Vannesa Asema Haamini Show Arusha Kufanyika, Ilikuwa Ikipigwa Vita.

Mwanadada Vanesa Mdee amefunguka na kusema kuwa hakuamini mpaka kufanyoka kwa show yake ya in love and money katika mkoa wa Arusha kutokana na ukweli kuwa show hiyo ilikuwa ikipigwa vita sana tangu hapo mwanzoni,

Vanesaa amabe kwa sasa yuko katika tour na mpenzi wake Jux  kwa ajili ya mshabiki na wameshazunguka baadhi ya mikoa zaidi ya mitano anasema kuwa ilikuwa ngumu kukamilisha show hiyo kutokana na ukweli kuwa kulikuwa na watu waliotaka isifanikiwe.

akiandika katika ukurasa wake wa instagram na twitter, vanesa anasema “nipo hapa leo kwa sababu ya kumtumainia mungu, na kumuamini yeye , maana hii show ya arusha ndugu zangu ilikuwa inapigwa vita zaidi ya kawaida.nikisema kwamba asubui ya jana yaani siku ya show nilikuwa nilishajiandaa kurudi Dar, sababu mambo yalikwama , would you believe me? lakini mungu ana malaika wake anaopigana na wanyonge .Let me start  by thanking my home town Arusha.”

Alichofanya Vanessa Mtwara Kuombeleza Kifo cha Patrick

Wikiend iliyopita ambapo karibia kila mtu alikuwa na mjozi kutokana namsiva mkuwbwa uliotikisa jii la Dar Es Salaam, baada ya msanii Muna Lov kufiwa na mtoto wake ambae alizikwa Jumamosi katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar.

Wasanii wengi walipata nafasi ya kuhudhuria mazishi ya mtoto huyo ingawa pia kuna wnegine hawakupata nafasi hiyo na vanesa mdee alkiuwa mmoja wa watu walishindwa kuhudhuria msiba kutokana na kuwa na show mjini Mtwara.

Lakini hii haikufanya vanesa ashindwe kuonyesha ni jinsi gani amefikwa na msiba huo na ndipo alipopanda jukwaani na kuwaomba masgabki zake kuzima taa na kuwasha simu ili kumuombea mtoto huyo.

Ndugu zangu  wa mtwarakama mnavyojua kuna msanii mwenzetu amefiwa na mtoto wake naomba tuchukue dakika chache kumuombea mtoto huyo,naomba mzime taa za jukwaan tafadhali na kuwashe taa za simu na kuziweka juu , tuonyeshe kwamba tuna upendona tumekuja kwa upendo.

Vannesa Mdee Aamua Kujipongeza Mwenyewe.

Mwanadada Vanesa Mdee amechoka kuvumilia na kusubiri sifa kutoka kwa watu wengine na kuamua kujipongeza mwenyewe kwa jitihada kubwa ambazo amekuwa akizinyesha na kupenyeza muziki wake kimataifa zaidi,

Vannesa anasema kuwa anajipongeza mwenyewe kwa sababu yeye ndie msanii pekee aArika Mashariki lakini msichana pekee wa Afrika kusaini deal kubwa Duniani lenye utafauti na madeal yote waliyowahi kusainiwa na wasanii mbalimbali.

Najipongeza mwenyewe kuwa msanii  pekee wa kike tanzania actually msanii pekee wa Tanzania na East Afrika kupata deal kubwa na yenye utofauti  na wengine .Ninafuraha sana kukutana na ma-director  wakubwa wa Universal , pamoja na kutumbuiza katika  ufunguzi wa afroforce …hii sio ndogo kwangu na hata kwa mashabiki zangu pamoja na watanzania kwa ujumla.

Wikiend hii zilisambaa picha nyingi za vannesa zikimuonyesha akiwa jukwaani ambapo alikuwa moja kati ya wasanii wakubwa walioimba katika tamasha la uzinduzi wa afro force

 

Alichoandika Jux Kwenye Birthday ya Vannesa.

Mapenzi kati ya vannesa na jux yanazidi kupamba moto hasa baada ya wawili hao kuonekana kushikana sana na kuamua kufanya vitu kwa pamoja katika baishara yao ya muziki.hata hivyo mapenzi yao hayajawahi kuathiri chchote katika mapenzi kiasi kwamba wawili hawa wanaonekana kushikamana sana.

Katika siku yake ya kuzaliwa, mwana dada Vannesa mdee leo, watu wengi wamepa pongezi tangu siku ianze lakini pia inafurahisha sana pale unapoona mtu wako wa karibu anapoamua kukutakia kheri ya siku iyo kwa maneno matamu na yenye kutia moyo, icho ndicho alichoamua kufanya jux na kuandika haya katika ukurasa wake wa instagram;

sijui niseme nini kitakachoweza kubeba uzito wa thamani ya maisha yangu, vannesa nitaendelea kumuomba mungu kila siku ili akupe maisha marefu na yenye afya tele.swala la kukupa furaha mimi nalimaliza mwenyewe vizuri kabisa,NAKUPENDAAA SANA my love.happybirthday

Vee na Jux ni Beyonce na Jay -z Wetu wa Bongo ;-Mimi Mars

Moja ya wanafamilia kutoka katika lebel ya Mdee Mimi Mars amefunguka na kusema kuwa kwa upande wake nawaona Vannesa Mdee na Jux ni kama beyonce na jay z wa tanzania kutokana na vile wanavyowea kuweka mahusiano yao vizuri lakini pia kuweka kazi zao zikaenda kama kawaida.

Mimi Mars ameyasea hayo alipokuwakatika show fupi ya uzinduzi wa tour yao itakayoanza hivi karibuni ikiwahusisha Vannesa na Jux kwa pamoja na kuznguka baadhi ya mikoa ya Tanzania kwa pamoja.Akijibu swali ambalo wengi wamekuwa wakisema kuwa wawili hao  hawawezi kudumu kwa sababu wanachanganya kazi na mapenzi  mimi mars anasema

Mimi ninaamini sana katika mapenzi na kazi kwa sababu ukiangalia hata wale wenzetu wa kule nje, kama beyonce na jay z pia wako hivyo kwaio na mimi nawaona kama ndio beyonce na jay -z wetu wa tanzania na ninaamini kwa kuwaona tu watafika mbali lakini mimi personally nisingependa kufanya kazi moja na mtu niliyenae katika mahusiano.

Vannesa Kwenda Kutumbuiza Mbele ya Rais Wa Gabon

Mwanadada mashughuli katika muziki ana anaefanya vizuri sana katika tasnia hii Vannesa Mdee amepata dili tena lingine la kutumbuiza mbele ya raisi wa Gabon kwa heshima ya muziki alionao nchini humu.

Akizungumza na bongo 5 Vannesa anasema kuwa , kutakuwa na tamasha kubwa litakalohudhuriwa na wasanii wakubwa  ndani na nje ya nchi akiwemo msanii Federic Gaccita na Harberto Gaccita ambao ni wasanii mashuhuli nchini humo.

Hata hivyo Vannesa Mdee anahistoria nzuri na  nchini hiyo kwa sababu aliwahi kufanya kazi na  Ali Bongo kutokana na kukutana kwao mwaka jana alipokuwa akifanya muziki wake na project yake ya African Queens aliyoifanya mwaka uliopita.

Katika Project hiyo, Vanessa aliwahi kufanya wimbo mmoja ambao haukutokana lakini kutokana na uwepo wake June 9 , inawezekana wimbo huo ukafanikiwa kutoka kwa mashabiki na kutumbuizwa jukwaani.

Mimi Mars Afunguka Tetesi za Vee Kuwa Mjamzito.

Msanii wa muziki  bongo fleva mimi mars amefunguka na kumtetea dadake vannesa mdee kutokana na tetesi zilizokuwa zimezuka siku za nyuma kidogo kuhusu Vannesa kuonekana kuwa ni mjamzito,Mimi Mars amesema kuwa dada ake amekuwa akila sana kwa sasa hivi na ndio maana amekuwa akiongezeka kila siku lakini sio kwamba vee ana mimba.

Akiongea na Funiko base ya Radio Five, Mimi Mars anasema kuwa kupenda kula kwa Vannesa kunasababisha watu kuhisi kuwa dada ake ni mjamzito lakini sio kweli na ni kitu ambacho hakiwezekani.

Hapana haiwezi kutokea,namuoa kila siku ni kwamba  anakula sana, mahaba ni mengi sana kwaio wanafurahia sana lakini sio hivyo na wala hana mimba .-Alifunguka Mimi Mars.

Vannesa ambae yuko katika mahusiano na msanii mwenzake Jux wamekuwa katika mapenzi kwa muda mrefu ambapo siku za nyumba ilitokea picha iliyomuonyesha Vannesa sehemu yake ya tumbo kuwa kubwa  na kusababisha watu kuhisi kuwa ni mjamzito.

Mimi Mars na Vannesa ni ndugu wa familia moja na wamekuwa karibu katika kusaidia kimuziki ingawa hawajawahi kufanya kazi ya muziki kwa pamoja.

Maneno ya Jux kwa Vannesa Yalivyowafurahisha Mashabiki.

Inaweza ikawa ndio couple bora katika mtandao kwa sasa bongo kutokana na ukaribu wao na mapenzi wanayoonyeshana wote wawili, inaweza kusemekana kuwa nguvu kubwa ya mashabiki inawafanya waendelee kudumu katika mahusiano hayo kwa sababu kipindi wamekosana mashabiki wengi walionyesha kuumia   na hata kupaza sauti ili wawili hao warudiane.

Kelele kubwa ya sasa kutoka kwa mashabiki sasa hivini wawili hao kuharalisha mahusiano yao na kufunga ndoa ili kuthibitisha kuwa wapo pamoja muda wote, kila wanapoweka picha katika mitandao mashabiki wamekuwa wakiweka maoni yenye kuonyesha kufurahi kuwaona pamoja wawili hao.

Wikiend hii Jux aliweka picha akiwa na vannesa mdee huku wakiwa katika pozi moja matata la kimahaba ambalo liliwakosha mashabiki wengi wa wasanii hao ambao ni wapenzi , lakini pia kikubwa kilichowavutia ni  maneno matamu Jux aliyoyaandika kwa Vannesa Mdee.

Ninachotaka kuona ni tabasamu  na furaha yako siku zote #bestfriend alafu don’t change your hairstyle  nazipenda saaana.-Aliadika Jux katikaukurasa wake wa instagram.

Vannesa Aamua Kutoa Fursa kwa Vijana wa Kike.

Mwanadada anaefanya vizuri katika anga za musiki nchini Vannesa Mdee ameamua kutoa fursa kwa wadada wanaojua kucheza kwa kuwapa nafasi ya kufanya nao video mpya inayokaribia kutoka hivi karibuni.

Vannesa ambae ameanzisha zoezi la kutafuta vijana wa kike wanaojua kucheza ili aweze kufanya nao ngoma yake mpya amewataka wadada hao kutoka sehmu mbalimbali tanzania kujirekodi wakiwa wanacheza na kuituma video hiyo kwenye Twitter na kuweka hashtag ya #pickmevannesa ili anaejua kucheza ataweza kuitwa na kufanyiwa usaili kwa ajili ya video hiyo inayokuja.

Wasanii wengi sasa wamegundua kuwa hata mitaani kuna vipaji amabvyo vinahitaji kufunuliwa katika anga za sanaa hivyo wameanza kufanya vitu vitakavyo wasaidia watu waliopo nje yatasnia ambao wanaweza nao pia wafanye kazi.

Wiki iliyopita mwanadada Lady Jay Dee,nae pia alifanya audition kubwa jijini Dar kwa ajili ya kutafuta vijana watakao weza kucgeza vizuri nyimbo za ndani na nje ya nchi.

Vannesa Mdee Aelezea Mauzo ya Album Yake.

Mwanadada Vannesa Mdee maefunguka na kuelezea jinsi album yake mpya ya Money Monday inavyofanya vizuri tangu imetoka mpaka sasa hivi.Vannesa ambae ndie msani wa kwanza wa kike kuwa na album na kuzunguka nchi nyingi kwa ajili ya kufanikisha upatikani na ujulikananji wa album yake hiyo amesma kuwa mpaka sasa album yake imekuwa ikifanya vizuri ingawa wapo baadhi ya watu wamekuwa wakimvunja moyo kwenye swala hilo.

Akiongea katika kipindi cha Friday Nite Live kutoka EATV na Sam Misago vannesa anasema kuwa  namshukuru mungu mashabiki wake wameipokea vizuri sana album hiyo na anaendela kuwaomba wazidi kumpa sapoti.

mauz yanaenda sana kwakweli na nimeshaajabu sana kuhusu swala la mauzo,na nimefurahi sana kuona kuwa watu kibao wameipokea alum yangu vizuri sana.its fun kuona kuna baadhi ya watu wapo na wanataka kunivunja moyo.mimi naenda bar nauzi cd mwenyewe nakutana na watu wananifukuza  wananiabi album zimepitwa na wakati.-Alifunguka Vannesa Mdee.

vannesa bado anatoa shukrani sana kwa mwaka 2018 kwa mashabiki wake ambo wamekuwa wakimsapoti sana katika kazi zake tena hasa mapokezi mazuri ya album yake hiyo.

Vannesa Mdee Atumia Zaidi Mil.100 kwenye Album Yake.

Msanii wa muziki wa bongo fleva vanesa mdee amefunguka na kusema kuwa ametumia zaidi ya mil10 kwa ajili ya kutengeneza album yake ambayo sasa hivi iko sokoni na amekuwa akiinadi katika vituo mbalimbali na hata kutembea nchi mbalimbali kwa ajili ya kuitangaza album hiyo.

Vannesa anasema kuwa ametumia fedha nyingi sana katika kutengeneza album yae hiyo lakini haoni shida yoyote kwa kuwa anawapenda na kuwajali mashabiki wake sana.

nimetumia ela nyingi sana katika kutengeneza hii album lakini sijajali sana kwa sababu nilitaka watu wamtambue kuwa Vannesa  katika kukua kimuziki, lakini  fedha hizo nililipa katika idara zote kuanzia wasanii waliopo katika album hiyo , matangazo, video na nk na bado naendelea kutoa kwa sababu kuna matangazo mengi.

Vannesa hajutii kabisa kutoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kutengeneza album hiyo,kikubwa ni kuangalia jinsi gani kazi hiyo  ingeweza kumuongezea heshima  na kuhakikisha kuwa inawafikia watu wote .

Vannesa anaingia katika orodha ya wasanii wachache wa kike wenye album Afrika na wanaofanya vizuru nje na ndani ya tanzania kwa kazi zao nzuri  amekuwa akiifanya.Hivi karibuni Vannesa aliachia album yake ya Money Monday katika viwanja vya mlimani City jijini Dar.

Picha za Vannesa Zilizoleta Gumzo,Inasemekana Ni Mjamzito.

Kuna picha zimekuwa ziki-trend katika mtandao wa instagram zinazomhusu Vannesa Mdee huku zikimuonyesha sehemu kubwa ya tumbo lake likiwa limetuna na watu kuanza kudai kuwa inawezekana msanii huyo ni mjamzito.Picha hizo zimeibua hisia tofauti kwa mashabiki wake huku weng wakionekana kufurahishwa na kumpongeza yeye na mwanaume aliyenae katika mahusiano ambae ni msaii mwenzake jux.

Mashabiki wamekuwa wakitoa maoni huku wakisema kuwa sasa ndio wanaanza kuamini kuwa wawili hao watafanikiwa kufnga ndoa kwa sababu mwanadada huyo tayari ameshadaka kibendi.Hata hivyo Vannesa na Jux wote hawaja-confirm swala hilo na wamekuwa kimya.

Vannesa na Jux wamekuwa  wapenzi kwa muda mrefu na wameoitia migogoro hapo katikati ya kuwafanya waachane kabisa lakini inawezekana kuwa msukumo mkubwa wa mashabiki umewafanya wasanii hao kurudiana tena na hata hivyo baada ya kurudiana , Jux alihaidi kuhakikisha kuwa hawatagomaban tena na kitakachofuata ni ndoa.

 

Hatimaye Album Ya Vannesa Mdee Yawafikia Mashabiki

Vannesa Mdee ni moja ya wasanii wa kike waliofanikiwa sana hasa katika swala la  kupiga hatua katika kukuza muziki wake, alikuwa ameshatangaza kwa muda mrefu kuhusu kutoa album yake na hatimaye ile ndoto yake imetimia.Vannesa anaweka rekodi ya wasanii wa kike wachache walioweza kufanya kazi zao za muziki mpaka kutoa album yake mwenyewe.Ni moja ya wasanii wanaotajwa karibia kila siku kuwa ni mpambanaji  katika kufikisha muziki wake mahali fulani.

Albumu hiyo ambayo pia inaonyesha kuwa ina nyimbo nyingi na zingine akiwa amewashirikisha wasanii wengine akiwepo mpenzi wake Jux inaonekana kupokelewa vizuri kabisa na mshabiki wake ambao walikuwa wakiisubiri kwa hamu album hiyo.

Akiwaalika mashabiki wake kuungana ane katika kuipokea album hiyo Vannesa Mdee jana alithibitisha kutoa kwa album hiyo na kuandika kuwa

‘Itis time..This is official album cover, #MoneyMondayTheAlbum….long time coming money monday.

 

Vannesa hivi karibuni alitangaza kusainiwa katika studi ya Unniversal , ambayo ni Menejiment kubwa Duniana yenye kulipa mkwanja mrefu zaidi na ni msanii wa kwanza Vannesa kusainiwa kwa ela iyo Afrika.

Hongera kwake vannesa kwa kufanikiwa kwa hilo lakini pia hamu na kiu kubwa ya mashabiki pia ipo kwa msanii diamond ambae pia ametangza kutoa albumu yake ya A Boy From Tandale itakayo toka kabla ya mwaka kuisha.

 

Balaa La Vannesa na Jux Jukwaa La Fiesta,Mapenzi Ni Mubashara.

Wakiwa bado wanakiri kuwa  hakuna mapenzi kati yao wasanii wawili Vannesa Mdee  pamoja na Jux wamewashangaza mashabiki kwa matukio yao ya kuimba pamoja katika matamasha mbalimbali ya Fiesta huku wakionesha kuwa hawana ugomvi wowote ilihali wamekuwa mbali katika mapenzi.wasanii hao ambao hata wamekuwa wakionekana waki-hang out pamoja katika mikoa mbalimbali tofauti na jukwaani wanaonekana kuwa bado na hisia kwa kila mtu kutokana na vile wanavyokuwa wakijiwakilisha jukwaan mbele ya mashabiki.

Tarehe 25, wikiendi iliyopita wasanii hao walipata bahati ya kutumbuiza katika jukwaa kubwa la Fiesta mkoani Dar Es Salaam ambapo waliwashangaza watu wengi baada ya kuimba kwa kuonyeshana mahaba na kuwa karibu zaidi.

Walipokuwa wakiimba mashabiki zao walikuwa wakishangilia na kupiga kelele za kuwataka wawili hao kurudiana, hata hivyo inasemekana kuwa wawili hao bado wanaendeleza mahusiano yao pamoja na kwamba wamekuwa wakikataa kuhusu kurudiana kwao.

Vannesa Mdee ni mmoja kati ya wasemaji katika kukanusha taarifa za kurudian kwao huku wakisema kuwa wamekuwa wasanii na wafanyabiashara kwa uda mrefu hivyo ugomvi wa kimapenzi hauwezi kuharibu kazi na biashara.

Vannesa na jux wakiimba kwa pamoja

Jux akimtengeneza Vannesa cheni kifuani kwake

Wakiwa pamoja jukwaani.

 

Vannesa Ajibu Tetesi Za Kurudiana Na Jux

Kumekuwa na tetesi nyingi mitandaoni kuhusu uhusiano wao wa karibu licha ya kuwa walikuwa wapenzi na wakaachana, wengi walitegemea watu hawa watakuwa maadui, wengine wakisema kuwa uwepo wao wa karibu unamaanisha kuwa wamerudiana kutokana na ahadi alizoweka Jux kuwa atafanya juu chini na watarudiana na Vanesaa Mdee.

Vannesa na Jux walikuwa ni moja ya couple iliyokuwa ukiwavutia watu wengi sana hasa muonekano wao walipokuwa pamoja, ukiachana na mapenzi lakini pia walikuwa wakifanya kazi ya muziki na biashara pamoja hiki ni moja ya vitu vilivykokuwa vikivutia zaidi.

Hata hivyo, baada ya tetesi za muda mrefu kuhusu kurudiana kwao hasa katika msimu huu wa tamasha la Fiesta ambapo mara nyingi walikuwa wakionekana kuwa pamoja na kuwa wote jukwaani na hata kuonyesha vitendo vya kukwepana kimahaba walipokuwa wakiimba Vannesa Mdee amuamua kufunguka na kujibu tuhuma hizo.

Vannesa alisema kuwa ukiachana na mapenzi lakini pia wao walikuwa wakifanya kazi pamoja na biashara, hivyo hata kama wamegombana katika swala la mapenzi haimaanishi kuwa wamapaswa kuwa maadui na kushindwa kufanya kazi pamoja.Wao watabaki kuwa washikaji tu na kufanya kazi na hakuna mapenzi.

kitu ambacho watu wengi hawajui ni kuwa jux ni mshikaji wangu sana,ni mt ambae tunapatana sana na tunaffanya kazi pamoja,na hata vitu vingi sana nje ya muziki jux amekuwa akinipa sapoti sana,kwaio hatuwezi kukaa tukagombana sasa hivi kwanza tunakuwa tukihatribu biashara. -Alifunguka vannesa

Vanesa ana Jux mara ya mwisho walipoonekana kuwa pamoja katika jukwaa la fiesta Morogoro Jux alikuwa akiimba kwa style ya kuomba msamaha ambapo Vanessa alimjibu atamsamehe akifika katika jukwaa la Mtwara, na walipofika mtwara wawili hao walionekana kuimba pamoja na kuonyesha ishara nzito za mahaba zilizofanya  mashabiki wengi khpji kama wamesharudiana au la.

Endapo wawili hao watarudiana itakuwa ni moja ya mambo yatakayo walidhisha mashabiki kwa sababu kwa muda mrefu mashabiki wamekuwa wakivutiwa kuwaona wawili hao kuwa pamoja na  wakiwaomba kwa muda mrefu wawili hao kutaka kurudiana

Vannesa Mdee Awajia Juu Mashabiki Kisa Jux

Msanii wa muziki Vannesaa Mdee amejikuta akiingia katika mgogoro na mmoja wa shabiki wake wa kike  pale ambapo aliyekuwa mpenzi wake kuposti baadhi ya picha na videos  za tamasha la Fiesta lililofanyika Iringa walipokuwa waki-perfom wote jukwaaani.Hata hivyo  shabiki huyo alimtolea Jux maneno ya kashfa kuwa kwanini anajikuta kumpost sana  mwanamke ambae ameshaachana nae wakati Vannesa  hana jitihada zozote za kumpost yeye na Vannesa hana kitu chochote cha kumpa kwa sababu mapenzi ya Vannesa kwa Jux yameshakwisha , inakuwa kama Jux anajipendekeza kwa Vannesa pale anapokuwa anapost picha zake.

Hata hivyo Vannesa alishindwa kuvumilia maneno ya shabiki huyo wa kike na kujikuta akimtolea povu na kumjibu kwa hasira kidogo na kusema kuwa yeye sio msemaji wake hata hivyo Vee anasema kuwa amekuwa akiona mwanadada huyo akitukana sana katika page ya Jux mara nyingi kwaiyo inawezekana anamtaka Jux kimapenzi labda anakuwa anashindwa kuongea.

Jux na Vannesa Mdee ni moja ya couple iliyokuwa ime-trend sana katika mitandano kipindi cha uhusiano wao, lakini baadae wawili hao walikuja wakagombana huku hakuna anaetaka kutoa sababu yoyote ya mifarakano yao, hata hivyo kwa muda sasa mashabiki wa Vanesa na Jux wamekuwa wakiwaomba sana katika page zao waweze kurudiana, lakin bado mambo yanaonekana kutokuwa mazuri. Kuachana kwao kimapenzi bado hakujafanya kiharibike kitu kwa sababu wawili hao bado wanaonekana kufanya pamoja katika kazi zao za kimuziki ukizingatia kuna baadhi ya nyimbo waliimba pamoja kipindi walipokuwa na mahusiano yao kwaiyo pale kunapokuwa na uhitaji wa wao kutokea pamoja mbele ya mashabiki wao wamekuwa wakifanya hivyo.

swala la mapenzi ni la watu wawili kwaiyo  mashabiki wanapaswa kusapoti muziki wa msanii wanaempenda bila kusababisha makwazo kwa wasnii wao, ingawa kwa Tanzania imekuwa ni swala la kawaida kwa baadhi ya mashabiki kuingilia sana mahusiano ya wasanii na kusababishwa makwazo kwa watu hao wanaowasapoti.Hivyo kama mashabiki wanawapenda wasanii wao basi wajikitye san akutoa ushauri kuhusu kazi za muziki na si vinginevyo.