Husna na Tunda Ndani Ya Sakata La Kuibiana Mwanaume

Mlimbwende aliyewahi kushiriki shindano la Miss Tanzania miaka ya nyuma Husna Maulid na video vixen maarufu Bongo Tinda Sebastian wamedaiwa kutibuana kisa bwana wanayemgombania.

Gazeti la ijumaa wikienda linaripoti kuwa Husna ambaye alikuwa na urafiki na Tunda alijikuta amesalitiwa na shoga yake huyo baaada ya kugundua kuwa amemchukulia bwana ake anayeitwa Ally.

Katika mahojiano aliyofanya na Gazeti hili, Tunda alisema watu wamekuwa wakizungumza sana kuhusiana na hilo kwamba ameibiwa bwana na rafiki yake Tunda kitu ambacho hakifahamu kwani anachojua yeye ni kwamba ana mpenzi wake mmoja tu anayejulikana kwa jina la G na ndiye rafiki yake pia.

Jamani naomba watu waelewe kwamba nina mpenzi wangu anaitwa G, huyo mwingine anayetajwa simjui na wala sina urafiki na mtu zaidi ya mpenzi wangu, huyo ndiye rafiki yangu wa karibu“.

 

Tunda Apania Kurudi Shule Kujiendeleza Kielimu

Video vixen maarufu asiyeisha vituko kwenye mitandao ya kijamii Anna Sebastian Kimario ‘Tunda’ ameweka wazi mipango yake ya kutaka kurudi shule kwa ajili ya kujiendeleza kielimu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Tunda amesema kuwa, lengo lake ni kuwa mtaalam wa mambo ya kompyuta hivyo anataka akasomee kozi ya Information Technology (IT).

Siku zote napenda kusomea kozi ya IT, ni kitu kilichopo kwenye ndoto yangu na kwa sababu sasa nimekua na kutulia, naamini nitasoma kwa utulivu kabisa“.

Tunda amekiri kuwa pamoja na kupoteza muda mwingi kufanya mambo ambayo amekuja kugundua kuwa hayana faida kwake kiasi hicho ameamua kutopoteza muda zaidi na kurudi shuleni kwani muda inamruhusu bado.

Tunda Adaiwa Kuzama Kwenye Penzi Zito na Tajiri Mtoto

Video vixen asiyeisha vituko kwenye mitandao ya kijamii Anna Kimario maarufu kama Tunda amedaiwa kuwa kwenye penzi zito na kijana mwenye mkwanja mrefu anayejulikana kama Tajiri mtoto.

Global Publishers wanaripoti kuwa, Baada ya kumwagana na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz kisha kuhamia kwa mtangazaji wa Clouds TV Casto Dickson, Tunda amemnasa jamaa anayefahamika kwa jina la Tajiri Mtoto wa Arusha anayedaiwa kuwa na umri wa miaka 27.

Kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti la Risasi Jumamosi ndugu yake Tunda ambaye ameomba hifadhi ya jina, alidai kuwa kwa sasa video queen huyo anatoka na kijana huyo anayefanya kazi kwenye migodi na kwa kuwa ana mkwanja wa kutosha, Tunda ameamua kuhamishia makazi yake Arusha.

Tunda kwa sasa anaishi mjini Arusha, amepata bwana mwenye fedha zake watu wanamuita Tajiri Mtoto kwani ana hela za mgodini zinamsumbua, wanaume wa Dar watamsikia tu na kumuona mitandaon”.

Baada ya tetesi hizi kusambaa gazeti hilo lilimsaka tunda na kumhoji kuhusiana na tetesi hizo ambapo alifunguka;

Nimehama ndio maisha ya Dar si yangu tena kwa sasa nina maisha mengine na kifupi sipendi sana kuanika mambo yangu naomba watu waelewe hivyo kama wanavyoniona mitandaoni”.

Tunda- Sitaki Kuhusishwa na Diamond Kwa Njia Yoyote

Video vixen maarufu Kwenye mitandao ya kijamii Anastasia Sebastian Kimaromaarufu kama Tunda amefunguka na kutoa tamko la kutotoa kuhusishwa na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Tunda ameongea hayo Ikiwa siku chache tangu taarifa zienee Kwenye mitandao ya kijamii kuwa yeye na Mrembo mwingine maarufu kama Officiallyn wanagombania penzi la staa huyo.

Wiki iliyopita kuna video ilisambaa Social Media iliyomuonyesha Tunda akibambuwa na Diamond katika Private Birthday party yake.

Tunda ambaye ameshawahi kuwa Kwenye Mahusiano na Diamond katika siku za nyuma amesema hana Mahusiano kwa sasa na Diamond na wala hamgombanii na mtu bali ni rafiki tu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Tunda ameandika posti hii:

Lynn na Tunda Vitani Kisa Penzi La Diamond

Video vixen aliyejizolea umaarufu Kupitia video ya wimbo wa Rayvanny ‘Kwetu’ Lynn ameingia Kwenye vita kali na video queen mwenzake Tunda Sebastian na inadaiwa kisa ni Diamond.

Global Publishers wanaripoti kuwa warembo hao hivi sasa ni kama Paka na panya kutokana na wote wawili kumpenda Diamond na kuchanganywa kwa wakati mmoja.

Kwa mujibu wa chanzo cha GPL, mrembo Lynn ambaye haambiliki kwa Diamond, mara baada ya kusambaa kwa video ya Tunda na Diamond pamoja  ndipo lilipotangazwa bifu jipya mjini kati ya Tunda na Lynn.

Si unajua ni juzi tu Lynn alidaiwa kuzawadiwa mpaka gari na Chibu (Diamond) wakati wa bethidei yake?

Sasa hiyo video ya Tunda imemtibua Lynn na timu yake kwa sababu Lynn humwambii kitu kwa Diamond ‘so’ sasa hivi ni mwendo wa vijembe tu huko social media (mitandao ya kijamii).

Wenyewe wanasema kama mwanamke akitaka kumtibua Lynn, basi ajisogeze kwa Diamond kama alivyofanya Tunda maana ameshasema kuwa yupo tayari kuolewa na jamaa huyo, sasa hataki mtu amtibulie”.

Baada ya Tetesi hizo za bifu gazeti hil lilimsaka Tunda ili kumhoji kuhusu bifu na Lynn ambaye alifunguka:

Jamani kama ujuavyo ile ilikuwa ni sherehe na kila mtu pale alikuwa ameshakunywa (amelewa) na wengi walikuwa wanacheza, nashangaa sana wameniona mimi tu ndiye nilikuwa nacheza na Diamond, kama siyo mambo ya ajabu ni nini?.

Mimi kucheza na Diamond imekuwa ishu kubwa, kitu ambacho kinanishangaza sana. “Ina maana watu waliniona mimi tu? Lakini mimi naona ni kitu cha kawaida kabisa kwangu hivyo watu wasipate tabu sana,” alisema Tunda. Alipoulizwa kuhusu mwanaume wake anasemaje juu ya video hiyo, Tunda alisema kuwa, kwa sasa hana mtu anayemhofia kwani alishaachana na Casto Dickson muda mrefu.”.

Lynn alipotafutwa ili kujibu tuhuma hizi alikataa kuzungumza chochote Lakini tangu sakata hili litokee Diamond ameonekana kwenye party mbili tofauti akiwa na video vixen mwingine maarufu kama Kim Nana.

“Sipendi Ujinga Nikiwa na Mwanaume”-Tunda

Video vixen maarufu Bongo Anastasia Sebastian maarufu kama Tunda amefunguka na Kusema tofauti na watu wengi wanavyomfikiria yeye anaweza sana kudumu na mwanaume Kwenye Mahusiano.

Tunda amewajia juu na kuwashangaa watu wanaomuona yeye  hawezi kudumu na mwanaume mmoja, lakini ni kwa sababu hapendi kufanyiwa ujinga kisha kunyamaza kama walivyo wanawake wengine.

Katika mahojiano yake na gazeti la Ijumaa Wikienda, Tunda alisema sasa hivi wanaume wengi wanapenda kuwachezea wanawake kwa sababu wanawajua ni dhaifu, lakini wangejitambua thamani yao wala wasingekubali kupelekeshwa na wanaume.

Sijui kabisa kitu kubembeleza mwanaume ni kitu ambacho sijajaliwa kabisa. Mimi najua kupenda kama mwanaume atakavyonipenda, lakini mambo mengine hapana, vitu vingine anatakiwa anifanyie mimi kama mwanamke wake”.

Siku za hivi karibuni Tunda alidaiwa kumwaga mpenzi wake wa Miezi kadhaa Casto Dickson na kuanzisha Mahusiano na Jamaa mwingine lakini juzi Tena ameonekana na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Tunda Abambwa na Diamond Baada Ya Kumwaga Casto (+video)

Socialite na video queen maarufu Bongo Tunda Sebastian amerudi Kwenye headlines baada ya kuonekana na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Tunda ameshawahi kusemekana kuwa Kwenye Mahusiano na Diamond lakini baadae alianzisha Mahusiano na Mtangazaji wa clouds Tv Casto Dickson.

Pamoja na kwamba Casto alichora bonge la Tattoo ya Jina la Tunda Kwenye Mkono wake lakini aliishia  wiki chache zilizopita na siku ya jana ameonekana Kwenye Birthday party Diamond.

Diamond alionekana akicheza na Tunda kwa ukaribu sana kiasi ya kupelekea kuzua tetesi za kuwa Tunda kamtosa Casto na Kurudisha majeshi yake kwa Diamond.

https://www.instagram.com/p/BodZvdkn_6e/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1mcmagtlbnvu

Siku ya jana ilikuwa ni Birthday party ya Diamond na housewarming party ya nyumba yake mpya ambapo alifanya Private party na kualika Mastaa kibao ikiwemo timu nzima ya WCB , Navy Kenzo, Dully Sykes, Billnas, Tunda na wengineo.

Tunda Afunguka Kuhusu Tetesi Za Kuwa na Mpenzi Mpya

Video vixen maarufu Kwenye mitandao ya kijamii Tunda Sebastian amefungukia tetesi za kuwa na njemba mpya na kuweka wazi kuwa yule ni rafiki tu hana Mahusiano naye.

Wiki iliyopita taarifa zilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii kuwa Tunda na mpenzi wake wa Miezi kadhaa Mtanagzaji Casto Dickson wameachana na mara moja kuna taarifa zilidai kuna mpenzi mpya.

Kupitia ukurasa wake wa Snapchat Tunda alisambaza screenshot ya FaceTime na mwanaume mwingine picha iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii na kusababisha kusambaa kwa Taarifa kuwa Tunda ana mpenzi mpya.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Vibes, Tunda amesema mwanaume huyo aliyekuwa anachati naye ni rafiki yake wa kawaida tu na siyo mpenzi wake kama watu wanavyodai.

Jamani nawashangaa sana watu maana siyo kila ninayeongea naye ni mpenzi wangu, huyu ni rafiki yangu tu wa kawaida hivyo nawasihi watu wasiwe na tafsiri za mapenzi tu kila wakati“.

 

Tunda- Sina Bifu na Hamisa

Video vixen maarufu Kwenye mitandao ya kijamii Tunda Sebastian ameibuka na kuweka wazi kuwa hana bifu lolote na Hamisa Mobetto na wala hajawahi kugombana naye.

Tunda na Hamisa walisemekana lies Kwenye bifu zito siku za nyuma na ikidaiwa kisa kilikuwa ni penzi la staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Inajulikana wazi kuwa Hamisa ana uhusiano na Diamond na hata kuzaa naye mtoto mmoja lakini hapo nyuma ilishasemekana kuwa Tunda alikuwa ana uhusiano na Diamond kwa muda mrefu.

Kuwepo kwa bifu hilo kulithibitika baada ya Tunda kutumia mtandao wa kijamii kumfikishia Ujumbe Hamisa Miezi kadhaa iliyopita na kusema kuwa Diamond hamtaki lakini anajipendekeza.

Lakini pia siku zilizopita Tunda alimpiga Dongo Zito Hamisa baada ya kusikia karudisha majeshi kwa Diamond ambapo alidai ni mjinga kwa kurudiana na Diamond.

Siku ya juzi Tunda kawatolea povu zito watu walioandika stori kuwa yeye na Hamisa wana bifu ambapo amedai kuwa hana ugomvi wowote na Hamisa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Tunda aliandika ujumbe huu huku akisisitiza kuwa hana bifu na Hamisa:

Hamisa hajawahi kujibu tuhuma zozote na Tunda na hata kumrushia maneno Kwenye mitandao ya kijamii.

Sijawahi Kupiga Picha Za Utupu- Tunda

Video vixen na mwanamitindo maarufu Tunda Sebastian ameibuka na kudai kuwa hajawahi kuvaa nguo z utupu au kukaa uchi hadharani.

Tunda amefunguka na kudai kuwa yeye hana kawaida ya kupiga picha za utupu bali vile anavyovaa ndivyo alivyo na ameshazoea kuvaa hivyo siku zote.

Tunda amesema picha za utupu ni pale mtu anapoenda studio na kupiga picha lakini zile anazopiga akiwa nyumbani kwake ni zinapaswa kueleweka ni picha za kawaida.

Unajua kuna picha za utupu kwamba ile mtu unaenda studio unaamua kuwa wazi na kupiga picha, na kuna jinsi mtu anavyovaa kama ni nguo fupi yaani kawaida ya yeye kuvaa yapo si utupu kuna tofauti, mimi sipigi picha za utupu”.

Kumekuwa na kawaida kwa wasanii wa kike Tanzania kupenda kuvaa nusu uchi na kujianika Kwenye mitandao ya kijamii kitendo ambacho serikali imekuwa inakemea kwa wasanii kufanya.

Tunda Amtupia Dongo Zito Hamisa Baada Ya Kumuona na Diamond

Video vixen maarufu Tunda Sebastian amerudi tena Kwenye headlines baada ya kumtupia Dongo Zito hasimu wake namba moja Hamisa Mobetto baada ya video zake za chumbani na Diamond kuvuja mtandaoni.

Usiku wa jana Diamond na Hamisa walizua gumzo baada ya kuonekana pamoja chumbani wakiwa wanakumbatiana kwenye mahaba mazito jambo lililozua gumzo kuwa wamerudiana.

Lakini muda mfupi baada ya Hamisa kuonekana na Diamond video zilizomuonyesha Diamond na demu wa kizungu wakila Madenda nazo zilivuja mtandaoni jambo lililowachanganya watu wengi kuona Diamond na wanawake wawili tofauti katika usiku mmoja.

Kama utakumbuka Tunda na Hamisa wameshawahi kuwa na bifu siku za nyuma huku ikiaminika kuwa walikuwa wanamgombania Diamond kwani wote wawili wameshahusishwa kuwa na Mahusiano na Diamond.

Tunda ameibuka na kumpa Dongo Zito Hamisa baada ya video zake na Diamond kusambaa mtandaoni ambapo amedai kuwa anamuonea huruma Hamisa maana amedhalilishwa na mwanaume ambaye ni wazi kabisa kuwa hamtaki.

Kupitia ukurasa wake wa Snapchat, Tunda kaandika maneno haya:

 

Tunda Awapa Ujumbe Mzito Wapenzi Wake Wote Wa Zamani

Model na video vixen maarufu Bongo, Tunda Sebastian ametoa ujumbe mzito kwa wapenzi wake wa zamani (ma-ex) na kuwaambia kuwa watamkumbuka tu.

Ingawa hajamtaja mwanaume yoyote kwa jina lakini Tunda alipata umaarufu zaidi hivi karibuni baada ya skendo yake na Diamond na tetesi zilienea kuwa amekuwa mchepuko wa staa huyo wa Bongo fleva kwa muda mrefu hadi alifikia hatua ya kumbebea mimba.

Baadhi ya wanaume ambao Tunda ameshawahi kubanjuka nao ambao ni mastaa ni pamoja na Diamond, Mfanyabiashara maarufu Kinje, na wasanii wa Bongo fleva Young Dee na Abdu Kiba.

Tunda alitumia ukurasa wake wa Instagram kufikisha ujumbe huo kwa wapenzi wake wa zamani ambapo amewaambia Maex wake  kuwa wakimuona anataka wajue walichokipoteza, wajutie kwa kumpoteza yeye na wajue kuwa kamwe hawatampata Tena.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika ujumbe huo uliosindikizwa na picha:

Dear Ex….when you see me, i want you to recognize what you have lost, and realize what your never getting back”.