Vera Sidika Athibitisha Kufanya Ngoma WCB

Mrembo anayetrend hivi sasa kutoka nchini Kenya Vera Sidika ‘Queen Vee’ ambaye hivi karibuni ameingia kwenye tasnia ya kuimba ametangaza kufanya ngoma yake ya pili ndani ya WCB.

Wiki iliyopita Vera alitengeneza headlines Baada ya kuachia wimbo wake ‘Nalia’ ambao ndani yake Alionekana model Calisah Kama video vixen.

Mpaka sasa Wimbo wa Vera unafanya vizuri sana kwani umepata watazamaji zaidi ya Laki Sita ndani ya Wiki moja na unatrend namba moja kwenye mtandao wa YouTube nchini Kenya.

Lakini hivi sasa Vera amekwisha tangaza ujio wa single yake mpya ambayo ameifanya na mtayarishaji wa muziki wa Label ya Wasafi WCB Laizer.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Vera ametangaza habari hiyo njema na kuandika:

Nani yupo tayari kwa ajili ya wimbo wangu mpya nilifanya Wiki iliyopita ambao umetayarishwa na producer mkali kutoka Wasafi Laizer?….Nitauachia pale tu Naliawutakapofikisha watazamaji milioni moja”.

 

Huddah Agoma Kuwekwa Kundi Moja na Vera Sidika

Socialite maarufu kutoka nchini Kenya Mrembo Alhuddah Njoroge maarufu kama Huddah Monroe amegoma kabisa kushindanishwa na hasimu wake Mrembo Vera Sidika ‘Queen Vee’.

Huddah amekataa kushiriki Tuzo za Black Entertainment Film Fashion Television and Arts (BEFFTA) ambapo yupo kipengele cha International Film and Fashion ambacho hasimu wake Vera Sidika pia amechaguliwa kushiriki na kusema kuwa hawezi kulinganishwa naye hata kidogo.

Huddah na Vera wamekuwa Kwenye mvutano wa muda mrefu na hata kugombana kwenye mitandao ya kijamii na sasa Huddah amegoma kabisa kishiriki tuzo hizo kutokana kuwekwa kundi moja na adui yake.

Kupitia mitandao ya kijamii Huddah ameandika haya kuhusiana tuzo hizo:

Mmenichagua katika tuzo ambazo wala sizifuatilii kabisa nipo bize na mambo yangu na ninafanya mambo yanayonihusu na sipo kwa ajili ya kulinganishwa na hao mlioniweka nao, kwa Afrika sina wakulinganishwa naye yaani sijaona labda USA (Marekani), nipo bize na brand yangu ya HUDDAH na kuangalia vipi naikuza sitaki ushindani na mtu”.

Huddah na Vera wamekataa mara kwa mara kuwa na bifu lakini matendo yao yamekuwa yakionyesha utofauti.

Vera Aibuka na Jamaa Mpya Siku Chache Baada Ya Kuachana na Brown

Socialite maarufu kutoka Kenya Vera Sidika ‘Queen Vee Bosset’ amedaiwa kuopoa mwanaume mwingine siku chache baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Msanii Otile Brown.

Vera na Otile Brown walimwagana siku chache zilizopita baada ya kila mmoja kumnyooshea kidole mwenziye kwa tuhuma za utapeli wa kimapenzi.

Siku kadhaa kupita baada ya kuachna na Otile Brown Vera ameonekana na jamaa mwingine ambaye hakutambulika kwa jina ambapo wawili hao walionekana wakiwa wanapata msosi katika mgahawa fulani jijini Nairobi.

Vera na Otile walimwagana huku chanzo kikieleza kuwa kila mmoja alikuwa akinufaika kwa upande wake. Inaelezwa kuwa, Vera alikuwa akimtumia Otile kutengeneza jina lake kuendelea kuwa juu wakati Otile alikuwa akimtumia kufanikisha muziki wake akimtumia kama video queen.

Siku Chache Baada ya Kuachana na Otile, Vera Sidika Aibuka na Mwanaume Mpya.

Ikiwa ni muda mchache umepita tangu mwanadada vera sidika kutoka kenya kutangaza  rasmi kuhusu mahusiano yake na msanii wa nchini humo Otile Brown, wiki hii mwanadada huyo ameonekana akiwa na mwanaume mwingine katika moja ya migahawa mikubwa iliyopo nchini humo.

Vera na Otile ambao walikuwa  wapnzi kwa muda mfupi sana walikuja kuacana ghafla bila wapenzi wao kutegemea huku ikisemekana kuwa vera alikuwa alikuwa akitafuta kukuza jina lake na biashara zake zaidi na huku Otile akimtumia Vera kwa ajili ya kukuza muziki wake na kumtumia mwanadada huyo kama video vixen katika nyimbo zake.

Hata hivyo mahusiano ya wasanii na watu maarufu yamekuwa yakishindwa kufanikiwa kutokana na kutokuwa na uaminifu lakini pia kunakuwa na malengo kadhaa ambayo mmoja kati yao anakuwa akitaka yakamilike na yakikamilika tu basi wanaweza kuachana.

Vera Sidika Athibitidha Kuwa Ni Mjamzito

Mwanadada ambaye ni mfanyabiashara maarufu kutoka nchini Kenya Vera Sidika au maarufu kama Queen Vee Bosset amethibitisha tetesi zilizokuwa zikisikika kwa muda mrefu kuwa ni mjamzito.

Inasemekana kuwa kwa miezi kadhaa blog mbali mbali nchini humo zimekuwa zikimuandika Vera kuwa ni mama kijacho.

Vera alithibisha taarifa hizo kuwa ni mjamzito siku ya Pasaka ambayo pia ilikuwa ilikueni sikuku ya wajinga ambapo kutokana na hill watu wengi hawakuamini taarifa hiyo wakiamini alikuwa anadanganya.

Lakini Vera ametumia tena ukurasa wake wa Snapchat na kuthibisha taarifa ile ni ya kweli wala sio masihara na kusindikiza pamoja na picha ikimuonyesha akiwa katika chunba cha daktari.

Vera amesema ataachia rasmi picha zake akiwa mjamzito wiki ijayo ili kuwaaminisha zaidi mashabiki zake ambao hawaamini mpaka hivi sasa.

Lakini pia Vera amesema anategemea kufanya sherehe ya kujua jinsia ya mtoto wake hivi karibuni (gender reveal party). Mpaka hivi sasa bado haijajulikana nani ni baba wa mtoto.

Hamisa Mobetto na Vera Sidika Wavurugana Kisa Zari

Hamisa Mobetto na Mrembo kutoka Kenya Vera Sidika maarufu kama Queen Vee, wameingia katika vita ya maneno mtandaoni kisa ni Zari.

Sakata hili lilianza baada ya Hamisa ambaye kwa sasa yupo nchini Kenya kukutana na Vera na kumrekodi wakati wanasalimiana na kisha kutuma hiyo video Snapchat. Tendo hilo liligeuka ugomvi kwani inajulikana wazi kuwa Vera ni rafiki kipenzi wa Zari ambaye ni hasimu mkubwa wa Hamisa (kwani wote wamezaa na Diamond)

Baada ya Video hiyo kusambaa mtandaoni mashabiki wa Zari walimjia juu Vera kwa kitendo chake cha kuwa na urafiki na Hamisa wakati ni adui wa shoga yake Zari. Baada ya kuona hilo ndipo Vera alipoingia mtandaoni na kuanza kujitetea kuwa hana urafiki na Hamisa bali alisimama kumsalimia mtu mwingine aliyekuwa na Hamisa na hakujua kuwa anarekodiwa na Hamisa.

Vera amedai hana urafiki na Hamisa na anashangaa kwanini alimpiga picha bila ruhusa.

Baada ya kuona hivyo Hamisa alimjia mjuu Vera na kudai kuwa aache uongo kwani alijua wazi kuwa alimrekodi na kabla hajaituma video ile alimuonyesha na akakubali, pia Hamisa amedai Vera alimuomba amtafutie mashabiki Tanzania pia alimualika Nyumbani kwake akamtembelee yaani kwa kifupi walikuwa mashoga ila saivi anamruka kwaajili anamuogopa Zari.

Hamisa amchana kuwa kwa sababu ana urafiki na Zari hana haki ya kumsema vibaya

Sakata halikuishia hapo kwani Hamisa alimrushia maneno Vera kuwa ni mtu mzima ovyo mwenye maziwa fake na kajichubua na Beta kamsema Hamisa kwa kitendo chake cha kuzaa na wanaume wenye hela ili wamsaidie maishani kwani hana kazi yoyote.

Vera akimchana live Hamisa
Hamisa akimpa makavu Vera

Mpaka sasa Zari hajachangia lolote juu ya bifu hili je unahisi nani yupo sahihi?

 

 

 

Harmonize awataja warembo wawili kutoka Kenya ambao wanampendeza sana

Harmonize alisafiri kuenda Nairobi, Kenya kupigia upato nyimbo zake. Staa huyo kutoka Wasafi Records WCB amefanya mahojiana na vitua vya habari kadhaa jijini Nairobi.

Katika mahojiano na kipindi cha Mambo Mseto ya Radio Citizen hapo jana, Harmonize aliulizwa kumtaja mrembo kutoka Kenya anayemgusa sana.

Mzazi Willy Tuva na Harmonize wakiwa Citizen Radio

Harmonize alicheka na kuwaza kwa sekunde chache kabla ya kusema kwamba Kenya iko na watoto wazuri wengi.  Hata hivyo alisema Huddah Monroe and Vera Sidika ndo wanampendeza sana.

“Suppose kama haugekuwa na Wolper alafu ibidi uwe na mchumba hapa Kenya ni mrembo mgani wa humu nchini Kenya ambaye huwa ana ‘Kugusa’ kinyama?” Harmonize aliulizwa.

“Kenya kuna watoto wazuri kabisa… …mtoto VERA hivi…. mtoto MONROE hivi….wako wengi bana, wote wako sawa,” alijibu Harmonize.

Huddah Monroe

 

Vera Sidika