Vanessa Mdee aandikiwa ujumbe huu na Juma Jux

Hata baada ya kuachana na Vanessa Mdee, msanii kutoka bongo Juma Jux ameonekana kuwa bado na hisia za kumpenda mremboh huyu.

Hivi karibuni kupitia mtandao wake wa kijamii, Jux aliandika ujumbe ambao umewaacha mashabiki wakifikiria kuwa ujumbe huo ulikuwa wa Vanessa Mdee.

Aliandika kusema;

Nakumbuka mara ya mwisho kufanya party ya Birthday yangu ilikuwa 2013, Miaka minne iliyopita. Sikuwahi kufanya party yoyote tena sababu nilikuwa na rafiki, mpenzi na mtu wa karibu kuliko mtu yoyote kwenye maisha yangu. Miaka yote iliyofata nilikuwa na yeye mpaka sasa atuko tena karibu kama mwanzo, Tumebaki kuwa marafiki wa kawaida tu. Uwepo wake tu ulikuwa ni zaidi ya chochote kwenye siku yangu ya kuzaliwa, Kuongea na yeye au txt yake tu ilitosha kukamilisha siku yangu. Ila sasa sidhani kama itakuwa kama mwanzo. Nitafarijika sana kama nitamuona hiyo siku. This time nataka kuparty na watu wangu nani anataka kuparty na mimi katika siku ya birthday yangu ?

Picha mpya za Vee Money za wazingua mashabiki, Ni kweli kuwa amenenepa? (Picha)

Msanii na mrembo wa bongo Vanesaa Mdee ameachia picha mpya usiku wa kuamkia leo huku akionekana kuwa ameongeza weight katika sehemu ambazo mtu hawawezi kosa kujua.

Vanessa aliwachia picha hizi kupitia mtandaow ake wa Instagram huku akizingua akina idris Sultan na mashabiki wake ambao huwa mkondo wa kwanza kujua anachofanya mkali huyu.

Picha hizi hata hivyo sio siri kuwa ni za kuvutia na nguo yake ya manjano na viatu vyake vya chini.

Hawa ndio wasanii wa Bongo ambao Lulu Diva anawakubali

Lulu Diva ambaye anajulikana kupitia mziki wake hivi karibuni aliwataja warembo wawili kutoka Tanzania ambao yeye anazitambua kazi zao.

Akizungumza kwenye interview, Lulu Diva alisema kuwa Vanessa Mdee na Lady Jaydee ni wasanii ambao wameweka bidii kwenye kazi zao. Aliendelea kuwasifu kuwa wawili hao wameipa Tanzania sifa kutokana na kazi zao za kuridhisha.

Lulu Diva pia alimtaja Beyoncé na Celine Dion Kama wanawake ambao anafurahia kazi zao za kimziki. Akiongea katika interview Lulu alisema,

“Kimataifa namuangalia sana Beyonce na Celine Dion. Nikimuangali Beyonce naangalia hadi life style yake anayoishi, nikimuangalia Celine namuangalia hata the way anavyoimba, anavyoweza ku-control sauti yake. Beyonce kuanzia swagger anavyoimba, anavyocheza jukwaani, anavyocheza mwenyewe kwenye video zake, mavazi hata life style yake akiimba nakubali sana.”

Baby Madaha aendelea kumchana Vanessa Mdee

Muimbaji Baby Madaha ameonekana kuwa na uchungu na mwenzake, Vanessa Mdee. Hivi karibuni alisema kuwa Vmoney hana kipaji chat kuwa msanii ambaye anatajwa kuwania tuzo zozote za muziki.

Baby J
Baby Madaha

Hata hivyo Baby Madaha haonekani kujuta kwa kusema maneno haya. Hivi karibuni akiongea na Bongo 5 Baby Madaha alidai kuwa kuna wasanii wakali kumshinda mrembo huyu wa Jux . Kulingana na Madaha, Vmoney bado hajafikia kitengo cha kuwania tuzo za kimataifa Kama anavyofanya kwa sasa. Madaha alisema,

“Mimi si shabiki wa Vanessa hata muziki wake, hata nyimbo zake sizisikilizi kabasa,”

Aliendelea kusema kuwa yeye anawatambua wasanii Kama Lady Jaydee na wengi even ambao wameonyesha talanta zao za kuimba kupitia mziki mzuri ambao wameachana. Aliongeza,

“Kuna wasanii wakali hawapewi tu nafasi, mimi ni shabiki wa Lady Jaydee, akina Mwasiti kuna wasanii wengi wanafanya muziki nzuri,”

Hata hivyo alisema kuwa yeye hana wivu kwa Vanessa Mdee ila tu ni maoni yake.

Kuna nini Kati ya Vanessa Mdee na baby Madaha?

Msanii wa Bongo baby Madaha amedai kuwa kwenye industry ya bongo hakuna waimbaji wa kike ambao wanatalanta ya kuwafanya kuwania Tuzo za kimataifa.

Akizungumza na watangazaji wa Sibuka FM katika kipindi cha 180 Power, Byno na Joco, baby Madaha aliskika akimgusa Vanessa Mdee kwa kusema kuwa kunawaimbaji wa kike ambao hutajwa kuwania tuzo mbalimbali ilhali hawashindi hata moja.

Hata hivyo maneno yake yalionekana kumlenga vanessa ambaye nimsanii wa kike kutoka Tanzania ambaye amewania tuzo kadhaa. Baby Madaha alisema,

“Tunapeleka watu kuwania tuzo wengine hawana vigezo vya hizo tuzo, especially nazungumzia kwa madada kuna dada mmoja yaani kila tuzo anaendaga lakini ashindi kutokana na nini hana qualification za hizo tuzo,”

Balaa! Jux awajibu wanaodhani uhusiano wake na Vanessa Mdee umekwisha

Kumekuwa na uvumi mitandaoni kuwa Vanessa Mdee na Jux Juma wameachana baada ya Vmoney kuonekana akiwa na wanaume tofauti kwenye picha ambazo zimekuwa zikisambaa mitandaoni.

Hata hivyo Jux amefunguka kuhusu maneno haya na kusema kuwa yeye anamuamini mpenzi wake kwani hata picha hizi zikichukuliwa yeye huwa akifanya kazi na hana tatizo na hilo.

Aliendelea kwa kusema pia yeye kuna wakati yeye hupiga picha na wanawake ambao anafanya kazi (project) na wao na hii haimanishi kuwa anatoka na wao. Jux alisema,

“Si kweli mimi nilimind, sababu kama kupiga picha za namna hizo Vanessa anapiga na watu wengi sana picha za namna ile. Naomba nirudi nyuma kusema hili tena wasichana kwenye tasnia yetu sisi wavulana ndiyo tunatakiwa kuwasupport sana kwa sababu wapo wachache.”

Aliongeza kwa kusema,

Muimbaji huyo ameongeza, “Mimi hata nikipiga picha na wanawake 10 hapa, watu watajua tu Jux anafanya video ila Vanessa akipiga picha hizo watu watasema huyu mwanamke mhuni.”

Dadake mdogo Vanessa Mdee asimulia changamoto alizopitia kabla ya kuwa maarufu

Mimi Mars ambaye ni dadake mdogo Vanessa Mdee hivi karibuni aliweza kufunguka kuhusu changamoto alizopitia kabla ya kuwa muimbaji maarufu bongo. Kama wasanii wenzake alitafuta njia za kuiingia kwenye movie za bongo lakini hakuwa na uwezo.

Akizungumza kwenye kipindi cha Bongo Dot Home cha Times FM, Mimi alisema kuwa dadake mkubwa Vanessa aliweza kumsaidia awezavyo na ata kutafuta usadizi kutoka kwa Lulu na Wema Sepetu kumpa shavu dadake lakini waliambulia patupu.

Hata hivyo Mimi Mars hana kinyongo na wasanii hawa kwani anaamini kuwa wakati wake haukuwa umefika. Katika interview yake Mimi alisema kuwa sasa hivi yeye na akina Wema ni marafiki wakubwa na ingawa hawakuwepo alipokuwa akiwahitaji, bado anawachukulia kama marafiki wa dhati.

“Nilishawahi kumuomba Lulu, Elizabeth Michael nakumbuka tuliwahi kuongea naye hata akina Wema kuomba kuingiza kwenye bongo movie lakini, Vanessa ndio alikuwa ananisaidia kuongea nao lakini kama walinipiga chini fulani hivi but it’s okay,”

Hivi sasa Mimi Mars anafanya vyema na wimbo wake na akona matumaini ya kwenda mbali kama dadake. Tazama interview yake hapa chini.

Ni kama mapacha: Vanessa Mdee aonyesha picha ya mamake akiwa msichana mdogo

Muimbaji wa Tanzania Vanessa Mdee ameacha mashabiki wake wakimfananisha na mamake baada ya kupost picha ya kitambo ya mamake mzazi.

Kupitia mtandao wake wa kijamii Vanessa Mdee alipost picha hiyo huku akumsifu mamake kwa urembo aliowapa watoto wake (Vanessa na madada zake). Aliandika caption kusema,

Hi Mommy ? Circa 1976 #MothersDay is everyday ? #SophiasDaughter #ChokerAndAll

Ata hivyo pia aliweza kuajulisha mashabiki wake jina la mamake na kwa mara ya kwanza muimbaji huyu aliweza kushare picha ya mzazi wake kitu ambacho yeye hupenda aukiweka kama private kwa kuwa ni personal life.

Ikiwa umekuwa ukijiuliza mrembo huyu alitoa wake umbo lake na uzuri wake basi tazama picha hii ya mamake akiwa mchanga.

Vanessa Mdee na mamake
mamake Vanessa Mdee