Tunda Amuombea Amber Rutty

Mwanadada ambae amekuwa na jina kubwa kutoka ana kazi yake ya kuwa video vixen katika video za wasanii mbalimbali , TUNDA ,  amefunguka na kusema kuwa wa sasa amekuwa muoga sana wa kufanya kitu chochote .

Tunda anasema kuwa anawaombea sana watu wanaofanya hivyo  kwa sababu hawajui lile walitendalo lakini pia anaomba hata Mungu awaongoze ili wasitake kurudia tena , na kwa upande wa Amber Rutty anasema hawezi kumsema kitu lakini anaamini kuwa mwanadada huyo kwa sasa atakuwa akipitia katika wakati mgumu.

Tunda anasema kuwa kwa sheria kali zilizopo sasa hii nchini inakuwa kazi  sana hata kwake kufanya vitu anavyoviita yeye kuwa ni vya kipumbavu kwa sababu anaogopa hajui nini  kinaweza kumpata .

Kama inakumbukwa , tunda aliwahi kuvujisha pia picha na video akiwa faragha na moja ya vigogo nchini lakini alijitokeza yeye na mhuiska na kuomba msamaha  na tangu hapo mwanadada huyo anasema kuwa amejifunza sana.

 

Tunda Atupa Jiwe Gizani Likimlenga Casto Dickson.

Mwanadada casto dickson ametupa jiwe gizani lakini jiwe hilo linaonekana kuwa na lengo la kumpiga Casto dicksona ambae alikuwa mpezi wake na kwa sasa wamekuwa hawaonekana kuwa pamoja tena kitu ambacho hata Casto mwenyewe amekuwa akikanusha kuwa hawajaachana lakini Tunda hajawahi kuongea kuhusu swala hilo.

Casto mabae mara nyingi amekuwa hataki kuonyesha wazi kuwa ameachana na Tunda amekuwa akikanusha swala hilo katika mitandao na hata anapokuwa katika mahojiano mbalimbali.

Katika ukurasa wake wa instagram, tunda aliweka picha yake huku akiwa ameandika caption yenye aneo kuntu kuhusu mahusinao hasa kwa watu walioachana huku mmoja wapo akionekana kutokubaliana na kuachana kwao.

Mwisho kabisa Tunda aliandika kuwa ukiachwa achika ikiwa kama ujumbe kwa mwanaume aliyekuwa nae katika mahusiano ambapo kwa hapa karibuni tu nda alikuwa katika mahusiano na Casto.

Huwa Nam-miss Sana Tunda:-AbdulKiba

Pamoja na kwamba sasa hivi inasemekana kuwa anatoka na mwanahabari Casto Dickson,lakini mwanadada Tunda ametwaja kuwa ndio mwanamke ambae hawezi kusahahulikana na msanii Abdul Kiba ambae ni mdogo wake na Ali Kiba.

Abdul Kiba alikiri kuwa katika mahusiano yake yote aliyowahi kuwa nayo, mahusiano ambayo hatokaa hayasahau ni  ya mrembo tunda ambae alidumu nae kwa muda wa miaka miwili .

Mahusiano ambayo sitakaa niyasahahu ni kipindi nipo na Tunda,kwanza tukikutana kupitia social network na nilimuelewa na yeye alinielewa na tukaweza kukutana, na tukaweza kuwa kitu kimoja ingawa ni muda kidogo kwa zaidi ya miaka mitatu hivi.

Abdul Kiba ansema kuwa ilikuwa ni vigumu sana kwa watu kushtukia kwa sababu ana kipindi hicho tunda alikuwa sio mtu wa kutoka toka kwa sababu alikuwa akikutana nae alikuwa ni mtu wa kukaa ndani au kwenye gari tu.

siko nae tena kwa sasa lakini tulikaa kama miaka miwili hivi ni haikuwa public sana ingawa kuna watu walikuwa wanajua lakini ilikuwa ngumu sana kushtukia kwa sababu hata tulikuw atukikutana ilikuwa muda mwingine anakaa tu kwenye gari.

inatokea kum-miss kwa sababu unapomuona kwenye mitandao alafu ulishawahi kuwa nae , kwaio inatokea.

Tunda Afunguka Skendo ya Kutoa Mimba Zaidi ya Nane

Baada ya picha nyingi kusambaa za mrembo Tunda akionea kuwa karibu na moja ya watangazaji wa vipindi pendwa vya Clouds Tv ,  Casto Dickson maarufu kama Sizkitaa, na kuonyesha kuwa mrembo huyo ni mjamzito , Tunda akumbwa na skendo ya kuwa anatoa mimba nyingi kila anapopata mimba na kusemekana kuwa mimba hizo zimeshafika nane mpaka sasa.

Akizungumza na Risasi, Jumamosi ya wikiend iliyopita mwanadada huyo amesema kuwa sio kweli kuhusu tuhuma hizo kwasababu hajawahi kutoa mimba hata siku moja.tunda nasema kuwa hata kama wanamzushia skendo kama hiyo haiwezekani mtu mmoja kutoa mimba zaidi ya nane.

Jamani kweli mtu anaweza kutoa mimba nane tena kwa kipindi cha muda mfupi tu,sidhani kama unaweza kuwa binadamu sahihi kabisa na binafsi sijawahi kutoa mimba kama watu wanavokuwa wanadai.

Tunda nasema kuwa inawezekana watu wanakwa wanamsema kutokana nkuwa tumbo lake kwa kipindi kirefu limekuwa  kubwa hivyo wakawa wanahisi hivyo  lakini kua kipindi amekuwa akifanya mazoezi na linapungua.

Hili tumbo wanaweza kuwa wanalishangaa lakini ni kubwa siku zote liko hivyo tena hasa kama sijafanya mazoezi muda mrefu na pia sijinyimi kwenye kula chakula kabisa, linakuwa kubwa .

Lakini pia tunda anasema kuwa watuwamekuwa wakimsingizia lakini yeye mwenyewe wala hajawahi kushika mimba hata mara moja “mimi napenda watu wafahamu kuwa sijawahi kushika mimba ya mtu yeyote kama wanavyosema  siku zote na wala sijawahi kutoa maana tumbo langu ndivyo lilivyo.”

Kwa kuonyesha kujiamini kabisa Tunda aliamua kumuweka wazi mtu ambae kwa sasa yupo nae katika mahusiano kuwa ni casto dickson.”kwa sasa hivi mtu wangu ni  Casto Dickson, maneno mengine sitaki kabisa kuyasikia kwa sababu huyu ndo natarajia kuzaa nae.”

Tunda Amuomba Msamaha Aunty Ezekiel Baada Ya Kumtukana Mtoto Wake

Video vixen na Socialite maarufu Tunda Sebastian amefunguka na kumuomba radhi msanii wa Bongo movie Aunty Ezekiel baada ya kumtukana mtoto wake na Mose Iyobo, Cookie.

Miezi michache iliyopita kulizuka bonge valangati baada ya Aunty Ezekiel kumuashia dude Tunda ambapo alienda kwenye ukurasa wake instagram na kumdai pesa yake aliyomkopesha pombe dukani kwake.

Baada ya hapo walianza kurushiana maneno ya kejeli na matusi hata Tunda alifikia hatua ya kumtukana mtoto wa Aunty Ezekiel ambapo alimuita mtoto wake kuwa ni mtoto mbaya dunia nzima.

Wikiendi iliyopita Tunda amemuomba msamaha Aunty Ezekiel kwa kumtukania mtoto wake na kudai kuwa zilikuwa ni hasira tu na hakupanga kumtukana mtoto wao.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Tunda alimuandikia Aunty ujumbe huu:

 

Kwa kipindi kirefu Kumekuwa na tetesi kuwa Tunda ni mjamzito na alithibitisha kuwa ni mjamzito kwa kuandika “Naomba msamaha kama mwanamke ambaye nitaitwa mama pia soon”. 

Kwa habari za chini ya kapeti zinadai kuwa ujauzito huo ni wa miezi mitatu na inasemekana kuwa baba wa mtoto huyo ni mtangazaji za Clouds Tv Casto Dickson ambaye ni Baba mtoto wa Munalove ambaye ni rafiki wa Tunda.

“Wanawake Tuache Majungu na Wivu Tusapotiane”- Tunda

Socialite na video vixen maarufu Tunda Sebastian amefunguka na kuwasihi wanawake wapendane na wapeane sapoti badala Kupikiana majungu na kuoneana wivu.

Tunda alijipatia umaarufu zaidi wiki chache zilizopita baada ya taarifa kutoka kimapenzi na Diamond Platnumz kuenea Kwenye mitandao ya kijamii na baadae video na picha za kimahaba akiwa na mume wa mtu mfanyabiashara Kinje kuenea mtandaoni pia.

Ikiwa jana ilikuwa ni siku ya kusheherekea siku ya Wanawake duniani Tunda amewapa ujumbe huo mzito wanawake Akiwasihi washike upendo na waachane na chuki kwa kushikiliana na kupeana sapoti ya hali ya juu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Tunda aliandika ujumbe huu:

Women today we need to be supporting each other to set an example for the next generation….Sio mawili tu na majungu bila mwisho… Happy Women’s day”.

Tunda Akiri Kuogopa Kumuongelea Tena Zari

Mrembo Tunda Sebastian ambaye ni Video queen maarufu amefunguka na kusema hatokaa kumuongela Zari wala kuvunjika kwa penzi la Diamond na Wema.

Tunda amedai amefikia uamuzi huo baada ya kukiri kuoga mvua ya matusi kila mara akifungua mdomo wake kuongelea jambo lolote linalomuhusu Zari amekuwa akiishia kuoga mvua ya matusi kutoka kwa Watanzania.

Tunda alipata umaarufu zaidi mwezi uliopita baada ya kupatwa na skendo ya kutoka kimapenzi na Diamond ambaye kwa kipindi hiko alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mzazi mwenzake Zari the Bosslady.

Kwenye Interview aliyofanya na Global Publishers Tunda alifunguka na kusema kuwa amefikia uamuzi wa kutokaa na kumzungumzia tena Zari kwani chochote kile anachokizungumza watu wataanza kumshushia mvua ya matusi na familia yake haipendi kuoana anatukanwa vile.

Kwenye mahojiano hayo Tunda ameongea haya:

Mimi kuhusu Zari au sijui ishu zao za kuachana kwao na Diamond au kitu chochote kinachohusiana na mambo yao sitaki kabisa kuzungumzia maana wengine sisi Damu zetu ni kama za kunguni nikisungumza chochote itakuwa ni shida tupo”.

 

Abdu Kiba: Tunda Alikuwa Mpenzi Wangu, Nimemiss”.

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na wimbo wake wa ‘Jeraha’ Abdu Kiba ambaye pia ni kaka wa Staa wa Bongo fleva Ali Kiba, amefunguka na kusema aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mrembo Tunda Sebastian.

Tunda ni video queen lakini pia ni maarufu kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu ya Msanii Diamond Platnumz. Tunda alijipatia umaarufu wiki chache zilizopita baada ya tetesi kusambaa kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na msanii Diamond lakini pia alizidi kupata umaarufu baada ya vieeo zake na Kinje kuvuja mtandaoni.

Ikiwa tunasherekea mwezi wa mapenzi ambapo juzi tu ilikuwa ni siku ya Wapendanao, Abdu Kiba alifunguka kwenye mahojiano na Millard Ayo Tv ambapo alidai kuwa alishawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Tunda na yalikuwa matamu kiasi ya kwamba alitamani yasivunjike.

Kwenye interview hiyo aliyofanya siku ya Valentine’s Day Abdu Kiba alizidi kufunguka:

Mahusiano ambayo yaliwahi kunifurahisha ambayo sikutamani hata yavunjike long time ago lakini kipindi hiko nipo na Tunda ambapo tulikutana kupitia social media nilimwelewa na vile vile alinielewa kwaiyo tukaweza kukutana na mwishowe wote tukaelewana ila muda kidogo kama miaka mitatu iliyopita na tulikaa kwenye mahusiano kwa miaka miwili lakini kwa sasa hatupo wote”.

Abdu Kiba amekiri kuwa penzi lao lilikuwa la siri kutokana na mazingira waliokuwa nayo ambapo amesema sehemu yao kuu ya kukutana ilikuwa kwenye gari hivyo watu wao wa karibu sana ndio walioshtukia mchongo.

Sipelekwi na Wanaume Mahotelini, Nalipa Mpaka Dola 400 Kulala Mwenyewe

Video queen maarufu kwa sasa Tunda Sebastian aliyetawala vichwa vya habari kutokana na skendo zake ameibuka na kudai kuwa habari za yeye kutembea mahotelini kudanga na kupelekwa na wanaume sio kweli kwani huenda mwenyewe na ana uwezo wa kujilipia hata shilingi dola  400 na kulala mwenyewe.

Tunda amepata umaarufu katika siku hizi za karibuni kutokana na skendo yake ya kutembea na supastaa  wa Bongo fleva Diamond Platnumz, huku ikisemekana kuwa ana ujauzito wake lakini pia muda huo huo alikumbwa na skendo ya kutembea na mume wa mtu ambaye ni mfanyabiashara maarufu Kinje, ambapo video zao wakila Debra zilisambaa mtandaoni.

Lakini pia moja kati ya skendo kubwa ambazo zimekuwa zikimuandama Tunda kwa muda mrefu ni tabia yake ya luxuriate kwenye mahoteli ya kifahari na kula chakula kizuri huku alikiri kama mitandaoni kwa was tabia yake ya kupenda kula kula ovyo.

Kwa habari za kimbea zimedai kuwa Tunda huenda mahotelini humo kudanga yaani kutafuta mabwana lakini pia hupelekwa na wanaume, jambo ambalo Tunda amelikataa kwa nguvu na kudai kuwa anashangazwa na tuhuma hizo kwani kiukweli ni kuwa huenda mwenyewe hotelini humo na kujilipia chakula anachokula lakini pia hujilipia kulala mwenyewe.

Kwenye mahojiano na Millard Ayo Tv, Tunda amefunguka yafuatayo:

Kwanza kitu ambacho kila mtu anatakiwa aelewe ni kwamba mimi napenda vitu vizuri napenda kula sehemu nzuri napenda kulala sehemu nzuri kwaiyo hata nyumbani kwangu mimi ni pazuri  kwaiyo hata ukiona nimeenda hoteli nzuri basi ujue ni hela yangu nimetoa maana siwezi nikasema nikale uswahilini hapana nitaenda kula kwenye hoteli nzuri na ni hela yangu sijawahi kwenda na mwanaume na najilipia mwenyewe mpaka dola 400”.

Lakini Tunda amekana tuhuma za kuvujisha video zake na Kinje wakiwa wanafanya yao na kudai was kuwa sio yeye kwani hata video zile hazikuwa kwenye simu yake.

Familia Yaamua Kumuweka Kitimoto Tunda Kuacha Skendo Chafu mitandaoni

Tangu mwaka umeanza Tunda amekuwa akisifika kwa skendo chafu kila kona katika mtandao ya kijamii, kila mtu anakuwa  anamsema yeye tena hasa baaada ya skendo yae ya kugombana na Aunty Ezekiel na kuvuja kwa picha zilizokuwa zikimuonyesha yupo na ‘sponsor’ mmoja mjini ambae ni mume wa mtu.

Ukiachana na sendo hizo mbili, Tunda amekuwa na skendo za kusema kutokana na tabia ya kuwa na wanaume tofauti tofauti kila siku na kuingia katika mahoteli makubwa makubwa kila leo kwa ajili ya starehe.

Baada ya video zile za siri kuvuja zikimuonyesha yupo na mwanaume mwingine , familia ya mwanadada huyo waliamua kumkalisha chini na kumuonywa kuacha kudhalilisha famila yao na yeye mwenyewe pia.Wazazi wa Tunda walionekana kuchukizwa sana na video hiyo na kusemekana kuwa tunda kwa sasa hayupo sawa na wazazi wake lakini walikaa chini na kumuonya kuhusu hilo.

Akiongea  na kukataa kutajwa jina lake moja ya marafiki wa tunda alieulizwa kuhusu hali ya watu wa karibu wa Tunda , mtu huyo alisema”familia ya Tunda walimuita chini na kumuweka kitimoto na kumsema sana na alihaidi kubadilika kabisa na akawaangukia wazazi wake na kuwaomba msamaha ingawa haikuwa rahisi sana kwake”

tunda alitafutwa na kuulizwa kuhusu swla hilo na ndipo alipothibitisha kuwa ni kweli wazazi wake wameathirika sana na video zile na anaona kabisa kuwa amewakosea.

Nimejifunza sana kwa maana ile video ilinichanganya  sana, wazazi wangu walikasirika sana sana,mpenzi wangu mpaka sasa haongei na mimi ila bado naendelea kumuelewesha  kwamba ile ilikuwa ni pombe tu.Nina imani atakaa sawa tu hasira zikiisha atanitafuta tu kwa sababu  najua ananipenda sana,nimejirekebisha na nimeacha kunywa pombe.

 

 

 

Tunda Amesema Haya Kuhusu Uhusiano Wake na Diamond Pamoja na Zari

Video queen maarufu Bongo Tunda amefunguk tena kuhusiana na uhusiano aliokuwa nao na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz na mpenzi wake Zari the boss lady.

Wiki chache zilizopita Tunda amekuwa akitawala vichwa vya habari mbali mbali katika mitandao huku mara zote akihisishwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Diamond lakini mara kwa mara amekuwa akikataa na kudai kuwa yeye ni shabiki wake tu na sivinginevyo.

Kwenye interview aliyofanya na Millard Ayo Tv, Tunda amefunguka na kusema yeye yupo karibu na Diamond kama shabiki lakini hana uhusiano naye lakini Zari hajawahi kuwasiliana naye wala kumtafuta kwa sababu hana cha kimwambia.

Narudia tena Mimi nahisi nasemwa sana kuwa na mahusiano na Diamond kwa sababu niko free kuweka wazi kwamba Diamond ndiye msanii ninaye mkubali sana kwa hapa Bongo tofauti na msanii mwingine sijawahi kuweka wazi nahisi ndio inapelekea watu kufikiria hayo lakini yule sio mpenzi wangu ni mtu tu ambaye namuheshimu   na yeye mwenyewe anaelewa support yangu kwake lakini sio mapenzi”.

Kwenye mahojiano hayo Tunda aliulizwa endapo ameshawahi kukutana na Zari au kumtafuta ili azungumze naye na jibu alilotoa kwa kung’aka ni amtafute Zari ili amwambie nini maana yeye anamkubali Diamond na wala sio Zari.

Tunda pia amefunguka na kudai kuwa hivi sasa yuko busy na kazi zake za kisanaa ambapo ameshirikishwa kwenye video mpya ya Barnaba.

Mose Iyobo na Tunda Warushiana Maneno Kisa Pombe

Dancer maarufu kutoka keen he label ya WCB, Mose Iyobo ameingia kwenye vita ya maneno na matusi na mrembo Tunda baada ya kutuhumiwa kuzulumu shilingi laki moja ya pombe ya Belaire.

Siku ya jana Aunty Ezekiel alianzisha kizaazaa na Tunda baada ya kuingia kwenye ukurasa wake wa Instagram na  kumdai pesa taslimu shilingi laki moja ambayo alimkopeshea pombe anzouza aina ya Beleire.

Lakini baada ya kudaiwa pesa hizo mara kadhaa Tunda alidai kuwa alipoenda kuilipia chupa hiyo Dukani kwao Aunty Ezekiel hakuwepo hivyo mtu aliyekuwepo alikuwa ni Iyobo ambaye ndiye aliyemkabidhi pesa hizo lakini alishangaa alipokutana na Aunty juzi akamdai wakati alishampa mumewe Iyobo.

Baada ya kuambiwa maneno hayo Iyobo aling’aka vibaya mno na kukana tuhuma hizo na kusisitiza kuwa hakupewa pesa hizo ndipo alipomtolea povu zito Tunda ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika maneno haya:

Ujinga nikubishana na mtu ambaye ameshafanya mambo yote ambayo wewe unafanya leo kama marudio unachotakiwa useme ni sina hiyo hela ntalipa siku fulani na sio kuanza kuongea ushamba  hawezi kutafuta kiki kwako ana mtoto maarufu kushinda wewe alafu kingine benten ni baba yako aliyekuzaa akashindwa kukupeleka shule umeishia kufumuliwa free unakosa laki ya kununulia pombe”.

Baada ya kutolewa povu hilo na Iyobo na Tunda naye alifunguka yaliyo moyoni mwake na kumjibu ambapo alimwandikia ujumbe huu :

Alafu na wewe Mose unakaa chini unaandika upuuzi kama huo kama ni kweli ni wewe umeandika basi huna Uso wa haya! Sasa nakuuliza swali moja tu kwa nini ulinoblock kukupigia kipindi Aunty ameanza kuniuliza kuhsu hela? Sikilizeni nyie hebu nitoleeni upuuzi wenu watu wazima mliokosa busara na akili kabisa yaani mimi nigombane na nyie Kisa laki moja? Kiukweli hata kama ningekuwa sina pesa siwezi kukosa laki “.

Lakini unakumbuka pale ambapo Mose aliposema mwanangu Cookie maarufu kuliko we we? Basi Funds alifika mbali katika ugomvi huo na kumuingiza mtoto wao kwa kumuita mtoto mbaya Tanzania nzima.

Baada ya Video Kuvuja Tunda Aomba Radhi kwa Mashabiki Wake.

Video queen hasieishiwa na matukio bongo Tunda, ameomba msamaha kwa mashabiki wake na watu wake wote wa karibu baada ya video zake na sponsor wake kuvuja na kuonyesha wakiwa katika mahaba mazito.tunda ambae jana aliingia katika ugomvi mzito na Aunty Ezekiel kwa sababu ya deni la kukopa pombe ameomba msamaha  kwa kuwa kuna mtu asiemjua amevujisha picha hizo.

Tunda anasema kuwa kuna mtu aliyeamua kufanya kitu hicho kwa maksudi ili kutaka kumdhgalilisha yeye lakini anaomba msamaha kwa sababu amejifunza kitu kupitia ilo.

Tunda anasema kuwa picha na video hizo zilishapitaga tangu siku nyingi kwa kuwa mwanaume alikuwa nae katika video na picha hizo walishaachana siku nyingi na mahusiano yalishaisha kitambo.’ninaomba radhi kwa kila niliyemhusu  na pia ninashangaa kwani ni umeamua iwe hivyo wakati ilishaisha na tulishamaliza kitambo bila ugomvi wowote.”

Pia Tunda ameomba msamaha kwa mke wa mwanaume huyo kwa kutembea na mume wake , mbaya zaidi ni kitendo cha kuvujisha hizo picha na kumdhalilisha mume wake.’sio muda wa kulaumu tena ,nisameheni wote inayowahusu has amke wa mhusika  na wote inayowahusu japo ilishapita’.

Tunda anaonekana kutokujua ni nani aliyefanya tukio la kuvujisha picha na video hizo lakini anamuomba  mtu huyo kvujisha na ushahidi wote uliobaki ili yaisha kabisa kuliko kuyatunza na kisha kuvujisha tena baadae ionekane kama vile vitu hivyo vimefanyika hivi karibuni.

katika mitandao ya kijaimi miezi kadhaa iliyopita zilitokea habari kuwa mwanadada huyo Tunda ana mahusiano ya kimapenzi na mume wa mtu anaejulikana wa jina moja la Kinje na kuwa huyo ndio anaemueka mjini.lakini skendo hiyo ilikaa kimya kwa muda mrefu mpaka jana zilipovujishwa tena picha hizo.

Aunty Ezekiel na Tunda Ndani ya Bifu Kali Warushiana Matusi ya Nguoni

Muigizaji wa Bongo movie Aunty Ezekiel amejikuta katika vita kali ya maneno na mrembo Tunda baada ya kupishana kuhusu malipo ya pesa ya pombe ambayo Tunda alikopa.

Siku ya Jana Warembo hawa waaili waliingia kwenye mabishano makali kwenye mtandao wa Instagram baada ya Aunty Ezekiel kwenda kwenye ukurasa wa Tunda na kumdai pesa yake kiasi cha laki moja alichochukua pombe ya Belaire.

Ambapo kwenye ukurasa wa Tunda Aunty Ezekiel aliandika maneno haya:

Baada ya Aunty kumuandikia vile inaelekea Tunda hakupenda kabisa kwani mara moja alianza kutokwa na povu kueleza kuwa alimpa pesa Mose Iyobo huku akimuita kiben-10 na kumtuhumu kwa kuitumia pesa ile. Hili ndio lilikuwa povu la Tunda:

 Uzee unakujia vibaya we we Bibi Mdashi na Una lako jingine nje ya pombe jibu ni lile lile ongea na Ben-ten wako akueleze pesa alipopeleka”.

 

 

Lakini habari chini ya kapeti zinafai kuwa kilichotokea ni kwamba Aunty Ezekiel anafanya biashara ya kuuza hizo pombe za Belaire sasa Funds alimpa ofa Diamond ya hiyo chupa moja ambayo ni laki moja kwa kipindi hiko Diamond na Tunda walikuwa wapenzi sasa baada ya Tunda kumuona juzi Diamond yuko na Wema na kusikia wamerudiana alikasirika na kugoma kumlipia tena ile pombe aliyompa ofa na hapohapo ndipo kizazaa zaa kilipoanza rasmi na wao kuja kurushiana maneno mtandaoni.

“Ati Madale State Lodge, au Madale State House?” Zari Aendelea kumpiga Madongo Diamond

Mfanyabiashara maarufu Zarinah Hassan ‘Zari’ ambaye pia ni mpenzi na mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz amejikuta anashindwa kuvumilia kinachoendelea mtandaoni na kumtupia madongo mpenzi wake.

Tangu wiki hii inaanza stori iliyotawala mitandao ya kijamii ni uhusiano uliopo baina ya Diamond na mrembo Tunda. Tangu mwanzo wa wiki kilichokuwepo ni tetesi tu na maneno ya watu yaliosemwa mpaka Jana video iliyosambaa mtandaoni ilitomuonyesha mdogo wa Tunda akijiachia Nyumbani kwa Diamond Madale.

Ifahamike kuwa nyumba ya Diamond iliyopo maeneo ya Madale ilibatizwa jina la ‘State house’ ikimaanisha mjengo wa raisi/ Ikulu na Guest House ikimaanisha nyumba ya kufikia wageni.

Baada ya stori ya Jana kutoka kuwa msichana huyo amejirekodi akitembea Madale lakini pia Hamisa na yeye ameshajirekodi akiwa Madame inaelekea uzalendo ulimshinda Zari ikabidi amrushie dongo hill la kuhoji endapo  nyumba hiyo bado ni jumba la raisi au imekuwa ni guest house?

Zari alihoji hayo kupitia ukurasa wake wa Snapchat na kuandika:

Ati Madale state lodge or Madale state house? Kuna mtu alikuwa anauliza akipanda Bajaji anashukia wapi? Mama yangu sio state house Tena….”.

 

Tetesi za Diamond kutembea na Tunda zimekuwa zikisikika mjini hapa kwa muda mrefu lakini wote wawili wamekuwa wakizikana lakini pia hivi sasa kuna habari zinazodai kuwa Tunda ni mjamzito na Diamond ndiye baba mtoto ingawa ni taarifa tu ambazo hazijathibitishwa na Tunda wala Diamond.

Vita ya Hamisa na Zari Yahamia Kwa Tunda

kwa muda mrefu wanamaa wawili hamisa mobeto na zari the bossy wamekuwa katika malumbano katika mitandao ya kijamii kuhusu nani kuwa juu zaidi ya mwenzie huku wote wakiwa wamezaa na bwana mmoja msanii mkubwa duniani diamond platinumz.

Mgogoro huu unaonekana kuendelea chini chini  lakini safari hii inaonekana kuhamia kwa mtu mwingineambapo   ni kati ya Hamisa Mobeto tena na Tunda ambae alishawahi kuwa video queen wa Diamond tena katika moja ya kazi zake.Siku kadhaa zilizopita kulikuwa na tetesi katika mtandao wa kijamii kuwa video queen huyo (Tunda) anatoka na msanii Diamond ingwa yeye mwenyewe alikanusha kabisa tetesi hizo.

Lakini mambo yanazidi kuwa moto tena hasa baada ya Tunda kuweka picha katika ukurasa wake wa instagram huku akiweka caption ambao inasemekana kuwa inalenga kutupia dongo kizani kwa Hamisa Mobeto.A

Alipoweka picha hiyo ambayo ilimuonyesha yupo katika kibao kata cha rafiki yake, ambapo hata Hamisa alihudhuria, Tunda aliandika caption ya kusema  “ebu angalia yule kinganganizi asiyejua maana ya kukataliwa na mwanaume‘ Maneno haya yanasemekana kumlenga Hamisa ingawa Tunda mwenyewe hakutaja jina la kinganganizi huyo.

lakini hata hivyo , inaonekana kuwa kwa muda sasa tunda amekuwa akiposti vitu vya kutaka kumuumiza roho hamisa mobeto , kwa mfano siku ya kuzaliwa kwa zari, tunda aliposti picha ya mwanamama huyo na kuandika “happy birthday mama T, wifi wa Taifa uliethibitishwa na Tbs,#nikiwamkubwanatakakuwakamawewe” Aliandika Tunda.

Ingawa mpaka sasa haijathibitika moja kwa moja lakini habari za chinichini zinasema kuwa tunda ana uhusiano wa kimapenzi na msanii Diamond.Lakini pia hata baada ya drama hizo zinazoendelea katika ukurasa wa instagram wa socialite tunda , hamisa hajataka kujibu chochcote kuhusu tuhuma hizo na wala kujibizana na mwanadada huyo.

Tunda na Hamisa wote kwa pamoja walishawahi kufanya kazi na Diamond katika moja ya nyimbo zake za mwaka uliopita wakiwa kama video queens katika wimbo wa Salome.