BASATA Watoa Msamaha kwa Rayvanny na Diamond Platinumz

Baraza la sanaa tanzania BASATA wameachia barua  na kuwatumia wasanii wawili diamond pamoja na mwenzake rayvanny kuwa wamekubaliwa ombi lao la kuomba msamaha na kwamba adhabu yao imeiesha kuanzia tarehe ya january 22 2019 baada ya kuonekana watiifu wa adhabu waliokuwa wamepewa.

wasanii hao walipewa adhab hiyo mwaka 2018 baada ya kukaidi maagizo yakuacha kuimba wimbo wa mwanza ambao ulionekana kutokuwa na maadili kwa jamii kitu ambacho wasanii hawa hawakuona kama ni swala lenye tija.

Hata hivyo wasanii hawa walifungiwa kufanya kazi yoyote na pia kufanya show sehemu yoyote kwa muda usiojulikana lakini kutoana na huruma ya walezi hao wa sanaa wameliangalia kwa jicho la pili na kuwatolea msamaha.

 

Fid Q , Steve Nyerere Wampa Pole Diamond kwa Ajali ya Sumbawanga.

Wikind hii diamond latinumz alikutana na ajali jukwaani baada ya jukwaa aliliokuwa ameandaliwa kwa ajili ya show yake huko mkoani sumbawanga liliporomoka na kumuangusah na kata majeraha baadhi ya sehemu katika mwili wake.

Kila mtu alilichukulia swala hilo katika uzito tofauti huku wengine wakisema kuwa ni kutokana na sifa ya  mkoa huo kufanya sana mambo ya kishirikiana , lakini mwisho wa siku unaona kuwa kuna vitu utokea kama ajali katika kila sehemu.

Wasanii mbalimbali walimpa pole msanii huyo  akiwepo Fid Q , katika ukurasa wake aliandika “poleni sana wana…siku zote hakuna kazi isyoosa changamoto…’ 

Inaweza kuleta sura mpya kwa mashabiki  kwa sababu hapa karibuni kundi la WCB walikuwa na mgogoro kidogo na Fid q hivyo haikuwa rahisi kuona msanii huyo akiweka mkono wa pole kwa wasanii hawa.

Rich Mavoko ku-perfom Wasafi Festival

Uongozi wa kundi la wcb ukiongozwa na msanii Diamond platinumz wamesema kuwa milango yote iko wazi kwa msanii Rich mavoko kufanya show katika show zao zinazozunguka kila mkoa kwa sasa hivi inayojulikana kama wasafi festival tour.

Akiongea  bila kinyongo, babu tale anasema kuwa hawana kinyongo chochote na msanii Rich mavoko hata kama hapo katikati kulitokea kutokulewana lakini wanapoenda kufanya nae kazi lakini kuna mambo hayakwenda sawa tangu hapo awali hivyo haikuwa rahisi kumuweka katika listi  lakini wanaahidi kumuwahi sana hapo mwakani .

Babu tale anasema kuwa kwa sababu rich mavoko alishafanya show  za tigo fiesta hivyo karibia mikoa mingi anayopita kwa sasa alishapita hapo awali lakini kama wangemuwahi mapema basi ilikuwa haina haja ya kuancha kumuweka katika listi.

Babu takle anasema kuwa kwa mwaka huu acha ipite lakini kwa mwaka ujao tamasha hili litakuwa kubwa zaidi na litaongeza mikoa na pia wasanii wataongezea zaidi na watamuwahi Rich mavko.

Wasafi Wasaliti Amri, Waamua Kufuta Wimbo wao You Tube.

Baada ya kukaa muda mrefu bila kutaka kufuata taratibu na maagizo ya BASATA , wasafi wameona haitakuwa vyema kuendelea kukiuka taratbu na maagizo ya uongozi huo hivyo kuamua kufuta wimbo wa MWANZA  katika channel yao ya you tube.

Tamko hilo ambalo lilitolewa mapema November 12 na katibu mtendaji kwa kufutwa kwa wimbo huo kutokana na kukosa kwa maadili tya wimbo huo lakini wasanii hao walikaidi, baada ya hapo  walikuja kupokea faini nyingine ya milion 9 ikiwa kama kosa la kukiuka kufuata maagizo ya BASATA.

Siku ya November 13 , wasanii waliamua kutekeleza agizo hilo na kufuta wimbo huo katka akaunti yao ya you tube,

Wimbo huo ulifungiwa ukiwa tayari umefiksha views zaidi ya milion moja katika chaneli hiyo ikiwa una siku mbili tu jambo ambalo sio la kawaida na ni ndogo ya wasanii wengi kufanikiwa hivyo katika maisha ya muziki.

Hata hivyo wimbo huo umefungiwa  baada ya kuonekana umetrumia amneno yasiyokuwa tasfiri kuwa na ushawishi wa kingono katka jamii.

Hata hivyo wasanii rayvanny pamoja na damond waliandika waraka mrefu kwa uongozi wa BASATA wakitaka wimbo huo kutokufungiwa au kupigwa katika channel mbalimbali usiku tu lakini BASATA wamekataa maomb hayo.

Mange Kimambi Amtolea Povu Makonda Kisa WCB

Mwanadada Mange Kimambi amefunguka na kumtolea povu Mh Paul Makonda kwa kile kilichodaiwa kuwa wasanii wa WCB wamekuwa wakiangaliwa kwa mambo mengi wanayoyafanya ambayo yanakuwa hayana maadili katika jamii lakini wakifanya wasanii wengine inaonekana ni kosa kubwa.

katika ukurasa wake wa instagram, Mange Kimambi meweka picha ya rayvanny akiwa anafagia pesa ze noti ya shilingi elfu 10 huku wakati huo huo msanii maua sama na Soudy Brown wakiripotiwa kuwa mahakamani kwa kosa la kusambaa kwa video iliyokuwa ikiwaonyesha wakiwa wanakanyaga pesa hizo.

Mange Kimambi analalamika kuwa Mh Makonda amekuwa akiwakingia kifua wasanii wa WCB huku wasanii wengine wakiwa wanateseka na makosa kama yao.

Ujumbe wa Rc Makonda Baada ya Babu Tale Kurudihswa Rumande

Ikiwa kesi ya Babu Tale bado haijaisha  na bado anaendelea na misuko suko ya kuwekwa rumande kutokana na kesi yake ya madai baada ya kuonekana kumdhulumu moja ya masheikh jijini Dar  baada ya kuvunja makubaliano yao ya biashara.

Hata hivyo Babu tale aliwahi kuitwa mara kadhaa mahakamani lakini alikuwa akikaidi agizo hilo la mahakama , hivyo hata alipolekwa mahakamnai siku za hivi karibuni na kushindwa kuayazungumza mambo kadhaa na anaemdai, Babu tale alitakiwa kurudi tena rumande kwa sababu naibu msajili wa mahakama kuu ambae alikuwa akitoa amri za kukamatwa kwake hayupo yupo likizo hivyo anatakiwa kumsubiri mapaka atakapo rudi.

Katika kuonyeshwa kuguswa na kufatilia yale yanayomkuta baba tale na akiwa kama mlezi wa lebel ya wasafi, kuu wa mkoa wa Dar, Paul Makonda aliweka  caption hii katika ukurasa wake wa instagram huku akiwa ameweka picha ya Babu tale.

 

Mpiga Picha wa Diamond Afunguka Kuhusu Picha za Hamisa

Mpicha picha wa Diamond anaejulikana kwa jina la lukmba amefunguka kuhusu picha za hamisa zilizowahi ku-trend sana katika mtandao siku chache tu kabla ya Zari kutangaza kuachana na Diamond na kusababisha watu kuanza kumtukana mpiga picha huyo kuwa yeye pia ni mnafiki kwa sababu amekuwa akipiga picha wanawake wa bosi wake bila kuwa na aibu ya kuwa nao karibu wote.

Hapo awali mpiga picha huyo amabe mara nyingi alikuwa akitembea na Zari muda mwingi kwa ajili ya kumpiga picha alikuja kuonekana akipiga picha kwa hamisa na ndipo watu walipoanza kupaniki na kumtukana .hata hivyo lukamba amefungua na kuongelea swala hilo na kusema akiwa kama mpiga picha wa lebel , Hamisa alikuja kupiga picha kwa ajili ya Photoshots za Wasafi tv.

Japokuwa watu walinitukana sana lakini mimi ninafanya kazi, boss wangu ana tv na  aliniambia kuwa natakiwa kufanya shooting za watu mbalimbali na sikufanya na hamisa peke yake kwaio nikafanya , ilivyokuwa na watu walivyoipokea ni tofauti.-Alisema Lukamba alipokuwa akiongea na Bongo5.

watu wengi walikuja juu na kumtukana kutokana na ukweli kwamba lukamba siku chache alikuwa akimpiga picha zar na ghafa kuhamia kwa hamisa , ndipo walipomuona msaliti kwa sababu wanawake hao wawili hawaelewani.

Queen Darlen Amtaka Harmonize Apunguze Uhuni Anamtesa Sarah

Mwanadada pekee kutoka katika kundi la wasafi, Queen Darlen amefunguka na kutoa ushauri kwa msanii mwenzake kutoka katika kundi hilo kwa kumtaka  Harmonize kupunguza tabia ya uhuni kwa sababu anamtesa sana sarah ambae ni mpenzi wake kwa sasa.

Queen Darlen amemtaka Harmonize kuacha kukata  tamaa katika kazi lakini amesmhauri kuwa inabidi apunguze kuwa na wanawake wengi na kutulia na mpenzi aliyenae kwa sasa amabe ni Sarah.

Apunguze uhuni,atulie mtoto wa watu maskini ya Mungu mzungu yule  anampenda ila yeye mhuni mdogo wangu ,mhuni sana , mdogo wangu maisha ya uhuni sio mazuri anakuwa kama mfalme sulemani. aache hizo.

Hata hivyo kuna tetesi zimekuwa zikisambaa hivi karibuni kuhusu Harmonize kugombana na mpenzi wake huyo wa kizungu huku sababu kubwa ikiwa ni wivu wa mapenzi.

 

Diamond Aonyesha Mjengo Mpya wa Wasafi

Haikuwa kitu raisi kwa hapo zamani mafanikio ya muziki kuonekana kama ilivyo sasa hivi, lakini pia nidhamu kubwa na juhudi ya kazi wanayoifanya kundi la Wasafi chini ya meneja wao Diamond Platinumz inatia moyo na hata kufarahisha sana na kuwa fanya wengine watamani mafanikio ya wasanii wa lebel hiyo.

Msanii  mkubwa nchini na nje ya nchi , Diamond Platinumz leo ameonyesha mjengo mpya kabisa wenye kuonyesha kuwa na thamani kubwa kabisa na kusema kuwa hayo ndio yatakuwa makao makuu ya wasanii wa lebel hiyo.

katika ukurasa wake wa instagrama ameposti picha hiyo na kusema kuwa hayo ndio makao makuu ya wasafi ambapo ndani ya ofisi hiyo kutakuwa na sehemu ya studio ya kurekodia, ofisi za WCB, kituo cha radio cha WASAFI FM na  kituo cha Tv kitakachoitwa WASAFI TV.

Tangu Diamond ameanza musiki amekuwa mstari wa mbele sana kusaidia vijana wengine waliokuwa na nia ya kufika mbali,amekuwa akiwaongoza na kuwafanya hata wao wajulikane kimataifa,wamekuwa wasanii wenye kujituma na hata mafaniko yao yamekuwa yakionekana.

Baadhi ya picha zinazowaonyesha wasanii wa lebel ya wasafi wakiwa pamoja.

Pongezi nyingi ziende kwa Diamond na Uongozi wake lakini pia kwa wasanii wote ndani ya lebel hiyo kwa kufanya vitu vitakavyotia hamasa kwa wasanii wengine kwa sababu mafaniko yao yanaoneka katika jamii nzima.

Aslay aeleza kwanini hawezi kubali kusainiwa Wasafi

Dogo Aslay ambaye yuko katika lebo ya Mkubwa na Wanawe amefunguka na kusema kuwa hawezi kubali kujiunga na lebo ya Diamond Platnumz – Wasafi.

Staa huyo wa Yamoto Band ambaye ameanza kutoa nyimbo zake binafsi amesema kuwa malengo yake yamezidi kuwa msanii wa Wasafi ya Diamond.

Aslay

Aslay alieleza kuwa mipango yake ni kufikia kiwango cha Diamond na Ali Kiba kwa hivyo hawezi kusainiwa na Wasafi kama anataka kufikia malengo yake.

“Kusainiwa WCB hapana, kwa sababu mimi nina ndoto za kuwa zaidi ya WCB au kuwa zaidi ya kitu kingine chochote, naamini nitakaza nitafika hizo sehemu, naweza kusema nina ndoto za kufika kama alipofika Chibu, nina ndoto za kufika kama alipofika Ali Kiba. Inabidi nikaze niwe mimi kama mimi nitafute njia ya kutoboa nifike level hiyo, yaani sio yeye pekee yake mtu yeyote, wakisema wanisaini siwezi kukubali sasa hivi”  Aslay alisema katika kipindi cha XXL ya Clouds FM.

 

Picha ya msanii mpya wa WCB ambaye Diamond alimtambulisha leo

Jana Mai tarahe 21 Diamond alitangaza kuwa atamtambulisha msanii mpya kutoko lebo ya Wasafi akifanya mahojiano kwa Clouds FM.

“Panapo majaaliwa siku ya jumatatu kesho, ntakuwepo kwenye LEO TENA ya Clouds fm na familia nzima ya @Wcb_wasafi tukimtambulisha Kijana mwenzetu Mwingine Mpya toka Mtaani, ndani ya @Wcb_Wasafi….. Sisi ni vijana ambao tumekulia kwenye umaskini na bado tupo kwenye kupambana namna ya kujikwamua kwenye umasikini… na ndiomaana tunajitahidi kadri ya uwezo wetu kila tukiona kijana yoyote mwenye nia na kipaji kumsaidia kwa kadri ya uwezo wetu, ili nae aweze kutambulisha kazi zake, na Pengine Mwenyez Mungu akimjaalia nae awe mkombozi kwenye Familia yake….Sio jambo Rahisi ni gumu, lakini kwa Sapoti yenu naamini tunaweza lifanikisha…Siku zote naomba mkumbuke WCB_Wasafi sio ya Diamond, ni ya vijana wote wapambanaji…na ndiomaana kila siku nawaomba Muendelee kuniombea na Kunisapoti, kwani Sapoti yenu ndio itayo nifanya hata kesho niweze kukuchukua wewe ama ndugu yako ili aje kukitambulisha kipaji chake na Mwenyez Mungu akijaalia kufikia Malengo…… USIKOSE kusikiliza Leo tena ya @Cloudsfmtz saa nne Asubuhi…Shukran?” Diamond aliandika kwa Instagram.

Diamond akiwa Clouds FM leo Mai 22

Hit maker huyo wa ‘Marry You’ alienda kwa kituo cha Cloud FM akiwa na Rayvanny and Lava Lava – msanii mpya wa Wasafi.

Rayvanny and Diamond wakiwa Cloud FM

Lava Lava tayari ameachia wimbo wake mpya ‘Tuachane’ akiwa Clouds FM leo. Wimbo wake pia unapatikana kwenye tovuti la Wasafi.

Msanni mpya wa Wasafi Lava Lava