Shabiki Atuma Maombi kwa WCB

Moja ya mashabiki wa WCB ameamua kuvunja ukimya na kutuma salamu kwa uongozi wa WCB kutokana na malalamiko ya chini chini kuhusu Tv hiyo  na radio yake kuwa mara zote wamekuwa hawataki kufanya mahojiano na wasanii ambao wanachipukia.

Shabiki huyo anasema kuwa mara kadhaa amekuwa akipokea malalamiko kutoka kwa sanii wa chii kuwa wamekuwa wakienda kuomba interview na kukataliwa na kuambiwa kuwa ili waweze kuapta nafasi ni lazima wawe na bifu na msanii mwingine.

Shabiki huyo anaendelea kwa kusema  hata kwenye swala la kuchagua wasanii pia wamekuwa wakifanya mahijiano na wasanii wakubwa wenye majina tayari na interview zimekuwa zikijirudia wakati huku mtaani kuwa wasanii wengi.

Lakini pia wanasema kuwa hii inatasfiriwa vibaya kwa sababu Diamond wakati anafungua Tv na radi hiyo alisema kuwa ni kwa ajili ya wasanii wa aina zote hasa wale wanaohitaji kusikika.

Harmonize Apishana Kauli na Uongozi Wake Wa WCB

Kwa miezi kadhaa sasa kumekuwa na tetesi kuwa Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutokea katika Label ya WCB, Harmonize hana maelewano mazuri na viongozi wa Label yake.

Siku ya juzi Harmonize alitoa taarifa ya kwamba EP hiyo ataiachia February 18 siku ya jana lakini ilipigwa ‘stop’ tena na uongozi wa WCB na kuahidi siku ya leo watatoa taarifa rasmi.

Jumatano hii mmoja kati ya Wakurugenzi wa WCB, Sallam SK ametoa taarifa ambayo inaonyesha kuna kitu kinaendelea kati ya uongozi wake na Harmonize.

TAARIFA KWA UMMA.. Maelezo ya utokaji wa EP ya Harmonize @harmonize tz : Uongozi wa WCB unaomba msamaha kwa ucheleweshaji kama ahadi ya awali ilivyo, muda mwingine msanii anakuwa na shauku kubwa kuwapa mashabiki wake burudani na kufikia sehemu anasahau kuwa hizo burudani pia ni biashara ambayo itakayompatia kipato yeye ili aweze kutoa burudani zingine, kama uongozi lazima tumuandalie misingi ya kibiashara ili anufaike na kazi zake pia, na vilevile tusiwe na matabaka ya kuwajali mashabiki wa sehemu moja pale kazi zinapotoka, inatakiwa kama uongozi kuhakikisha kazi ya msanii inapatikana sehemu zote kukidhi hamu za mashabiki wote, kingine unapofanya kazi na wasanii waliopo lebo kubwa inahitajika lebo zao waweze kutia saini mikataba ya mirabaha ili nyimbo ziweze kuwepo kwenye mitandao yote ya mauzo ili isilete matatizo kwenye lebo zao. Kwahiyo ukubwa wa EP ya Harmonize ilihitaji kupitia yote hayo ili iwe tayari kufika kwa mashabiki, tunashukuru Basata walitoa ushirikiano mzuri kuzikagua nyimbo kwa muda muafaka na hakutokua na tatizo la wimbo unatoka halafu unafungiwa. Kwa haya mafupi sasa EP ya Harmonize ya #AfroBongo itatoka rasmi wiki ijayo chini ya Lebo ya WCB Wasafi. Tunaomba radhi kwa yoyote tuliyemkwaza kwa namna moja ama nyingine tunajua bila nyie mashabiki hakuna WCB. MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI BONGO FLAVA ??“.

Taarifa hii inaibua maswali mengi juu ya mahusiano kati ya WCB na muimbaji huyo Uongozi wa WCB haukutangaza kwamba Harmonize ataachia EP kama ilivyo kwa wasanii wengine wote wa WCB.

“Siwezi Kutoka WCB, Diamond Ni Mtu Mmoja Poa Sana”-Mose Iyobo

Dansa maarufu kutoka WCB ambaye anafanya kazi kwa Msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz kwa muda mrefu, Mose Iyobo ameibuka na kudai kuwa bosi wake  huyo ni mtu poa sana.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, Mose Iyobo amefunguka na kusema Bosi Wake Diamond ni mtu poa sana na ni bosi mzuri kufanya naye kazi.

Diamond ni mtu fulani ambaye yupo poa sana yaani Siwezi kusema nitoke pale (WCB) eti niende sehemu nyingine! Labda nikafungue kitu changu mwenyewe”.

Lakini pia Mose Iyobo ametupilia mbali Tetesi Za kuwa analelewa na mzazi mwenzake Aunty Ezekiel na kudai anatengeneza hela nzuri tu kama Dansa wa Diamond hivyo hahitaji kulelewa.

Nalelewaje wakati nafanya kazi kwa Diamond? Nikimwambia Diamond nataka gari Fulani yaani inachukua dakika chache tu”.

 

 

Tumekoma Hatuwezi Kurudia Tena Makosa-Babu Tale

Meneja wa Kampuni ya Wasafi (WCB) Babu Tale amekiri kuwa adhabu waliyopewa wasanii wake Diamond na Raymond Mwakyusa’ Rayvanny kufungiwa miezi miwili, imewafundisha na hawatarudia tena.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la mwananchi, Babu Tale ameweka wazi kuwa adhabu waliyopata Diamond na Rayvanny imekuwa somo kwao wote na hawatorudia tena makosa.

Kwa kweli kwa muda wote ambao wasanii wetu walikuwa wamefungiwa pamoja na kusitishwa kwa tamasha letu la Wasafi, tumejifunza mengi, hatuna budi kuishukuru BASATA na serikali kwa ujumla tunachowahaidi ni kwamba tumrjifunza mengi na hatutarudia tena”.

Diamond na Rayvanny walifungiwa mwaka jana Desemba 15 na kuzuiwa kufanya maonyesho ya nje na ya ndani hata hivyo Wiki chache zilizopita BASATA Ilitangaza kuwafungulia rasmi.

 

Diamond Afungukia Hatma Ya Wasafi Festival

Msanii wa muziki wa Bongo fleva na CEO wa WCB Diamond Platnumz amefunguka na kuzungumzia mipango ya Wasafi Festival mara Baada ya kuachwa huru na BASATA.

Katika mazungumzo yake na Waandishi wa habari siku ya leo, Diamond amewataka mashabiki zake waendelee kuwa wavumilivu  kuhusu tamasha lao la Wasafi Festival kwani bado wanafikiria kama walianzishe upya au waendelee kufanya shoo mikoa iliyobakia, lakini kwakuwa tayari wameshafunguliwa basi hakuna shaka juu ya hilo watawajulisha kitachoendelea.

Namshukuru  mwenyezi Mungu kwakuniweka hai na salama mpaka nafika hapa, lakini pia kabla yakuanza chochote pia niishukuru serikali yangu pendwa kwakunifungulia kifungo ambacho nilikuwa nacho, maana kifungo kinafunguliwa tu na neema hizo zinakuja.

Niwashukuru watu wote ambao wameisapoti Wasafi Festival, nawashukuru sana kwa sababu mapokezi yalikuwa makubwa hatukuyategemea, lakini mimi na menejimenti yangu tulikuwa tunajadili tumalizie ile mikoa iliyobaki au tuanze na upya mwaka 2019, japo mzani unaelemea mwaka 2019 ili watu waliokuwa bado hususani mikoa ambayo hatujenda wawe na hamasa zaidi, hivyo tunawaomba mashabiki zetu wasichoke kutusapoti na kuendelea kuzifatilia kazi zetu nzuri“.

Diamond na Rayvanny walifungiwa na BASATA mwishoni mwa mwaka jana baada ya ku-perform wimbo wao wa Mwanza Nyegezi kwenye Tamasha lao la Wasafi Festival jijini Mwanza, wimbo ambao umefungiwa na Baraza hilo. Lakini juzi Baraza hilo lilitangaza kuwafungulia baada ya kuomba radhi.

Diamond Asema Sababu Iliyokuwa Inawapeleka Kutoa video nje

Msanii diamond platinumz amefunguka na kujibu moja ya maoni ya shabiki kwa kumwambia kuwa sababu kubwa ya wao kuwa wanatoka nje ya nchi kipindi cha nyuma na kwenda kutoa video marekani au afrika ya kusini sio maeneo ya kutolea video lakini ni kwa sababu hawakuwa na vifaa vya kufanyia kazi zao na zikaonekana kuwa nzuri.

Akijibu katika uwaja wa maoni ambapo moja ya mashabiki aliandika  ” tanzania kumbe tuna maeneo tu mazuri  na hakunaga ulazima  wa wasanii wetu kwenda nye ya nchi kutafuta location za video ” diamond nae akamjibu shabiki huyo “ hatukufata locations , tulifata vifaaa na teknolojia zao …ila kwa sasa tumenunua wenyewe na kufungua productions wenyewe  na ndio maana tunauwezo wa kushoot popote… na ndio maana halisi ya mapinduzi ya kiburudani”

Shabiki anavutiwa a na kusema hivyo baada ya kuona video mpya iliyotoka ya msanii mbosso.

Diamond Atangaza Ujio Wa Msanii Mpya Wa Kike WCB

Msanii wa muziki wa Bongo fleva na Mkurugenzi wa Music Label ya WCB Diamond Platnumz ametangaza rasmi kumsaini Msanii wa pili katika label ya WCB.

Diamond alitangaza habari hiyo njema siku ya Ijumaa kwani kwa muda mrefu Label hiyo imekuwa na utaratibu wa kudai ni wasanii wa kiume tu bil kuwapa nafasi wasanii wa kike.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Diamond ameandika ujumbe huu:

About to introduce a FEMALE Artist….. Coz i believe Women they can, if you Empower them….” (Nipo mbioni kumtambulisha msanii wa kike (WCB), kwa sababu naamini wanawake wanaweza, wakiwezeshwa)“.

Mpaka sasa haijajulikana ni Msanii gani wa kike ambaye atatambilishwa ingawa Baadhi ya mashabiki wamekuwa wakihisi nafasi hiyo huenda akaipata mwanadada Nandy ila Diamond mwenyewe hajathibitisha hilo.

 

Mh Lusinde awagomea BASATA kuhusu Wimbo wa Mwanza.

Moja ya wabunge katika bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania mh lusinde kutoka mtera amefunguka na kuwataka baraza la sanaa kuacha kufanya kazi za ubabaishaji kwa kutaka kufanya kazi na kutoa hukumu za wasanii kulingana na klosa husika na sio kwa kuwakomoa wasanii.

Lusinde anasema kuwa basata wamekuwa wakifanya wasanii waishi kwa uoga wakati wana vipaji vya kuwafikisha mbali, Lusinde amesema hayo ikiwa ni siku cahche tangu BASATA walipotoa msamaha wa wasanii hao kuendelea kufaya show zao za nje ambazo zilsainiwa nje ya adhabu waliopewa kwa muda usiojulikana kutokana na kukaidi maagizo ya baraza hilo.

Wasanii hawa wawili kutoka WCB, Diamond na rayvanny wamepewa adhabu kwa muda usiojulikana kutokana nakuaidi agizo la kuacha kuimba wimbo huo jukwaani lakini wasanii hao waliimba wimbo huo , hivyo kuwafanya wapewe adhabu.

Mh lusinde anasema kuwa kama wimbo huo kuimbwa ni makosa basi hakuna haja ya kuwa na kata yenye jina hilo kwa sababu hata watu waapoitamka  basi wanakuwa wanatamka matuzi hivyo waachane nayo tu na kubadili jina hilo.

Hata hivyo mh huyo ametaja serikali kuingilia kati swala hilo kabla halijaonekana kuwa na mtazamo tofauti na wa wasanii wengine pia.

Meneja Wa Harmonize Afunguka Kuitosa WCB

Meneja wa staa wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB, Harmonize anayejulikana kama Mr. Puaz amethibitisha kuachana na Harmonize kwa like alichodai ni kukosa maelewano.

Licha ya Harmonize kuwa chini ya WCB Lakini pamoja na wasanii wengine wa label hiyo wana mameneja tofauti ambao wanasimamia kazi zao.

Kwenye mahojiano na Gazeti la Risasi la Mchanganyiko, Mr. Puaz alikiri kuacha kufanya kazi kama Meneja wa msanii huyo Lakini amekana kuwa na Bifu na msanii huyo wala Label ya WCB.

Ni kweli kwa sasa mimi na Harmonize hatufanyi kazi pamoja kwa sababu ya kupishana kauli; lakini haimaanishi mimi na WCB hatufanyi kazi au hatutafanya kazi.

WCB ni familia yangu ambayo ukaribu wangu na wao ulitokana na urafiki wangu na Diamond hivyo siwezi kuiacha, panapo kuwa na nafasi ya mimi kuhitajika kutoa mchango wangu nitaendelea kutoa kama mwanafamilia“.

 

BASATA Wakanusha Taarifa Za Kuwafungulia Diamond na Rayvanny

Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limekanusha taarifa za kuwafungulia wasanii Diamond Platnumz na Rayvanny wanaotumikia adhabu ya kutojihusisha na muziki kwa muda usiojulikana baada ya kufanya makosa mbalimbali ndani ya kipindi cha miezi miwili.

Taarifa hiyo imekuja baada ya msanii Diamond kutangaza kwenye mkutano wa waandishi wa habari jana kuwa wameruhusiwa kufanya tamasha la muziki, Wasafi Festival’  nchini Kenya.

Siku chache zilizopita wasanii hao kupitia mtandao wa Instagram Walionekana wakifanya mkutano na waandishi wa habari nchini Kenya kutangaza maonyesho yao yanayoendelea, lakini alifajiri taarifa ya Basata ilisema kuwa hawajatoa ruhusa kwa wasanii hao.

Baada ya kauli hiyo kutoka kwa wasanii hao kutoka WCB, BASATA walitoa tamko lao na kusema:

Ikumbukwe kuwa Desemba 18 tuliwafungia kutojihusisha na sanaa kwa kipindi kisichojulikana kwa kuimba kwa makusudi wimbo Mwanza tulioufungia kwa sababu za kimaadili,

“Baraza linasisitiza kuwa halijawafungulia wasanii hao, pia linawaonya kuacha kutoa taarifa za uongo kabla halijawachukulia hatua kali zaidi,” imeeleza barua hiyo.

 

WCB Waongeze Ushirikiano na Wasanii Wengine.:-RC Zanzibar

WASANII wa Zanzibar na Tanzania bara wametakiwa kuimarisha mahusiano na ushirikiano baina yao ili kusaidia maendeleo ya muziki wa kizazi kipya katika pande zote mbili za Jamhuri ya muungano Tanzania.Wito huo umetolewa na mkuu wa mkoa wa mjini magharibi alipokutana na timu ya wasanii kutoka lebo ya ‘Wasafi Clasic’ ya Dar es salam na Zenji Flavour Unity (ZFU) ofisini kwake Vuga walipomtembelea kuelekea tamasha la Wasafi 2018 linalotarajiwa kufanyika kesho.

Ameeleza kuwa pamoja na kuwepo kwa mashirikiano ya muda mrefu, ipo haja pande mbili hizo kukaa chini na kufanya kazi pamoja ili kuimarisha vipaji vyao sambamba na kuwasaidia wengine kufiukia malengo yao.

Ayoub ambae pia ni mlezi wa chama cha wasanii wa muziki wa kizazi kipya Zanzibar alishauri kuanzishwa kwa mashindano ya kutafuta wasanii bora wa Zanzibar watakaoweza kuunganishwa na lebo ya muziki ya WCB rai ambayo iliungwa mkono na Afisa Mtendaji Mkuu wa lebo hiyo msanii Naseeb Abdul ‘Diamond’ na mlezi wa lebo hiyo Said Khamis Fela ‘Mkubwa Fela.

Aidha Ayoub aliupongeza uongozi wa lebo hiyo na Mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar ZSSF kwa kukubaki kuwajumuisha wasanii wa Zanzibar katika tamasha hilo jambo alilosema litawasaidia kujitangaza na kuongeza uzoefu wa kushiriki matamasha makubwa kama hilo sambamba na kuwataka wazingatie sheria na taratibu zinazosimamia sanaa nchini.

Nae msanii Naseeb Abdul ‘Diamond’ amemshukuru Mkuu huyo wa mkoa kwa kuunga mkono kazi zinazofanywa na wasanii wa ndani na nje ya zanzibar jambo ambalo linawawezesha kuitikia kaulimbiu ya serikali zote mbili za kuwataka vijana kufanya kazi.

alisema, hatua ya serikali kuendelea kufuatilia shughuli zinazofanywa na wasanii zinathibitisha kuwaunga mkono ili wafikie ndoto zao jambo ambalo aliahidi kuliendeleza ili kundi kubwa zaidi linufaike.

Alieleza kuwa katika tamasha hilo mbali ya burudani wanayoitoa wameweza kufanya shughuli mbali mbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kutoa misaada katika taasisi za elimu, wajasiriamali na kwa Zanzibar wanategemea  kutoa misaada katika skuli na kituo cha afya cha Chumbuni ili viweze kutoa huduma nzuri kwa jamii.

Awali akitoa taarifa katika kikao hicho mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa ZSSF Khamis Thani alieleza kuwa mfuko huo umeamua kuungana na lebo hiyo ya muziki kwa lengo la kurudishga faida wanayoipata kwa jamii kwa kuimarisha wajasiriamali na kutoa misaada ya kijamii.

Diamond, Rayvanny na Mbosso Wapata Ajali Stejini Sumbawanga (+Video)

Msanii wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB Diamond Platnumz na wasanii wenzake Rayvanny na Harmonize walipata ajali katika Steji ya Wasafi Festival iliyokuwa inafanyika mkoani Sumbawanga.

Shoo hiyo ilifanyika siku ya jana 9 Desemba katika uwanja wa Nelson Mandela ambapo wasanii hao walikuwa wanaperfom wimbo wao pendwa kabisa wa ‘Zilipendwa’ lakini ndipo balaa lilipotokea Baada ya wasanii hao kula mieleka.

Lakini baada ya kudondoka kwa Diamond akifuatiwa na Mbosso wasanii hao waliinuka na kuendelea na shoo na iliripotiwa kuwa hakuna Msanii aliyepata majeraha makubwa zaidi ya michubuko ya hapa na pale.

Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale alitoa taarifa kuwa wasanii hao wanaendelea vizuri na hakuna aliyeumia.

Baada ya sakata hilo Kupitia ukurasa Wake wa Instagram, Diamond Platnumz aliposti video hiyo na kuandika:

https://www.instagram.com/p/BrK67ZVlDFX/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=d9geezbdwlgj

Joseph Kusaga Ajibu Tuhuma Za Kumiliki Wasafi Tv na Radio

Mfanyabiashara maarufu na Mkurugenzi wa Vlouds Media Group Joseph Kusaga amejibu tetesi zinasombaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kumiliki vituo viwili vya runinga na radio, Wasafi TV na Wasafi FM.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Clouds 360 cha Clouds Tv, Joseph Kusaga amefunguka kuwa yeye anamiliki karibia vituo vyote vya radio za vijana hapa Tanzania.

Hapana mimi sitakwenda huko, mimi  namiliki radio zote za vijana, radio zote za vijana mimi namiliki, kwa njia moja au nyingine, ukimuita Seba atakwambia umenielewa. Lakini labda ni kwa sababu ya kuongeza wigo, labda wigo wetu sisi unaweza ukawa hautoshi, mimi nashiriki kwenye industry yote ya burudani”.

Lakini pia Kusaga alipoulizwa kuhusu umiliki wa Wasafi Tv na Radio hakutaka kuweka wazi kuwa anamiliki zote lakini badala yake alisema anamiliki redio nyingi za vijana hapa nchini ikiwemo Jembe Fm ya Mwanza na Safari Fm ya Mtwara.

Wiki iliyopita kwenye Gazeti moja Kuna taarifa ilichapishwa kwamba Mke wa Kusaga anamiliki nusu ya hisa za Wasafi Tv na Radio na hata Mitambo ya Wasafi inawashwa Clouds Media.

Diamond Platnumz Aanika Ndege Mpya Ya Wasafi Festival

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini na CEO wa WCB Diamond Platnumz ameitambulisha ndege ambayo itakuwa na jukumu la kubeba wasanii Watakaoperfom perfom kwenye stage ya Wasafi Festival Mombasa.

Ndege hiyo inadaiwa kuandaliwa na waandaaji wa shoo hiyo ambapo watatumia wasanii wa WCB kuwachukua jijini Dar na kuwapeleka Mombasa maalum kwa ajili ya shoo huku wengine wakidai amenunua Diamond japo mwenyewe bado hajaweka wazi kama ni ya kununua ama ya kukodi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond ameandika maneno haya:

WCB Kumiliki Ndege Yao Wenyewe

Bosi wa kundi la Wasafi ameitambulisha ndege yao itakayokuwa ikitumika katika mizunguko yao katika kipindi hiki cha Wasafi festival hasa pale watakapokuwa wamefika Kenya ambapo watafanya show hiyo Desemba 2.

Fununu zinasema kuwa ndege hiyo i enunuliwa na Diamond platinumz huku wengine wakisema kuwa ni ndege imeandaliwa na waandaji wa tamasha hilo huku  yeye mwenyewe akikaaaa kimya kutokuzungumzia swala hilo hata kwa mara moja.

katika ukurasa wake diamond aliweka picha hiyo huku akisema baadhi ya maneno yenye kuonyesha kiburi cha kuwa na umiliki halaliwa ndege hiyo.

 

Young Killer Adai Wasafi Festival ni Ukombozi Wa Kweli Kwenye Burudani

Msanii wa muziki wa hip hop nchini Young Killer ameibuka na kulimwagia sifa kibao Tour ya WCB ya Wasafi Festival Baada ya kushiriki katika tamasha Lao la kwanza mkoani Mtwara.

Young Killer Msodoki amefunguka kwa kulisifu tamasha la Wasafi Festival na kudai kuwa ni ukombozi halisi katika sekta ya Burudani Nchini Tanzania.

Katika mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Young killer amefunguka haya zaidi kuhusu shoo hiyo:

Ujio wa Wasafi Festival ni mkubwa na umekuja kiutofauti sana na kiukweli tasnia yetu inahitaji vitu kama hivi kwa sababu haya ni mapinduzi kwani muda mrefu tumekuwa tukimiss matamasha yamekuwa machache kwaiyo kuja kwa Wasafi Festival ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu kwani inaonyesha ni kwa jinsi gani Sanaa yetu hivyo Big Up sana kwa Wasafi”.

Young Killer pia atakuwa mmoja wa wasanii Watakaoperfom kwenye shoo nyingine ya Wasafi Festival itakayofanyika Mkoani Iringa siku ya Leo.