Hili ndilo jambo Tanzania yaongoza Afrika Nzima

Tanzania imechangia asilimia 19.3 ya jumla ya wageni wa kimataifa kupitia anga (international air arrivals) ukilinganisha na asilimia 18.2 ya Kenya, asilimia 17.2 Misri na asilimia 12.1 ya Afrika Kusini katika kipindi cha kuanzia September 2016 hadi January 2017.

akwimu hizi ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la ufuatiliaji wa masuala usafiri wa ndege, ForwardKeys ambayo hulinganisha ukataji tiketi za ndege zaidi ya milioni 16 kila siku ili kuiweka Afrika kwenye ramani ya utalii duniani.

Kwa jumla, Afrika Mashariki ina asimilia 16.4 ya ufikaji wa wageni kwa njia ya anga. Na kwa ujumla pia, kuna ongezeko la asilimia 10.3 ya ufikaji wageni Afrika. Soma zaidi ripoti hiyo hapa.