siku nyingi na wala hukana haja ya kuwaaminisha watu kuwa wapo pamoja.

Ikumbukwe kuwa wiki chache zilizopita mwanadada tahiya aliwahi kumtuhumu Hamisa kuwa amemuibia mpenzi wake na kwenda nae Zanzibar ambap baadaya hayo jamisa aliamua kumtambulisha mwanaume huyo.

Siku hizi mbili zilizopita, katika ukurasa wake wa snap , mwanadad tahiya aliamua kuweka picha ya saa ya mwanaume huyo kuonyesha kuwa wawili hao wapo katika mahusiano, hivyo kiajana huyo aliamua kukanusha .

Alichopost Tahiya katika ukurasa wake

Alichojibu kijana huyo baada ya kuona post ya Tahiya

 

Hamisa Mobetto Afungukia Skendo Ya Kuiba Bwana Wa Mtu

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Hamisa Mobetto ambaye Wiki iliyopita aliingia kwenye headlines Baada ya kudaiwa kuiba bwana wa mrembo aitwaye Tahiya.

Tahiya ambaye ameshawahi kutajwa kuwa kwenye mahusiano na Diamond, alimtuhumu Mobetto kwa kumchukulia bwana ake anayeitwa Alex ambaye anatajwa kuwa mtoto wa Kigogo mmmoja hapa nchini.

Kushoto: Hamisa Akiwa na Alex Kulia: Tahiya Akiwa na Alex

Tahiya  aliposti picha ya Mobeto kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuandika maneno haya; “Hamisa Mobeto achana na wanaume za watu.”

Baada ya muda mwanadada huyo akaposti tena meseji zao zote alizokuwa wakijibizana na mwanamitindo huyo kwenye mtandao wa WhatsApp ambapo Tahiya alionekana akimsihi Mobeto aachane na mpenzi wake lakini haikusaidia kwani mwisho wa waliishia kujibizana maneno mabaya huku kila mmoja akijiona anaweza zaidi ya mwenzake.

Baada ya skendo hiyo kutawala mitandao ya kijamii Gazeti la Risasi Mchanganyiko lilimsaka Hamisa Mobetto ili kupata Ukweli kwa upande Wake ambapo alifunguka na kusema:

Mnataka niwaambie nini, mlichokiona ndiyo hichohicho isitoshe mimi siyo mtoto mdogo kwa hiyo naelewa ninachokifanya, sijaiba mwanaume wa mtu ila alikuja mwenyewe na nampenda nifanyeje sasa”.

 

 

“Siwezi Kupiga Picha Za Uchi”- Tahiya

Socialite maarufu Kwenye mitandao ya kijamii Tahiya amefunguka na kuweka wazi kuwa kitu ambacho hawezi kufanya ni kupiga picha za uchi na kuziweka Kwenye social media.

Tahiya ambaye alijizolea umaarufu baada ya skendo ya kutoka kimapenzi na staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amesema yeye ni mwanamke anayejiheshimu hivyo hawezi kupiga picha za utupu:

Tahiya amefunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na Planet Bongo ya East Africa Radio  na kufunguka haya:

Huwezi kuniona mimi Instagram nimeposti picha ya uchi wala kuniona nimemtukana mtu wala kufanya vile vitu vya ajabu ajabu kwa sababu mimi ni mtu ambaye najielewa na najua nataka nini.

Najua miaka mitano kutoka sasa nataka kuwa wapi ndio maana natengeneza mazingira mazuri hivyo watu watanijua kama Tahiya Mrembo lakini sio kwa kiki za picha uchi.

Lakini pia Tahiya amewaasa wasichana kuwa makini na picha wanazoweka Kwenye internet kwani ni vitu vinavyoweza kuwaathiri baadae hata vizazi vyao.

Tahiya Amuomba Msamaha Zari Baada Ya Video Yake Yenye Utata na Diamond Kusambaa (video)

Mwanamitindo na mrembo anayejulikana kama Tahiya amekiri kuwa alimuomba msamaha mpenzi wa Diamond, Zari baada ya video yao kusambaa.

Wiki chache zilizopita video clip iliyomuonyesha Tahiya akiwa na mkali katika muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz wakiwa wamekumbatiana kimahaba kusambaa na kusababisha sintofahamu. Baada ya kuhojiwa Tahiya alikataa kuwa na uhusiano wowote na Diamond huku akidai kuwa Diamond ni ndugu yake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Dizzim Online, Tahiya aliweka wazi kuwa yeye ndugu wa Diamond kwahiyo hakuna kitu chochote kinachoweza kuendelea baina yao na anamuheshimu Zari kama make halali Diamond;

Unajua mimi nina ukaribu na Diamond kwa hiyo watu walivyoniona kwenye birthday yake na mimi kuwa karbu naye watu wakachukulia vibayq ila kitu watu hawajui Diamond ni mtu poa sana ni mtu wa famiia, hata Zari hakuwa na neno na ile video ila zaidi ya hapo watu wanatakiwa wajue kuwa namheshimu sana Zari na pia namheshimu Diamond na kwa ujumla nawaheshimu kama mume na mke na kama Zari amechukulia vibaya ile video naona ni muda nimuombe msamaha kwa ile video, ila sikutegemea Kama watanzania wanaweza kuikuza ile ishu”.

Pia Tahiya alikataa tuhuma alizorushiwa kuwa alionekana amelala nyumbani kwa Diamond Madale .

Hii ndio Video ya Diamond na Tahiya iliyozua haya yote: