“Nilikuwa Napenda Kwenda Kuvua Samaki”-Wastara

Msanii wa filamu za Bongo movie Wastara Juma maarufu kama Wastara Sajuki amefunguka na kuweka wazi kuwa alipokuwa mdogo tabia yake mbaya ilikuwa kupenda kuvua samaki.

Katika mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Wastara alisema enzi hizo alipenda sana kucheza kwenye mito na mara nyingi alikuwa akiwashawishi watoto wa mtaani kwao, huko Morogoro kwenda kuogelea na kuvua samaki, kitendo kilichokuwa kinawakera sana wazazi wa watoto hao.

Ukweli niliwasum¬bua sana wazazi hasa wa watoto wengine kwani wapo ambao walikuwa hawap¬endi watoto wao kuvuka eneo la nyumbani lakini mimi nilikuwa nikiwashawishi tunakwenda mtoni na tuna¬vua samaki wakubwa na wadogo”.

Lakini pia Wastara aliweka wazi kuwa mbali na kuvua samaki Lakini pia alikuwa anapendeleea kwenda maporini kuangalia wanyama kama ngedere.

Wastara Ahaidi Kutodondosha Machozi Mbele Za Watu

Muigizaji wa Bongo movie Wastara Juma ameibuka na kuweka wazi kwa kuanzia Hivi sasa watu wasahau kumuona akihuzunika na kudondosha machozi mbelewya kadamnasi kwani amekuwa jasiri.

Wastara amefunguka na kusema kuwa ingawa amepitia changamoto nyingi hasa mwaka 2018 Lakini ameamua kayakata machozi na kusema kuwa mwaka 2019 utakuwa mwaka wake  wa Furaha.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Wastara alisema kuwa watu wamekuwa wakimuona ni mtu wa kulia kila wakati, lakini mwaka huu ameamua kuyakataa machozi, hatalia tena anataka kuwa mtu mwenye furaha siku zote, lakini pia asiyaoneshe machungu yake kwa kila mtu kama yatazidi atalia kimoyomoyo.

Watu wengi wameshanichukulia kuwa mimi ni mtu wa kuonewa huruma kwa yale niliyopitia, lakini nataka kuwaambia kuwa sasa nimebadilika kabisa sitaki kuyaonesha tena machungu yangu hadharani maana kuna wengine wanakukebei na siyo kukuonea huruma“.

Mbali na Kupitia kipindi kigumu cha kusimbuliwa na Mkuu Wake lakini mwaka jana mwishoni Wastara alikumbwa na jaribio la mwisho Baada ya kuibiwa kila kitu katika kampuni yake ya kupiga picha.

Gari la Wastara Lakamatwa Bandarini, Aiomba Msaada Serikali

Baada ya mwanadada wastara kulalamika siku chache zilizopita kuhusu swala la kuibiwa na majambazi vitu vyake vya kufanyia kazi hivi karibuni , ameibuka tena na kulilia swala la gari lake kutoka nje ya nchi kukwama bandarini huku sababu ikiwa ni Pesa.

Wastara anasema kuwa gari hilo alilopewa msaada na marafiki zake kutoka nje ya nchi limefika tanzania siku nyingi lakini amekuwa akishindwa kulitoa bandarini hapo kwa sababu ya fedha.

Wastara anasema kuwa ameshakwenda mpaka kwa waziri kufatilia swala hilo lakini bado haoni kama kuna msaada wowowte anaweza kupatiwa kwa watu aliowafikia zaidi ya maumivu,

Wastara anasema kuwa watu hao waliamau kumpa gari hilo baada ya kumuona akiwa anaangaika sana na matatizpo yake ya mguu hivyo kuamua kumrahisishia kwa kumpa usafiri ili aweze kufanya mambo mengine kwa urahisi zaidi,

Wastara anasema kuwa watu wasihangae kama atakufa ghafla kwa sababu amekuwa mtu wa mawazo sana muda owte kutokana na maisha anayoishi ya kuwa na mawazo muda wote.

Wastara Ataja Sababu Za Kupenda Kuolewa

Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali maarufu kama Wastara Juma au Wastara Sajuki amefunguka na kuweka wazi sababu za kupenda kuolewa.

Wastara ambaye mpaka sasa ameshaolewa ndoa nne aliwahi kukaririwa siku za nyuma akisema akitokea mwanaume mwingine wa kumuoa Yupo Tayari kwa ndoa yake ya tano:

Katika mahojiano yake aliyofanya na Global Publishers, Wastara ameweka wazi kuwa sababu kubwa inayomfanya mpaka apende kuolewa ni kutafuta faraja ya moyo wake na wanaye kupata baba sahihi ingawa wakati mwingine mambo yamekwenda asivyotarajia.

Unajua mimi ni binaadamu kama wengine ambapo nimekuwa nikitamani kuishi na mume ili nijisikie niko na mwenzangu na wanangu wawe na mtu wa kumuita baba ingawa wakati mwingine mambo yamekuwa yakienda tofauti.

Lakini pia Wastara alipohojiwa sababu kubwa zinazopelekea mpaka kuachika mara kwa mara aliweka wazi kuwa ni hawezi kuzitaja kwani kila ndoa imeisha kwa sababu zake na changamoto za kipekee.

Wastara Atafuta Mbinu Mpya Kwa Ajili Ya Kusaidia Wamama na Watoto

Muigizaji wa Bongo movie mwanamama Wastara Juma maarufu kama Wastara Sajukia amefunguka na kusema amekuja na project mpya ambayo imejikita katika kuhakikisha inatoa msaada kwa wamama na watoto.

Wastara ameweka wazi kuwa kupitia priject hii ataweza kutimiza ndoto yake ya kusaidia jamii aliyokuwa akiiota kila siku.

Kwenye mahojiano yake na Risasi Jumamosi, Wastara alisema yeye kama kioo cha jamii na mambo aliyopitia kwenye maisha, ameamua kuanzisha mradi huo alioupa jina Anzia Hapa Wastara akiwa na nia ya kuwasaidia akina mama na watoto.

Kama unavyojua, mbali na kuwa msanii, mimi ni Balozi wa Wanawake Afrika kupitia Shirika la Wanawake na Watoto la Sweden (Asovu). Nimeamua kutimiza ndoto yangu ya kusaidia watoto na wanawake, pia kwa kupitia chama hicho ambapo rasmi nitakizindua Jumamosi (leo)”.

Wastara ameweka wazi kuwa kwa Kupitia project hii basi anaamini atasaidia wanawake na watoto wengi ambao nao wanahitaji msaada kama yeye na kusaidiwa na Watanzania wenzake.

Mimi ni Rafiki Mkubwa wa Mzee Kimambi:-Steve Amjibu Mange.

Badada ya kuchafuliwa katika mtandao Steve Nyerere amemjibu katika uwanja wa maoni mwanadada mange kimambi baada ya kumtaja kama moja  ya watu waliowai kuwa na mahusiano na mwanadada Wastara Juma miaka ya nyuma.

mange ambae alianza kumshambulia wastara kwa kumtukana na kisha kuanza kutoa siri na mambo ya ndani ya mwanadada huyo huku akimtukana matusi alisema kuwa Steve nNyerere na Wastara waliwahi kuwa wapenzi hapo awali kipindi Wastara ayari akiwa na ulemavu wa mguu.

Hata hivyo  baada ya kuona maneno hayo hayavumiliki, Steve Nyerere aliamua kujibu Mange Kimambi chini y apost yake hiyo kwa kumwambia kuwa yeye amekuwa rafiki mkbwa sana wa baba yake kwa miaka mingi kwanini anaamua kumdhalisha mitandaoni.

weee DADA Mange kimambi mimi ni rafiki mkubwa sana wa baba yako mzee kimambi toka enzi hizo huna wakubwa DADA,  kwani mimi na wewe tuna ugomvi mtoto wa rafiki yangu.

Mange Alipua Bomu, Asema Wastara na Steve Nyerere Waliwahi Kuwa na Mahusiano Hapo Nyuma.

Mwanaharakati Mange Kimambi amefunguka na kusema kuwa mwanamuziki na muigizaji wastara juma aliwahi kuwa na mhausiano ya kimapenzi hapo nyuma na msanii mwenzake seve nyerere lakini hakuna aliyewahi kujua na kwa sababu ilikuwa ni siri.

Wawili hao ambao wamenza kutukanana katika mitandao ya kijamii na kutishiana kutoleana siri mpaka za ndani imekuwa ni kama swala ambalo hakuna aliyetegemea kuwa lingeweza kufikia lilipofikia sasa.

Akiandika waraka mrefu wenye matuzi na kebehi nyingi mange kimambi amesema kuwa Steve Nyerere aliwahi kuwa na mahsuaino na mwanadada huyo lakini wastara  anajifanya kuwa ni mgonjwa wakati anaweza kutoka kimapenzi na wanaume tofautu tofauti ilhali hajali ugonjwa alaiona.

Wastara ambae ahap awali aliptajiwa mambo ya steve nyerere alimjibu kuwa mambo ya steve nyerere ni ya zamani kabla hata ahajapata ajali , akimaanisha kuwa ni kipindi ambacho alikuwa hajaolewa lakini mange alikanusha  na kusema kuwa ni kipindi hiki cha ugonjwa wake ndio alikuwa katika mahusiano na Steve Nyerere  na pia mdogo wake Alikiba pia.

Mama mbona unajitetea nimeanza kukutajia ya steve nyerere unaanza kujitia eeti ooh ya zamani, eti ni mambo ya miaka 10 iliyopita wakati steve ame**** wakati ukiwa umeshakatwa mguu…..Ma***a kilema wewe , …Ki**** hata kiwe na miaka20…..malaya mchafu wewe ume***** mpaka na abdul kiba hivyo ivyo na kigulu chako. unapenda sana watoto wadogo wastara.

Wastara Afunguka Kuhusu Kiki za Nusu Utupu.

Mwanadada Wastara Juma amefunguka na kusema kuwa hivi karibuni anategemea kurudi katika maswala ya  sanaa baada ya kukaa kwa muda mrefu kutokana na kuumwa kwake lakini hiyo haifanyi yeye kutafuta kiki ili kujirudisha katika sanaa kama wanavyofanya wau wengine.

Wastara anasema kuwa wasichana wengi wamekuwa wakipiga picha za nusu utupu na kuziweka katika kurasa wa mitandao kwa ajili ya kutafuta kiki kitu ambacho kinawapa kiki lakini yeye hawezi kufanya hivyo hata siku moja.

Nina amini kuwa nina mashabiki wengi sana ambao wananipenda sana na sidhani kama watapenda nibadilike na kuanza kuva nguo za utupu kwa ajili ya kutafuta jina  kama vijana wa sasa, binafsi sijafikilia kubadilika ili kushindana nao hivyo nitaendelea kufanya kazi zangu kama nilivozoea.

 

Kwa Sasa Sihitaji Msaada Wowote wa Watanzania:-Wastara

Msanii wa maigizo Wastara Juma ambae hapo awali alikuwa akikaririwa kuomba msaada wa watanzania ili kuweza kufanikisha maswala ya matibabu nje ya nchi amefunguka na kusema kuwa kwa sasa hana mahitahi yoyote ya msaada kutoka watanzania ila maombi yao tu kutokana na magonjwa anayoomba.

Wastara ambae alirudi kutoka nchini India kwa matatibabu na msaada huo alipatiwa na watu mbalimbali akiwepo rais wa tanzania, anasema kuwa anaomba watanzania wamuombee sana kwa sababu kwa sasa atakuwa akitumia dawa maisha yake yote.

Kwa sasa kwakweli sihitaji msaada wowote kwa watanzania zaidi ya maombi yao ili nizidi kuendelea vizuri,kinachonisumbua kwa sasa ni matatizo ya mgogo na kichwa kuna dawa nimeandikiwa na daktari maisha yangu yote.

 

Wastara Asema Alishamuona Israel Mara Nyingi.

Msanii wa bongo movies Wastara Juma amekiri na kusema kuwa kwa jinsi ambavyo hali yake ya afya ilivyokuwa mbaya kuna kipindi alikuwa akimuona Israel kabisa mto aroho akitaka kuichukua roho yake lakini mungu alikuwa bado anataka yeye aendelee kuisi  na ndiomaana hata sasa bado yuko hai.

Wastara ambae hivi juzi amereudi kutoka India alipokuwa amekwenda kutibiwa matatioz yake ya mguu na mgongo na kuonekana kuwa na tatizo lingine kwenye kichwa anasema kuwa kwa sasa  hali yake imeimarika na hilo ni jambo la kumshukuru mungu kwa sababu anaamini kuwa mungu bado anampenda sana.

nimeshamuona israel mtoa roho mara nyingi sana kwakweli,lakini kwa sababu mungu ananipenda   ndio maana bado ninapumua na ninaamini kuwa  mungu ataendelea kunipa uhai  kutokana na majaribu mengi na makubwa niliyoyapitia.-Alifunguka wastara alipokuwa anaongea na mwandishi mara baada ya kurudi kutoka katika matibabau yake.

Wastara Amjibu Mange Kimambi Kuhusiana na Tuhuma Zake za Utapeli

Muigizaji wa Bongo movie Wastara Juma amefunguka na kumpa majibu mwanaharakati wa mambo ya siasa mtandaoni Mange Kimambi baada ya kudai kuwa haumwi na anafanya maigizo.

Mange Kimambi alimtolea tuhuma nzito Wastara kuwa haumwi na anatumia pesa za michango kufanya biashara na hata alipofika India kwenye matibabu alirusha picha mtandaoni akiwa amechomwa dripu lakini Mange alisema dripu ile ilikuwa imechomekwa kisanii na ametapeli wananchi hela za michango.

Siku ya jana Wastara aliwatolea akitokea nchini India kwenye matibabu na kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5 alimjibu mange Kimambi kuhusiana na tuhuma alizomrushia akidai kuwa ametapeli fedha za watu na serikali:

Kwanza siwezi nikamridhisha kila mtu kwa sababu mtu yule anayesema haya ni maigizo alafu kuna hamsini au ishirini wanamfuata hiyo tu inatosha kukuonyesha tofauti ya uelewa tulionao Watanzania Halafu watu wanasapoti kitu wasichokijua kisa tu Mange kawaambia sindano inaelekea chini lakini hajmwajafanya hata research kujua ukweli lakini siwezi kuwalazimisha wanielewe maana mwisho wa siku mimi na Mungu wangu ndio tunaujua ukweli wale wanaomuamini yule waache wamuamini cha msingi mimi nimetibiwa na nimerudi salama ingawa sijali na kabisa”.

 

Wastara: Milioni 43 Nilizochangiwa za Matibabu Hazijatosha na Nina Mpasuko wa Fuvu

Muigizaji wa Bongo movie Wastara Juma ‘Wastara Sajuki’ amedai kuwa pesa ambazo wananchi na serikali ilimchangia kwa ajili ya matibabu jumla ya kiasi cha shilingi milioni 43 hazijatosha.

Wastara ambaye anasumbuliwa na matatizo ya mguu ambaye alikatwa mguu mmoja miaka kadhaa iliyopita baada ya ajali ya gari aliomba msaada mapema mwaka huu wa matibabu ambapo alichangiwa jumla ya shilingi milioni 43.

Alisafiri wiki chache zilizopita kuelekea nchini India kwa ajili ya matibabu na alirudi siku ya jana ambapo alipokelewa na wasanii wenzake wa Bongo movie uwanja wa ndege.

Baada ya kuwasili jana Wastara aliongea na waandishi wa habari na kusema kuwa pesa alizochangiwa kiasi cha shilingi milioni 43 hazikutosha hivyo amelazimika kuuza mali zake ili pesa zitimie kwa kudai madaktari wamemwambia ana matatizo zaidi ya miguu na mgongo.

Lakini pia Wastara amedai baada ya kufanyiwa vipimo kwa kina amegundulika ana tatizo kwenye fuvu lake la kichwa ambalo hilo ndilo lilikuwa likimfanya asipate usingizi bila yeye mwenyewe kujitambua.

Wastara Amlilia Rais Magufuli

Msanii wa bongo fleva ambae pia ni mwanaharakati, Wastara Juma ambae pia ni mke wa marehemu sajuki ameomba msaada kwa viongozi wa serikali akianzia kwa Raisi Magufuli ili aweze kuoata ela ya kwenda nje kwa ajili ya matibabu.

Wastara ambae amekuwa akitembelea mguu wa bandia kwa zaidi ya miaka minne sasa baada ya kupata ajali ya pikipiki iliyomfanya kukatwa mguu anasema kuwa amekuwa akitibiwa nchi India ambako alitakiwa kwenda tena kwa ajili ya matibabu tena tangu mwaka uliopita lakini  ilishindikana baada ya kushindwa kukusanya fedha za kwenda kurudi kwenye matibabu.

Wastara ameomba msaada kwa viongozi ,mashabiki  na watu wote wenye nia nzuri kwa sababu kwa hivi sasa amekuwa anateseka sana na maumivu ya mgongo yanayomfanya kuzimia kila wakati na kunywa dawa za maumivu kila muda hata bila kujua idadi yake.

Akielezea sababu iliyomfanya ashindwe hata kukusanya ela za matibabu , Wastara anasema kuwa kuna kipindi aliingia mkataba na kampuni moja ya simu inayojulikana kwa jina la KZG, ambao walishindw akumlipa ela yake aliyotegemea ingemsaidia kwa matibabu,wastara anasema kuwa kila kitu anachofanya kwa ajili ya kupata pesa kinaishia mahakamani na kukosa haki yake.

Kwa Wastara sasa anachohitaji ni msaada tuwa kupata ela kwa ajili ya kwenda kuhudhuria kliniki yake huku nchini India , lakini pia amewataka watu kuacha kuwa wanafiki kwa kukataa kumsaidia sasa alafu waka jitokeza siku ya msiba wake wakitoa vitu kwa ajili ya mazishi.

Ikumbukwe kuwa Wastara ambae alikuwa mke wa marehemu Sajuki akipata ajali ya pikipiki akiwa na mumewe na kukatwa mguu ambapo baadae aliweza kupata mguu wa bandia.Lakini hata hivyo kinachompata wastara sasa kilishampata mumewe ambae alikuwa akisumbuliwa na magonjwa ya kansa anaalitakiwa kwenda kutibiwa nje ya nchi lakini kutokana na uhaba wa kufedha walikaa muda mrefu bila kuhudhuria kliniki yake mpaka mauti yalipomkuta.