Ali Kiba Ndani Ya Ngoma Moja na Timaya Wa Nigeria

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Ali Kiba amepata shavu la maana Baada ya kushirikishwa kwenye Albamu mpya ya Msanii wa muziki kutoka Nigeria Timaya.

Album mpya ya staa Timaya wa Nigeria inayoitwa Chulo Vibes’ ikiwa na jumla ya ngoma tisa ambapo imewashirikisha wasanii tofautitofauti akiwemo BurnaBoy,Machel Montano.

Kupitia ukurasa wa instagram wa Timaya ameweka cover ya Album yake bila kutaja tarehe rasmi ya kuichia sokoni huku ngoma yake na Alikiba ‘Number One’ ikishika nafasi ya tano ndani ya Album hiyo.

https://www.instagram.com/p/BtkgvsoAKTG/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=qumrgkjw6lre

Ali Kiba Kufanya Kolabo na Staa Kutoka Nigeria

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini Ali Kiba amethibitisha kufanya kazi na staa wa mkubwa wa muziki kutoka Nigeria anayejulikana Kama Enitimi Alfred Odom ’Timaya’.

Msanii huyo amempa shavu staa wa Bongo fleva Ali Kiba kwenye EP  yake ya ‘Chulo Vibes’ ambayo inategemewa kuingia sokoni ndani ya mwaka huu.

Tanya amethibitisha taarifa hizo ukurasa wake wa Instagram ambapo aliandika maneno haya:

My BROTHER @officialalikiba from TANZANIA came through on the EP. CHULO VIBES is ???”.