Picha 5 za shabiki wa Man United aliyeingia uwanjani kumkumbatia Rooney Gor Mahia ikimenyana na Everton

Klabu ya Everton kutoka Uingereza ililaza Gor Mahia ya Kenya mabao 2-1 katika mechi iliyochezwa jana Alhamisi katika uga wa Benjamin Mkapa jijini Dar-es-Salaam.

Rooney, mshambulizi wa kitambo wa Manchester United ambaye alijiunga na Everton, alifunga bao la kwanza la timu yake mpya.

Staa huyo ambaye ako na mashabiki duniani nzima alivutia watu wengi kuenda kutazama mechi hio baina ya Gor Mahia na Everton.

Shabiki wa Manchester United aliingia kwa uwanja wakati mechi hio ilikua inaendelea na kumkumbatia Rooney kabla ya polisi kumtoa kwenye nje.

Tazama picha ya shabiki huyo hapo chini:

  

Picha 5 za Wayne Rooney akitua Tanzania na timu yake mpya

Wayne Rooney ametua Tanzania pamoja na kikozi nzima cha Everton tayari kumenyana na timu ya Gor Mahia kutoka Kenya Alhamisi hii.

Mshambulizi huyu mashuhuri duniani alijiunga na Everton kutoka klabu ya Manchester United siku chache zilizopita.

Everton itamenyana na Gor Mahia katika shindano la Super Cup ambalo linaandaliwa na SportPesa – kampuni ambalo linadhamini Gor Mahia and Everton.

Rooney na wachezaji wengine wa Everton wataanza kufanya mazoezi leo jioni katika uga wa Benjamin Mkapa jijini Dar.

Tazama picha za Rooney na kikozi nzima cha Everton wakiwasili Tanzania hapo chini: